*Swali. Katika process za uchumba kuelekea ndoa ni sahihi kijana wa kiume kumuomba binti pesa au akopeshwe na binti?*
ANAJIBU: Ev Elisha Kazimoto(Mwanasaikolojia)
*WhatsApp 0755444078*
_Niweke bayana dhana ya uchumba kisaikolojia ndo tupate mwanga wa kujibu swali hiki kwa ufasaha_
✍ Neno *Mchumba/Wachumba* _Ni mtu au watu wa jinsia ya kike na kiume walio katika mahusiano ya kati,ya maridhiano ya kuoana na kuishi pamoja kama mke na mme, waliozungatia vigezo vifuatavyo_:-
1⃣ Wamependana kwa hiyari upendo wa kuwa mtu mke na mtu mme, upendo *Tosherevu* (Selective & Specific Love) yaani umechagua kati ya wengi,umebaini huyu tu ndo anafaa na h as. una mwingine. ( *_Kama unatafuta,una mtu hujafikia kiwango hiki cha upendo, Kisaikoljia ni marufuku kumwita mchumba_*)
2⃣ Mmefuata taratibu za kiroho(kidini) au kifamilia za kuonyesha ridhaa ya wazazi au walezi wa pande zote mbili kuridhia mchakato wenu wa uchumba kuanza.( *_Ikiwemo barua ya posa,utambulisho kwa familia, kwa mchungaji(kwa wakristo),kulipa maali, kuvishana pete za uchumba nk_*)
3⃣ kupima afya zenu kwa madhehebu yenye taratibu za kupima
✍Mambo hayo yakizingatiwa ndiyo msingi wa uchumba wenye *_Mwelekeo wa ndoa_* kinacho baki ni Akili ya mtu binafsi aliyeko kwenye mahusiano kumsona mwenzake kufahamu ni mtu wa aina gani, ni mkweli ki kiasi gani,ni muwazi kiasi gani, vision yake iko imara kiasi gani, present action yake hiw it define future life, hiyo ni akili binafsi ya mahusiano ya kisaikolojia kubaini kama mtu ni tapeli,mtu sahii,nk( *_kwa ufupi uchumba una terminology 2 tu, Muda wa Kumsoma mwenzako tabia na Muda wa Maandalizi ya harusi_*)
✍ Kwakuanza kujibu swali letu: _Suala la Kuhudumiana kama wachumba ni jambo jema na muhimu kwa watu walio serious kama vigezo tajwa hapo juu, ila akili,uangalifu na kiasi vizingatiwe iki kuepusha maumivu ya moyo.( Katika mambo yote Akilini mwako inabidi ujue *Uchumba Si Ndoa muda wowote ikiwepo sababu kubwa ya msingi unavunjika*) kwa hiyo mambo yote mnayo yafanya iwe kusaidiana,kufabta maendeleo uwe na taadhari akilini.
✍ *Kuhusu kijana kumkopa binti* Si suala la kukopa tu,hata binti kumuhudumia kijana kimavazi,kipesa,kumfungulia miradi nk, kama mme we mtarajiwa haina ubaya *_Inategemea kiwango cha Akili alocho nacho msichana, na anavoona mwenendo wa mahusiano yao na hali halisi ya kiuchumi ya kijana_* tafsiri zingine za kujishusha,unapoteza heshima, nk inategemea mitazamo yenu na nia yenu ya mahusiano ni dhana potofu kama wasemavyo wengine, *kuoa mke msomi kukuzidi,mwenye cheo kukuzidi,nk utadharauliwa* ni ufinyo wa akili ya mahusiano kisaikolojia maana Upendo wa ndoa *Never deal with Envirimental issues but Internal & unconditional issues* yaani moyo wako umempenda kwa sifa za ndani na si ana nini kwa nje hiyo ndo tunaiita REAL LOVE. Kwa mazingira hayo badala ya kumkopa utamsaidia tu, maana ni kwa manufaa yenu( Ustawi wake ni ustawi wako)
✍ NB: Kisaikolojia kulingana na ongezeko la usanii, kushuka kwa akili( ongezeko la watu walovurugwa kisiasa,kijamii,kiuchumi,kiroho nk, tunashauri umakini uwepo sana katika kuhudumiana, wengine wamegeuza mahusiano kama mradi wa kuendesha maisha,na kusababisha majeraha mengi kwa wapenzi wao. Ndiyi maana tunanema hudumianeni watu wenye akili,umemsoma mwenzio kiasi kikubwa na watu mlo katika uchumba kama vigezo pale juu siyo uchumba wa WhatsApp ,Instagram na fb na wa uchochoroni, wa kuiyana wachunba na kupeaba promises kibao,hata wazazi hawa mfahamu ,hata barua ya posa haipo, ndo unajitundika kumfungulia duka,isafiri,unaenda bank kukopa unampa mkopo wako,my friend utapata ugonjwa wa kisaikolojia wa kuwachukia watu wa jinsia yake milele pale atakapo kusaliti na ku break relationship. Kumbe wewe ndo ulitumia akili fupi kuendesha mahusiano.
Quote: *_Katika kuanza mahusiano Kijana akili yake huwa juu sana,na ya msichana ushuka sana(anapoteza akili kiasi flani), na mkioana mwana mke anaongezeka akili, mwanaume anapoteza akili kiasi flani_* (Kuwa Makini na Mahusiano is not simple as you think)
*Imeandaliwa na Msaikolojia na Mshauri, mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa. Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)*
WhatsApp 0755444078
No comments:
Post a Comment