*Mada mpya*
*Kuna ulazima gani kufanyia honeymoon gest/hotel na si nyumbani imakaaje hii..utamaduni huo ni mzuri...kuna maandiko yasaport hii...vitu gani vinafanyika huko saidi ya sex..ntafurahi kupata majibu.*
ANAJIBU: EV ELISHA KAZIMOTO
*WhatsApp 0755444078*
_Hapa kwanza niweke vizuri mtazamo wa swali kabla ya kushughulikia hoja Potofu ambazo huwa watu wanazijenga kuingiza hisia zao kwenye hoja huru_
👉 *_Kuhusu ulazima wa kwenda Honeymoon kwa mabibi harusi baada ya kufunga ndoa, HAKUNA ULAZIMA( maana yake Ukienda hakuna shida,usipoenda hakuna shida, kitu kikisha kuwa na ulazima maana yake kisipo fanyika hivo kuna athari kubwa)sasa hapa hakuna ulazima ILA KUNA UMUHIMU WW KISAIKOLOJIA NA KIJAMII(Umuhimu maana yake,jambo hilo lapendeza likifanyika hivyo maana kuna vitu vitafanikiwa, ila hata isipo fanyika hakuna athari ila kuna vitu vitakosekana, huo ndo umuhimu)_*
👉Kwa Habari za *Maandiko ya neno la Mungu kuthibitisha ulazima au kutokubalika, HAKUNA ANDIKO/FUNDISHO HILO ila itategemea mtazamo na tafsiri binafsi ya mtu na msimamo wake* ila kuna Falsafa za kisaikolojia
👉Kuhusu kuwa *Utamaduni huu ni mzuri au mbaya, hii inategemea na mwono wa mtu binafsi* kisaikolojia _Uzuri au ubaya uwa katika macho ya mtu binafsi na si katika kitu chenyewe, tafsiri yako na mwono wako ndo unaotafsiri ubaya na Uzuri wa kitu_
✍ Baada ya kuwela vizuri Dhana 3 za swali, sasa niingie kuuzungumzia honeymoon na maharusi.
*HONEYMOON (Eneo la mapumziko kwa maharusi baada ya kufunga ndoa) Guest au Hotel* ni maeneo ambayo maharusi uchagua kwenda kwa mapumziko kwa siku zozote zile 1,2,5,10 kulingana na uwezo wao,matashi yao, au Budget ya Kamati ya Harusi. Kwa nini watu waende Honeymoon hotel/guest baada ya kufunga ndoa? *Ziko sababu kadhaa za kisaikolojia na kijamii( hakuna sababu za kiroho kama ilivyo, mkiamua kwenda nyumbani kwa bwana harusi,hakuna sababu za kiroho ila sababu za kijamii)*
1⃣Kutafuta Faragha(Maala tulivu,pasipo na mwingiliano wa sura za wenyeji).
_Sababu hii ni muhimu kwa mazingira ya watu ambao wanaoana ndo mara yao ya kwanza kujutana kimwili(Mabikira) kuna changamoto nyingi za watu mabikira kukutana kimwili siku za mwanzoni, (kwa wana wake,kisaikolojia ni watu wanao jali sana privacy sanaa katika sex kuliko wanaume), mwanamke ili afanye sex kwa uhuru na ajiachie na aifurahie,hupenda kujihakikishia USIRI, ukimya,( sasa kulingana na maisha,kuna watu wanaoa wapo kwenye nyumba za kupanga,au nyumba zao ila hazina uhuru, kisaikolojia ni makosa makubwa kufanya rendo la ndoa kwa kujiiba,kujibana,kujishtukia uwepo wa watu,au kusikiwa. Ndiyo naana Hotelini au guest inakupa uhuru wa kujiachia kihisia._
2⃣ *Sababu ya Mapumziko ya Kisaikolojia* Harakati za harusi na mapambano ya harusi huchosha mwili na akili, ndiyo maana watu hupenda kutafuta sehemu tulivu,mazingira mapya ambayo hayata kudai kuyaweka sawa tena ila tu ,uke,unywe na upumzike, bila mwingiliano na mtu yeyote na maeneo hayo niya hotel au guest, nyumbani hakuna utulivu, mnafunga ndoa tu, wapo watu wanakaa hapo kwako ndugu,jamaa wengine wanakuja kusalimia kesho yake haluna utulivu unaohitajika kwa watu wapya. Guest au Hotel mnakuwa na muda wa kutulia kutathimini na kupongezana mwa safari yote ya mwaka 1,2,3 5... Bila usumbufu wa mtu yeyote.
*NIWEKE BAYANA DHANA CHACHE POTOFU ZINAZOIBULIWA*
👉 *_Dhana ya Kuacha baraka za ndoa Guest/ hotekini badara ya Nyumbani_* _Hii ni dhana dhaifu kwa watu dhaifu kiroho. Baraka siyo mchanga au jasho,au kimiminika kwamba vikimwagika tunaviacha kule, baraka zinabebwa katika mionyo kwa imani na si katika nguo. Kama unahisi maombi unayoombewa ya harusi yanakaa kwenye suti na shera na ngozini, wewe huna tofauti na mbeba irizi,ila bado mchanga kiroho. Kumbuka hauendi hotelini kuzini,kwamba unarnda kuanguka, unaenda kwa mapumziko na tendo halali na takatifu._
👉 *Dhana ya Kuzoa mapepo* Hii ni dhana ya watu wasiokomaa kiimani, kuna maeneo mengi kila kona,kuanzia njiani,shule,vhuoni,sokoni na hewani,mapepo yanakaa ila wana wa Mungu tunaishi na tunatembea huko na kule bila kuvaliwa na mapepo, kama unahisi hotelini ndo kuna mapepo, bado ufahamu wako wa kujua ulimwengu wa roho wa giza na wa nuru unafanyeje kazi zake uko chini sana. Mapepo yanavaa Nafsi wazi isiyo na Mungu,au dhaifu kwa imani au yenye dhambi,popote pale,shambani,njiani nk.
👉 *Dhana ya Guest/ Hoteli kuna uchafu mwingi unafanyika* hii ni dhana ya mtu mwenye ufahamu mfupi,karibu kila kitu kina uchafu, unajua Daladala(mabasi) kuna unachafu mwingi,kuanzia wa ukahaba mpaka wa kimatambiko? Unajua nguo hiyo ya mtumba unayoivaa alivaa kahaba nani au mtu mwenye mapepo gani? Ofisini unako fanya kazi unajua seat hizo zimekaliwa kwa shuguli gani? Labda niseme huu ni uchanga wa kiroho. *swali la msingi: Ukisafiri uwa unaenda na kitanda chako? Guest au hoteli unaenda kulalia nini? Au wahubiri wanapo kodishiwa hoteli,guest huwa wanaenda na vitanda vyao! Hujui sisi tubapokanyaga tunanguvu ya kumiliki na kupatawala,panatakaswa kwa matumizi yetu? Isingekuwa hivo kuna vitu vingi tungeviacha, ilibidi tumiliki vya kwetu popote duniani.*
_Ndo maana katika maombi ya Yesu akaombea wanafunzi wake,kwamba Baba siombi uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu_
👉 *Dhana ya Kuharibu pesa* Hii ni Dhana ya Akili ya kiumaskini na mtu maskini, Pesa haitakuja kutosha au kuingezeka kama haitumiwi,kujibana siyo kutajirika ila mpangilio wa maisha na malengo.
✅ Aina ya harusi yako ndo inatoa picha uende wapi,hivi unajua pesa ya honeymoon inatoka kwenye Kamati ya harusi ambayo ni michango ya watu ya harusi ambayo si pesa yako ya kuanzia maisha
👉Lakini dhana hii ya umaskini imezifanya ndoa za walokole watu wajiitao wa rohoni *Kuchuja* tangu mnaoana hakuna zawadi za surprised wala kutoka out, january mpaka December ni ndani kisa, eti kutumia laki 1 kwa out, au laki 3,si bora ufanye maendeleo🤔🤔, maendeleo gani yanayozidi kuendeleza furaha na shangwe ya ndoa?.
*MY TAKE* _Kama mtazamo wako haupo katika kutumua pesa ili ije nyingine, tulia,ila wenye mawazo ya kuongezeka na kufanikiwa,wabatumia Pesa kujenga saikolojia zao ili wafanye maendeleo kwa utulivu wa kifikira. Tangu umebana pesa umewahi kufanya kitu gani cha kutishia watu wanaotumia pesa kujenga saikolojia zao? Mbona maisha yakawaida, usiishi kwa kujibana ukingojea kutajirika kutoka hewani, mafanikio ni pamoja na kuwa na saikolojia iliyo huru na kufunguka._
*_Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)_*
WhatsApp 0755444078
No comments:
Post a Comment