*SWALI*: Bwana Yesu asifiwe.
*Ninaomba kujua kuna nguvu gani ya kiagano ktk bikira ya mwanamke.*
Au kuna agano gani alilonalo mwanamke ktk mwili wake km agano la mwanamke au mtoto wa kiume kutahiriwa baada ya siku nane kuzaliwa.
*Anajibu Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 07554440708.
_Kwanza naona muuliza swali ameuliza maswali mawili lakini yote yana dhana moja ya Agano la damu,kote kwa pnde mbili, kwa jinsia ya kike na kiume_
✍ *Agano ni nini kwanza* _Ni maridhiano,makubaliano baina ya pande mbili kwa sababu maalumu za kiupendo,kisheria,kimalengo._
✍ Agano laweza kuwa la maneno, viapo vya maneno,la uhai wa mtu,mnyama,ndege nk na la damu.
✍ Mara nyingi, *_Agano la Damu lina nguvu kubwa kuliko agano lolote,maana ni agano la uhai, (katika damu ndimo kulimo uhai)_* na Mungu tangu mwanzo alitumia agano ili la damu kwa watu wake, na shetani anapenda kulitumia kwa kuwa kuna nguvu ya uhai ambayo ndo maisha ya mwanadamu.
*Kutoka 24 : 8 - Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.*
✍ *Nianze na suala la Bikira kwa mwanamke* _ Bikira kwa mwanamke ni Alama ya Uaminifu wake kwa mume wake, ni Agano la mwili kati yake na mume wake(mwanaume).
✍Na Bikira ilikusudiwa iwe agano la mwanamke na mume wake,siyo na mume mwingine.👇👇👇👇👇
*Kumbukumbu la Torati 22 : 17 - angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji.*
_Ubikira ulifatiliwa kwa ukaribu mno,na kuweka mavazi(mashuka)kuthibitisha kama mwanadada huyu alikuwa bikira au la,na mavazi yele yalipelekwa kwa wazee wa mji kuwaonyesha huyu alikuwa bikira.
✍Katika ubikira ndimo kulimo damu,damu ndiyo agano la kuungwa na mume huyo( Labda ni semee kwanza kuhusu tendo la ndoa, Lile tendo lina kazi ya kumuunganisha mtu na mwenzie kihisia, & kimwili, na alama ya *_Agano la kuunganishwa ni Bikira na Nguvu ya Agano hilo la kuunganishwa Katika ndoa ni Damu ya Ubikira_* (Sex inakuunga na mtu huyo mnaye sex)
👇👇👇👇👇👇👇
*1 Wakorintho 6 : 16 - Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.* Ndiyo maana likaitwa Tendo la Ndoa, watu maalumu,ili likuunge na alokuchagua Bwana,siyo ujiunganishe na kila mtu,ilikusudiwa uungwe na mmeo au mkeo.
Na Agano hilo lilikuwa ni kwa faida ya wana ndoa kwani Ubikira kwa mume na mke, _Ni Ishara ya Uaminifu, Uvumilivu, Upendo, Heshima katika ndoa_.👇👇👇👇
*Mambo ya Walawi 21 : 13 - Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.*
✍Ulitakiwa umwoe mwanamke katika ubikira wake, kulikuwa na maana kubwa na umuhimu mkubwa wa kuunganishwa na mtu mwenye Alama na Nguvu ya Agano la mwili. Japo wengi wa watu wa leo wamelichukulia kiurahisi suala la Ubikira, ndiyo maana na ndoa nyingi zinachangamoto kubwa sana ,fujo na vurugu, kuna vitu vinakosekana vya kiagano, vinavyo imarisha agano.
✍ Kufunga ndoa kuna agano la maneno lina tumika, ila Alama na Agano hilo huwa ni pete, na Nguvu ya Agano lake la mwili kwa mwanaume ni Ubikira. *_Sasa ondoa mtazamo finyo, na wa kujitetea kwa udhaifu wako, kuwa mbona ziko ndoa nyingi za waliooana bikira ila zina changoto nyingi kuliko za waliooana bikira hakuna, huo ni mtazamo finyu, wala hilo Halibadirishi formula ya Kimungu ya kuufanya ubikira uwe agano la ndoa_*
✍ _Kwa sababu hii niwatake wadada wote ambao hawajaolewa na bado wana sifa hii ya ubikira tafadhari tunza na bado nguvu ile ipo kwenye ulimwengu wa roho na kinatenda kazi. *Tunza Bikira* uliye poteza kwa kutojua, enzi za ujinga, au kwa kujua yaani ukiwa katika wokovu, hakikisha unakuwa mwaminifu katika maisha yako yote ya ujana Mungu atakutokea kwa njia nyingine._ Tafuta somo langu linalosema *Uzaliwa wa kwanza, part 1,3 & 3*
✍ *Suala la Kutahiriwa* hili nalo lilikuwa ishara ya agano kati ya watu na Mungu, agani nalo hili liba nguvu ya damu,au alama ya damu.( Hili ni Agano la mwili)👇👇👇👇
*Mwanzo 17 : 13 - Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.*
Lakini hili liliashira Usafi, Agano hili lililenga kuobyesha usafi wa watu wa Mungu kwa hiyo katika agano la kale Israeli walilifatilia sana. Tendo hilo hilo lilifanywa na YESU kwa kumwaga damu na kututahiri mioyo yetu(Tohara ilihusisha kuondoa magovi ya miili ya mwanaume(katika uume) kama ishara ya usafi,damu ilimwagika. Baada ya Kifo cha Msalama cha Yesu kila amwaminiye tayari anatahiriwa roho yake, govi la dhambi la roho linavuliwa na damu ile ile ya msalaba inakuwa imetumika kama utakaso.👇👇👇👇
*Wakolosai 2 : 11 - Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.*
✍ Sasa baada ya kuokoka, au kwa waliookoka *Tohara/Kutahiriwa* kimwili(govi la uume) halipo kiroho tema kimaagano, limebaki kiwa ni tendo la *Kiafya/ Sayansi* ila halina mahusiano tena ya kiroho.👇👇👇👇
*1 Wakorintho 7 : 19 - Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.*
_Kwa sababu hii niwashauri watu wote wamama kwa wababa, kutafuta kutahiriwa mioyo yao maana kuna magovi ya dhambi zao,na humo ndo kuna agano takatifu la damu ya YESU lililo imara na la milele. Kwa kuhitimisha, Tuulinde ubikira wetu ambao ni Uzaliwa wa kwanza(Malimbuko ya miili yetu na roho zetu) ili tuyapate yale mema yaliyowekwa katika ubikira(limbuko)_
*_Ulikuwa na Mchambuzi wa masuala ya Kimahusiano na Ndoa Kisaikolojia na Kiroho_*
EV ELISHA KAZIMOTO
WhatsApp 0755444078
No comments:
Post a Comment