Sunday, 25 December 2016

MATAPELI WA MAHUSIANO

💊💊 *MATAPELI WAEPUKE KATIKA MAHUSIANO*💊💊
   *_By Ev Elisha Kazimoto_*
   *0755444078*
_Shalom vijana wote mlio kwenye urafiki na mlio kwenye uchumba,dawa ya kuganga majeraha yasiyo na sababu hii hapa_
💉 Mara nyingi watu wakiingia katika mahusiano wanapenda mpaka wanakuwa vipofu,hawaoni hatari☠☠☠,wanajiachia kwa kila lugha,kila tendo,kila eneo,mwisho wa siku wanaishia kulia😭😭😭.
💉Unapaswa kujua mambo haya  katika unapoanza urafiki au uchumba,ndo utawakwepa *Matepeli na Wahuni wanao Jeruhi mioyo*
1⃣ *_Si kila mmoja anahitaji urafiki,au Uchumba ana Akili timamu_*  Nikama lugha ngumu ila ndo ukweli,kuna watu unaanza nao urafiki,uchumba akili zao siyo sawa,hawawezi kujua gharama ya moyo wako ikoje katika mahusiano hayo,hawajui umempa moyo kiasi gani,aulindeje asikujeruhi,ila wao wana *Maamuzi ya kukurupuka yasiyo jali Hisia zako* huyo hana akili timamu,usipo kuwa makini atakufanya maisha yako yote ya urafiki,uchumba au ndoa kujeruhika na kulia mara kwa mara.( *_Kumtambua, Angalia anavyo kuchukulia kila siku,maamuzi yake kwako,na ikitokea mkatofautiana maamuzi yake yakoje_*
Usijiue bure,epuka tapeli huyo.
2⃣ *_Si kila anaye anzisha mahusiano na wewe Amedhamilia kukuoa,kuolewa na wewe(kuingia katika ndoa)_*  Ndivyo ilivyo,watu wana sababu nyingi za kuja kwako kwa lugha ya kuchumbia au kuchumbiwa,  _wengine wameachwa wana majeraha yao,wanahitaji wakutumie upoze majeraha yao ili wale wawapendao wakute wana mioyo iliyo tulia,imekauka damu_ *kwa hiyo wewe unatumika kama Transformer Pozo🙄🙄🙄* wengine hawahitaji upweke,wanatafuta watu wakuwaondolea upweke ilavsi kuingia nao kwenye ndoa,...Ukijiachia kwa watu hawa utalizwa sana,utangoja sana. ( _Kumtambua mtu huyu, hana mtazamo wa future,hapendi kuzungumzia hatima ya mahusiano yenu,ni mdadisi sana juu ya habari zako,ila za kwake anaficha sana, ana maigizo mengi kuliko uhalisia katika mahusiano,hapendi kuingia gharama sana kwaajili yako(gharama ya muda,upendo,kujali,kutoa nk) yeye anahitaji atimiziwe mambo yake ila ya kwako anaya ruka)_* Ukizubaa unapigwa mimba,au unapiga mimba mtu halafu hakuna ndoa,au unavuliwa👉👙na kuachwa.
3⃣ *_Si kila anayeanzisha mahusiano na wewe,wewe ndo mtu wake wa kwanza,huwenda wewe wa 20_*
Kama hukujua kanuni hii,utaumia sana,unahitaji kuwa mtu wa kutafakari,kila anaye anzisha mahusiano na wewe ya uchumba au ya urafiki hajaanza na wewe, *_Kuna mwingine ametoka kuvua👉👙wadada kama 10 na wote alikuwa akiahidi kuwaoa lakini kwanza aonje tunda😋mwisho anawapiga chini, na kuna walio vuliwa👉👙karibu na watu 25 wee wa 26,ameisha ona na kuzoea utamaduni huu wa kuvuliwa na kila mchumba,rafiki,sasa ukikausha bila kumvua👙,moja utapigwa chini, mbili Utashawishiwa na kutegwa mpaka uingie mtegoni._ Kuwa tambua watu hawa,ni  *Wepesi kuomba ngono kabla ya ndoa,wanahimiza,na kusisitiza ngono ndo muoane,au ndo atafurahi au kukuamini,kukupenda*, Luga zao za mitego mitego, wanaomba sana picha za utupu zako,hawawezi kuthibiti hisia zao,waongo. Kuwa makini na hao ukimwamini atakuchezea na kukuacha.
4⃣ *_Si Kila anaye kuja kuanzisha mahusiano na wewe yupo peke yake,ameachana na mtu wake wa kwanza_*   Msaikolojia mtaalamu wa mahusiano na Ndoa  *Ev Elisha Kazimoto* Nakujuza haya uyajue Usiumizwe ovyo na Matapeli,.... _Kuna watu wanaanzisha mahusiano huku wakiwa na watu wao,yaani anatafuta *Spare Partner* wewe unayeingia naye katika mahusiano unakuwa *Stabilizer* ya mahusiano yake,ukibahatika unaweza chukuliwa wewe akaachwa kabisa wa kwanza,au mkaachwa wote_  (Kumtambua mtu huyu, mara nyingi wanakuwaga busy sana,kila ukimwambia mbona mawasiliano yetu yana dolola,utaambiwa niko busy sana,mambo mengi,mbona huniamini,kama vipi tafuta mtu mwingine asiye na ubize, wana majibu ya shortcut, hawana lugha za kubembeleza,ni wakali...wanapenda ngono,wasichana wanapenda kuchuma cash sana,ukiwa mbaili kwao wanaingia mitini🌴🌴🌴.) Kuwa makini nao ukimpa mwili wako anapotea.
💉 *Mchumba Makini,mwaminifu utamjua tu kwa haya hapa* Wala hakuna haja ya kutafuta tochi ni wazi wazi utamuona...
*_Kijana au binti kwanza,anaheshimu lile agano la neno lake la nakupenda uwe mke au mme wangu wa ndoa,anajali,anaheshimu mwili wake na wa kwako,anahofu ya Mungu hayuko tayari kumkosea Mungu, Pili hataki kuumiza wala kumuuzimizwa na mtu wake,anajitahidi kutatua changamoto za mahusiano kwa amani, anaimarisha mawasiliano hata kama yupo busy sana na shuguli na kazi,lakini muda wa mawasiliano na mwenzake lazima upatikane,Tatu anawaza na kupangilia harakati za ndoa na maisha na kumshirikisha mwenzake kila hatua,hataki kuchelewa sana kuingia katika ndoa, hutasikia kuomba ngono wala mambo yote machafu,lakini nimshirikishaji sana wa mambo ya Mungu na ratiba za Kimungu,kama ibada,kusoma neno,kumtumikia Mungu,maombi na kufunga na kuvumilia katika yote mpaka mfike ndoa._ Mtu huyu ukimpata umepata tunu,zawadi,na upendeleo kwa Bwana.
💉💉 *_Mpaka hapo binti/kijana umejua nani wa kuoana naye,nani wa kupiga chini haraka sana ili usiumie_*💉💉
      By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)
     0755444078
( _Mtaalamu wa Saikolojia ya Mahusiano na Ndoa_)

Tuesday, 20 December 2016

DIRA YA KUPATA MCHUMBA

🍇🍇 *NINI DIRA YANGU YAKUMPATA MWENZI WANGU*🍇🍇
  *_By Ev Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*
_Haleluya🙋🏻‍♂ vijana wote wa kike na kiume,karibu tuendelee kufunguana macho na masikio ili usifanye makosa yatakayo gharimu kupoteza furaha yako,vision yako,huduma yako na ufalme wa Mungu_
*_N̥ͦḁͦḁͦm̥ͦ k̥ͦu̥ͦn̥ͦḁͦ m̥ͦḁͦm̥ͦb̥ͦo̥ͦ y̥ͦḁͦn̥ͦḁͦs̥ͦu̥ͦm̥ͦb̥ͦu̥ͦḁͦ v̥ͦi̥ͦc̥ͦh̥ͦw̥ͦḁͦ v̥ͦy̥ͦḁͦ v̥ͦi̥ͦj̥ͦḁͦn̥ͦḁͦ,k̥ͦḁͦt̥ͦi̥ͦk̥ͦḁͦ h̥ͦḁͦr̥ͦḁͦk̥ͦḁͦt̥ͦi̥ͦ z̥ͦḁͦ k̥ͦu̥ͦi̥ͦn̥ͦg̥ͦi̥ͦḁͦ k̥ͦḁͦt̥ͦi̥ͦk̥ͦḁͦ n̥ͦd̥ͦo̥ͦḁͦ,n̥ͦḁͦo̥ͦ h̥ͦu̥ͦj̥ͦi̥ͦk̥ͦu̥ͦt̥ͦḁͦ w̥ͦḁͦk̥ͦo̥ͦ n̥ͦj̥ͦi̥ͦḁͦ p̥ͦḁͦn̥ͦd̥ͦḁͦ, l̥ͦe̥ͦo̥ͦ M̥ͦt̥ͦḁͦḁͦl̥ͦḁͦm̥ͦu̥ͦ w̥ͦḁͦ M̥ͦḁͦh̥ͦu̥ͦs̥ͦi̥ͦḁͦn̥ͦo̥ͦ n̥ͦḁͦ N̥ͦd̥ͦo̥ͦḁͦ m̥ͦw̥ͦḁͦn̥ͦḁͦs̥ͦḁͦi̥ͦk̥ͦo̥ͦl̥ͦo̥ͦj̥ͦi̥ͦḁͦ E̥ͦv̥ͦ E̥ͦl̥ͦi̥ͦs̥ͦh̥ͦḁͦ,n̥ͦḁͦk̥ͦu̥ͦm̥ͦe̥ͦg̥ͦe̥ͦḁͦ t̥ͦe̥ͦn̥ͦḁͦ f̥ͦu̥ͦn̥ͦg̥ͦu̥ͦ h̥ͦi̥ͦl̥ͦi̥ͦ l̥ͦḁͦ f̥ͦḁͦi̥ͦd̥ͦḁͦ k̥ͦw̥ͦḁͦk̥ͦo̥ͦ h̥ͦḁͦs̥ͦḁͦ w̥ͦe̥ͦw̥ͦe̥ͦ m̥ͦt̥ͦu̥ͦ w̥ͦḁͦ M̥ͦu̥ͦn̥ͦg̥ͦu̥ͦ u̥ͦl̥ͦi̥ͦy̥ͦe̥ͦ o̥ͦk̥ͦo̥ͦk̥ͦḁͦ._*
🍇 Kuna vitu kadhaa vinaangaliwa sana na vijana katika kumtafuta mtu wa kuishi naye, kama vile; *Elimu,Uchumi mzuri,Kabila,Umbo,rangi,Imani na Kazi uliyo nayo*  _Hivi vyote ni vitu muhimu sana kwa ndoa,ila ni vitu vinavyo weza kukutoa machozi baada ya kuingia katika ndoa pindi tu,kama ulivibeba vikuongoze kumpata mwenzi pasipo maarifa._( *Nitachambua kimoja,kimoja na faida yake au hasara katika ndoa*)
🍇Kwanza kabla ya kuoa au kuolewa,kabla ya kuweka vigezo vyovyote vikuongoze,jiulize maswali haya ndo utafanya the Best Selection:
1⃣ Kwa nini nataka kuoa au kuolewa?
2⃣ Nahitaji wa kuniongeza au kunipunguza?
3⃣ Nahitaji kwenda mbinguni baada ya kuoa/kuolewa au Jehanamu?
_Hayo ni maswali ya kijana yoyote aliye na akili timamu,aliyekomaa kiroho,anaye fanya mambo kwa faida_
*T̆ŭj̆ĭb̆ŭ m̆ăs̆w̆ăl̆ĭ h̆ăy̆ŏ 3,h̆ăl̆ăf̆ŭ t̆ŭv̆ĭăn̆ğăl̆ĭĕ v̆ĭl̆ĕ v̆ĭp̆ăŭm̆b̆ĕl̆ĕ.*
🍇1.Mara kadhaa kila mtu ana jibu swali la kwanza kwa namna yake kulingana na msukumo ulio nao ndani unao kupelelea kuoa/kuolewa, *_Hila jibu la msukumo huo laweza kuwa sumu kwa ndoa yako,maana msukumo huo ndo utakupa kupanga vipaumbele kadhaa vya mtu unaye mtaka_*
💈Kuna wanao taka kuingia kwenye ndoa, *Kwa sababu age mate/classmate  wake wote wameisha ingia Kwa ndoa* _Huyu ni rahisi kumkuta amechukua mtu kulingana na age mate/classmate wake walivyo chukua watu wa aina flani( Competition Marriage)_ hapa waweza pata au umia.
💈Wapo wanaoingia kwenye ndoa, *Kwa kutaka kuridhisha familia au Kampani yake*  _Hawa wanaingia kwenye ndoa kwa kusikiliza mawazo na mashauri ya familia au kampani yake,wanataka nini,wanamsemeaje mme/mke wa aina flani_ (Third Person Marriage) hapa napo kuumia kuko nje nje,uchaguzi wako ni mdogo sana kwa aina hii.
💈Wapo wanaoingia kwenye ndoa, *Kwa sababu wamezidiwa na hisia,kazi,au wahahitaji huduma flani,Kupata watoto*  _Hawa sababu hizo zikipatikana wanaifurahia ndoa ila ikikosekana au kuwa na mapungufu katika upatikanaji,hujutia maamuzi yao_( Conditional Expectation Marriage ), ndoa hii lile lililo tarajiwa likikwama ndoa inakuwa chungu,na huchagua watu kwa kukadiria.
💈Wapo wanaoingia katika ndoa, *Kwa lengo la kutimiza kusudi la Mungu,Kutaka kupata mtu wa kutimiza Maono yake,kumpa support ya kazi ya Mungu,Kutimiza furaha yake*  _Watu hawa,mara nyingi huyatafuta mapenzi ya Mungu,huchunguza sana nani anafaa,huogopa kukosea,hulinda mahusiano yao na Mungu_ (Positive Perception Marriage), Hawa kigezo chao cha kwanza kwa anaye mtaka awe mwenza wake,ni *Awe Mcha Mungu*
🍇2. *Kabla ya kufanya maamuzi ya kuoa au kuolewa,jiulize kama mtu unaye taka kuambatana naye maishani mwako,atakuongeza kiroho na kimwili au atakupunguza*, Kosa kubwa la vijana nikuangalia shape na sio Vision,kabila na siyo Unako kwenda,Elimu na siyo furaha ya ndoa nk,nk. Unaweza pata mtu kulingana na hisia zako za haraka,au mtazamo wa jamii lakini ukashuka kimaisha kila mwaka kiroho na kimwili.Hapa kunahitaji tafakari kubwa sana.
*_Faida kubwa ya kuoana na mtu sahihii ni kukusaidia kupiga hatua ya maendeleo ya kiroho na Kimwili_* Elimu,kabila,pesa au shape havikupi nguvu ya ku face future yako kwa ujasiri.
🍇3. *Suala la Kwenda mbinguni au Jehanamu linategemea mtu uliye fungamanishwa naye katika safari ya maisha yako. Mtu sahihii atakupa nguvu ya kupambana kiroho na kushinda,hatimaye kwenda mbinguni,na mtu mbovu,atakuwa kikwazo,changamoto ya jitihada zako za kuutafuta ukamilifu na utakatifu,na mwisho wa changamoto ni kushindwa na kuishia jehanamu.
*_Katika hili,ahiitajiki elimu,pesa,kabila wala shape,hapa inahitajika mtu mchaji wa Mungu_*
*M̠c̠h̠a̠n̠g̠o̠  w̠a̠ V̠i̠t̠u̠ v̠i̠n̠a̠v̠y̠o̠ v̠u̠t̠i̠a̠ v̠i̠j̠a̠n̠a̠ k̠a̠t̠i̠k̠a̠ n̠d̠o̠a̠,n̠a̠ h̠a̠s̠a̠r̠a̠ z̠a̠k̠e̠*
📱 *Elimu*, ni nzuri katika familia pale walioipata wakiitumia vizuri,na wakiitawala isiwatawale, kazi  ya Elimu katika familia itawasaidia kufanya mambo kiurahisi,kuwa na mtazamo wa mbali,na kuwasaidia kuandaa kizazi cha wapenda elimu.
_Elimu hiyo hiyo,ukimpata mtu mwenye ulimbukeni na elimu,atakuumiza katika maamuzi,katika life style ya kuishi,kiburi,jeuri,kurafuta usawa au kukandamiza,hali hii itafuta furaha ya ndoa_
📱 *Kabila* Unaye tafuta kuoa kabila flani au kabila lako,ni jambo jema maana unafaidika kuondoa utata na usumbufu wa kujifunza mila,desturi na lugha mpya za kabila lingine,lakini kuwa na uwezo wa kuthibiti mila usizo zitaka.
_Lakini kwa kabila hilo hilo,ujue Hakuna kabila kamilifu,mapungufu yale yale yakiinuka yanaweza chafua ndoa yako_
📱 *Uchumi* ni nguzo nzuri kwenye familia ila inahitaji imilikiwe na watu walokomaa kiroho,na kiichumi wanaoweza itiisha pesa na mali visiitawale ndoa na hisia,mbali na hapo mnaweza pata pesa,na mali zakutosha lakini mkaishi kwa mpasuko wa ndoa.
_Mke/mme wa kuoa soyo mwenye well off kiuchumi,ndo ndoa itakuwa nzuri,pesa haiendeshi ndoa pesa inanogesha ndoa ikitumiwa vizuri._
📱 *Umbo na Rangi* ni vivutio vya macho kwa vijana wengi,hila havina tafsiri ya Tabia ya mtu, ni vitu vya nje vinavyo badirika kulinfana na mazingira.
_Umbo na rangi,ukiviweka mbele siku mabadiriko yakitokea utaichukia ndoa_
📱 *Imani katika Bwana* Imani nikitu cha msingi kwa faida ya safari ya ndoa yenu ya kiroho na kimwili katika maisha.
_Ukichukuana na mtu dhaifu kiroho,au mpagani,mwana dini tu,utakuwa na wakati mgumu sana kuiwekea ndoa yako ulinzi,utashuhudia migogoro mingi sana ya ndoa isiyoisha na malezi mabaya ya watoto,lakini kushinda mapito na majaribu kwenye maisha yako itakuwa vigumu,lakini kuachana kupo nje nje_
*_U͓̽k͓̽i͓̽w͓̽a͓̽ K̈ïj̈än̈ä Üs̈ïf̈ür̈äḧïë M̈äz̈ïn̈g̈ïr̈ä ÿä n̈j̈ë ẗü ÿä ün̈äÿë m̈üön̈ä,ẅäz̈ä n̈d̈än̈ï äm̈ëb̈ëb̈ä n̈ïn̈ï k̈ïn̈äc̈ḧö ẅëz̈ä f̈än̈ïk̈ïs̈ḧä ḧäẗïm̈ä ÿä m̈äïs̈ḧä ÿäk̈ö,j̈äp̈ö n̈j̈ë n̈ï k̈üz̈ür̈ï k̈ẅä ḧïs̈ïä z̈äk̈ö üs̈ïp̈äd̈ḧär̈äü,ïl̈ä ẅäz̈ä s̈än̈ä k̈ẅän̈z̈ä M̈äḧüs̈ïän̈ö ÿäk̈ö n̈ä M̈ün̈g̈ü ÿän̈äïm̈är̈ïs̈ḧẅäj̈ë?_*
       *N̈d̈öä s̈äf̈ï Ïn̈äf̈ür̈äḧä k̈üü,n̈d̈öä ÿä k̈ük̈ür̈üp̈ük̈ïä ïn̈ä m̈äüm̈ïv̈ü m̈äk̈äl̈ï ÿäs̈ïÿö ël̈ëz̈ëk̈ä*
(  _C̈ḧäg̈üä n̈ï v̈ïp̈ï ün̈äẗäk̈ä üïs̈ḧï_)
     *B̈ÿ Ëv̈ Ël̈ïs̈ḧä K̈äz̈ïm̈öẗö*
       *0755444078*

Sunday, 4 December 2016

KUOA BINTI MSOMI/MWENYE ELIMU NI MWIBA?

🏆🏆 *HOFU YA VIJANA KUOA MKE ALO NA ELIMU KUBWA AU KIPATO KUKUZIDI*🏆🏆
   *_By Ev Elisha Kazimoto_*
      *0755444078*
_Shalom,vijana,mabinti na wale ambao mmeisha ingia ndoa,nitegee sikio la ufahamu na uelewa,mwana saikolojia na mchambuzi wa masuala ya Ndoa *Ev Elisha(Baba Eve)* nikupe Maarifa ya Changamoto hii ilo na shida kweli hata katika ndoa_
✍Kumekuwa na kigugumizi kwa baadhi ya vijana cha *_Hivi nioe kweli huyu dada msomi,mwenye mshahara kunizidi,mwenye uchumi,anayetoka familia Matawi ya juu,si ntapoteza heshima ya uanaume?Ataniheshimu kweli?_* Lakini imeenda mpaka kwenye ndoa wapo wanao juta kwa mke kuwa na uwezo wa kifedha au Elimu,vimegeuka fimbo kwa mwanaume ndani.
✍Hapa kuna shida pande zote mbili,kijana huu ni mtazamo potofu,usitumie makosa ya wengine kujipa jibu kwa maisha yako,unapaswa kujua kila mtu ana Neema yake na mfumo wake wa ndoa,inategemea umejipangaje kuingia kimaarifa na kiroho na kisaikolojia.
✍Kwa wamama na mabinti hii nichangamoto kwenu,ambayo inaweza kukufanya,uchelewe kuolewa,au uchezewe tu na wajanja,na mama katika ndoa,uishi maisha yote ya ndoa bila kuifurahia.
_Sasa ambatana nami katika uchambuzi huu katika point 9_
1.Tunapo oa au kuolewa,hatuoi au kuolewa na Elimu,Cheo,Pesa wala Utajiri wala Kabila, tunaoa au kuolewa na mtu ambaye anaweza kutufanya tufikie vision zetu,anaye toka kwa Bwana,wakunisaidia,kufika mbinguni na duniani kutimiza ndoto zangu.
_Haijalishi ni mtoto wa waziri,wanapesa chafu,ana masters mimi ni form 6 au 4 au STD 7,kinacho matter tumependana kwa dhati ili tuwe pamoja_au tumependana kwa sababu flani
2.Vijana mnahitaji kufahamu jambo moja,msiwe na fikra potofu,hatutengenezi unyenyekevu/utii wa mke,au hatupati heshima kutoka kwa wake zetu kwa kuwanyima fursa,au akiwa hana elimu,au hana pesa,kila kitu ananitegemea basi hapo atanitii,atakuwa mnyenyekevu na heshima kwangu, huo ni ufinyu wa akili ya mwanaume,hofu,kutojiamini na hufai kuwa kwenye orodha ya wanaume wa ukweli.
Ukitengeneza ndoa ya namna hiyo,huo ni utii feki,heshima feki,na akija kuzipata pesa,au maarifa utaumia.
3.Ni uzembe wa akili na wakimaisha kutaka kuoa mwanamke asiye kupa changamoto,ambaye kila kitu ni ndiyo,ndiyo....hana mawazo ya challenge,hamuwezi fika mbali hata kiroho,kimaendeleo,lakini mwanaume utakuwa na mzigo mkubwa wa kubeba familia....Nini maana ya msaidizi?mtu wa kuishughulisha akili yako,ikilala anaiamsha,usije kujisahau kama kichwa cha familia.
4.Unapooa oa mtu wa kukufaa,awe na pesa,elimu maadamu umempenda,anauwezo wa ku make future na wewe, Elimu,au Pesa siyo maisha ya ndoa,maisha ya ndoa nizaidi ya pesa,inahitajika akili na upendo wa dhati,japo Elimu na pesa vina mchango flani katika maisha ila siyo kigezo cha ndoa ya furaha.Wapo maprofesa,masters,degree, pesa chafu na utajiri lakini ndoa ni moto. Ndoa ni zaidi ya vitu hivi vionekanavyo
5.Kati ya Mwenye Elimu au Maarifa nioe yupi,lazima tujue Terms hizi mbili.. *Elimu* _Ni nyenzo inayo fungua ufahamu wa mtu na kumpa mwanga(maarifa)namna ya kuendesha maisha, ipo Elimu rasmi ya darasani na isiyo rasmi itokanayo na jamii na maisha ya kila siku._
*Maarifa*  _Ni ujuzi unao msaidia mtu kufanya jambo sahii,muda sahii,Eneo sahii kwa Lengo sahii_  Kwa tafsiri hizo mpaka hapo unaweza kujua uoe yupi.
*My comments, Kuishi na mtu asiye na maarifa hamtaenda mbali wala ndoa haiwezi kuwa ya furaha*
6.Wadada,na Wanawake mloolewa ndo mmewajengea vijana na wanaume wenu mtazamo wa *Kiubabe,na Kujiami na Hofu*  _binti kwa kadri unavyoongeza madarasa unaongeza Jeuri,Kujiona,Dharau kwa namna hiyo hujitengenezei mazingira ya kuheshimiwa,kupendwa,ila unatengeneza mazingira ya *Kusugua benchi la Ushangazi(Ubachela) miaka 28,30,34,37*  hata 40_ wakati walo maliza la 7, form 4, form 6 wakafeli wanaolewa na wanaenjoy maisha ya ndoa kwa furaha, sare utawashonea,michango utatoa na harusi utaudhuria nyingi na *Kwaito utacheza sana* utarudi nyumbani wavulana wanakuogopa kama Ukoma.(Vidato vyako ulivyo vitukuza havita kuvika pete 💍ya uchumba,wala kukufanya uitwe Mrs.
_Pata saikolojia hii wewe dada kwa mwana Saikolijia (Ev Elisha Kazimoto) kwakadri Unavyoongeza vidato au uchumi,jishushe,thamini watu wote,aliye soma,asiye soma,aliye na pesa na asiye na pesa, *Ongea na Watu wa Rika zote,fani zote za kazi* dharau fani flani ya kazi,ujipachike kwa mtu wa fani maarufu,usipo mpata huko wa kukuoa,utatamani hata Kondakta awe mme wako wewe mwenye Masters_
7.Mama uliyeolewa,Elimu yako,miradi,pesa,biashara yako pesa za familia uliko toka na kuwa na ndugu wakubwa serikalini,haviwezi jenga ndoa yako,wala havina mchango wowote,unamdharau mmeo au ndugu,wazazi wa mmeo,hujielewi wewe,ungekuwa wee wathamani ungekaa kwenu,ukaolewa na Elimu au pesa yako,au kwenye ukoo wenu ungeolewa huko ili ukae na kiburi cha pesa na elimu yako na umaarufu wa familia yenu, *_Ila kwakuwa ulikubali kutoka kwenu,na pesa zako na elimu yako, mimi mwalimu wa Mahusiano na ndoa nataka ni kwambie, Wewe na Familia yako Ni Maskini wa Hali ya Juu_*  Eeh....naona unaishangaa lugha hiyo, narudia kwa mkazo,  *Wewe na Familia yako Nimaskini wa Hali ya juu* maana yake ni nini?👇👇
_Kama kwenye familia nzima,na pesa zenu,umaarufu wenu,vyeo vyenu,na elimu yako na mshahara mkubwa, *Amekosekana wa Kukuoa* Mpaka ukaolewa na mtu mwingine,tena wa maisha ya kawaida, basi *Kuwa Mpole* huyo ndo BOSS wako na familia yako._
Weka vitu vyote chini,nyenyekea,tii mmeo linda ndoa yako acha ukorofi na dharau,penda familia ya mmeo na wathamini, *Zaidi ya yote Mweshimu mmeo kuliko mtu yeyote*
8.Lakini wanaume niwa taadharishe,mmesababisha shida ya ndoa zenu,mmeolea familia?yaani mmekuwa dhaifu kuzisimamia ndoa zenu,ndo maana vita ,ugomvi wa mkeo na mawifi,mashemeji,mama yako hauishi,shida ni nini,mke wako ume waachia wengine,kila mtu ana uhuru wa kuzungumza,kuonya,kulaumu,kusuta,upo kimya tu!Weka mipaka mkeo ni wako siyo wafamilia kurusha rusha,yaani kila mtu anaweza kuamua mkeo aweje,huu ni ufinyu wa maarifa,hujui yeye ni mgeni,na yuko mmoja kwenye familia ninyi mpo 12,kila mmoja akimshambulia afanyeje lazima Ajihami...ndo maana watakuja wa nyumbani kwenu anaenda kutembea,au analala na yeye anatafuta usalama,ninyi mpo 12 yeye 1,sasa Jeuri ndo mtu wake wa 2.
_Mwanaume muwekee mkeo mazingira ya usalama na kuheshimiwa na ndugu na wazazi na watu wote wanao kuhusu_
9.Wana ndoa,kuweni na muda wa kuzungumza,kuangalia kero,shida na madhaifu yenu na mwambizane ukweli kwa upendo na amani,mjenge ndoa yenu, *_Kuzira,kununa,kiburi,ukalip havijengi,na havita wasaidia,baladala yake inaingizwa kwa rekodi ya ndoa za migogoro na kipumbavu_* Rekebisheni mapungufu yenu ninyi ni wanadamu mpo duniani siyo mbinguni. Jenga heshima ya ndoa mlee watoto wenu kwenye maadili mema hawa watoto wasio na hatia.
*_Mwisho ndoa inahitaji akili na uvumilivu kwa mwenzako,mtaishi miaka yote mpaka uzee kwa furaha na upendo_*
     _@By Ev Elisha Kazimoto_
        *0755444078*

Friday, 2 December 2016

LAZIMA ADUI YANGU AFUTILIWE MBALI

🚧🚧 *LAZIMA ADUI ZANGU NIWAFUTILIE MBALI*🚧🚧
     *_By Ev Elisha Kazimoto_*
        *0755444078*
_Shalom makamanda wa Bwana,watu wa vita,nakuletea ujumbe huu ili uwe hodari na moyo wa ushujaa Adui zako zamu yao imefika ya Kufutiliwa Mbali kwa mkono wa Mungu wenye nguvu_
🚧 Ujumbe wetu leo, *_Nikuwafutilia mbali na Kuwakatilia mbali maadui zetu_*  Kwa nini kufutilia mbali adui zako,ni kwasababu uovu wao wanao utenda katika maisha yetu ni mwingi mno,hauvumiliki,Lazima wafutiliwe mbali.👇👇👇👇
*_Mwanzo 6 : 7 - Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya._*
🚧👆🏻Mpaka Mungu anatoa maamuzi ya kumfutilia mbali mwanadamu na kila kiumbe,ni uovu,matendo mabaya yalikuwa yameuchukiza moyo wa Mungu.
🚧Kazi wanayo ifanya maadui katika maisha ya watu ni *Uovu mkubwa usiovumikika*,hebu tafakari mfumo wa maisha yako ulivyo vurugwa na wachawi,haki yako ilivyo porwa na maadui zako,ndoa yako ilivyo vurugwa,Elimu yako ilivyo shambuliwa,uchumi wako ulivyo tawanywa na Maadui, uovu huu ni mbaya sana hauvumiliki, *_Lazima Adui Akatiliwe mbali_*👇👇👇👇
*_Zaburi 118 : 12 - Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali._*
🚧Kukatilia mbali,kufutilia mbali ni kuondoa,kupoteza alama,sura za Adui katika mazingira yako tunapoelekea mwisho wa Mwaka,yako matatizo mengi ulokutana nayo maishani,ukiwa ni mpango na mchezo wa maadui zako,sasa zamu yao kufutiliwa mbali. _Mungu alitumia  Gharika kufutilia mbali mwanadamu mwovu na viumbe vyote, Gharika hiyo hiyo,ipo ya ulimwengu wa roho kuwafutilia mbali watesi wetu_👇👇👇👇
*_Mwanzo 7 : 4 - Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali._*
Siku hizi zilizobaki 29 kuhitimisha mwaka, *Ni siku za kushusha Gharika ya Moto kwa Wachawi,waganga wa kienyeji,Viongozi wanao pora haki za wanyonge* mpaka watakapo kuwa Wamekatiliwa mbali,tuingie mwaka  2017 kwa Ushindi na uzina wetu.
🚧Katika mwisho wa Mwaka,miezi kama hizo,wapo maadui na wana wa giza *_Wanazitumia Safari za watu kupata Damu ya Kafara kwa kusababisha Ajali,Pokea Neno la Kinabii leo katika mkesha huu wa OPERATION futilia mbali maadui, Hakuna Damu yako,wala ya jamaa yako itakayo kwenda na Kafara za Wana wa Giza katika jina la Yesu_* Bwana atatuma malaika katija safari zako zote,za mwendo wa miguu,kwa vyombo vya moto utakuwa salama, *Na kila adui atakaye jisogeza kupora Uhai wako,Atakatiliwa mbali,yeye ndo Atakuwa kafara ya Wenzake kwa jina la Yesu* Yesu tulie naye ni moto ulao👇👇👇
*_2 Samweli 7 : 9 - nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani._*
🚧Inuka kwa uhodari na ushujaa,tuombe Maombi ya vita,ya kiwakatilia mbali adui zetu,piga wachawi,piga waganga wa kienyeji,piga maadui wanao otea uhai wako,ndoa yako,elimu yako,kazi yako,upo uweza wa Mungu wa kuwakatilia mbali, *_Lazima adui zetu watupe visogo na si vifua,watakimbia huku tukiwakatilia mbali kwa jina la Yesu,mahali ulipo Sema Nitavuka Mwaka kwa Ushindi,Adui zangu Mmekatiliwa Mbali_*
_Ujumbe huu ni Mahususi kwa wana wa Mungu,watu wa vita,watu walio na uchungu na kazi ya Mungu watu wanaotamani kuishi ili wamtumikie Mungu_
*Mungu Akuhifadhi Umalize mwezi huu wa December salama uingie 2017 kwa Ushindi, Ameni*
    _BY EV ELISHA KAZIMOTO_
     *0755444078*

Thursday, 1 December 2016

JIPENDE NDO UPENDWE

🚧🚧 *HUWEZI KUPATA MCHUMBA KAMA HUJIPENDI*🚧🚧
    *_By Ev Elisha Kazimoto_*
         *0755444078*
_Hello πŸ™‹πŸ»‍♂πŸ™‹πŸ»‍♂ vijana na mabinti,hii zamu yenu kumeza dawa ya kuzuia ubachela na shangazi usio na sababu kwako_ vijana wa kike na wakiume wamefikia hatua ya kutafuta dawa za kuleta mvuto wa kimapenzi,wengine kusaka maombezi kila kona ili wapate wachumba,lakini bado hali ni tete,no mchumba ila kuharibiwa maisha na kuishia zinaa tu,hakuna anayekubali kuishi na mtu ndani.  *_Sasa unajua sababu yake? Mtaalamu wa saikolojia ya mahusiano na ndoa, Ev Elisha Kazimoto nakuletea uchambuzi huo_* Fuata nami:
_Ukiwa kijana,ishi maisha ya kujipenda,kujikubali,yanayo vutia,yanayo kuvitia wewe hata watu wengine,kuwa na maisha ya kujiamini,yenye mpangilio,yenye ushawishi,mwanamke/mwanaume ahiitaji sana sura anahitaji umakini wako wa maisha_
🚧Lazima kwanza kijana ujue, Mahusiano ni ushawishi wa Hisia za mtu ziambatane nawe,kumiliki na kuteka Hisia za mtu mwingine,kumfanya ahisi uwepo wako maishani mwake ni ukamilifu wa mapungufu yake lakini ni faida kwake.
🚧 Sasa kwa lugha hiyo ya kisaikolojia,nimuhimu tuanze kujiuliza hivi ninapo taka kuanzisha mahusiano ya uchumba ili niishi na mtu huyu,KWELI nina uwezo na nguvu ya Kumiliki Hisia zake,na yeye akajiona yuko salama na amefika? *_Hapa ndipo watu hupoteza wachumba au kukataliwa_*
🚧Hisia hubatana na mtazamo wa Physical Appearance ya mtu,personality ya mtu na Prsentation ya mtu kwa watu ndivyo huvuta au hufunga hisia za mtu juu ya mtu.
🚧 *Kuna vitu unahitaji kuwa Makini Kama hujapata Mchumba,na wakati ukiwa na mchumba*🚧
⚓ Kuwa makini kauli zako, _Unapo kuwa kijana upo katika nyakati za kuoa au kuolewa bado unatafuta,chunga kauri zako,_ Kuna vijana kwa mabinti kabla ya uhitaji mkubwa wanakuwa na kauli za kibabe,za kujiona,za dharau,za kuonyesha hana uhitaji mkubwa na mambo ya mahusiano, *_Unacho paswa kujua kisaikolojia Kauli zako zinaishi,zinatangaza akili yako na maisha yako,kauli hujenga ngome inayo yeyusha hisia za mtu_*  Kuna watu hupenda kusema,mimi _siwezi oa/olewa na kabila flani,kimo flani,rangi flani, kada ya kazi flani,hizo kauli zina nguvu ya kufuta hisia za mtu ambaye ange vutiwa na wewe_  Lakini pia kauli zina sifa ya kusbaa haraka kwa watu,zikisambaa wakati huna uhitaji wa kuoa/kuolewa huwezi kuona shida,ila ukifika wakati wa uhitaji utatamani upite kila kona kwa kila mtu unatengua kauli but it is too late.
🚧Kuwa makini na Uvaaji wako, hiki ni kitu kinacho wakilisha Personality yako,mpangilio wa maisha yako,kwa hiyo kama hujali namna ya uvaaji wako inawakilisha namna usivyo makini katika kupangilia maisha au mambo katika maisha yako( *Unaishi Rough*),unahitaji kujua kwamba hisia zinaenda na mvuto wa mwonekano wa mtu(Hapa si zungumzii kumiliki nguo nyingi),uwezo wa kujiweka vizuri kwa nguo hizo ulizo nazo, kumechisha. Kila mtu anapenda mtu *Presentable* kwa watu,ndoa haiishii chumbani,ni pamoja na mwingiliano na watu,sasa kila mtu hapendi *Kumili Kituko* mtu asiye jijali. Je,umepoteza wachumba?jiulize uvaaji wako ukoje.
🚧Kuwa makini na kampani ya Marafiki zako; Marafiki ni watu wanao share(milikishana tabia),kama marafiki zako tabia zao ni mbaya,una hati hati ya kutopata mme/mke, ukishaambatana na mtu flani watu wanajua na wewe niwa hivyo, *_Usije jifariji kwamba mimi huyo ni rafiki yangu tu,ila mambo yake simo_* hiyo unaamini wewe,walio nje wanajua na wewe niwa hivyo. Sasa hiyo inaweza kukugharimu kupata mtu wa kuoa/kuolewa naye.
*_Leo nimesema na wewe vitu hivyo vichache, kwa Masomo   mengi ya mahusiano,ndoa na Saikolojia katiks maisha ya mahusiano kutana na Mchambuzi Mtaalamu wa Saikolojia ya mahusiano na ndoa Ev Elisha Kazimoto, Katika Blog ya Material Adimu, na Group la WhatsApp (Material Adimu University)kujiunga ni kwa Interview, lakini pia muda si mrefu madara maalumu ya Uponyaji wa Kisaikolojia katika  Mahusiano na Ndoa yataanza,Mawasiliano ni 0755444078*
           _By Ev Elisha Kazimoto_

MWANAMKE NA UCHUMI(PART I)

🍇🍇 *MWANAMKE NA UCHUMI*🍇🍇
  *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*
_Haleluyaa wanawake jeshi la Bwana, nakusalimia kwa jina la Bwana, leo nakuja kwako tena, na somo la uponyaji wa ndoa na familia yako kama Mwanamke mlinzi na mjenzi wa familia. Somo hili lina lenga kukufungua ufahamu wako, uweze kuiletea furaha familia yako, lakini pia kukupa nguvu ya kuwa mshauri mwenye nguvu_  *Sisemi kukupa nguvu ya kumtawala mume wako, au kukupunguzia unyenyekevu na wajibu kwa mmeo kwa sababu ya kuwa na kipato flani cha kuwezesha kuratibu masuala yalo binafsi na ya familia*
🍇 Hapa nazungumza nguvu ya kuleta radha ya ndoa tulivu na yenye dira ya kimaendeleo.
_Sasa tuongozwe na maandiko makuu mawili katika somo hili la Mwanamke na Uchumi, *Mhubiri 10:19, 9:16*,hivyo fuatana nami mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa Ev Elisha (Baba Eve)_
*_Mhubiri 10 : 19 - Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote._*
🍇 Kuna vitu hatupaswi kujifanya hatuvioni, hau havipo, wala tusizame kiroho sana tukasahau tupo duniani mwilini, panapo hitaji jitihada tuweke, panapo hitaji maombi tuombe, panapo hitaji akili tutumie ili tuziridhishe nafsi zetu na tumwabudu Mungu kwa uhuru.
🍇 Pesa ni muhimili wa mambo mengi katika ndoa, Pesa ina chochea upendo, furaha, amani, utulivu, na maendeleo. Pesa ikiwepo migogoro midogo midogo inapungua, kero ndogo ndogo za kimaisha zina pungua, mawazo yanatulia na mpaka hisia za tendo la ndoa zina jaa, maana akili imetulia.
🍇   *_Uchumi ukiyumba kwenye familia, muhanga wa kwanza ni mama, ndiye anaumia zaidi, wanafuata watoto, mume ni muhanga wa mwisho_*
🍇 Kwani, watoto wakishikwa na njaa wana mlilia baba? Kwani hali ikiwa ngumu anaye ikimbia familia ni mama,? Mwanaume anaweza kwenda kutafuta pesa miaka 3 hajarudi, mama huwa anaacha familia? Baba anaweza tembea huko na kule, akala libandani, lakini mama hawezi kula nje ya nyumba mpaka aletee watoto kwanza wale.  *_Sasa ndo unaweza kujua mama ulivyo na mzigo wa kuhakikisha familia yako ina tengamaa kiuchumi_*
🍇 Lakini wanawake wengine wamejisahau baada ya kuona mme ana kipato flani, ameridhika, hajishughilishi na chochote, *_Na hali hii imemfanya kupoteza nafasi yake ya ushauri kwa baba, na kumfanya kuziba kinywa muda wote😷😷😷, kwa sababu hana mchango wowote katika uendeshaji wa familia👇�👇�👇�👇�👇�
*_Mhubiri 9 : 16 - Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi._*
👉�👆�Wanawake wengi, wamekosa uhuru wamepoteza uwezo wa kusikilizwa kwa kutokuwa ma kipato hata kidogo.
🍇Kumbuka sizungumzii kutumia pesa kama fimbo kwa mwanaume, hapo utabomoa ndoa, na huwenda hata usifanikiwe kuwa na kipato,  *_Nafundisha Mwanamke na Uchumi Kwa maendeleo na ustawi wa Ndoa yako_*

  *UFANYE NINI KUWEKA MSINGI WA KIPATO?*
🍇 Jitambue wewe ni Mwanamke wa Aina Ipi? ( Wakuajiliwa, Kujiajili, Msomi au Hukusoma, Mlemavu au Nina viungo vyote?)
🍇 Heshimu mme wako, na Mthamini kwanza,  kumbuka hakuna mume anaye weza ruhusu ufanye mchakato wa kuimarisha uchumi wako na familia kama ndani tu, huna pesa we ni *Jeuri* ukiwa na pesa itakuwaje?
🍇Jenga mahusiano mazuri na watu,  huwezi kuwa huingjliani na watu, huelewani na watu ukajipanga kufanya biashara, utamuuzia nani? (  *Katika Uchumi watu ni mtaji wako)*
🍇Angalia mahitani ya mazingira uliyomo, yanahitaji nini, ujipange kuyapa mahitaji hayo.
🍇Jifunze, mambo kwa wengine upate ujuzi wa mambo mbali mbali huwezi jua la kukuokoa ni lipi?
🍇 Jiamini na jikubali kuwa unaweza kufanikiwa malengo yako.
🍇Usiogope Hasara, hasara ni sehemu ya faida

KIJANA NA MCHUNGAJI WAKE KATIKA KUPATA MWENZI

🏁🏁  *KIJANA NA MCHUNGAJI WAKATI WA KUOA/KUOLEWA*🏁🏁
   *_By Ev Elisha Kazimoto_*
      *0755444078*
_Shalom, shalom vijana mlio na safari ya kuelekea kwenye ndoa takatifu, ndoa ya baraka ndoa ya kukusaidia ufike mbinguni, leo nakutana na wewe katika uchambuzi huu muhimu, wa Nafasi ya mchungaji wako katika kuindea ndoa yako_
🏁 Kuna vijana ambao maisha yao kanisani huwa hayaeleweki, na wala hawana muda na mpango na mchungaji, miaka yao yote awapo kanisani, *_Ila ukifika muda wa kuoa au kuolewa ndipo wanaanza kujisogeza kwa mchungaji_*  ndo ruti za kufanya kazi kwa mchungaji zinaanza, kushugulika kanisani kunaanza, ni muda tu uhitaji wa kuoa/kuolewa unapo fika sasa hapa upo jatika hatari kubwa na uhuni.
🏁 Vijana wengi hawajui umuhimu wa mchungaji wake mpaka muda wa kuoa,/kuolewa maana utafanya yooote, ila lazima upite kwa mchungaji wako kwaajili ya kuiandaa ndoa yako, sasa hapa huwa ndo vijana wanachemka. *Angalia umuhimu wa mchungaji wako*👇�👇
� *_Malaki 2 : 7 - Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana wa majeshi._*
✍� Kijana unaenda kuoa, kuolewa, mnakubaliana kuoana, unaenda kwa mchungaji *_Anakwambia Huyu kijana/binti hakufai, maisha yake siyo mazuri, mchawi huyu, ametoa mimba huyu 3, kijana huyu atakuwa mzigo kwako mvivu kweli_* mnafanya maamuzi gani baada ya maneno hayo ya mchungaji?
✍� Vijana, wengine huamua kuto washirikisha wachungaji mambo yao ili wasije wakawaharibia dili lao, _Hivi kweli ungekuwa kijana unaye mpenda Mungu, unajituma kanisani na upo karibu na mchungaji wako, kweli unaweza kunuwazia mchungaji wako kwamba ukimuhusisha mahusiano yako atakiharibia dili?!_  *Hapo wewe ni muhuni ndo maana una wasiwasi wa kuto mwambia mambo yako mchungaji wako*
✍�Hivi, unaamini mchungaji wako anamfahamu sana huyo mchumba unaye taka kuoana naye kuliko wewe? Je, madhaifu ya kiroho na kimwili ya huyo unaye taka kuchumbia unayajua, unahisi nani wa kukusaidia kama si mchungaji wa huyo mtu wako?
✍�Lakini vijana wamewatupilia mbali wachungaji, wanaanza mahusiano, Uchumba mpaka ndoa, bila kumuhusisha mchungaji kwa kika hatua, baada ya kuoana ndoa inaanza kuyumba ndo umuhimu wa mchungaji unaanza kuonekana, mnampa ratiba za maombi ya kufunga sikuu 7.awaombee huu ni upuuzi.
✍�Kuna vijana muda wa kuoa /kuolewa, _wanawaona wachungaji hawapo kiroho, wanaweza kutumiwa na shetani kuharibu uchumba wao, hivyo hawawahusishi,_  hata wakiwahusisha kidogo, mchungaji akishauri, wanagoma hii imepelekea ndoa nyingi kuwa na majanga, kuvunjika, kukosa amani.
✍� Kijana pamoja na kuwa upo kiroho zaidi au umepoa, mchungaji ana nafasi ya pekee kukushauri katika safari ya ndoa unayo iendea,  *_Si semi mchungaji kukuchagulia mke/mme wa kuoana naye japo anaweza kukushauri_* 👇�👇�
*1-Samweli 3:1-9*
1   *_Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri._* 

2 Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), 

3  _na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;_

4 basi, wakati huo Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa. 

5 Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena. 

6 Bwana akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena. 

7  *_Basi Samweli alikuwa hamjui Bwana bado, na neno la Bwana lilikuwa bado halijafunuliwa kwake_*.

8 Bwana akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa Bwana ndiye aliyemwita yule mtoto. 

9  *_Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake._*
✍�👆�Kuna vitu wewe huvijui, lakini mchungaji anaweza kukutatulia mambo hayo, na ukapata mtu sahihi.
✍�Wapo wachungaji feki, lakini wapo wachungaji original, lakini kama kijana utakuwa uko vizuri na Mungu utamjua mchungaji feki na original mapemaa wala si muda wa kuchumbia au kuchumbiwa, na kama unajua mchungaji wako ni feki kwa nini kuendelea kukaa chini yake? Lakini vijana muda wa kuoa na kuolewa ndo huwa wanawaona wachungaji wao kuwa ni feki, hapo utazoa bomu.
✍� Kijana anaye weza fanikiwa katika hatua ya ndoa yake, mi yule ambaye yupo karibu na mchungaji wake hata kabla ya kuanza harakati za kuchumbia/kuchumbiwa, huyu kijana atafaulu saba.
✍� wachungaji wengi, kijana ukisha zama kwenye mahusiano ndo unaenda kumshirikisha mchungaji, huwa wana nyamaza kimya ili kuepusha shari, _Ushauri wangu kwako kijana, jenga mahusiano mazuri na mchungaji wako, mchungaji awe kama mzazi wako, ili kwa hatua hii muhimu akusaidie usije oana na mtu ambaye ni Bomu kwenye ndoa_
✍�  *_Mfanye mchungaji rafiki yako, ili Upate kumfahamu vizuri kama ni feki au original, na ndipo katika hatua za uchumba akikushauri hutakuwa na wasiwasi naye_*
_Kwa leo niishie hapa, ila jifunze kws Samweli na Eli, usijiaminishe sana, mchungaji ana nafasi yake muhimu kwako_
  *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*

KUPATA MKE/MME SIYO BAHATI NI KANUNI

*USITEGEMEE MME/MKE SAHIHI KAMA WEWE SI MTU SAHIHI.*
   *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
💖Kumekuwa na maswali mengi ktk maisha ya vijana ya ntampataje mke au mme sahihii
💖Ukweli ni kwamba mtoa mme /mke ni Mungu mwenyewe tu  na ndo mwasisi wa ndoa
💖Kwa hiyo kama wewe si mtu uliye na mahusiano mazuri na Mungu usitegemee Mungu kukupa mtu wa watofauti, mzuri, mkamilifu, au utaomba omba Mungu akujibu kwa kukufunulia mtu wako
💖Mungu hafanyagi makosa, Wewe ni tapeli wa kiroho, utakutanishwa na tapeli mwenzio wa kiroho (biblia inasema, nitakufanyia msaidizi wa kufanana na wewe)
💖Tangu uokoke hajawahi kuombea mambo ya Kimungu, kazi ya Mungu na Mungu akakujibu aidha kwa Neno lake, maono, njonzi, ndoto, kwa manabii nk, Leo hii unataka kuolewa/kuoa ndo unasema Mungu amenifunulia 😜, Mungu kasema nami 😝, aliwahi kusema na wewe nini mbali na mke /mme?
💖Unaishi maisha ya kutoaminiwa na Mungu wala wanadamu, halafu unahitaji ukiomba siku mbili Mungu aachilie mtu makini 🙅🏻
💖Unajua kabisa mimi nimeokoka ila dhambi mbele kwa mbele, unahisi ukiomba Mungu mke/mme utapewa wa aina gani
💖Umeharibu wadada wa watu kwa kufunua uchi wao, Umeharibu vijana wa watu kwa kuwazanisha ktk mapenzi kwa mwili wako, halafu unaomba Mungu akupe mke Bikra 😜😜🙅🏻au mme pure😜😜🙅🏻🙅🏻, unahisi hayo maombi yatajibiwa ❗❓
😡🙅🏻USITEGEMEE MAKUBWA USIPO JITUMA 😡🙅🏻
👥 *MUDA GANI UNAMUOMBA MUNGU NAYE AKAKUPA MWENZI*👥
❤Miongoni mwa makosa makubwa yanayo fanywa na vijana ni kujiachia ktk wokovu na kutulia bila kumuhusisha Mungu ktk maisha na mipango yao mpaka polee wanapo hisi kubanwa na uhitaji
❤Vijana wengi wanahisi kumpata mke au mme ni suala la kwenda na kuchagua au kuchaguliwa, kwa hiyo wanaanza kuomba kwa kasi pale wanapo hisi Umri umeenda huku hawapati mtu, ndo maombi makali yanaanza huku akijalibu kwa kila mmoja kuvizia
❤Mke/mme anaandaliwa katika maombi kwa muda mrefu, hata hujawa na presha, ukifika wakati akija tayari umeisha mhakikisha ktk ulimwengu wa roho hakuna utata
❤Lakini Mungu hatoi waume au wake wa kufua nguo na sex tu, Mungu anatoa msaidizi wa kukusaidia katika kazi zote za Kimungu na kibinadamu alokupa Mungu, baada ya wewe kuonyesha Uaminifu wa kuzifanya kwa bidii,.
❤Kwa hiyo kwa mtu alookoka muda wake wa kupata mwenzi ni ule muda ambao Mungu akimtazama anaona kazi yake, kazi zako vimekulemea /unavinya kwa Uaminifu ndo muda huo Mungu anamleta msaidizi wa kukusaidia
❤Kama uko vzr na Mungu, Usiumize kichwa cha mbona hawaji, simpati, wee piga kazi ieleweke ya Mungu na ya kwako, atavutwa hata kama yupo wapi hujawahi muona
(maneno haya ni roho tena uzima) nina ushuhuda mrefu sana kuhusu mahusiano, Nimefunguliwa ufahamu wangu kuomba kuhusu mke nikiwa darasa la(V), nimepata mke sahihii wangu wa kuoa 2014 kwa mkono wa Mungu mwenyewe si kwamba tulifahamiana kwa muda mrefu(ndo wengine wamejibana) ufahamu wao mpaka apate aliye somo naye shule
❤Jiachie kwa Bwana, mtumikie Mungu, mwamini Mungu utapata mke/mme sahihii kwa wakati.
🔥🔥 *MAPITO YA MAHUSIANO* 🔥🔥
💎Ukurasa huu wa mahusiano, umekuwa 💉💉💉kwa wengi, umejeruhi wengi, ume 😭😭wengi, ume 🔪💏wengi, lakini pia Imetia wengi Nguvu 💪🏻💪🏻na maarifa mengi
💎Asilimia kubwa karibu 95%wameingia katika ndoa na watu ambao siyo walio anza mahusiano kwa mara ya kwanza (yaani alo oana naye ni mtu wa 2,3,4....9)katika maisha yake kuwa na mahusiano.
💎Wengine kwa kupitia katika mahusiano hayo mengi, wameunizwa na kujeruhika, wanaogopa mahusiano kama 🐅🐅🐉🐉, wengine wameanguka na kurudi nyuma kiimani, wengi wamepewa maumivu ya maisha kama kuzakishwa mtoto na kuachwa, kuachiwa magonjwa, kuondolewa sifa ya ubinti (Bikra) na kuachwa
💎Sasa unapo tafuta mtu wa kuoana naye na unapo mwomba Mungu ujue Kuna watu wa aina hiyo, ukipewa alo umizwa, Unauwezo wa kuganga moyo wake? Ni watu wachache 5%anaanza na mtu huyo wa kwanza ndo wanaona. (Ni wachache mno)
💏  *SABABU ZA KUPITIA MAHUSIANO MENGI PASIPO KUJUA*💏
💞Kufuata Mkumbo wa marafiki, maana yake hukumuuliza Mungu akakuruhusu uanzishe mahusiano hayo
💞Kutimiza au kuziba Gap la kisaikolojia la hisia na upendo, SI kibali cha Mungu
💞Tamaa ya macho na mwili, ukiingia siyo ulipata amani ya Kristo ndani yako
💞Ulihitaji msaada kwa mtu, akakusaidia akamiliki na hisia zako, siyo ulipewa na Mungu
💞Ulishinikizwa na wazazi, ndugu au marafiki, na si mpango wa Mungu
💞Ulihisi umechelewa Kuingia ktk Tasnia ya mahusiano ya kimapenzi, ukaamua ujiwahi, SI muda wa Mungu
💞Mungu alisema nawe uingie ktk mahusiano hayo ili akufundishe mambo ya msingi, unyoshwe usije ukawa mzigo kwa mtu wako sahihii ajaye
🚫Katika sababu hizo unaweza kukuta umepitia mahusiano hata 10 usipo kuwa makini.
  *SABABU ZA UCHUMBA KUVUNJIKA*
💔Kukosa Uaminifu, endapo utaonekana hauna hauna msimamo wa kutulia na mchumba wako, ukatangatanga na wengine utavunja uchumba
💔Kugundulika kwa tabia isiyo weza kuvumilika, endapo mwenzako ataona tabia mbaya isiyo vumilika anaweza kuvunja uchumba,
💔Kuwa na misimamo mikali isiyo vumilika,
💔Ukiwa msiri, mtu usiye wazi kwa mwenzako Unafanya mambo kimya kimya
💔Kutegemea makubwa kwa mwenzako, ulihisi mwenzako atakuwa matawi ya juu kumbe wa kawaida
💔Marafiki wenye wivu, ukiendekeza kushauriwa shauriwa na marafiki watavunja uchumba wako
💔Kukosa mawasiliano ya karibu na mchumba wako, unapo anza mahusiano chunga mawasiliano yawe ya uhakika
💔Kutojali hisia za mwenzako, unaweza kumjibu unavyo taka, unaweza kumpotozea kimawasiliano hata wiki, au siku 2/3
💔Kuanza ngono kabla ya Kuingia katika ndoa, fasta mtavunja uchumba
💔Kukosa mipango ya maisha, kuendesha mahusiano ya kitoto yasiyo na mipango
💞  *NJIA ZA KULINDA UCHUMBA* 💞
💘Mpende mwenzako kwa viwango vya kutosha
💘Mwamini mwenzako, na wewe jiamini, kuwa chaguo lako liko sahihii
💘Usiruhusu mazoea ya karibu sana na watu wa jinsia tofauti na wewe, watakuletea kutoaminika kwa mwenzako, au migogoro katika uchumba wako
💘Jenga tabia ya kusikilizana, kama Kuna jambo lijadilini na mlitatue kwa pamoja
💘Jenga tabia ya Kusaidiana katika mambo mbali mbali, endapo mwenzako anashida, ibebe kwa mzigo uitatue
💘Ombea sana uchumba wenu, na muwe na ratiba maalumu ya maombi ya kulinda mipango yenu
      *_By Ev Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*

NAMNA YA KULINDA UCHUMBA WAKO

*UKIPATA MCHUMBA JIPANGE VIZURI*
   *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
         *0755444078*
*_SIRAHA ZA KULINDA UCHUMBA WAKO._*
🌟Maombi, usiwe mvivu kuombea uchumba wako kila siku, kumfunika mwenzako kwa damu ya Yesu mwenzako, macho yake, hisia zake, na moyo wake, ukuwaze wewe tu. Mlinde dhidi ya mashambulizi, kataa roho za breakup, kuchokana n.k.
🌟Mawasiliano ya karibu. Msiruhusu kuweka interval kubwa ya muda bila kujuliana hali hata kwa sms. Ukisha tangaza kuingia ktk vita ya mahusiano, usikwepe Gharama ya pesa na muda, hiyo ni kwa usalama wa uchumba wenu.
🌟Epuka ku test hisia za wasichana /wavulana wengine mbali na mwenzako, utalowea huko au utajiumiza kisaikolojia. Wapo watu wana wachumba lakini wana wajaribu watu wengine kudate nao, kama kuwatania, hiyo ni sumu kubwa.
🌟Ridhika na chaguo lako, usimlinganishe mwenzako na wasichana /wavulana wengine, may be ulo wahi kudate nao itakusumbua kiakili na kuleta breakup,.
🌟Usithubutu kuzungumzia zungumzia your past partners inamuumiza mwenzako, inaweza tengeneza sumu ya mahusiano yenu.
🌟Kuwa muwazi kwa mwenzako. Mtafika mbali kwa amani.
🌟Usiwaamini marafiki zako hata kama wameokoka ambao hawajaoa au kuolewa, ukawaunganisha unganisha na mchumba wako, watakuliza 😪😪😪, watakuzunguka, mtaachana halafu unasikia kesho wameoana.
🔥🔥🔥🔥mimi 👐🏻🙅🏻kukuunganisha na 👉🏻💁🏼wangu, ujue umepata kibali, mbele za Mungu na mimi na hapo dk za mwisho, sikupi no, hutaongea naye mara kwa mara, KULINDA UCHUMBA WAKO KAZI 👮🏽🔫🔫💣🔪 *_YAJUE MAMBO HAYA KABLA YA KUINGIA KATIKA NDOA._*
Kuna mambo itabidi uyafanyie utafiti na uyajue kabla ya Kuingia katika ndoa.
💥Nikiingia katika ndoa, sitaishi kwa maamuzi yangu binafsi, lazima nijue mwenzangu anasemaje ktk maamuzi yangu. (Hapo jifunze kumshirikisha mchumba wako mambo yako)
💥Ninawajibika baada ya kuoana, kuwajibika kwa familia mbili na si moja tena, bila upendeleo.
💥Itanilazimu kumlinda mwenzangu kihisia, kijamii na kiafya,.
💥Itanilazimu kumpendeza mwenzangu kuliko mtu mwingine yeyote.   *_JIPANGE KUSHUGHU LIKIA VYANZO VYA MIGOGORO KATIKA NDOA._*
🌟Kabla ya Kuingia katika ndoa jipange kisaikolojia kushughulika na vyanzo vya migogoro katika ndoa vifuatavyo.
💢Kuto tambua nafasi yako na ya mwenzako. Ukishindwa kujua kuwa mimi ni baba au mama mwenye nyumba, na kujua huyu ni mke wangu au mme wangu na kumpa nafasi yake na kuiheshimu, fahamu unatengeneza jehanamu yako ya ndoa.
💢Kupendelea upande mmoja wa familia katika kutoa huduma, au kukaribisha wanafamilia. Wekeni mikakati namna ya kuzihudumia familia zenu kama wana ndoa na si kama mtoto wa familia.
💢Kutowekana wazi vipato vyenu, na matumizi yenu. Ukitaka amani itawale ktk ndoa, weka wazi mapato na matumizi yako, ninyi si ni mwili mmoja?
💢Kuto wajibika ktk nafasi yako ktk familia.
💢Kuwapa uhuru mkubwa ndugu na wazazi kuwa waamuzi ktk mambo ya ndoa yenu.
💢Kuto tunza siri za ndoa yenu, kutaipasua ndoa
💢Kuto kuwa na moyo wa kusamehe na kuachilia.
Kubishana na kushindana na mwenzako, Kutopenda kushuka mbele za mwenzako.
💢Kuwa mtu wa kujihesabia haki hata katika makosa, na kuwa mzito wa kuomba msamaha.
💢Kuwa mtu wa kumlaumu mwenzako kila wakati.
💢Kujisahau kuwa umeoa au umeolewa, yaani kuendeleza mfumo wa maisha ya ubachela, kujiachia na watu wa jinsia tofauti yako kupitiliza
🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟
    *_By. Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*

TAALUMA YA TENDO LA NDOA(PART IV)

*_Sehemu Ya 4⃣ ya Somo la Taaluma ya Tendo la Ndoa_*
    *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*
_Ndoa ni tamu, tendo la ndoa ni muda wa kutuliza akili iliyo changanywa na mbo meengi ya dunia, tendo la ndoa ni muda wa kuunganisha nafsi na kuibua furaha ya upendo wenu katika ndoa, Tendo la Ndoa ni muda wa shukrani na pongezi za kiwanho cha juu kwa wana ndoa katika mema yote mnayotendeana, tendo la ndoa ni kipindi cha kuthibitisha msamaha wa dhati kwa wana ndoa kwa changamoto zilizo jitokeza kati yenu mkahitirafiana, kwa hiyo lifanye tendo la ndoa kwa ubora, uzuri, shahuku na furaha kuu, ili ni tendo tamu sana kama ndoa yako haina migogoro_
Ambatana nami katika uchambuzi huu na Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa( *Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve))*
✍�  *_Kwenye sehemu hii ya nne, tunaingia kitandani kabisaa, muda wa kazi yenyewe inayo lipuaga mioyo ya watu kila ikitajwa, kuonwa, kuwazwa_* 🏡 *MANDHARI YA NDANI KWAAJILI YA TENDO LA NDOA* 🏡
💺Tendo la ndoa siyo la kitandani tu, mtakichoka, yapo mandhari mengi ya kushughulika na mka enjoy zaidi
💺Kama mna nyumba ya kwenu, vitu kama sofa la double au watu 3,liwepo master bedroom, Office chair, viwepo vitawasaidia kubadiri mandhari ya kufanyia tendo la ndoa
💺Wekeni taa ya mwanga wa rangi, hafifu, ndo mtacheza game vizuri kwa raha, ukitazama reaction ya mwenzako katika macho na molii, midadi ikupande vizuri
💺Inapendeza tena sana, Mwana mama kama mpo ndani (hasa chumba) kuvaa nguo za pekee kama night dress (mini, transparent ya ukweli, nyepesi, inayo onyesha mpaka ndani)
💺Mwanaume vaa pensi nyepesi, siyo unavaa pensi la jeans 🙅🏻😡, iwe ni siku ya game au not wana ndoa mlale na nguo laini, nyepesi
💺Inapendeza tena sana, mnapoanza kuandaana muwe mmevaa hizo nguo nyepesi, mnavyo zidi kuchemka ki hisia, umvue mwenzako nguo, siyo anajivua, na unamvua kwa dizine ya kimahaba 😘
*_MIKAO/STYLES ZA TENDO LA NDOA_*
🚁Ukitaka kulifurahie tendo la ndoa, mlifanye kwa mikao ya aina mbali mbali, hamtachoka, hutamboa mwenzako (Usikalili baba juu mama juu, lisaa lizima 😡😡🙆🏻🙆🏻aliyeko chini unahisi anafurahi au anaomba umalizie haraka)
🚁Anza na mkao ambao ni mwepesi sana utakao ruhusu kasi za mwanzo kwenda nao (mwanzoni watu wanaanza kwa kasi kubwa wakilitafuta bao la kwanza lililo karibu sana)
🚁Iko mikao mingi ila ni vigumu kuielezea bila drawing(na humu haturusu picha yoyote wala video yoyote) nje na na picha ya utambulisho. (Ila itaelezewa ile inayoelezeka zingine kabuni mwenyewe)
🚁Ya kwanza huta ikwepa Missionary style (ni common kwa kila mtu,) Baba juu mama chini, simple but very sweet kwa kila mmoja
🚁Missionary imegawanyika katika makundi kama 3 wakati mnaendelea mnaweza badili badili katika makundi yake
🚁Kupakatana, baba kumpakata mama, hapo ni vizuri muwe kwa Office chair, lakini hata kitandani si mbaya
🚁Kupiga magot mkiwa mmeelekeana
🚁Kusimama,
🚁mama Kusimama na mguu mmoja akakanyaga kitanda akiwa ameshikiria ukuta
🚁Kusimama mama akapandisha mguu kwa kiuno cha baba
🚁 Mama piga magoti inama Hakikisha kichwa kina gusa godoro kiuno ndo kiinuke juu, baba tokea kwa nyuma
🚁Mama piga magoti simamaia mikono mfano wa mnyama wa miguu minne, baba tokea kwa nyuma
🚁baba lala chali mama kaa ki dizine flan juu kama ume chuchumaa chooni, ukalie mtambo halafu anza kama una kaa na kuwa inuka kidogo kidogo uhakikishe kwenye kaa na inuka yako mtambo hauchomoki
✍�Baba lala chali, mama piga magoti ukitazama upande alipo nyooshea miguu mmeo, ukalie mtambo, anza kunesa nesa juu ya mtambo Hakikisha hauchomoki
🚁Baba lala chali mama kuwa juu face to face, hapo mama wewe ndo dereva, chezea unavyo taka maana wewe ndo controller unataka mtambo ukusugue pande zipi
🚁Mama lala chali chini ya kiuno chako weka mto ili uinuke juu baba apige magoti mama muwekee baba miguu mabegani
🚁Mama lala kifudi fudi chini ya tumbo kwa chini weka mito hata mwili au mmoja ili kiuno kiinuke juu, baba piga magoti anza kazi
🚁Lala wote upande mkielekeana uso
🚁lala wote mkielekeana uso mmoja apandishe mguu juu ya mwenzake hasa mama
🚁lala upande kuangalia upande mmoja ila baba ndo awe nyuma ya mama
Ziko mikao mingi ila ni vigumu kuielezea out of drawing. Ila hiyo itakutosha na wewe buni ya kwako, tendo la ndoa ni ubunifu
💏 *_MAMA HAKIKISHA HAYA MAMBO UNAYATIMIZA_* 💏
💋Miguno na ukelele wa mahaba unasikika utamfanya mmeo asichoke haraka
💋Ukiwa chini Hakikisha unakata kiuno, unazungusha kiuno taratiibu, huku ukimpapasa papasa mmeo mwili wote
💋Hakikisha akipiga bao akichomoa mtambo uchezee mtambo kwa mbewembwe zote, wanaume Wanapenda sana na wanajisikia rahaaaaaa ukishika shika mashine zao, ukizi massage
💋Chezea kifua cha mmeo kiwe na Garden au la chezea
💋Chezea vizuri kwa umakini vitunguu (korodani) za mmeo ndo moyo upo hapo usizi bane utamuua, zikune kune
✍�Jambo la msingi katika mchezo huo usio na referee, *_Msiwe mabubu_* zungumzeni tena sautibza kimahaba siyo sauti za kiaskari👮🏻, halafu mwambie mwenzako, unajisikiaje mnapo endelea na mchezo, aguse wapi, apigeje *Rhythm* za in and out, ushikwe wapi, afanye nini ukisikie raha, usikae kimya huo ni uwanja wako wa kufurahia mchezo sema.
_Mpaka hapo mtakuwa mmepeana raha na hakuna atakaye ona mwenzake mzigo, hutatamani kuchepuka wala hutoliona tendo la ndoa kero kwako._
     *_Mwisho wa Uchambuzi_*  
_By Ev. Elisha Kazimoto_
    *0755444078*

TIBA YA NDOA

💈💈 *USINGE DHARAU MAMBO HAYA MADOGO, NDOA YAKO INGEKUWA SALAMA*💈 💈
   *_By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
(Psychologist & Counselor)
      *0755444078*
💈 _Shalom, shalom mwana ndoa na mwana ndoa mtarajiwa, leo nakuja na uponyaji wa Mahusiano, Uchumba na Ndoa kwa pamoja ili tupunguze msongo wa mawazo au tuondoe kabisa hizo( *Stress*)za ndoa tuishi kwa furaha na huyo mke wa ujana wako_👇�👇�👇�👇
*_Mithali 5 : 18 - Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako._*
💈Huwezi kumfurahia mke wako, mme wako kama mmeyasahau mambo madogo madogo ya kisaikolojia yanayo funika hisia, yanayo jaza kikombe cha upendo cha moyo, yanayo punguza na kufunika udhaifu wa mwenzako na kumuona mtu wa maana na kamili maishani mwako.
💈Ndoa ahiitaji misuli 💪, inahitaji akili sana, na maarifa, hapo utaifurahia ndoa yako. ( _Unaye jiandaa kuingia katika ndoa usijiandae kupambana, kukabiliana na mtu, jiandae Kisaikolojia kumpendeza mwenzako, kumlinda mwenzako, kumuhudumia mwenzako, kumtia moyo mwenzako, kumwambia wewe ni wapekee kati ya wanawake wote/wanaume wote wewe umewapita wote)_👇�👇�👇�👇
*_Mithali 31 : 29 - Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote._*
💈Sijui kama unaelewa lugha hii na maana hii, yaani mpaka unamuoa huyo, au unakubali kuolewa na huyo, maana yake huyo ndo amewapita wote! _kama ulioana na huyo basi kwakuwa alikupa mimba polee(unahitaji msaada wa wana saikolojia tukusaidie umpende tu), kama ulioana na huyo kwakuwa wazazi walikutafutia, alikusaidia tu kulipa ada ya chuo, unahitaji msaada wa Kisaikolojia upende tu_
💈Sasa kama amewapita wote,  *Mchepuko wa nini?* maana tendo la kumuoa, kukubali kuolewa naye si kwamba hawakuwepo wengine, ila uliona huyo ndo mtatembea pamoja, sasa kama ni hivyo ( *Mke wa pili wa nini?*)
_Kuna vitu unavikosea katika kuishi na mwenzako_
💈Leo Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa,  *_Ev. Elisha Kazimoto_*na kualika ukae wq kujifunza ili ijue, mambo madogo, madogo ya kisaikolojia ulo yadharau ndo yamefanya *_Umchoke Mwenzio_* wakati kwanza, ndo mna watoto 2,miaka 5 ya ndoa, je mkisha kudlfikisha miaka 50 mtakuwa mnatafutana kwa panga🗡🔪🔫kuuwana? Ni wakati wa kubadiri MTAZAMO ndoa siyo vita wala nguvu ndoa ni Akili, na mimi leo Mwana Saikolojia nakupa Akili ya mambo madogo ulo ya sahau, yarudie, usiwe na aibu, huyo siyo mgeni ni mpenzi wako, yafanye usimwonee aibu kwamba atanishangaa nitaanza anzaje,? *_Anza hivyo hivyo kama ulivyo kiwa unaanza kumshushua mistari ya kumchumbia, au kumkubalia ombi lake, kwani ilikuwa rahisi? Ila si ulitimiza hazima yako? Si ndo maana mpo wote_*
💈Sasa Tuangalie haya mambo madogo yanayo hitaji akili ya kuzaliwa na ya mazingira siyo chuo wala sekondari yalivyo na nguvu kwa ndoa yako. _Tutanguliwe na Andiko hili👇�👇�👇�
*_1 Wakorintho 15 : 34 - Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe._*
✍�Unashauriwa kutumia akili ipasavyo, sasa waweza nusuru ndoa yako, mahusiano yako kwa kutumia akili hii hapa.
❤❤  *RADHA YA NDOA*❤❤
_Mwana ndoa Radha yote ya ndoa ipo hapa, siyo kwenye magari yako, pesa zako, PhD zako wala uzuri wako, kazania hapa_
✍�  *_Baba mke wako anahitaji kusikia kila mara neno NAKUPENDA MKE WANGU,_*  Hii ni miongoni mwa dawa ya hatari kwa ndoa maana ukishasema nakupenda mke wangu, haipo siku utawaza kumsaliti, hauta mpiga, hauta mtukana, ila utampenda, utamtunza na kumjali. (Asipo sikia neno hilo, furaha yake inapotea, na ikipotea ndo mwanzo wa migogoro ya ndoa)
✍�  *_Mama mmeo anahitaji kuona unaangaika kumtimizia haja yake_* mmeo anataka kuona ametoka kazini, au safari unaangaikaje kumuhudumia,? Apate maji ya kuoga, chai/juice, chakula umeandaa kitanda apumzike nk.
✍�  *_Baba, mkeo anahitaji kusikia ukimsifia, wewe mzuri, umependeza leo nguo yako, ulivyo suka nk_* mara nyingi mambo mengi wanawake wanafanya ni kwaajili yako mme wake, akivaa, akijilemba, akisuka anategemea kuna Neno litatoka kwa Mr, kwamba nimependeza. (Akilikosa sasa atachomoka nawale wanao msifia, moyo utahama kwako, ataanza kutamani kuzurura ili watu wageuke, wapige miruzi, wamsifie ndo anaridhika) *_Wanaume hawa watu Wanapendaga sifa_* usipo mpa sifa anakudharau moyoni na anaona hukidhi viwango vya kuitwa mme, maana waume wengine nje wana sifia balaa.
✍�  *_Mama mmeo anahitaji kuona lugha yako niya upole, na unamsikiliza_*  mwanaume ameumbwa kuwa mtawala, ukitaka Amani, msikilize, mshauri kwa upole, ndani ata akikosea usipayuke na kukoroma kama unamkoromea mwanao, mwambie, *_Lakini mpenzi wangu hapa umenikwaza, sijajisikia vizuri_* inatosha, kwani ukivimba na kuzira ndo utambadirisha, huyo anaitwa kichwa, mme, mtawala, kuwa mpole tu utaona ndoa itakavyo noga.
✍� *_Baba, mama mwenzako anahitaji kusikia unamuita jina zuuri analo lipenda_*  Radha kubwa kwa mpenzi wako, katafute kote duniani, kama (Mchepuko/Hawala) anamwitaga mmeo, mkeo... Mama John, baba Joyce, au anamuita... Peter, Makulata📢📢)  haipogo hiyo, wanaitana (  *_Honey, Baby, Mpenzi, Sweet, Love nk_*) Ndo maana mnaibiwa waume na wake zenu, jina zuri lina nguvu kubwa kwa mtu (ndo maana Biblia ikasema Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi *Mithali 22:1*) sasa endelea kumuita mwenzako Makulata, wenzako wanamuita Honey, au muite baba Kristopher wenzako wanamuita Hubby wangu. Ndoa hiyo umeiuza.
✍�  *_Baba, mama mwenzako anahitaji kuona pale tu anapo kuambia tucheze mchezo wetu, unafurahi na kumwambia haina shida mpenzi wangu hilo tu? Twende nikupe raha_* Fatilia makahaba wote wanaoinmba waume za watu na wake za watu kama huwa wana udhuru kwenye tendo la ndoa, walo 🆓 24hrs, sasa wewe mpaka udanganywe, utegeshewe kama panya na karanga ndo aingie mtegoni! Hujui kulinda ndoa. _Mwenzako akikunong'onezea uhitaji onyesha support kubwa, na asione kama umelazimishwa, na kama hauko vizuri tumia ufundi mkuu wa kumshawishi kwa amani muahirishe mchezo mtoe pointi 3 za mezani._
✍�  *_Baba, mama mwenzako anahitaji kupata zawadi kutoka kwako_* Unajua zawadi si lazima iwe kubwa, zawadi ni Ishara, au kiwakilishi cha hisia zako juu ya mwenzako kwamba una mpenda, unamjali, unamthamini, ni special.  Kwa hiyo jifunze kumtafutia zawadi mwenzako hata chocolate, pipi ukiileta rasmi kwaajili yake ni kubwa kuliko kumpa pesa laki moja ya matumizi huku na masimango.
💈💈 _Kwa leo niishie hapi, anza na hayo, siku nyingine ntakuletea mengine, ulikuwa nami Mchambuzi Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa, Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve), kwa masomo zaidi Tembelea Facebook kwa jina la  Elisha Kazimoto, utakutana na Pages 3 za nafundisho yangu, Like, share utakuwa umejiunga nami. Na kwa ukaribu sana, mada, maswali na majibu njoo Whatsapp kwa no. 0755444078, uombe kujiunga na chuo mafundisho kiitwacho *MATERIAL ADIMU UNIVERSITY 🎓* kama utafaulu Interview. Ni mafundisho Chini ya Maadili ya  Kiroho (Mahusiano, Uchumba na Ndoa)_💈💈
   *By Ev. Elisha Kazimoto*
     *0755444078*