🌹🌹 *SEHEMU YA PILI YA SOMO LA TAALUMA YA TENDO LA NDOA*🌹🌹
*_By Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
*0755444078*
_Haleluyaa wana ndoa mnao shiriki baraka za mwili, na saikolojia njema(Tendo la Ndoa), kuna vitu vingi vizuri na vinaleta raha kwenye maisha, ila Tendo la Ndoa lisilo la kujiiba, kuogopa kufumaniwa, kupata magonjwa, weee ni raha tupu!_ Ndio maana nakuletea Mwendelezo wa somo hili ufanye mambo ya viwango, achana na sex za wanyama za kukurupuka, au sex za kuanza kubembelezana na mpaka wengine kuongana( *_Yaani ili ufanye sex na mwenzako mpaka umuonge, umbake, mlazimishane, aaha wewe unategemea kupata raha wapi?_*) kaburini au... Maana ukiishi katika ndoa unavizia Tendo la ndoa kama anaye vizia tarehe za mshahara kwa Simbanking hautokuja kisimulia raha ya ndoa.
🌹 _Raha ya Ndoa siyo nyumba, pesa, magari na biashara kubwa, Raha ya Ndoa Upate Penzi Tamu(Hot) kwa mwenzako, mkiwa na vicheko, furaha, amani hamu kila mmoja na mwenzako, mpeane mahaba bila masharti, kukunja uso, bila malalamiko ya mimi nimechoka bhana ila haya ntafanyaje sasa, mpeane kwa amani, haloo, utatamani ungezaliwa ukakuta upo kwenye tendo la ndoa, utatamani miaka isiende mkawa wazee, utatamani ukae muda wote na huyo, hutoona makahaba, wanaume wahuni, asubuhi, mchana, usiku kichwani atakuwemo huyo tu mmeo/mkeo_ ( *Na huo ndo usalama wa ndoa*)
🌹Kuna kesi nyingi za michepuko, kugomea tendo la ndoa, kutoona umuhimu, shida wana ndoa hawajajua Kina cha Tendo la Ndoa na nguvu yake.
🌹_Kuwa mbabe, au kuwa na vitisho, haviwezi linda ndoa yako (hapa sizungumzii mambo ya kiimani, wote tunajua mlinzi wa kila kitu ni Mungu) ila hapa natoa Maarifa ya mwili ujue saikolojia na nguvu ya tendo la ndoa kwenye maisha yako, usije nunua gari, jemga nyumba au fungua miradi ukasema hapa mke wangu au mme wangu nimemuweza hatakuwa na tamaa, *_Hujasikia wanawake matajiri wanalipa house boy pesa ili alale naye? Au baba anapanda housegirl shapeless, kidogo, kachafu_* Kwa hiyo usitumie uzuuuri wako unavyo zuzua watu mtaani, usipo mzuzua mmeo kitandani atatembea na hata watoto wa primary, house girl wako, halafu unakuja kusema, yaani wanaume hawa🤔🤔hawaridhiki house girl mwenyewe mshambamshamba😜😜😜 utaibiwa na washamba hao hao.
🌹Au ukadhani kwa pesa, na mali mke wako atatulia, tumia kitanda vizuri, uone kama kuna mtu ana tamaa za nje, huyo atakuwa na mapepo ya ngono👉👹👹👹 akaombewe tu, au chunguza kabla ya kuoana mlikutana wapi, kama mlikutana kwenye kukata mitaa ya kuvua, na kuvuliwa👉👙 anaweza asiache, ameisha athirika na wewe ulichangia kumuathiri, ulimfundisha na ukamzoeza wizi, hapo Rudini kwa Mungu wote. _Kazi yangu leo Mwana Saikolojia na mshauri wa Mahusiano na Ndoa *(Ev. Elisha Kazimoto)* ni kukufungua Akili, ulinde ndoa yako kwa kutumia kitanda_ *_Mwana ndoa asifiwi kwa kumili utajiri, na mapesa, au urembo, mwana ndoa anasifiwa anavyo mudu Kitanda, yaani hata mkimaliza, kama ni mzee anasema Eeeh nina mke, au mwana mama anasema, Eeeh we funga kazi saluti_*
🌹 Sasa kuna majanga mawili yanawakumba wana ndoa, moja _Mwanaume anaamua kumpiga mafimbo kwa fujo, mama analia, lalamika hapo ndo amasema eeeh nimemtoa machozi_😏😏😏 wee huo ushamba, hiyo ni michezo ya malaya wa kununua kwa siku 2/3 siyo mkeo.
Mkeo mlize kwa furaha siyo kwa fujo za mieleka, huyo unategemea mmalize akupikie, akupelekee maji ya kuoga, akanyonyeshe mtoto wako, fujo za nini, unamkomoa nani, ukirudi kesho ukakuta bado anaugulia mauvivu? Utachepuka au utajiona mjanja au mgonjwa wa akili? *_Tendo la ndoa ni Raha si karaha_*
🌹 _Janga lingine ni watu kuangalia mavideo ya ngono ya wazungu wanao fanya biashara ya kujiuza, siyo mke na mme, wale ni part time sex Hunter, wapo kwa kibarua, wsna ma style kibao ya ovyo, magumu, ya ufilaji, kukunjana migongo nk, dk, 2,1,4 kistaili kimeisha, sasa wewe unayaleta kwa mkeo au mmeo, mnaye kaa wote, hamlipwi, halafu mna masaa 2,na kesho, na keshokutwa, hamjionyeshi kwa watu, unamkunja anaumia, au mnashindwa kupata raha nzuri kisa unaiga style ile ya mzungu, na mkishindwa, unamdharau mkeo/mmeoi, ndo mnaanza kurushiana maneno, wewe huwezi, hujaona kwenye video alivyo jikunja,_ *Mmeiga vitu vya hajabu mmeharibu ndoa, tendi la ndoa mmeliogopa, mmeanza kuchepuka* _Wengine mmeiga wazungu na kulambana sehemu za siri, wenzako wasafi hawana magonjwa, pesa ipo, afya ipo, checkup kila muda, na wewe unaanza kulamba, muda si mrefu maugonjwa ya ajabu ajabu, pesa hauna za kujiweka vizuri, nguo ya ndani unavaa hiyi siku mbili, na unaifua umekaa nayo mwaka mpaka ina tobo, wenzako nguo za ndani zinafuliwa kwa dawa, zinakaushwa, kila siku anabadiri na hiyo harudii, utamiiga utamuweza?_ Acha kuiga mambo ya ajabu utaharibu ndoa yako bure.
🌹 Balaa lingine, ni la watu wanao mjua Mungu ninyi mlioa na kuolewa hasa ndoa ya Kikristo, ambayo haturuhusu kuivunja kwa sababu yoyote, isipo kuwa kifo, haturuhusu mtu kuchepuka, kuoa mke wa pili, sasa wengi wametumia Nafasi hiyo kunyanyasa wengine kuwanyima tendo la Ndoa, kuwapa kwa mgao kama umeme wa mbagala na tandika,maama anajua hauta mfukuza, huta chepuka, hitampiga, hutaolewa pemgine au kuoa mwingine, _Na huu ni ufinyo wa akili na wewe ulistahiki *Usiolewe mpaka miaka 45 au usioe mpaka miaka 50 maana Hufai kuishi katika Ndoa, lakini unafaa uwe mjane, au mgane, maana hujui ya ndoa_
🌹 Mmeleta migogoro ya ndoa wenyewe, michepuko wenyewe, halafu unaanza maneno mme huyu anatabia mbaya, mke huyu anatabia mbaya, vipi kitanda mnakitendea haki?
🌹 *_Kuna balaa la dhana moja imekuwa kero kwenye ndoa, imezoeleka kwamba mme ndo amuombe tunda mke, kila siku, asipoomba mama anachunaa, au Mwanamke anatamba kwamba sikupi tutaona, hivi kwanini mnatengeneza mfumo wa tendo la ndoa anaye paswa kuomba ni mme tu, ndo anahaja sana? Kisaikolojia na kisayansi, na kibiblia kweli mwanaume anahitaji tendo la ndoa sana kuliko mke, kwa watu wengi, japo wapo wanawake mpaka wanalilia😪😪😪kitu ila siyo wengi_
Sasa tengenezeni mazingira ya uhuru, na kila mmoja ajitie katika uhitaji wa tunda hilo, huo ndo usalama wa ndoa yenu, na ulinzi wa ndoa yenu ukidharau, mtu anakuwa mwaminifu, inafikia hatua ustaarabu unamshinda, huyoo👉🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻💃🏻💃🏻💃🏻💃🏻💃🏻anaenda kuifuata njeee unabaki kulia na kulaumu. Sasa tubadirike
🌹 _Ninapo maliza Uchambuzi huu sehemu ya pili, bado safari yetu ni ndefu katika Uchambuzi wa Taaluma ya Tendo la ndoa, endelea kuwa nami, ntakuletea faida za Tendo la ndoa Kisaikolojia uone ambavyo hupaswi kuwa mzembe kumega keki hii👉👙ya ndoa_ kuna furaha kubwa na amani katika kushiriki tendo la ndoa na mwenzako.
*_Ulikuwa nami mchabuzi wako, Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa, Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
🌹🌹*0755444078*🌹🌹
Tuesday, 29 November 2016
TAALUMA YA TENDO LA NDOA(PART II)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
IKO POA SANA
ReplyDelete