Tuesday, 29 November 2016

MAISHA SALAMA YA UCHUMBA

💘💘 MAISHA SALAMA YA UCHUMBA💘💘
    By Ev. Elisha Kazimoto
         0755444078
_Hizi ni miongoni hoja zinazo eleza maisha ya wachumba wa Kimungu, namna wanavyoweza endesha uchumba wao wakashinda changamoto nyingi za dhambi na maumivu yanayo wakumba wachumba wengi wasipo kuwa makini_
👉�Fuatana na mimi katika uchambuzi wa swali muhimu lililo ulizwa,  *Niishije na mchumba wangu, apate upendo wangu vizuri, lakini tusiingie dhambini?*
❤❤Katika MAADILI YA UCHUMBA, Kuna mambo yanashauriwa kibiblia na kihekima za kibinadamu ili muwe na Amani na mafanikio katika safari ya ndoa yenu iwe ya ushindi
❤Miongoni mwa mambo ya Kimungu katika uchumba ni haya..
🙅🏻Ikimbie zinaa, msifanye uasherati (1korintho 6:18, Waefeso 5:3-4)
🙅🏻Tunzeni utakatifu, kwa kuwa makini na mazingira yanayo weza wafanya mpoteze ushuhuda wa Kristo mbele za mataifa (1-Timotheo 4:11-13)
❤❤ *MAADILI YA UCHUMBA ya Kihekima za kibinadamu ni haya,*❤❤
🌹Msiwe na mazoea sana na mchumba wako, yatapunguza Heshima na adabu ktk ndoa yenu
🌹Msiwe na Tabia ya kutembeleana mara kwa mara mkiwa wawili peke yenu, hii inaweza wapelekea, katika kuanguka dhambini, (itawatengenezea vishawishi vya dhambi) mkiizoea
🌹Msianze kuhudumiana huduma kubwa ambazo ni za kindoa, kama kupikiana, kuandaliana maji ya kuoga, kuoga pamoja, kupata mapumziko chumbani kwa mchumba wako, hii inaweza pelekea, Kuanza kukosoana sana na Kupunguza upendo, inaweza waondolea mipaka ya kuonana wachumba na kuonana kama wana ndoa, ambayo yaweza washawishi muingie ktk zinaa
🌹Msipeane zawadi kubwa zinazo gharimu mfumo wa maisha, kama kununua kiwanja, gari, na mambo makubwa, maana uchumba si ndoa, hauna mkataba, mtu anaweza badirisha msimamo, utaumia sana kwa Gharama zako, na huwezi fanya maamuzi ya kisheria, ndoa tu ndo ina sheria 🌹🌹 *ZAWADI KWA WACHUMBA* 🌹🌹
🌹Ni vizuri kuelewa, mchumba ni nani na kabla ya kutoa zawadi au kupokea zawadi
🌹Mchumba ni mke /mme mtarajiwa, ambaye taratiibu za kiroho na kijamii zimekamilika, mnatambulikana kama wana ndoa watarajiwa
🌹Kwa jamii zingine, ukisha toa taarifa kwa wazazi kuwa umepata mchumba, hasa mdada, na posa ikapelekwa, mka ruhusiwa kuendelea na michakato mingine, Wazazi hawawi Responsible kwa mahitaji yoyote ya binti, isipo kuwa mchumba wako akuhudumie mpaka mnaoana
🌹 *Mantiki kubwa hapa, ni zawadi kwa mchumba NI MUHIMU SANA, ILA SI LAZIMA, WALA SI FUNDISHO LA KIBIBLIA*.
🌹Sababu za kupeana zawadi ;
💧Kuonyesha kujali, care, upendo (Upendo si maneno ni maneno na vitendo) Matendo ndo yamewekewa mipaka, yasiwe matendo ya dhambi, zawadi haitengenezi dhambi kwa wachumba, zawadi inakuwa mzigo na mlango wa dhambi kwa marafiki wasiojua wanaelekea wapi, ukipewa zawadi, halafu ukaambiwa nilipe sex, utafanyaje na huyu hana haja nawe ndo maana ya Andiko hili 👇🏻👇🏻👇🏻 Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
Mithali, 15 :27
💧Kusitiri, kuziba mapungufu kwa mwenzako, ili kusaidia ustawi wa maisha yake, na penzi lenu
Si vizuri unachumbia mtu, unachumbiwa na mtu, anapata tatizo, unakausha eti kisa hamjaoana, hata katika mizani ya kiroho unakuwa umepwaya 👇🏻👇🏻Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, walewal wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
54 1 Timotheo 5 : 👆🏻mchumba wako ni mke /mme mtarajiwa, niwa nyumbani mwako hasa, kumbuka si zungumzii marafiki na uchumba wa kitapeli, na zungumza kwa wana wa Mungu wanaojua wanafanya nini na kwa nini mbele za Mungu
🙇🏽🙇🏽Tafakari, una kazi, mchumba wako hana, anadaiwa kadi ya pango, nani anawajibika kuilipa, Wazazi au mchumba wako, Kuna event inahitaji nguo na mchumba wako hana uwezo kwa muda huo, nani anawajibika kutatua tatizo hilo
🙇🏽🙇🏽Mbali na changamoto hizo, kwa mambo ya furaha, huwezi ona hii nguo, kiatu, saa, mkufu nk, nimnunulie mwenzi wangu? Dhambi iko wapi? Je, Yale uyanunuayo atayatumia wapi si ni ktk ndoa yenu? (Si fundisho la biblia, ila nakutazamisha hekima za kibinadamu)
🙇🏽🙇🏽Zawadi ikiwa ni dhambi na wale unao wapa zawadi si mchumba, SI ndugu yako, na Pengine ni jinsia yako tofauti, na hapo unawatendesha dhambi? Tafakari 🙇🏽🙇🏽
👴🏻👴🏻👳🏻👳🏻 *USHAURI WA HEKIMA ZA WATU WALO TUTANGULIA,*
👉🏻Msifanye mambo (zawadi) yatakayo waondolea amani na utulivu moyoni, mfano unamnunulia kiwanja, nyumba gari, utakosa uhuru wa kuitumia muda wote unawaza at ghairi utapata hasara gani,  unawaza visasi
❤❤Zawadi ni ishara ya upendo, usijifariji, iwe kiroho au kimwili, Upendo na zawadi huwezi kuvitenganisha (Yohana 3:16)ila zawadi ziwe na kiasi ili kuzuia jaribu la kuumia moyo endapo safari ya ndoa haitafikiwa ❤❤ ❤❤Unapo Mtembelea mchumba wako, inashauriwa mtofautiane katika number ya jinsia, msichana mmoja wavulana wawili, au Wasichana wawili mvulana mmoja, nk
❤Pili kumsaidia mwenzako kazi endapo amepatwa na shida ni sahihii, inakuwa haipendezi inapo kuwa mazoea kufanya kazi kama wajibu wako Mwana ndoa kumbe ni kutoa msaada, hiyo ndiyo inatiliwa mashaka, nakuona mipaka Imepitwa, na unapo enda kutoa msaada, nenda na mtu ili mlinde ushuhuda, na usalama wa roho zenu
_Ulikuwa na mchambuzi mwl.wa Mahusiano na ndoa, Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_
   *0755444078*

No comments:

Post a Comment