๐๐ *SAIKOLOJIA YA MAHUSIANO*๐๐
*_BY EV ELISHA KAZIMOTO_*
*0755444078*
_Shalom mtu wa Mungu,leo nimeona nikuletee uchambuzi maalumu kuhusu MAHUSIANO kwa ujumla,hapa ntazungumzia mahusiano ya kirafiki,ya uchumba na ya ndoa_
๐Mahusiano ni suala la kisaikolojia yaani linalo husu(Akili,fikra ma hisia),wengi wetu tumejikuta tukipoteza marafiki wetu muhimu,wachumba wakituacha,ndoa zikianza migogoro hata kuachana,shida ni ufinyo wa Taaluma ya Saikolojia ya Mahusiano.
๐ *_Leo Mtaalamu wa Saikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa( Ev Elisha Kazimoto) na kuletea uchambuzi ulobeba Siri za uponyaji wa Mahusiano yako_*
๐Huwezi kuwa na mahusiano imara kama _Hujui kwa nini Umeingia katika Mahusiano hayo_ Hii imekuwa na changamoto katika mahusiano ya urafiki,uchumba na hata ndoa, kama umeingia katika mahusiano yotote Hujui nini kimekusukuma kuanzisha mahusiano hayo,ni rahisi sana kushindwa kuendesha mahusiano hayo,lakini pia ni rahisi kuvunja mahusiano hayo. *_Nina maanisha kwamba,Kisaikolojia mtu anaye jua kuwa nimeanza mahusiano haya kwa faida kadha wa kadha,hatokubali mazingira korofi yabadirishe Kusudi lake,furaha yake_* Mtu mwenye lengo imara lenye faida kwa nafsi yake,hayuko tayari changamoto kubwa wala ndogo,zi sitishe Kusudi la mahusiano alo yaanzisha.
Mfano,nirahisi sana kuvunja uchumba,kama hujajua kwa nini umeamua kuanzisha uchumba na mtu huyo, au ni rahisi kutokubali kusuruhisha mgogoro wa ndoa yako,na kuona ni bora kila mtu awe kivyake kwa sababu hukujua kwa nini uliamua kuoa/kuolewa na huyo mtu.
*_Kisaikolojia nina maanisha kwamba,mpaka unaamua kuanzisha mahusiano ya uchumba,au kuoana,umejiridhisha,kuwa huyu mtu ninaye ungana naye anavitu muhimu ndani yake kuliko mtu mwingine awaye yote ndo maana ukaamua kuanza mahusiano naye,na kama unaona huyo mtu hakidhi kiu ya moyo wako ni vyema usianzishe mahusiano naye maana utaathiri mfumo wa kuwaza,kunena,kutazama katika maisha yako,utakao kugharimu kuishi maisha bandia yasiyo yako.
๐ Lakini pia,Saikolojia inakutaka kutambua GHARAMA ya mahusiano kabla ya kuanzisha mahusiano yoyote. *_Hii ina maana kwamba,ujiridhishe uwezo wako wa kujubali kulipa au kubeba gharama yoyote itokanayo na mahusiano yawe ya urafiki,uchumba au ndoa_* Kitu chamsingi cha kujua,Gharama ya mahusiano huongezeka kulingana na nafasi(umbali) na unufaikaji: yaani gharama ya rafiki ni ndogo kwasababu ya umbali wake kwako na unufaikaji ni ndogo, Gharama ya mchumba inaongezeka maana umbali unapungua na unufaikaji unaanza kutarajiwa,na Gharama ya Ndoa ni Kubwa mno maana umbali ni *Zero Distance* na unufaikaji ni mkubwa maana mnashiriki maisha ya pamoja mpaka miili yenu mnashirikiana hapo ni gharama kubwa.
_Kwa hiyo kama hujawa na uwezo wa kulipa gharama kubwa,usifanye maamuzi ya kuingia katika mahusiano ya Uchumba na ndoa,baki kwenye urafiki_
*Baadhi ya Gharama za Mahusiano*
⚓Mahusiano yanahitaji Muda wa Kutosha. _Kama bado unathamini muda wa mambo yako sana kuliko kitu kingine,tulia usiingie kwa mahusiano utavunja mahusiano ndani ya miezi michache_ Mahusiano yanahitaji muda,mwenzako unaye anza safari naye anahitaji kutumia muda wako kukufahamu,ajiridhishe kama unafaha kuwa mtu wa kuambatana naye maishani. Ukiona unahisi kero kupotezewa muda na mwenzako iwe kwa mazungumzo,kutoka out,kupumzika,kupanga,na kufanya shughuli alokuhusisha,jua wewe bado kisaikolojia ni mdogo(mtoto)hujakomaa huruhusiwi kuingia katika mahusiano maana mtapigizana kelele na mwenzako za hujali,uko busy na mambo yako mtaachana.
⚓Gharama ya Kuomba Samahani. Unaweza kuona ni jambo dogo kumbe hii ni Gharama kubwa inayoshinda wengi na kupelekea mpasuko wa mahusiano. Kama bado kinywa chako ni kizito kusema nisamehe mke wangu,mme wangu,mchumba wangu,usianzishe majusiano hayo hayatadumu. *_Maana hakuna asiye kosea,ila namna gani unatatua makosa_* Samahani ni nguzo kubwa katika mahusiano,kama huwezi lipa gharama hiyo,usiingie kwa mahusiano.
⚓Gharama ya Kupenda. _Kila anaye taka kuanzisha mahusiano tafakari kama bank ya moyo wako ina Akiba ya Matendo ya Upendo ya Kutosha yakumshibisha unayeingia naye katika mahusiano,kama hujajaza bank yako,subiri,utaachwa katika njia panda utakosa thamani ( *Upendo unaambatana na kutoa,kujinyima,kulinda,kufurahisha,kubembeleza,kusikiliza,kujali na kusifia*)kama haya mambo huyawezi usiingie kwa mahusiano.
⚓Kuna Gharama ya kuheshimu na kutii. Kama unaona huwezi kuwa msikivu,kufuata na kutii kwa mwenzako kwa sasa,usifanye haraka kuingia,jipange kwanza uandae saikolojia yako,kuongozwa(Ewe mwanamke) ndo utaifurahia ndoa au uchumba.
⚓Gharama ya Kuachana na wazazi,ndugu na marafiki. Kama bado hukawa na uwezo wa kutengana na wazazi na ndugu marafiki zako wa mwanzo,ili uambate na mfanye maamuzi yenu kama wana mahusiano,basi ujaribu kuanzisha mahusiano,mtavurugana na mwenzako mapemano. Ila ukifikia viwango vya kuwela mipaka kati ya wazazi ,ndugu na marafiki dhidi ya mmeo/mkeo ili wasiwaingilie hapo umekomaa kisaikolojia.
⚓Gharama ya Vita ya Kiroho, pamoja na kuenjoy maisha ya mahusiano,mnapaswa kujua, kwa kadiri unavyoongeza mtu pembeni yako ndivyo unavyoongeza uwanja wa vita na nguvu ya kushinda. *Sasa kama huwezi kujisimamia kupambana dhidi ya ufalme wa giza mwenyewe,usiongeze ukubwa wa vita kwa kuanzisha mahusiano a mtu,mtapigwa kabla hamjafika mbali,au mtaishi kwa kuumia sana,hamtafurahia maisha* Ndo maana kuna umuhimu wa kujiridhisha unaingia na nani katika mahusiano,ni mpambanaji au mzembe!.? Polee kwao wanao zoa watu dhaifu.
๐Lakini katika yote mahusiano yanahitaji Akili sana kuliko nguvu katika kuyaendesha,ndoa zingekuwa na amani,wachumba break up zingepungua.
( *Nataka nikutafakarishe jambo moja ninapo hitimisha uchambzi huu*)
_Hivi Unajua Mahusiano ya Ndoa ndo Kilele cha mwisho cha furaha ya mwanadamu hapa duniani? Je,unajua ukikosa furaha katika ndoa huna njia mbadala wa furaha katika masha,hat ukichepuka huwezi kuwa na furah kama ya ndoa yako.? Je,unajuakuwa ni Gharama ndogo kupoteza haki zako binafsi ili uli ulinde Furaha ya ndoa yako,kuliko kupigania kupata haki zako binafsi na kufuta harufu ya Amani ya ndoa..?_
*Ulikuwa na mimi mchambuzi wa Masuala Mahusiano na Ndoa,Mwana Saikolojia Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)*
_Masomo mengi ya mahusiano,uchumba na Ndoa tembelea kwenye Blog yangu Material Adimu, pomoja na group la WhatsApp la Material Adimu University na pages mbalibali za facebook kwa akaunti ya Elisha Kazimoto_
*_Tayari ninalo Darasa maalumu la Uponyaji wa Kisaikolojia katika mahusiano,Uchumba na Ndoa(Darasa hili ni free kujiunga Ila sheria zake kali na Competition ni kubwa,linajaa mpaka watu wengine wapunguzwe wengine waingie,usichoke kujaribu ukipata link Maana hii ni Taaluma inayotolewa kuponya majeraha yaliyotokana na mahusiano,migogoro ya ndoa,kupewa mbinu mpya za kushinda changamoto za mahusiano,mbinu za kisaikolojia na za kiroho za kuendesha uchumba au ndoa kwa raha sana.Darasa hilo linaitwa( Psychological Healing Class_*)
Mawasiliano ya WhatsApp na kujisajiri katika Darasa hilo ni:
*0755444078
Tuesday, 29 November 2016
SAIKOLOJIA YA MAHUSIANO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment