Tuesday, 29 November 2016

MWANAUME NAKUTAFAKARISHA NAFASI YAKO

NAKUTAFAKARISHA MWANAUME
BY EV. ELISHA KAZIMOTO
             0755444078
💺💺Wewe mkuu wa kaya, Mwanaume, unajua mkeo si trekta? Mbona kazi yako ni kuagiza tu, kuagiza tu, huwezi fikiria kuwa mke wangu naye anachoka, anatumia Damu kama mimi ni msaidie kazi kidogo, au ni muwekee mazingira ya kumrahisishia kazi? AU kwa kuwa anajituma tu jalalamiki ndo maana hujali, (kwa hali hii upendo hauwezi dumu ktk ndoa yenu)
💺Wewe mkuu wa kaya, Mwanaume kwa nini mkeo aonekane nje ya Umri wake, msichana ulimuoa yanki yanki, anajipenda, akikanyaga ardhi inaitikia, akipita mtaani watu wanageuka, Leo umemuweka kwako, utadhani mkimbizi, ameporomoka, maziwa , kifua, tumbo kiuno havitofautiani, hana umbo maalumu (Aloo jali mkeo, mfanye akae ka kabinti kadogo dogo)
💺Muweke mkeo avutie kuanzia kwako mpaka na watu wengine (ndo maana hutaki kuongozana naye, unadai amechoka, kwani alo mchosha ni jirani? Kubaliana na hali hiyo    🚁🚁We mkuu wa Kaya, nini maana ya kuoa, ni kuwa na mpikaji na mfuaji wa nguo? Hujui Mwanamke ni Assert kubwa na chachu ya maendeleo ya familia yako? Mbona Unafanya mambo kimya kimya bila kumshirikisha? (Hapo amani huwezi kuiona ktk ndoa kwa namna hiyo)
🚁wee mkuu wa kaya, Mwanaume bado unajisifia kuwa mke wangu ndo analisha familia na kufanya maendeleo yenu, hujielewi, yaani unabweteka muda wote usome magazeti na kuangalia mpira simba na yanga mkeo ndo atunze familia (husitegemee Heshima)
🚁Mkuu wa kaya, Mwanaume  kuwa kichwa cha familia si tiketi ya kuwa mbabe, mkali mpaka mkeo anashindwa kupiga story na wewe (usitegemee furaha katika ndoa yako)
🚁Mkuu wa kaya, Mwanaume unasahau Heshima ya Mwanaume ipo katika mambo makuu 2,kuwajibika kwa familia kuitunza vizuri na kukalia mchezo wa wakubwa wa usiku vzr? Yaani unaacha mkeo anajinunulia nguo zote, eti kisa nimfanya kazi anamshahara, (hata kama mkeo anakuzidi mshahara, kipato mfanyie shopping, yeye kujinunulia si mbaya, ila asijihudumie kama mjane) Jenga Heshima 💖💖Mwisho wa uchambuzi wa sehemu ya kwanza ya ndoa kwa leo tutaishia hapa....
💖Ndoa Inapendeza sana mkielewana, mkiwa na kauli moja, mnakaa mnapanga mipango pamoja
💖Ndoa Inapendeza sana, mkiwa mnaheshimiana, mnapendana, mnacheza pamoja, mnataniana
💖Ndoa heshimu upande wa familia ya mmeo, naye aheshimu upande wa familia ya mke wake
💖Ndoa Inapendeza sana, mkiwa wabunifu wa mambo yenu, si kila kitu mnakopi kwa wengine
💖💖Mwisho wa uchambuzi 💖💖
  *_BY EV. ELISHA KAZIMOTO_*
    *0755444078*

No comments:

Post a Comment