Tuesday, 29 November 2016

SIFA ZA MTU ANAYE FAA KUWA MME/MKE WAKO

🌳🌳  KIJANA/BINTI ANAYE FAA KUWA MME WAKO/MKE WAKO🌳🌳
             Ev Elisha Kazimoto
                 0755444078
Shalom, shalom vijana watumishi wa Kristo, leo napenda niongee na wewe kijana wa kiume na wa kike, unaye tamani kuoa, au kuolewa, au umechumbia au umechumbiwa, au bado unatafuta, au umetafutwa ila hujatoa jibu la ndiyo au hapana, basi kaa mkao wa kusikia ili nikuletee uchambuzi huu wa nani Anafaa kuitwa mmeo, au mkeo katika kizazi hiki kigumu_ Fuatana nami Mtaalamu na mchambuzi wa mahusiano na Ndoa *_Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_* Tutanguliwe na Neno hili la kijana huyu mfano wa kuigwa tuchambue hapo. 👇👇👇👇
*Mwanzo 39:4-12*
4  *_Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake._*

5 _Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu._ Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba

6 Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu. 

7   *_Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami._*

8   *Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.*

9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe.  *_Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?_* 

10  _Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye._

11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; 

12  *_huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje._*
✍ Katika uchambuzi huu nazungumza na watu wanao mjua Mungu, yaani waliookoka ndiyo wanaweza kunielewa zaidi maana nita nena kibliblia zaidi kuliko kitaaluma(Kisaikolojia).
✍  *_Kijana unaye tafuta mke au mme, kwanza jiulize maswali haya usije zunguka na kutafuta kisicho kuwepo, au ukavamia kisicho kuhusu au ukaokota kilicho tupwa kwa sababu hakina thamani_*    *JIULIZE:=*
👉 _Mahusiano yangu na Mungu yako vizuri?_
👉 _Hivi kweli mimi najitambua kwa nini nipo duniani_?
👉 _Hivi Nafaa kuwe mme/mke wa mtu makini au nichukue wa kawaida?_
👉 _Hivi nimejitunza au nimeisha jiharibu?_
👉Hivi nimeizoea zinaa au siijui, na niko tayari kumpata mtu kama mimi au tofauti na mimi?
👉 Kama niliharibu ujana wangu,bado nashawishika kuanguka anguka? Kama bado hata katika wokovu naanguka anguka kweli nitapata mtu sahihi?
👉Nina uaminifu gani kwa Mungu sasa hivi kufuta historia zangu mbaya?Mungu aone sababu ya kuachikia kitu cha pekee kwangu
👉 _Hivi Nastahili kupewa msaidizi au nipewe mtu wa kukaa naye?_
👉 _Hivi nina maono gani ya kimaisha?_
✍ Basi kijana yeyote mwenye akili njema anaye oa/kuolewa kwa malengo lazima awaze na ajibu maswali haya, mbali na hapo uwe unahitaji mtu wa kufua, kupika, mtoko, kukupa matumizi ya saloon na wa kuzaa naye.
✍ Kijana unaanzaje kuchumbia/kuchumbiwa bila kupima mahusiano yako na Mungu? _Hujui mahusiano yako na Mungu ndo yanatoa jibu la upate mke/mme wa aina ipi?_ Huwezi kuwa tapeli kwenye Wokovu, njia zako za kona kona, hueleweki umeokoka au nimwana jumuiya ya ibada, halafu ukategemea Mungu akuchomolee kifaa kikali kizuri, kinacho mpenda Mungu, kilicho wekeza maisha yake ya ujana kwa Yesu, *NEVER SAHAU* Mungu si dhalimu kiasi hicho, utapata Tapeli mwenzako, ili mtapeliane, mpandishane presha kila siku ninyi kwa ninyi. *_Na uliye na mahusiano mazuri na Mungu unahitaji mtu mwenye mahusiano mazuri na Mungu ili uendelee kwenye kasi hiyi mbele za Mungu_* Usipo mungoja Mungu utachukua mtu wa kushusha viwango vyako vya kiroho siku kwa siku.(MUNGU HAWEZI KUKUOA MTU FEKI WAKATI WEWE NI ORIGINAL)
✍ Kijana unaanzaje kuchumbia /kuchumbiwa wakati hujitambui kwa nini upo duniani, that means huna malengo ya kimaisha zaidi ya kula, kuvaa, na kununua hivyo unavyo taka kununua,  *_Kijana asiye ishi kwa malengo, asiye na malengo ni mzigo katika ndoa,_*  Unampango gani wa kukulinda ili uishi miaka mingi duniani na mmeo/mkeo? Kama huna mpango wa kuleta faida katika ufalme wa Mungu wewe ni uchafu katika mazingira hivyo utatupwa kwa dustbin muda wowote ( *You are pollutant*),  Kijana anaye Faa kuoa /kuolewa ni yule aliye jiwekea malengo ya kuyatimiza katika miaka ya uhai wake na anatamani ajaye maishani mwake awe mchango mkubwa wa kuyatimiza.  *_Wewe unaye ishi kwa kuwa kumekucha, ukiambiwa na huyo unaye mtaka muwe mme na mke, Ukaulizwa nini Maono yako ya kimaisha na mikakati ya kuyafikia utajibuje?_*
Unajua maono si kila mtu anaweza ya beba.
👉 Sasa ikiwa utazoa yoyote maadamu amekubali, au anaonekana ni umbo namba nane, sura ya *_Kwetu Pazuri_* Six pack, Sura na umbo au fedha havitimizi, kubeba naono, unamwitaji mtu anaye tazama mbele,
✍ Kijana unaanzaje kutafuta mtu makini, wakati wewe haupo makini? Unaishi maisha yasiyoeleweka, hayana mpangilio, *_Huna mpangilio wa mavazi,_* nguo unavaa yoyote tu, heleni, mkufu, viatu, lip shine na 👜 handbag kila kitu rangi yake, hujui ni shati gani la kuchomekea au kutochokea.  *_Huna mpangilio wa kula, njiani unatembea unakula, kwa watu wengi umeshika andazi unakula,_* Unaongea wee huna break, kila neno, kila story unaijua,  kweli umakini ni mdogo, ukipata mtu makini utamtesa, atakuwa na kazi kubwa kukupanga ukae sawa. *_Dada vipi chumba chako, wigi, losheni, ndoo yakuogea, underwear, sufuria, vyote vipi sehemu moja kitandani, unaloweka nguo kufua siku 3 kama anayeloweka mahindi ya kupanda._*
Ukiolewa na kuzaa watoto vidaso si vitakuwa mezani na kwa makochi/sofa?
👉 Kama unataka mtu makini nawe jiweke makini uvutie, mwonekano na hata huko unako kaa, uwe na mpangilio wa maisha, ndoa ni taasisi kubwa, inapokea wageni wengi wa kila aina msije tia aibu mkawa gumzo la mtaani.( *Badilika*)
✍ Kijana unaanzaje kuchumbia/kuchumbiwa bila kuji fanyia tathmini umeishi maisha gani, umejitunza? Au ndo hivyo kuna maeneo huwezi pita kila mmoja anajua mwili wako, kila mtaa wa pili una mtoto, wengine umewakataa, ulo wakubali 4, sita 6 umegoma, halafu kwenye maombi unaomba Mungu nipe bikra safi, na unamuuliza binti kama siyo bikra unampiga chini, kwani wewe bikira?

👉 Na wewe dadaangu, vipi mbona kila mtu anaye kuja una mpiga kibuti👢, unataka mchungaji na mwinjilisti, kijana aliye jitunza safi ndo unamsubilia, umejiuliza?  _Wanaume wangapi wanajua mwili wako, ulowafunulia malinda👉👙?, umetoa mimba ngapi,? Una watoto wangapi?_ Sasa kijana wa watu asiye jua kitu huyo pastor na Ev, huyo unaye taka mbona sasa utakuwa unamuonea? ( *_Omba tu maombi mazuri ya Mungu nipe wa kufanana na mimi na wa Kunitosha_*)  kubali haki itendeke na Mungu ni wa haki 100%
✍ Kijana unaanzaje kuoa/kuolewa bila kujiuliza kama unahitaji msaidizi au mtu wa kukaa naye tu?  *_Ninamaanisha wewe uko busy na mambo ya Mungu au yako? Kumbuka msaidizi anayetolewa na Mungu, anakuja kukutia nguvu kwa kazi alokupa Mungu, soma mwanzo 2:1-20 uone chanzo cha Adamu kupewa Hawa ilikuwa ni kazi_* sass wewe unategea mambo ya Mungu dakika za mwisho umeisha banwa unauhitaji wa mke/mme ndo tunakuona kudeki kanisa, kufagia, ruti za kwa mchugaji kufua, kunyoosha nguo, hizo ni kazi za zima moto, zina lengo la kunasa mtu.
👉 _Jenga tabia ya kupiga kazi ya Mungu kwa moyo wa kumpenda siyo kazi ya kuwinda mtu, hapo utapata mjanja kama wewe anayeigiza._
👉Wewe kijana unaye mtumikia Mungu kwa bidii, ongeza kasi, tumika kwa moyo huduma yoyote, kazi yoyote uliyo na mzigo nayo ifanye kwa huaminifu Mungu lazima akupe msaidizi Sahihi, ukipewa msaidizi ndoa yako itakuwa na amani, ila ukipewa mtu wa kukaa naye maana wote hamna ajenda na mambo ya Mungu, mtatifuana muda si mrefu na itakuwa ndoa isiyo na baraka. ( *_Kauli mbiu yangu ni Piga Kazi Upate Chombo_*)  Usipo piga kazi unapata Mzigo.
✍ Kijana unaanzaje kuoa /kuolewa bila kujiuliza upana na uzito wa maono yako na mtu gani anaweza kuya beba,  _Si kila kijana, binti anaweza beba maono yako, wengine mkioana tu unarudi kuwa mpagani, au unarudi zero kiroho hata kimwili._  Ndiyo maana Kijana Unaonywa sana usithubutu kuokokesha mtu ili muoane, au kuolewa, kuoa mwana dini tu hiyo ndoa mtayumba na hamtakuwa na uwezo wa kupiga hatua za kiroho kwenda mbele. Oana na mtu anaye mpenda Mungu mwenye mzigo na mambo ya Mungu utaenjoy maisha. Tendo tu la kumpenda Mungu sana ni ulinzi wa ndoa yako, mpaka hapo presha za michepuko, vibao hakuna. Maono yako ndo uhai wako yakifa inabidi na wewe ufe, maono ndo yanakufanya uishi.
*_Na nena nawe kijana kama niliye shinda, mi ni shahidi wa maneno haya, jipange kama kijana utamuona Mungu akikutokea, achana na Dhana ya watu kuwa dunia imeharibika, hakuna mabikra, wala vijana walio jitunza, huo ni uongo wa adui, bado akina Yusufu, akina Ev, Elisha, Evelyne(Mama Ev. Elisha walio jitunza wapo) Mungu atakupa sawasawa na uaminifu wako, usi panic, usikate tamaa, mwangalie Bwana atakuletea A pure wife or husband_*
✍ _Mwisho, masomo mengi, mengi yapo Facebook, nitafute kwa jina la Elisha Kazimoto, huko utakuna na pages hizi, Hazina ya Maarifa, Prophet Elisha anointed person, Bado Liko Tumaini Ministry, lakini pia kama unahitaji kujiunga na group langu la Whatsapp la mafundisho ya Mahusiano, Uchumba na ndoa, nitafute whatsapp kwa no hizo hapo juu na chini ya somo, utakuja inbox ufanye Interview ndipo nikuunge, si kila mmoja anaingia Group Hili linaitwa Material Adimu University 🎓 limekuwa faida kwa vijaba wengi, ndoa nyingi, unaweza pata nafasi au ukakosa uwe na amani tu,_
  *Mungu Akubariki tukutane katika uchambuzi mwingine*
_By Ev. Elisha Kazimoto (Baba Eve)_
    *0755444078*

No comments:

Post a Comment