Tuesday, 29 November 2016

MWANAMKE USIACHE NYUMBA YAKO WAZI(PART II)

🌷 🌷 Sehemu ya Pili ya Somo, Mama Usiache Nyumba Yako Wazi🌷🌷
  By Ev. Elisha Kazimoto
      0755444078
1⃣πŸšͺ Chumba cha MawasilianoπŸšͺ
πŸ‘‰� Ni muhimu mama ujue, chumba cha Mawasiliano katika familia yako(Ndoa) ni chumba muhimu, kinacho weza jenga au bomoa ndoa yako. Katika chumba hiki binaangaliwa vitu vifuatavyo:=, πŸ’§ *Unaongeaje na mmeo,(na watu wa nyumbani mwako),πŸ’§Unajibu je unapoulizwa, uwe una furaha au umekwaza unajibu(kauli), πŸ’§Unaulizaje,  πŸ’§Unaombaje kitu kwa mmeo, uwe na furaha au umekwazwa kauli yako inatoka vizuri au la?*
πŸ‘‰� Unahitaji kuwa makini unapowasiliana na mmeo, unatumia ukali?, sauti ya kuvimba? Kuzira? Au unashusha hasira na kuwasikiana vizuri? Kuna wengine wana ndoa wakisha kosana wanageuza watoti kituo cha mawasiliano,  (mfn. _Kamwambie baba yako....., mama yako akija kamwambie......) na wengine wanatumia simu sms tu tena sms kavu haina mvuto_) (  *sms =ninetoka,  mboga hakuna, mtoto anaumwa*)
πŸšͺ Kwa hiyo mama funga mlango wa chumba cha Mawasiliano kwa kutumia lugha safi, ya  upolee, ya mahaba unapo wasikiana na mmeo. Muwe mmekwazana au la usibadili sauti ya kuwasiliana.
*_Mithali 9 : 13 - Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu._*kuwa makini usiwe miongoni mwa wanawake wanao piga kelele kwenye nyumba, utaibomoa, acha kulaumu, laumu, acha majibizano ya kibabe na mmeo, acha kugombana na vyombo ndani kisa umekwazwa, *Usipige Kelele, Zinabomoa Ndoa yako*
2⃣πŸšͺ *Chumba cha Utawala*πŸšͺ
πŸ‘‰� Mama unahitaji kujua kuwa katika nyumba yako, kuna chumba cha Utawala kilicho na Viti viwili, Kiti cha Mtawala(mmeo) na kiti cha Msaidizi/Mtawaliwa(mke-wewe)
_Hata siku moja, usijaribu kukaa kwenye kiti cha mtawala, utaibomoa nyumba yako, mfumo wa utawala uliwekwa na Mungu mwenyewe, usibadirishe mfumo kama unahitaji amani_πŸ‘‡�πŸ‘‡�πŸ‘‡�πŸ‘‡�
*_Mwanzo 3 : 16 - Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala._*
πŸ‘‰� Lazima ujue tabia za mtawala ndo utaufunga mlango wa chumba chako kikawa salama. Tabia za mtawala(mmeo)... *Kusimamia mambo,  Kuonya, Kuzuia jambo, Kuruhusu jambo, Kusikilizwa, Kuheshimiwa, Kuhudumiwa* Ukitaka amani na vicheko timiza Tabia za mtawala(mmeo) ukipindua, au ukaamua kidharau kumbuka tabia hizi si za kidini, kielimu wala kiukoo ni Mungu aliziwela ndani ya mwanaume hivyo ukipindua lazima moto uwakeπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯ ndani ya nyumba. _Linda, funga chumba chako kwa kutimiza matakwa ya mtawala._
3⃣πŸšͺ  *Chumba cha Maombi*πŸšͺ
πŸ‘‰� Kama mama mjenzi na mlinzi, tena mama unaye mjua Mungu, maombi kwako kiwe kipaumbele kwenye maisha yako kwaajili ya kuiweka salama nyumba yako.  _Maombi ni silaa kubwa ya ulinzi,_, kuwa na muda wako wa kuombea mmeo, watoto  na watu waliomo nyumbani mwako. *Kumbuka Ndoa ni taasisi inayowindwa na adui kuliko taasisi yoyote kwenye maisha ya mtu*  kwa nini? _Ukivuruga Ndoa, umevuruva familia, na umevuruva kanisa na ukivuruga kanisa umevuruga Taifa(2Nyakati 7:14) halitafanikiwa suala la Mungu kupinya nchi._πŸ‘‡�πŸ‘‡�
*YEREMIA 9:19-21*
19  *_Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu._*

20  _Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia_.

21   *_Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu._*
πŸ‘‰�πŸ‘†Mama katika maombi yako ndo muda wa kushughurika na mauti za ndoa, migogoro, vijitabia vibovu, majanga ya fedheha, mfano... Miongoni mwa vitu vya kuombea,  *Kataa mauti za ujanani, kwa nini uwe mjane na bado una nguvu? Kwa nini uache watoto wadogo? Siyo mpango wa Mungu, tumepewa miaka 70/80,kataa Ajali ziletazo ulemavu, kwa nini furaha ipotee? Kataa magonjwa ya fedhea na majuto-kupooza, ukichaa, kupoteza nguvu za kiume, kwa nini kuumia? Mlilie Mungu ni mwaminifu mauti yoyote isipande kwenye madirisha ya nyumba yako.*
_Shughurikia vijitabia vya mmeo usivyo penda, kwa watoto na hata kwako, mwambie Mungu niondolee vijitabia vinavyo muudhi mme wangu_
*_Masomo haya, na mengine mengi yanapatikana katika Pages zangu za Facebook, account hizi,  Hazina ya Maarifa na Elisha Anointedman, Prophet Elisha Anointed person, Bado Liko Tumaini Ministry_* Huko utakuta masomo mengi yatakayo kujenga kiroho na kimwili.

No comments:

Post a Comment