Saturday, 15 September 2018

VITA YA KIROHO NA KISAIKOLOJIA

💣💣 *UNAWEZA KUSHINDA VITA YA KIROHO ILA UKASHINDWA VITA YA KISAIKOLOJIA(ENVIRONMENTAL PRESSURE )*💣💣
    *_Na Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078)_*
.......
.......
_Shalom mtumishi wa Bwana,wewe uliyeokoka ni mwana wa ufalme wa Mungu,na ni Askali wa kiroho katika jeshi la Bwana,nakusalimu katika jina la Bwana_
🔫Moyoni mwangu limewekwa neno hili kwa nguvu sana,niseme nawe uliye mtumishi wa Bwana na muhudumu wa Madhabahuni pa Bwana,kwanza wewe ni wa muhimu katika ufalme wa Mungu,pili wewe ni mtu hatari sana katika ufalme wa giza,tatu Vita yako na mawindo yako hayapangwi kireja reja yanakuwa *_Carefully,Systematic Organized_* sijui kama umeelewa, yaani yanakuwa yanaandaliwa kwa Umakini mkuu,na kwa mpangilio maalumu na balaza la kuzimu la shetani.
🔫Unajua kwa nini vita ya mtu wa Mungu,mtumishi wa Mungu aliyesogezwa katika daraja ka kuwa muhudumu wa madhahuni pa Bwana,vita yake inapangwa kimkakati na utulivu wa hali ya juu sana ili kumnasa? *_Ni kwa sababu, Level yako nirahisi Kumshtukia adui yeyote kwa njia zozote na ukamshinda_* kwa mitego yoote ya dhambi,na ukengeufu wowote ni rahisi kuushutukia ukiletwa kwako. _kwa hiyo wewe unaletewa vita ya Kisaikolojia(Environmental Pressure )ambayo inaambata zaidi na *Nature yako/Personality & Character /Mfumo wa mazingira yako* yaathiri saikolojia yako ili ikupelekee Kukosa_
💣Nisikilize nikupitishe kwa watu hawa ambao ilikuwa ni *Vigumu shetani kuwa kosesha,kulingana na viwango vyao vya kumjua Mungu na nafasi zao mbele sa Mungu* ila Adui alitumia Saikolojia (Environmental Pressure )kuwakosesha, si semi kukuvunja moyo,au kuhalalisha kushindwa,ila NAKUTAADHARISHA kama mtumishi wa Bwana,na mtu wa vita ujipange kushinda kote kote kiroho na kisaikolojia. Tuna watumishi wengi Kiroho wako vizuri sana na adui anajua hilo,ila Kisaikolojia ni wadhaifu,kwa hiyo muda wowote faulu inaweza chezwa maishani mwao kupitia saikolojia na mambo mengi yakaenda ndivyo sivyo,hawajatenda dhambi,bado wako na Mungu ila Wamepunguzwa kasi kisaikolojia.
1⃣ *Musa* ni miongoni mwa wanadamu wenye sifa pekee ya kuongea na Mungu *Uso kwa uso* mtu wa aina hii kumkosesha ni vigumu mpaka utumie NATURE( environmental pressure ). Katika upako wake ule ule, *_Aliambiwa na Mungu auambie mwamba utoe maji Israeli wanywe, yeye Akaupiga kwa fimbo mara 2_*
7 Bwana akasema na Musa, akinena,
Hesabu-Numbers 20:7

8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
Hesabu-Numbers 20:8

9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru.
Hesabu-Numbers 20:9

10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
Hesabu-Numbers 20:10

11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.
Hesabu-Numbers 20:11

12 Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.
Hesabu-Numbers 20:12
👉👆Kosa la Kisaikolojia lilifanyika hapa ndo likapelekea kosa la Kiroho kuto mtii Mungu. Sababu ya Musa kupiga Mwamba mara 2 badala ya kuuambia mwamba ni( *Environmental Pressure*) Maudhi ya watu kwenye mazingira,kumbuka wako mwilini(upako wako haukuondoi mwilini,haukufanyi usisikie,usione, ila unaweza kukusaidia kukwepa matokeo yakusika,na kuona)sasa inategemea Unaijuaje saikolojia yako katika mazingira yenye changamoto ndo Uiombee isivurugwe. Kilichofanyika kwa Musa na Haruni ( *Walipata Stress kutoka kwa watu*)Matusi,dharau,kelele tunataka maji,tunataka maji, mmetuleta kutuua, wakati hawa wanaowaongoza wamejitoa muhanga kwa Farao kwaajili yao,wamefanya mambo mengi wakati wako jangwani,lakini bado *_People they are shouting to them as the useless leaders_*  Sasa kutibu Stress yao Musa na Haruni ilibidi ifanyike powerful Reaction, Majibizano yakuonyesha how strong and important they are kwa watu ili Saikolojia zao zikae sawa ndo waendelee na safari. Wakapiga mwamba mara 2 na maji yakatoka,wakanywa, heshima yao ikarudi,wakaonekana katika sura waliyotaka wao waonekane wasidharauliwe,lakini kumbe wakawa wameharibu Destiny  yao. _Kwenye maisha si kila mara utashambuliwa kiroho *Unaweza shambuliwa kisaikolojia ili ukosee kiroho* Kuwa makini na Nature yako ni ipi( Hasira,Kutokubali kushidwa,Mwongeaji sana,Mwoga,nk)vyaweza kukufanya ushambuliwe kisaikolojiana ukakosea kiroho._
2⃣Mtu mwingine ni *Eliya* huyu ni mtu hatari sana katika huduma yake,ni mmoja wa Manabii wenye nguvu aliye mkabili mfalme Ahabu,akafunga mvua isinyeshe kwa muda wa miaka 3.5 na akairuhusu ikanyesha,na akawachinja Manabii wa Bahali 450 mwenyewe. Mtu huyu ni vigumu kumtikisa kiroho, *_Nabii huyu alishambuliwa Kisaikolojia na Mwanamke mmoja, Yezebeli mke wa mfalme Ahabu,kwakumtumia ujumbe kuwa,kesho nakuchinja kama ulivyo chinja manabii wangu 450_* Taarifa hii tu,ilichanganya Eliya kisaikolojia( Hii ni *Environmental Prsussure*)akaamua kukimbia kwa hofu na kujiombea kifo kwa Mungu. Swali,Je, waweza amini mtu aliye mkabili mfalme,kufunga mvua na kuiruhusu,kuchinja manabii 450 peke yake anaweza leo letewa taarifa ya mwanamke kuwa kesho atamuua naye Akakimbia? *Jibu si kwamba hakuwa na Imani, alipata Psychological Attacks* kutoka kwenye mazingira,reaction ikawa ni kuponya roho yake.
1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.
1 Wafalme 19:1

2 Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.
1 Wafalme 19:2

3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
1 Wafalme 19:3

4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.
1 Wafalme 19:4

5 Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule.
1 Wafalme 19:5
👉Shambulio la Kisaikolojia linakupata kama wanadamu wa kawaida, siyo kama mtumishi wa Mungu,likikupata tafakari kabla ya maamuzi yoyote,Tafuta connection kati ya saikolojia yako na Roho yako ndo ufanye maamuzi,ila ukijiona kwakuwa mimi nimeokoka,natumika,ni mtumishi mkubwa,siwezi kushambuliwa kiroho ni kweli we kiroho ni vigumu kushambiliwa, Kisaikolojia je? Maana wee bado ni binadamu kama wengine,unasikia,unaona,unasema,Unaumia,unapenda kama binadamu huko ndo unashambuliwa,fanya maamuzi yako yoyote kwa kutuliza saikolojia yako kwanza Utatenda kwa Busara sana,utashinda vita nyingi mno.
3⃣Mtu wa tatu na mwisho katika ujumbe huu(japo wapo wengi ) ni *YESU KRISTO* Hapa ndipo utaona Ukubwa wa Vita ya Kisaikolojia katika maisha ya watumishi wa Mungu(Tunao simama madhahuni) _Yesu alikuwa mwanadamu kwa asilimia kadhaa,(kwa kuwa aliuvaa mwili huu wetu,na kuishi duniani kama sisi miaka 33)na alikuwa Mungu asilimia kubwa kwa kuwa alikuwepo tangu milele,nakuzaliwa kwake hakukuwa kwa hatua za kibinadamu(Yohana 1:1-5),na Yesu alikuja duniani Akijua kabisa ninakuja kuokoa wanadamu kwa njia ya mateso na kufa msalabani,na kufufuka siku ya 3._ kwa hiyo Yesu kwa lugha nyingine alikuwa anaishi akijua mwanzo na mwisho wake,siyo kama sisi tunaoishi kwa imani tukitazamia mwisho wetu kwa imani,no.... yeye alijua kila hatua,anayopitia,nani atahusika na atakuwaje mpaka mwisho.
👉Yesu huyu huyu(Mwana wa Mungu/Mungu mwenyewe)katika mwili alikutana na *_Shambulio la kwanza la kiroho-akiwa kwenye maombi siku 40_* MATHAYO 4:1-10 Alilipiga kiurahisii kwakuwa lilikuja kiroho naye kiroho ni chuma.
👉Shsmbulio la pili kwa *_Yesu lilikuwa la Kisaikolojia(Hisia za uchungu na mateso)alipo enda kuomba wakati saa inakaribia ya kukamatwa na kuteswa ili atimize kusudi lake, aliogopa,akaomba maombi haya "Baba Ikiwezekana Kikombe hiki kiniepuke...."_* Hapa alikuwa anapambana na Environmental Pressure(Mwili ulikuwa una sense maumivu ya mateso yatakavyo kuwa)Akili ikaanza kusoma kukwepa dhoruba hiyo,....Ila *Yesu alitulia,aka connect Saikolojia yake akairudisha kiroho akapata jibu,papo hapo akabadiri maombi akasema, "Si kama ni takavyo mimi bali mapenzi yako yatimizwe"* 

Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.
Mathayo 26:39

hiyo ndo tofauti ya walioshindwa na akiye shinda.
_Nimalizie kwa kusema watumishi wa Mungu,tupo katika dunia yenye *Pressure kubwa* juu ya sakolojia zetu, katika mwili tulio nao Tumevaa saikolojia ya Hisia(hasira,furaha,uzuni,uchungu na kupenda) Tulia sana,sana katika kufanya maamuzi ya maisha yako popote pale(Ukiroho Hauondoi Nature yako,ila unaweza kukusaidia kufunika Nature yako ukitulia vizuri na kujitambua wewe una React vipi katika changamoto zinazo shambulia maisha yako,status yako,kazi yako,huduma yako,ndoa yako ndo uombe Mungu akusaidie kutulia kabla ya kufanya maamuzi,yawe ya vitendo au ya Maneno,waweza hisi adui anakuandama kumbe uwezo wako wa Ku Control Nature yako wakati wa shambulio la Kisaikolojia ni Mdogo_.
*Mungu akubariki,ukiyajua haya,nyumbani kwako,kwenye ndoa,kazini,kwenye huduma yako utakuwa mtu wa pekee sana.*
Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha kazimoto.

Monday, 10 September 2018

WADADA KUWA SINGLE MOTHER

*Swali: hili limeulizwa lina jibiwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa*
.kumekuwa na wimbi LA mabinti nawaskia wanasema wanataka kuwa single parents, kwba wazae tu watoto wao na wawalee na wasiwe na attachment yoyote ya mume na mke,

1. Je ni kwamba wadada hao hawataki kuolewa
2. Je ni kwamba wanapeda kuolew ila wanaume wanakataa kuwaoa
3. Je wamekosa wa kuwaoa?
4. Je km MTU anahiari kuzaa zao ni kwanini wasiishi pamoja?

Note: walio wengi ni wadada wanaofanya kazi za kuajiriwa au kujiajiri
........................................
*_Ev Elisha Kazimoto,Whatsapp 0755444078_*
*Kwanza hii lugha ya Single Mother ni ya Ushetani,upagani na Ukengeufu*
👉Huu ni uhuni,uasherati wa machukizo kwa Bwana.
👉Unaanzaje kuzaa bila ndoa?, unakusudia kulea mtoto peke yako hivi utamlea katika njia zipi?naye akuwe awe single mother au father? Mungu alikusudia malezi ya baba na mama(mithali 22:6).
👉Suala siyo sababu ya msingi ya kuhitaji kuwa Single mother, shida ni Vijitabia vinavyo chipuka baada ya kuanza kuona Nuru ya Uchumi mzuri na Umaarufu
1⃣Wadada wengi wakisha kuwa na elimu au pesa WANAOTA VIBURI na kujiona wanaweza endesha maisha,hawahitaji kuwa chini ya mtu,wanahitaji uhuru sana,hawahitaji kunyenyekea mtu,(hicho ndo kiburi cha wadada) *_Ndo maana hawataki kuolewa,maana ndoa kanuni yake lazima uwe chini ya mwenzako(mwanamke)_* hutaki kuww chini ya mwenzako Usiolewe.
*_16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Mwanzo 3:16_* wanawake baadhi waliosoma na kuwa na vijisenti hawataki kutawaliwa Wanahitaji watawale kwakuwa wamepata pesa au umaarufu.
👉Angalia wimbi kubwa la *Wadada/Wamama WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI,angalia niwangapi wapo kwenye ndoa,wangapi wanahitaji ndoa,wangapi WAMEWAACHA WAUME ZAO na kuwa Single mother na kujiita MADAM....,hawa watu hawajawahi kuokoka ila WALIOKOKESHWA na mazingira,ila ukija kufatilia kiundani, ni KIBURI kwa waume zao,hawahitaji kutawaliwa,kupangiwa ratiba, wanahitaji waende sawa sawa na umaarufu wao* Wengi waimbaji wanajiita Madam,Single mother, ila ni Vijitabia vyao ndo vimewapelekea kuachika,SIYO USUMBUFU WA WANAUME ila wao ndo wasumbufu. _Hivi wanaume wa waimbaji wote wa nyimbo za injili ndo wasumbufu tu_‼kama hawajaachika,wana mgogoro mkubwa wa ndoa. (Hapa kunahitajika tafakari kubwa siyo kurusha mpira kwa mtu)
👉 *_Ndoa niya watu wawili wenye Akili Timamu_* akisha patikana mmoja mwenye kichaa,inabidi mmoja aongeze uwezo zaidi mara mbili ya mwanzo ili kutuliza kichaa cha mmoja.
2⃣Si kwamba Wanaume wa kuwaoa hawapo wanaume wapo wengi, *Ila wanaume wa kuoa wadada wa type ya tabia zao hawapo* Labda kuwasaidia wadada,wanaume hawaoi Sura,wala shape,wala elimu yako na pesa, wanaoa Mke anayefaa kuishi naye wakatimiza ndoto zao za maisha. Sasa mtu wa kutimiza ndoto za mwenzake lazima awe amejipanga kwa NIDHAMU(Awe na akili timamu)ya kutotanguliza maslahi yake ila ya mwenzake.
3⃣Wanaokubali kuzaa nao hawawezi kuwa walezi, *Mnapaswa kujua kuna watu wanafaa kwa Sex ila si kwa Ndoa, na wengine wanafaa Kwa ndoa ila si sex* ( _Mpaka utafakari sana ndo uelewe sentensi hii ya kisaikolojia_). Kwa hiyo wanaume hawazai nao kwasababu wanahitaji kulea watoto nao ila kwasababu Wanaweza kutimiza Tamaa zao za sex za muda mfupi bure bila kuonga ila kuongwa.
*_Nihitimishe kuwa, wadada wenye mawazo haya na wale mlojichomoa kwa waume zenu mna Laana kubwa ya Matumbo yenu,hampaswi kuwaza kuzaa wala kulea watoto Hamna Maadili ya Kulea_* Msituharibie kizazi cha kesho Rudini kwa Mungu Mfuate neno la Mungu kama mmeamua Kuokoka, kama hamkuamua kuokoka basi jivueni hilo jina la ULOKOLE.
_By Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali - Mithali 17:11)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.

Friday, 7 September 2018

WAIMBAJI NA NDOA

💔💔 *CHANGAMOTO YA WAIMBAJI KATIKA NDOA*💔💔
*_Swali linaulizwa,na linajibiwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali- Mithali 17:11)_*
...........
...........
salaam mwalim wa class

Kabla sjaokoka nilioa baadae nikapata neema ya wokovu mimi na mke wangu
tuumeenda na kuzaa watoto wa 3
maisha yalikua poa tu
teacher kilicho tokea mpaka tumetengana na mke wangu ni hiki

mke wangu ali record albam ya nyimbo 9 tumekua begakwa bega nae
mpaka siku yauzinduzi wa albam yake
ugomvi ulianzia kat yangu na baba mkwe kunitaka nitoe laki7
akidai yeye anagalimia shorting na matangazo kwenye Radio
nika mwambia mzee iyo pesa sina ila ninalak 3 tu akakasilika na kuonda kwa mchungaji wangu nakunisemea nina kibuli simsikilizi
mbaya zaidi anamwambia mchungaj mimi sio type ya kumuoa mtoto wake
mi nimka vumilia mpaka siku ya uzinduz
sasa baada ya uzinduz mke akagomewa kuja kwangu baba mkwe akidai kwa binti kua anakuja kuitajilisha familia yangu
baada ya mwezi mke aliludi akakaa kidogo akarudi tena kwao mpaka leo ajarudi

binti anadai misiwezi kuja kwako wewe umskilizi baba yangu na ulinioa bahat mbaya tu
mi si type yakuolewa nawe

teacher nambie nifanyaje

je pana wokovu kweli apo
maana anaendelea kuimba makanisa mbalimbali

naomba ushauri wako mwalimu wangu

kazi njema😭😭
..................................
..................................
*Anajibu Ev Elisha(Whatsapp 0755444078)*
...................................
*HUYU NI MGONJWA MAHUTUTI, TUFUNGE MADA KWA KUMSAIDIA KIROHO NA KISAIKOLOJIA*
_Kwanza kijana nampa polee kwa changamoto hiyo ya ndoa,Lakini pia nampa polee kwani alikuwa mpagani akaokoka akitegemea akiokoka anatua mizigo,bahati mbaya mke,na mkwe wake wakamtwika nyingine ila Asikate tamaa Bado Liko Tumaini kwa Bwana_
👉Ni seme na mke, kwanza mwanamke huyu amegeuka kuwa miongoni mwa WANAWAKE WAPUMBAVU(MITHALI 14:1) yaani ni miongoni mwa wadada ambao HAWAKUSTAHILI KUOLEWA na mtu yeyote maana,hawajui Thamani ya mume,thamani ya Ndoa,thamani ya Malezi ya watoto(unaachaje watoto walelewe na mzazi mmoja kisa pesa za uzinduzi) na thamani ya Wokovu(Kwa lugha nyingine Huyu mmama ALISHAACHA WOKOVU,NI MPAGANI,HAJUI MAANDIKO,HAJUI MAANA YA HUDUMA ya Madhabahuni.(Tafuta google Semina yangu ya masomo 11,shemu 1 hadi ya 11 kuhusu Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu, Huduma ya Madhabahuni)-By Ev Elisha Kazimoto)andika MATERIAL ADIMU
👉Tendo la kuruhusu moyo wako ufanye maamuzi ya kutoka kwa mme wako bila kufukuzwa,bila ugomvi, kisa ni PESA ZA UZINDUZI WA ALBUM(Huduma)huu siyo Uchanga kiroho ila ni UKENGEUFU WA MOYO.
👉Huduma unayopigania kuifanya,hiyo ni huduma ya 2 kwako, HUDUMA YA KWANZA NI NDOA YAKO(Huyu ni mpagani kabisaa)si kwamba na MUHUKUMU ila ndivyo barua ya Matendo yake inasomwa
*_Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;_*
*2 Wakorintho 3:2*
(Yesu alitwambia tutawatambua kwa Matunda yao)ntawaoa vigezo vya matunda yake.
👉Nimesema huyu mwanamke anamtumikia Mungu gani? Huduma gani anayofanya? Huduma ya kwanza SI UIMBAJI,huduma ya kwanza ni NDOA YAKE.👇👇👇👇
*_34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe._*
*1 Wakorintho 7:34*
👉Mpaka hapo amekwenda kinyume na Neno la Mungu,amekengeuka, Kwa tabia hii anakazi kubwa ya kupenya katika utumishi, ila nikimtafakari kiroho nakuta ameisha Vamiwa na Maroho yanayowashambulia waimbaji( *_Roho za  Kiburi,Roho ya Tamaa ya Pesa,Roho ya Zinaa_) Mpaka hapo viashiria vya hizi roho zote 3 anazo.(NTALETA SOMO LAKE BY EV ELISHA KAZIMOTO)
1⃣ *Kiburi* Tayari anakiburi kikuu biblia imekiita cha Uzima.Yaani kumgomea mmeo na kurudi nyumbani kwenu,kumshtaki kwa mchungaji kisa pesa hazikukamilika laki 7,yeye amepata 3,ni dharau,ni jeuri ni Kiburi kikuu(hapa hakuna unyenyekevu wowote inaousema Biblia wa mke kuwa nao kwa mmewe.

*_Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;_*
*1 Petro 3:1*
👉👆Huyu mwanamke anaweza kumfundisha nini mwanamke mwenye changamoto ya ndoa ambaye mme wake hajaokoka? _Kwanza nachelea kama kati ya hao watoto 3 walozaa kuna wa kike, Anahitaji kuombewa sana maana mama yake amemuharibia SOKO LA KUOLEWA tangu kwenye ulimwengu wa mwili mpaka wa roho.
2⃣ *Tamaa ya Pesa* Hii roho imeisha mvaa tayari,unaweza ona lugha za baba yake ndo za mtoto,baba anasema ukirudi unaenda kuitajirisha familia(yaani wamefanya uimbaji wa huduma kuwa mradi wa biashara)hapo utasema anamtumikia Mungu au anatafuta ugali? na mwanae anakaa HARUDI KWA MMEWE( *Hivi wee mwanamke Umeolewa na Baba yako?*)au ndo tambiko la kuzimu ili utoke kimziki uachane na mme wako ukae na baba yako ndo nyota yako itoke.( _Natamani ujumbe huu umfikie unapozunguka kwenye magroup halafu anitafute ni msaidie, Mauti inamtafuta tena mauti zote ya kiroho tayari alishaanguka bado ya kimwili_) Ndoa ni zaidi ya pesa hizo( *Ka albamu kwanza ni kamoja,anahisi yeye amekuja na upako awafunike watu wenye mafuta ya uimbaji moaka ukitazama sura zao unaona utukufu wa Mungu? Huyu mafuta ni ya magomvi na mafarakano*) Si hitaji kuwa Nabii kwake ila nisemalo ni hili kwa mwendo wake huu,asipo tubu Ataishia ALBUM 1 nayo itakosa soko,kabda ATOE KAFARA KUZIMU WA MWEZESHE ila kwa Mungu ninaye mjua anaye tumia Roho wake mtakatifu kuinua huduma asahau kusonga mbele.
*_Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu._*
*1 Wakorintho 14:33*
👉Kwa hiyo aimbe ila ajue anaimba chini ya uongozi wa *Roho Chafu/roho Mtakafujo siyo Roho Mtakatifu.* wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndiyo wana wa Mungu.(Warumi 8:14)
3⃣ *Roho ya Zinaa* mpaka sasa roho ya zinaa inamwendesha,aidha inamwandaa vema aitumikie au mpaka hivi ninavyoongea NI MZINIFU WA KUTOSHA.( _Sababu ni kwamba,unatoka kwa mme,tendo la ndoa unashiriki wapi,waweza kutoliona lina umuhimu sasa,ila shetani yupo,washawishi wapo,wengineunaowaita mabosi wako,waimbaji wenzako roho ya zinaa inatembea. Ukikutana mwimbaji mwenye pepo kama lako amemuacha mke wake kisa hawaendani wote mtaanza zinaa chafu_)
👉Wewe mwanamke haya maneno ya kwanza Alikuoa kwa bahati mbaya( *yawe yanasemwa nawe au baba yako*)wote wewe na baba yako mnawokovu wa kifafa, Kama ni kwa bahati mbaya jua wewe mke NDO BAHATI MBAYA(TENA MKOSI) na mwanaume alifumbwa macho kuja kwenye Familia ya watu Wanaoolewa kwa Bahati mbaya si kwa mapenzi ya Mungu,kwa lugha nyingine familia yenu mnahitaji maombi ya ukombozi kuwavua huo ubahati mbaya.
👉Nikuulize imekuwaje Umezaa na mmeo watoto 3 Kwa bahati mbaya? Najua SEX YOYOTE UWA INAFANYWA NA WATU WANAOFURAHIA NA KUPANGA ISIPO KUWA YA KUBAKWA.(nina somo langu la sex siya bahati mbaya niya makusudi kabisa masna ina hatua 11,tafuta google somo hilo by Ev Elisha Kazimoto) ilikuwaje hao watoto 3 mkawazaa kwa bahati mbaya?
👉Kabla ya kuanza kuimba hamkuoana kwa bahati mbaya baada ya uzinduzi ukaanza kujiona kwenye screen na mwenzako haonekani ndo ukahisi alikuoa kwa bahati mbaya.‼
👉Aisee na baba yako hakustahili kupewa uzao,ilibidi Mungu afunge tumbo Lake awe tasa *Maana hana uwezo wa Kulea* baada ya kuzalisha watumishi wa Mungu anazalisha vibaraka wa shetani tena kwa makusudi si bahati mbaya.
*_6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee._*
*Mithali 22:6*
👉👆 _Haya maneno yaweza kuwa magumu kwa watu wenye roho nyesi,ila kwa watu wa rohoni hii no tiba,kuna watu wanahitaji Kukaripiwa na kuonywa_

*_Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote._*
*Tito 2:15*

👉Kuna watu wanatuchafulia wokovu inatia uchungu. *WAIMBAJI MNATUPELEKA WAPI MNA NINI LAKINI*
1⃣Single mothers wengi ni waimbaji,si kwamba waume wao wamekufa ila WAMEACHIKA(ninyi mna laana ya Lusifa ila hamjui kuikimbia)
2⃣ Wanaoongoza kwa uzinzi na uasherati waimbaji wenye vi Cd na vi DVD(shida ni nini?)
3⃣Wenye kiburi ni waimbaji(mmemuiga Role model  wenu ibirisi eeh) naye alikuwa mwimbaji hatari.
4⃣Wasiofanya kazi za kuwaingizia vipato ila wanazunguka kanisa hadi kanisa kuimba,kuuuza CD,DVD na kuomba pesa baada ya kuimba eti ya nauli na kutegemezwa ni WAIMBAJI, kwa hiyo huduma imekuwa kitega uchumi? Kafanye kazi za kuwaingizia vipato ndo mtatumika bila kutolea macho kikapu cha sadaka.
👉 *_Ndo maana wengi mnatunga nyimbo za ajabu ajabu,siyo za mwongozo wa Roho mtakatifu,mnatunga za mashabiki_*) Badirika.
👉Nije kwa baba wa huyu mwanamke,sijui kama yeye bado yupo kwenye ndoa,ana mkewe bado au walishaachana,au amekufa,maana hata si msikii mama akitoa kauli kwa mwanae kwamba Rudi kwa mmeo. *_Umri mlio nao kama wazazi hata mpka mkaozesha,mnawajukuu huu ni Umri wa Busara_* yaani ilibidi umfukuze mwanao mwambie karudi kwa mmeo.
👉Eti unamsemelea mkweo kwa mchumgaji eti mkweo HAKUHESHIMU kwa pesa tu ndo hakuheshimu,hujui ndoa ni TAASISI INAYOJITEGEMEA, huna Mamlaka YOYOTE ya kunyoosha mkono wala mdomo kwa Ndoa ya mwanao HATA KIDOGO, sijui imani ya dhehebu lako ni ipi...Biblia imesema MTU ATAMWACHA BABA NA MAMA ATAAMBATANA NA MME WAKE/MME WAKE sasa wee unataka mwanao aambatane nawe?kwani wee ndo mmewe na mme wake ndo mzazi?
👉Umejitafutia Laana baba,maana kinachotenganisha ndoa NI KIFO TU(BIBLIA IMESEMA) sasa wewe ni KIFO?
👉Wazazi ni washauri katika ndoa ya mtoto wao SIYO WAAMUZI, waamuzi ni hao wawili waliooana,nimekerwa na lugha ya (UKIMUOA KWA BAHATI MBAYA),hukupokea Mahari,hukufanya harusi,hata kama walibenana hawakuja kujitambulisha walipokuwa bado wapagani?mzee mbona unaaibisha rika yako na wokovu wako..
👉Unataka mkwe wako Akusikilize,akutii....Maandiko ya wapi,yaani umenyosha mkono umegusa ndoa yake akutii na kukuheshimu TENA AMEKUSTAHI NA AMEOKOKA KWELI ungekutana na Wainjilisti ilibidi Uongozwe sala ya Toba upya na kufundishwa neno la Mungu.
👉Pesa unapanga laki 7 atoe,wee unajua kipato chake,hata ungejua kwani hazina matumizi mengine? Na mwenye jukumu la kuhakikisha pesa inapatikana siyo wewe baba ni ULIMI WA MKE WAKE,kama mke amekuwa Jehuri kisa ka album 1,hata hiyo laki 3 ametoa basi tu kwakuwa ameokoka ila ilibidi hata sh 10 asitoe.Maana huduma inayo bomoa ndoa haipaswi kusapotiwa na watu hata mbingu.
👉Mwisho ni mshauri huyo baba, *_Amwambie mke wake aseme kauli ya mwisho anarudi au harudi,na amuulize baba mkwe wake umeamua kunivunjia ndoa yangu?au unamrudisha mke wangu jibu watakalo toa akubaliane nalo atulie amshukuru Mungu,asimame na Yesu wake huyo mke amemwacha mwenyewe soon huyo mwimbaji mtasikia kaolewa, au ndo walee wanaojiita MADAM( nina somo la Unajiita Madam kumbe kahaba umeshimdwa ndoa tafuta google by Ev Elisha Kazimoto). Wakati ukifika Mungu atakuondolea kikombe hicho mbele huko waweza pewa mke mwingine,ila siyo sasa tulia lea watoto wako_
*_Ukikuwa nami mchambuzi wa masuala ya ndoa na mahusiano, Ev Elisha Kazimoto(MJUMBE MKALI -MITHALI 17:11)_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

Tuesday, 4 September 2018

KULIPA MAHARI KUBWA AU NDOGO

💰💰 *TAFSIRI YA MAHARI KUBWA AU NDOGO KATIKA NDOA*💰💰
_Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Mwanasaikolojia_ *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
.......
.......
*MADA YA MAHARI HII IKO KIJAMII ZAIDI NA KISAIKOLOJIA KWA SEHEMU*
_Labda niseme kwanza, *Kiwango Cha Mahari,Hakitafsiri Thamani ya mwanamke,Tabia yake,Ubora wake na Faida anayo kwenda kuizalisha kwenye Familia yake* Ni mfumo tu ambao familia(Mzazi)ameamua kuuchagua Kujiridhisha Husia zake na moyo wake na mazingira yake ya kiuchumi basi,na uwezo alio nao wa kuitafsiri ndoa ya mtoto wake_
🏓Mahari kubwa,haituonyeshi kuwa huyu binti amelewa kwa *Maadili pekee* ambayo mmewe ataenjoy tangu anamuoa mpaka wanazeeka. Badala yake waweza lioa hata mil 100,na Ng'ombe 100 hata msimalize mwaka mmeisha achana, na mwingine akaleta Kilo 50 za sukari kama shukrani wakaishi kwa amani mpaka uzee na wakawa baraka kwenu wazazi.
👆Unielewe sijasema Mahari ndogo mdo inakupa ndoa ya Amani, mimi nakuonyesha *_Hakuna mahusiano ya mahari kubwa na Ubora wa mwanamke_* Suala linabaki pale pale kuwa Ubora wa mtu unategemea na Yeye binafsi anavyo mjua Mungu.
🏓 *Vijana kuogopa mahari kubwa na kuchelewa kuoa* hizi nisababu Binafsi za Kiuchumi japo yaweza kuwa kichocheo ila siyo sababu ya kimsingi, maana wapo *_Vijana ambao hata akiambiwa Mahari mil 20 haimpi shida,ila nao wanachelewa kuoa_* Shida ni Kumpata mtu Sahii wa kuishi naye Milele mpaka kaburini na Usipoteze Ndoto zako(Hilo ndo linawapa watu shida na kusababisha kuchelewa)
👉Unajua kuna watu *Wanajipenda,wana Vision kubwa* hawahitaji kuvipoteza kirahisi na kujipa stress ya maisha,ukizingatia ndoa ni Mkataba wa Kudumu(wa milele).Uchague vizuri,au vibaya na Excuse.
🏓Lakini wazazi kazima tujiulize kabla ya kupiga mtu mahari, *_Nini tafsiri ya Mahari,je ni shukrani kwako mzazi,ni kifuta jasho,ni kodi,ni mshahara wa kazi uloifanta ya kulea?_* ukijiuliza haya maswali hutaoanga mahari kubwa,isitoshe watu hawajui, *_Mahari yoyote iwe ndogo au kubwa, ukimpiga kijana jua Umemuunganisha na mwanao_* oesa anatoa mme wa mwanao,Akiangaka popote akapata oesa ata akauza gari kale(kama analo)ili kulipa mahari Maisha magumu siyo ya wazazi wa kijana,au kijana peke yake ni ya kijana na mwanao(mke wake)na watoto wao ambao niwajukuu wako.
👉Mbaya zaidi umebana nafasi ya wewe kusaidiwa na wanao (hao familia mpya)kwa viwango vikubwa. Ambapo ungepata dharula ya gari mkwe akaja na binti yako wajakubeba ukaenda kama mfalme,watakoia pesa kukutumha uende kwa daladala au tax ya kukodi.(kwa hiyo *Maumivu ya Mahari kubwa,anaugulia kijana na wewe mzazi*) huna ulicho save.
🏓Binti ni Referee mkubwa awezaye kuweka mambo sawa kuhusu mahari na kijana akalipa kwa wakati bila maumivu.
👉Wadada mnapaswa kujua *_Kutolewa Mahari kubwa Siyo kuthaminiwa,wala kuishi maisha ya kutodharauliwa kwenye ndoa_* Maisha ya ndoa ni kitu kingine,mahari kitu kingine,elimu au uchumi mkubwa wa familia yenu ni kitu kingine. Havina mahusuano na maisha ya amani,furaha na upendo,badala yake anaweza Laaniwa baba yako na mama yako kwa kukuozesha kwa mahari kubwa kumbe ndani we ni USELESS(MITHALI 14:1).
🏓Wewe binti ndo unayeenda kuishi na huyo mme ambaye leo anakamuliwa hadi senti ya mwisho(mnaanza maisha mkiwa hoi,madeni kibao kika kona,na hamuwezi rudi kwa wazazi kuomba wawasaidie muendeshe maisha,utapata faida gani sasa)
👉Ilibidi binti *_Usimame kuwashawishi wazazi mpaka walegeze kwa kiasi ambacho mmeo ataweza kiurahisi_* halafu mkishaoana mnajipanga Kuwahudumia wazazi wenu pande zote kwa ukaribu mkuu.
*_Ni hitimishe hivi,Kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kupanga, Lolote utakalo litamani litaleta majibu,hasi au chanya ila ujue, Mahari kubwa,au ndogo,sherehe kubwa au ndogo Haipimi Ubora na Uzuri wako,ila mwisho wa mzunguko wewe ndo Utaumia na Mwenzako wengine tutabaki na kumbukumbu ukilipiwa mahari mil 15,harusi mil 70,ila maisha ya Amani au Kilio ni yako na Mmeo_*
Mchambuzi wako wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Mwanasaikolojia *Ev Elisha Kazimoto.*
Whatsapp 0755444078

MCHUMBA KUDHARAU HISIA ZAKO

🏓🏓 *KUDHARAU HISIA ZA MWENZAKO*🏓🏓
_Swali limeulizwa refu ila linalenga kujua kama watu wameanzisha mahusian,wkakaa kwa muda,mmoja akajichomo bila sababu za msingi wala kumwambia kiasi,baada ya muda na aliyeachwa akapata mtu maisha yakaenda,baadaye yule aliyemwacha mwenzake anaanza usumbufu wa kumtaka tena warudiane na huku anamtu mwingine tayari utafanyaje_
*Amajibu Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
........
........
*HII MADA INAHITAJI KUITAZAMA KIROHO NA KISAIKOLOJIA*
1⃣Kiroho kama kijana unapaswa kujua mke au mme anatoka kwa Bwana,kumpata unapaswa kujiridhisha kama uliye mpata anatoka kwa Mungu au kwa tamaa yako. Uliye mpata kwa Mungu tumia Gharama zote kumlinda hata itokee changamoto gani.
👉Na unapaswa kujua mahusiano yoyote yakivunjika tafuta ni kwa sababu gani yamevunjika ili ujiridhishe na maamuzi hayo ili usiingie kwenye mahusiano mengine kumbe yule bado anatibiwa na Bwana atarudi tu au uwe huru kuruhusu mahusiano mengine huyo amepita,amekuoa shule ya mahusiano basi.
*Pata somo langu la Break up kwenye mahusiano inaumiza ila ina sababu zake* nenda google (Ev Elisha Kazimoto) au fb kwenye oage zangu (Elisha Kazimoto) au omba kwenye group watu wanalo.
2⃣Kisaikolojia Mtu asiye thamini HISIA ZAKO ana maamuzi ya ovyo,yasiyo zingatia Moyo wako( kama huyo anaamua kukuacha bila sababu, hata kama kuna changamoto au tatizo,hamjazungumza kuona kwa shida hii basi tuachane kwa amani,hamkai kupeana muafaka na mkono wa kwa heri) anakupotezea anaenda huko na huko baadaye anarudi kwa lugha za upole,swali ni ULIPO NIACHA ULINIFUNGIA HAPA NIKUSUBIRIE WEWE? Wewe ndo mwanaume au mwanamke pekee kiasi kwamba unaweza ni Dump halafu muda wowote unao utaka wewe ukaja uka ni Pick😏😏😏.
👉 _Tuelewane haoa kuna mtu anakuja kwako,unasema NO,au haumpi jibu ka ndiyo wala hapana,anaenda huko na huko halafu anarudi huyu hana shida,ika nazungumzia mlioanzisha mahusiano,mmenda muda,miezi 5,mwaka 1 nk,anakupiga chenga kienyeji anapotea,hana mpango na wewe tena,baadaye anajisogeza kukutaka mrudiane huyu ni mbaya kama Ukoma_
Lazima uwe na akili ya kulinda hisia zako,mtu asiye thamini moyo wa mtu katika Love ni Hatari sana kwa Afya yako.
👉Kama lijamaa linakuacha kisa limepata mtu flani kuliko wewe pengine kwa tamaa zake, akienda huko nako anavuruga kwa tabia yake wanaachana anakurudia wewe KAMA KIPORO CHAKE yaani Kisaikolojia hawa TUNAWAPAGA  SENTENSI KALI( *Umehisi mimi ni Cheapest kiasi kwamba sina thamani ya kupenda au kupendwa na mtu mwingine isipokuwa wewe tu?* When you dump a Gold others Pick it Silently.
👉Kama umeishaingia mahusiano mengine usijivurugie mahusiano tulia ba uliye naye, huyu anayeanza usumbufu wa kusema *_Shetani alimpitia_* (kuwa naye makini,urafiki mpaja shetani kwenye safari zake binafsi anaamua kukuoitua umpe Company huyo ni hatari)  just block number yake na utulie na uliye naye. Usianze kuli ganisha watu itakuharibu kisaikolojia.
*Akiweza aombe mahusiano yako yavunjike halafu akae kama miaka 2,ndo umfungulie gate aje kwa unyenyekevu na uhakika kutoka kwa Mungu* usijirahisi kiwepesi hivyo unawezavunja haya,mkarudiana halafu roho ile ikainuka akakuacha tena,au mkaoana naye Asikuthamini,nikama umeokotwa hukuwa na mtu wa kukushika mkono kama asingekuwa yeye Kurudi.
*_Mchambuzi wako Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078

Monday, 3 September 2018

NJIA YA MUNGU KUKUONYESHA MCHUMBA

❣❣ *NJIA YA KUJIBIWA MCHUMBA*❣❣
*_Swali limeulizwa hapa chini,na Anajibu Mwanasaikolojia na mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
......
......
*Kuna swali lilitaka kujua njia zipi Mungu anaweza tumia kumjibu mtu aliyeomba mke au mme*
👉Kwanza,hapa tuwekane sawa watu wote vijana kwa mabinti. *_Vijana wengi wanapenda kujibiwa na Mungu wakati wakitafuta mchumba,labda niwape Experience ya kiroho, Suala la Mungu kutumia njia yoyote kumjibu mtu Linategemea Mahusiano ya Kiroho aliyo nayo yeye na Mungu_* si kwa sababu umeamua kufunga na kuomba siku 21 eti unamshawishi Mungu akujibu unaweza ukaenda hata 40 na Usijibiwe au usijue kama umejibiwa na Mungu.
👉Shida ni kwamba  vijana wengi wakati wa maisha yao ya kawaida kabla ya kuingia katika uhitaji mkubwa wa ndoa wanakuwa hawana mpango na Mungu,hawana maombi,hawana utakatifu,hawafanyi kazi ya Mungu kwa bidii, ila uhitaji ukiingia ndo wanaanza kubadiri gia ya kumshawishi Mungu,sasa mara nyingi Mungu Hafanyiwi maigizo kama wanadamu inabidi kama ni maombi yawe ndo maisha yako,utakatifu uwe ndo maisha yako,kutumika iwe ndo maisha yako.
*_Biblia imeweka wazi Nature ya Mungu,ukiwa na maisha ya kumpotezea Mungu wakati hauna shida,ukifika wakati wa shida yako naye atakupotezea_* Hujawai kufunga kuombea kanisa,kazi ya Mungu,maisha yako ya kiroho na kujua namna gani Mungu anajibu unasubiri *Kufunga wakati wa Kutafuta mke au mme* Unahisi utajibiwaje?
24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
Mithali 1:24

25 Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu;
Mithali 1:25

26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
Mithali 1:26

27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
Mithali 1:27

28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
Mithali 1:28

👆Kijana unahitaji kujipanga mapema sana kuwa na tabia ya kuwasiliana na Mungu ili kujua *_Wewe kama wewe Mungu anapendelea kukujibu kwa njia gani?_* kila mmoja ana njia kubwa,lango la kuongelea na Mungu,kupokea taarifa za Mungu.
👉 Ila vijana wengi wamekalili kuwa njia ya *_Kuonyeshwa mke au mme ni NDOTO/MAONO_* ndo lugha za vijana karibu wote Utasikia NIKAOTA,NIMEONYESHWA hii njia shetani ameisha wachungulia wengi amewapiga kwa wake bandia na waume bandia kwa KUITA NDOTO.
👉Mungu anazo njia nyingi za kusema na watu wake kuwajulisha,kuwapa taarifa ya kinachoendelea au kujibu maombi yako, JAMBO KUBWA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU YAKOJE mpaka Akuheshimu na Kukujibu? Mungu hatumii njia moja ziko nyingi.
14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
Ayubu 33:14

15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Ayubu 33:15

16 Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
Ayubu 33:16

17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;
Ayubu 33:17

👆Usikalili jiweke katika Position ya kumsikia Mungu kwa njia nyingi ila Ukimzoea Mungu atakupa YOUR CHANNEL (Njia yako maalumu)yakumsikia.
1⃣Mungu anaweza tumia watu kukupa jibu lako(watu wakawaida)unahutaji kuwa na maarifa ya kiroho na macho na masikio ya kiroho kujua huyu mtu katumiwa na Mungu kunijibu ombi langu hata yeye bila kujua.
2⃣Mungu anaweza tumia Watumishi wake(Wahudumu wa Madhabahuni)wakapewa jibu lako wazi au wakatumiwa bila kujua.
3⃣Mungu anaweza tumia Amani ya Moyo juu ya mtu au jambo(kuiruhusu amani au kuifunga amani)uwe makini kuielewa amani ya Mungu na amani ya nafsi yako(Amani ya Mungu haina conditions za matamanio)
4⃣Mungu anaweza tumia Neno lake kukupa mwanga sifa,na njia ya majibu yako.
5⃣Mungu anaweza tumia Maono kukujibu(maono huwa wazi na clear)
6⃣Mungu anaweza kutumia Ndoto kukujibu(ndoto zinakuwa na mafumbo flani unaitaji kuomba zaidi kujua tafsiri yake.
_Hizo ni baadhi ya njia unazoweza pewa jibu lako,njia zote zinahitaji uwe vizuri na Mungu na ujizoeze kumsikiliza Mungu_
*Ulikuwa nami katika uchambuzi Mwanasaikolojia na mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078

UKABILA KATIKA NDOA

💈💈 *UKABILA KATIKA NDOA*💈💈
*Swali* _Kuna watu,vijana au familia kukataa kuolewa au kuoa kabila flani na kutaka kabila flani hili lina maana gani na umuhimu gani katika ndoa?_
*Anajibu Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
.......
.......
.......

_Hii ni mtazamo wa Kijamii,ambao ni mapokeo ya wazee wetu yaliyo lenga kujenga Koo na tamaduni moja za watu wanaoelewana katika Mila na Desturi_
👉Tangu enzi hizo za mababu zetu ndoa haikuwa haki ya mtu binafsi anayeoa au kuolewa,ila ilikuwa ni haki ya Kifamilia(wazazi),ndiyo maana Wazazi ndo walio husika na kumtafutia Kijana wao mke kutoka katika familia waliyoipenda na waliyo hisi inatabia njema,marafiki,na malezi mazuri ya binti au kijana lakini wanaendana kitamaduni/kimila,na kijana au binti hakuruhusiwa kubisha,kukataa mchumba huyo,na wazazi pia walihusika na Kumlipia kijana Mahari.
👉Mfumo huu ulilenga kulinda (Family Species ) mfumo huu umetoka katika BIBLIA ambapo Mungu aliagiza watu waoane ndani ya kabila lao,ndo maana unamuona Rebecca anamwagiza Yakobo ujombani ndo aende akachukue mke kule kwa Labani, Isaka pia, na wana wote wa Israeli waliagizwa Wasioe nje ya Kabila lao.(Taifa lao)
👉Utofauti wa Kabila ulitafsiriwa utaleta utofauti wa mila na desturi jambo litakalo pelekea Kuingiza mambo mapya kama Kuabudu miungu mingine na kutoa kafara kama za watoto,kupitisha watoto kwenye moto ambayo ni machukizo kwa Mungu wa Israeli. Ili kulinda mahusiano yao na Mungu iliwabidi waoane wao kwa wao..
👉Tabia hii imeendelea mpaka tamaduni zote za dunia wanapenda kuoana wao kwa wao ili kukinda mila na Desturi zao.
.....
.....
....
*Uchambuzi unae delea angalia zama hizi kiroho na kimwili kwa nini kuna mwingiliano wa makabila* Uko na Ev Elisha Kazimoto
👉Kijamii kwa sasa mambo yamebadirika sana na miiko ya mababu imefutika aidha kwasababu mbalimbali ikiwemo...
1.Maendeleo ya kijamii(Utandawazi)ambapo kumekuwa na mwingiliano wa jamii,kabila,taifa kila kona kiasi kwamba mipaka ya kiutamaduni imefutika,kulingana na watu kuwa pamoja katika kazi,shule,biashara na nyumba za ibada hii imeleta utamaduni sawa wa pamoja na watu kuanza kutamaniana na kuelewana na kuona waweza ishi pamoja.
2.Wazee wa zamani wamepungua walioshika mila na desturi na kuwaridhisha watoto wao,kwa sasa watu wanaendesha familia kulingana na mchakato na kasi ya nchi,na elimu walizopata.
3.Suala la Utumwa(Colonization )kwa jamii za Kiafrika limeathiri mifumo mingi ya kijamii na tamaduni zetu.
4.Mwingiliano wa jamii na watu unaoletwa na biashara,elimu,siasa na dini umeondoa mipaka ya kulimda tamaduni husika. Ndiyo maana ndoa sasa haifuati kabila inafuata level ya mwimgilianao na kuelewana baina ya watu wawili(ndo utamaduni wao)
👉 *_Kibiblia Kabila linamaanisha nini kwa sasa na linazingatiwaje katika ndoa?_* _Hili ni swali la msingi kwa sasa, Kwa watu waliookoka Bado Maadili ya Ndoa kwa mujibu wa Kuzingatia Kabila Upo palepale..Wooote waliokoka Tumezaliwa katika Familia ya Kristo kwa Neno na kwa Roho wa MUNGU kupitia Damu ya Yesu Kristo tuna share Common blood group ya Yesu(Ufunuo 5:9-10, Yohana 1:11-12, 1Yohana 5:1-10, 1Petro 2:9-10) kwa kutaja machache baada ya kuwa katika Kristo sasa tunakuwa na sifa zifuatazo._
1.Kabila la Watakatifu
2.Taifa la wana wa Mungu walioitwa kwa jina la Bwana.
👉Sisi tunaagizwa Kuoana watu wa Kabila moja ili kulinda utamaduni wetu wa(Ibada mbele za Mungu wetu, utakatifu wa maisha ya mwili na roho,utumishi wa madhabahuni pa Bwana)
👉Kuoana na mtu asiyeookoka ni Kuoa nje ya Kabila lako ambapo utaingiza mambo mageni katika kabila la watakatifu wa Mungu jambo ambalo hakimpendezi Mungu(utavuruga utamaduni wa ibada,utumishi na utakatifu).
👉Kwa kijana aliyeokoka yeyote awe binti au kijana wa kiume.... *_Anacho zingatia Ni Kuoana na Kabila la Watakatifu kutoka Taifa la Wana wa Mungu_* siyo makabila ya kijamii haya kwetu hayana nguvu,ndo maana tunapo okoka Utu wetu wa Kale unabadirishwa ikiwemo mila na desturi zisizo faa,ukorofi, vyote vinamezwa tunakuwa wapya watu wenye Utamaduni mmoja wa Utakatifu.
👉Wengi wanaogopa kabila flani wanatelekeza wake, wanaua waume,wana ukahaba,hawa wakorofi,wagomvi,nk....Jambo ambalo kwa waliookoka Hayo yote ni Marufuku na tumeyaacha tumegeuzwa na kuvikwa utu mpya tabia mpya,biblia inasema sisi tuwe Wanana(wapole),magomvi,uasherati na uchafu wote tumeambiwa visitajwe kwetu na mambo mengi yakumfanya mtu kuwa mwema, sasa utaogopa nini tena? *_Sisi tunachoogopa ni Kuoana na mtu ambaye utu wake wa ndani haujageuzwa hapo ndo majanga tabia zote za Asili anazo na zinamwendesha hapo ndo  utakoma kama umeoana naye_*
Kwa kuhitimisha niseme Suala la Ukabila katika ndoa,watu wasio na viwango vizuri vya Kiroho ndo vinawapa shida,kuogopa kabila hili au lile...Ukweli ni kwamba Makabila Yoote yana Ubovu wake na Uzuri wake,hakuna kabila la kusimama likajisifu kuwa hilo ni kabila Perfect,ila tunatofautiana matatizo basi...Kabila liliokamilika ni la Watakatifu kutoka Taifa la wana wa Mungu basi.
👉Watu wenye uwezo,vijana waliookoka vizuri suala la kabila,elimu,uchumi siyo kipaumbele kwao maana hivi ni nyongeza katika CV kubwa inayo hitajika kwa mme au mke na vinatolewa na Mungu mda wowote. Ndiyo maana Binti yule uliye mkataa kuwa hana pesa wala kazi nzuri unamkuta ndo ana Bonge la ndoa na maisha SUPER,na wewe ulotafuta Pesa kabla ya mapenzi ya Mungu unalia na pesa zako wala huzifaidi nazo zimeisha,ulitafuta Elimu nzuri huifuarahii,ulitafuta kabila zuri ukasahau Kabila la Watakatifu,ndo sasa unachanganyikiwa mwenzako haeleweki,wengine wanatafuta wazungu au waafrika wa nchi flani yaani hataki aoane na Mtanzania au mkenya mwenzake, umeacha kutafuta Taifabla Wana wa Mungu sasa unataka Talaka ukae peke yako hizo ndo athari za Kuwa Shallow kiroho,ila walio na uwezo kiroho wanajua mambo yote ya Mwilini mafanikio yanatoka kwa Baba wa mbinguni aliye Yote katika Yote wanjua muda wowote maisha yao yaweza badirishwa kikubwa wakae CONNECTED NA MUNGU hilo ndo jambo kubwa.
*_NB: Unajua Adamu alikuwa kabila gani na Hawa alikuwa kabila gani,unatafuta wa kufanana nawe katika kusudi la Mungu_*
    By Ev Elisha Kazimoto(whatsapp 0755444078)