Tuesday, 31 October 2017

FAIDA YA SEX

*FAIDA ZA SEX YA MARA KWA MARA NI KWAWANANDOA TU,KWAKO KIJANA NI SUMU KUBWA HATA KUDUMBUKIA MARA MOJA*

_Kwanza niondoe dhana ambayo hasa vijana wa kiume na wakike uitumia kuji defend ili wafanye sex au michezo ya sex, kwa kisingizio kwamba ukikaa muda mrefu bila ku sex kuna matatizo makubwa kama kupata shida za kiafya au tatizo la ugonjwa wa chekelea *Hili ni pepo la ngono, Mungu hakuumba watu wajichafue kabla ya muda wake ili kuepuka chekelea na magonjwa ya kubuni.* Suala ni Kijana kukaa na Mungu vizuri na kuwa na muda na mambo ya Mungu na kuwa busy na shughuli zako,mwili wako utakaa sawa, binti hutavamiwa na vimapepo vya kuchekelea na kutamani ngono_.

*KWA WANA NDOA*
👉🏾Kwa waliooana sex ni kitu kimoja muhimu sana kwa watu walio couple kina faida zake muhimu kisaikolojia katuka kuijenga ndoa ikawa imara sana.
1.Sex kisaikolojia inafungua nafsi za wanandoa na kuruhusu furaha
2.Sex inapunguza au kuondoa stress(msongo wa mawazo)
3.Sex inaufanya mwili kuwa mwepesi
4.Sex inatuliza akili na kumfanya mtu kufanya shughuli zake kwa umakini bila kukosea kosea(hasa wale wa ofisini,wana mahesabu,wanaofanya kazi za typing, na wanao hudunia wateja)
5.Sex unamfanya mtu kuwa na uso wa furaha(welcoming face)
6.Sex inawaungamisha wana ndoa kinafsi(kuaminiana na kupendana).
7.Sex ina leta heshima na kujaliana kati ya wana ndoa ikifanywa kwa ubora.

*MADHARA*
👉🏾Kana mtaifanya mara kwa mara ila pasipo ufundi, mtaichoka, mtaumizana,mtatamani kutoifanya kwa muda mrefu.
👉🏾Kwa mwanaume ni kuchoka mwili,maana inahitaji nguvu.
*NB: _Sex ina madhara machache kwa watu washamba wanaoikurupukia madhara ni marefu, ila ushauri huwa ni huu jaina haja ya mara kwa mara kila siku,kila siku wakati mpo wote milele, hata chakula kutamu ukikila kila siku mnakichoka,ila uzuri wake uko palepale, pia wanaume hushauriwa kila mechi,usifunge mabao zaidi ya 3 kiafya, kumbuka bao kutoka ni nguvu kubwa unachomoa, (ndo maana biblia ikasema usimoe nguvu zako kahaba). Kama itakuwa mara kwa mara basi funga bao 1,2.. Kwa kadri mnavyo sex mara kwa mara nguvu ya kupakua maya ili ufunge bao usogea nyuma mupungua, ndo maana mtu aliye kaa mwezi,1,2,3 bila kusex na yule ambaye kwa wiki ni mara 5, mkianza pamoja kusex yule wa maea 5 kwa wiki atachelewa sana kufunga goli la 1, ila wa miez 2,3 hata dk3 haziishi ameisha funga goli la 1_*
Sex inafaida kwa waba ndoa kwa mabachela inakongoroa nafsi,moyo,akili hata sura na kukuzalishia hatia. Tulia ufikiwe kwenye foleni yako.

By Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078

Monday, 23 October 2017

KUHUDUMIANA KIUCHUMI WACHUMBA

*Swali. Katika process za uchumba kuelekea ndoa ni sahihi kijana wa kiume kumuomba binti pesa au akopeshwe na binti?*

ANAJIBU: Ev Elisha Kazimoto(Mwanasaikolojia)
*WhatsApp 0755444078*
_Niweke bayana dhana ya uchumba kisaikolojia ndo tupate mwanga wa kujibu swali hiki kwa ufasaha_
✍ Neno *Mchumba/Wachumba*  _Ni mtu au watu wa jinsia ya kike na kiume walio katika mahusiano ya kati,ya maridhiano ya kuoana na kuishi pamoja kama mke na mme, waliozungatia vigezo vifuatavyo_:-
1⃣ Wamependana kwa hiyari upendo wa kuwa mtu mke na mtu mme, upendo *Tosherevu* (Selective & Specific Love) yaani umechagua kati ya wengi,umebaini huyu tu ndo anafaa na h as. una mwingine. ( *_Kama unatafuta,una mtu hujafikia kiwango hiki cha upendo, Kisaikoljia ni marufuku kumwita mchumba_*)
2⃣ Mmefuata taratibu za kiroho(kidini) au kifamilia za kuonyesha ridhaa ya wazazi au walezi wa pande zote mbili kuridhia mchakato wenu wa uchumba kuanza.( *_Ikiwemo barua ya posa,utambulisho kwa familia, kwa mchungaji(kwa wakristo),kulipa maali, kuvishana pete za uchumba nk_*)
3⃣ kupima afya zenu kwa madhehebu yenye taratibu za kupima
✍Mambo hayo yakizingatiwa ndiyo msingi wa uchumba wenye *_Mwelekeo wa ndoa_* kinacho baki ni Akili ya mtu binafsi aliyeko kwenye mahusiano kumsona mwenzake kufahamu ni mtu wa aina gani, ni mkweli ki kiasi gani,ni muwazi kiasi gani, vision yake iko imara kiasi gani, present action yake hiw it define future life, hiyo ni akili binafsi ya mahusiano ya kisaikolojia kubaini kama mtu ni tapeli,mtu sahii,nk(  *_kwa ufupi uchumba una terminology 2 tu, Muda wa Kumsoma mwenzako tabia na Muda wa Maandalizi ya harusi_*)
✍  Kwakuanza kujibu swali letu: _Suala la Kuhudumiana kama wachumba ni jambo jema na muhimu kwa watu walio serious kama vigezo tajwa hapo juu, ila akili,uangalifu na kiasi vizingatiwe iki kuepusha maumivu ya moyo.( Katika mambo yote Akilini mwako inabidi ujue *Uchumba Si Ndoa muda wowote ikiwepo sababu kubwa ya msingi unavunjika*) kwa hiyo mambo yote mnayo yafanya iwe kusaidiana,kufabta maendeleo uwe na taadhari akilini.
✍ *Kuhusu kijana kumkopa binti* Si suala la kukopa tu,hata binti kumuhudumia kijana kimavazi,kipesa,kumfungulia miradi nk, kama mme we mtarajiwa haina ubaya *_Inategemea kiwango cha Akili alocho nacho msichana, na anavoona mwenendo wa mahusiano yao na hali halisi ya kiuchumi ya kijana_* tafsiri zingine za kujishusha,unapoteza heshima, nk inategemea mitazamo yenu na nia yenu ya mahusiano ni dhana potofu kama wasemavyo wengine, *kuoa mke msomi kukuzidi,mwenye cheo kukuzidi,nk utadharauliwa* ni ufinyo wa akili ya mahusiano kisaikolojia maana Upendo wa ndoa *Never deal with Envirimental issues but Internal & unconditional issues* yaani moyo wako umempenda kwa sifa za ndani na si ana nini kwa nje hiyo ndo tunaiita REAL LOVE. Kwa mazingira hayo badala ya kumkopa utamsaidia tu,  maana ni kwa manufaa yenu( Ustawi wake ni ustawi wako)
✍ NB: Kisaikolojia kulingana na ongezeko la usanii, kushuka kwa akili( ongezeko la watu walovurugwa kisiasa,kijamii,kiuchumi,kiroho nk, tunashauri umakini uwepo sana katika kuhudumiana, wengine wamegeuza mahusiano kama mradi wa kuendesha maisha,na kusababisha majeraha mengi kwa wapenzi wao. Ndiyi maana tunanema hudumianeni watu wenye akili,umemsoma mwenzio kiasi kikubwa na watu mlo katika uchumba kama vigezo pale juu siyo uchumba wa WhatsApp ,Instagram na fb na wa uchochoroni, wa kuiyana wachunba na kupeaba promises kibao,hata wazazi hawa mfahamu ,hata barua ya posa haipo, ndo unajitundika kumfungulia duka,isafiri,unaenda bank kukopa unampa mkopo wako,my friend utapata ugonjwa wa kisaikolojia wa kuwachukia watu wa jinsia yake milele pale atakapo kusaliti na ku break relationship. Kumbe wewe ndo ulitumia akili fupi kuendesha mahusiano.
Quote: *_Katika kuanza mahusiano Kijana akili yake huwa juu sana,na ya msichana ushuka sana(anapoteza akili kiasi flani), na mkioana mwana mke anaongezeka akili, mwanaume anapoteza akili kiasi flani_* (Kuwa Makini na Mahusiano is not simple as you think)
*Imeandaliwa na Msaikolojia na Mshauri, mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa. Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)*
WhatsApp 0755444078

Saturday, 21 October 2017

ZINAA SIYA BAHATI MBAYA

*Swali : UMEJIENGAGE  KWENYE UHUSIANO NA MTU AMBAYE SURELY UNAJUA NI MTU KUTOKA KWA MUNGU NA NDIVYO ILIVYO THEN KATIKA KUWA KATIKA MAHUSIANO MKAJIKUTA KATIKA DHAMBI YA KUFORNICATE JE NINI KIFANYIKE KUNUSURU MAHUSIANO YENU NA HAMTAKI KUACHANA BADO MNAPENDANA SANA SANA*.

_Majibu mafupi kutoka kwa Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
*Toba ya zinaa inagharama kubwa kama ilivyo gharama kufanya zinaa* kabla hujafanya zinaa kuna hatua ngumu,na za makusudi watu wanazipitia,na ndo maana kwa Tafsiri yangu ya kiroho,kisaikolojia,na kimwili *Hakunaga suala la Ninejikuta nimezini, yaani bahati mbaya nimeanguka kwenye zinaa* hakuna kitu cha namna hiyo kwa zinaa, isipo kuwa *Mtu aliye vamiwa ghafla na kundi la watu,au mtu mwenye nguvu, akambaka* na hapo uwe umeonyesha jitihasa za kumshinda,amekushimda nguvu,siyo amekukanata kidogo unarusharusha tu mikono na miguu halafu unatulia aendelee, hiyo ni *Umejibaka*
*ONA HATUA ZA ZINAA NDO UTAJUA SIYO YA BAHATI MBAYA AU KUJIKUTA* Ili ukienda kutubu,usifikiri nikitoa sadaka Mungu ananisamehe fasta,aliye kwambia Mungu ni kama TRA kuwa na uchu na sadaka yako nani,kwanza anasema sadaka ya mwenye dhambi ni chukizo kwake *Inanuka* na watu wamejidanganya,anasheratika,anakimbia kutoa sadaka,nakujikopa anajikopa atoe hata laki 1,hiyo ni hewa,hata baraka hakuna, mwingine eti anafunga 3 kavu chumbani anatubu hiyo umefanya ila bado hujaigusa zinaa.
1⃣ Unamshawishi mtu,na kumfanyia kila likilo zuri,ili mradi akuweke akilini mwake(uibue hisia zake za ngono)
2⃣ Unamuomba au kumtengenezea mazingira kumuonyesha unahitaji ngono(unalazimisha asome hisia zako na kukubaliana nazo)
3⃣Mnapanga eneo la kukutana lisiwe la wazi(mnahakikisha hakuna wa kuwaona wala kuwasumbua mpaja mmalize yote)
4⃣Mnakutana na kuanza kupandishana hisia za mwili kwa kufanya vitendo vya kupasha miili joto la zinaa(mpaka hapo umejikuta tu,yaani hujui?)
5⃣Mnaamua kuziba macho ya aibu, unaondoa nguo ya juu(aibu ya kawaida)
6⃣Mnaondoa nguo ya kati ndogo(aibu ya kati)
7⃣ mnaondoa nguo ya ndani 👙aibu kubwa(mpaka hapo unajikuta eeh)
8⃣Mnaamua kujiweka mlalo mzuri ili mpate raha ya kina,miguu na mikono na macho vinashiriki kutafuta pozi zuri la penetration of .....(bado wewe hujui,umejikuta)
9⃣ Unaanza in and out na kujiliza unajiliza,na wewe maneno ya mahaba yote yanakutoka(bado uko kwenye bahati mbaya!) Tapeli mkubwa wewe,unamdanganya nani kuwa umejikuta.
1⃣0⃣ Una ejaculate, bado ni bahati mbaya
1⃣1⃣ Unamaliza round 1,unaenda second selection mpaka 3,au unaishia na moja, (bado ni bahati mbaya) muhuni mkubwa wewe
1⃣2⃣ Mnamaliza,mnajipanguza ma uchafu yenu(bado nibahati mbaya)hujielewi wewe
1⃣3⃣ Mnavaa nguo ya kwanza hadi ya mwisho,mnatoka kwa interval ya muda eneo mlilo kubaliana kukutana(halafu unasema bahati mbaya)jambazi mkubwa wewe
1⃣4⃣ Unafika nyumbani unampigia simu kama amefika salama(bado tu mmejikuta mmeanguka) wee umelaaniwa kabisa.
*_Uongo huo hata shetani mwenyewe hajawahi kuutunga_*
_Usiwadanganye watu,sema matamaa yamenipelekesha nikaona niyape yanachokihitaji, na hili ngazi zote hizi 14 ziporomoke kwa toba,kaianike dhambi hiyo wazi kwa watumishi wa Mungu wakuombee na wakushauri la kufanya,wewe huji la kufanya *Maana wewe ni marehemu tayari* marehemu atafungaje,atatoaje sadaka? Nenda wakufufue kwanza ndo ujue la kufanya.
*Ev Elisha Kazimoto*(Sii entertain dhambi,wala kuipaka mafuta)
WhatsApp 0755444078

UMUHIMU WA HONEYMOON

*Mada mpya*

*Kuna ulazima gani kufanyia honeymoon gest/hotel na si nyumbani imakaaje hii..utamaduni huo ni mzuri...kuna maandiko yasaport hii...vitu gani vinafanyika huko saidi ya sex..ntafurahi kupata majibu.*

ANAJIBU: EV ELISHA KAZIMOTO
*WhatsApp 0755444078*
_Hapa kwanza niweke vizuri mtazamo wa swali kabla ya kushughulikia hoja Potofu ambazo huwa watu wanazijenga kuingiza hisia zao kwenye hoja huru_
👉 *_Kuhusu ulazima wa kwenda Honeymoon kwa mabibi harusi baada ya kufunga ndoa, HAKUNA ULAZIMA( maana yake Ukienda hakuna shida,usipoenda hakuna shida, kitu kikisha kuwa na ulazima maana yake kisipo fanyika hivo kuna athari kubwa)sasa hapa hakuna ulazima ILA KUNA UMUHIMU WW KISAIKOLOJIA NA KIJAMII(Umuhimu maana yake,jambo hilo lapendeza likifanyika hivyo maana kuna vitu vitafanikiwa, ila hata isipo fanyika hakuna athari ila kuna vitu vitakosekana, huo ndo umuhimu)_*
👉Kwa Habari za *Maandiko ya neno la Mungu kuthibitisha ulazima au kutokubalika, HAKUNA ANDIKO/FUNDISHO HILO ila itategemea mtazamo na tafsiri binafsi ya mtu na msimamo wake* ila kuna Falsafa za kisaikolojia
👉Kuhusu kuwa *Utamaduni huu ni mzuri au mbaya, hii inategemea na mwono wa mtu binafsi* kisaikolojia  _Uzuri au ubaya uwa katika macho ya mtu binafsi na si katika kitu chenyewe, tafsiri yako na mwono wako ndo unaotafsiri ubaya na Uzuri wa kitu_
✍ Baada ya kuwela vizuri Dhana 3 za swali, sasa niingie kuuzungumzia honeymoon na maharusi.
*HONEYMOON (Eneo la mapumziko kwa maharusi baada ya kufunga ndoa) Guest au Hotel* ni maeneo ambayo maharusi uchagua kwenda kwa mapumziko kwa siku zozote zile 1,2,5,10 kulingana na uwezo wao,matashi yao, au Budget ya Kamati ya Harusi. Kwa nini watu waende Honeymoon hotel/guest baada ya kufunga ndoa?  *Ziko sababu kadhaa za kisaikolojia na kijamii( hakuna sababu za kiroho kama ilivyo, mkiamua kwenda nyumbani kwa bwana harusi,hakuna sababu za kiroho ila sababu za kijamii)*
1⃣Kutafuta Faragha(Maala tulivu,pasipo na mwingiliano wa sura za wenyeji).
_Sababu hii ni muhimu kwa mazingira ya watu ambao wanaoana ndo mara yao ya kwanza kujutana kimwili(Mabikira) kuna changamoto nyingi za watu mabikira kukutana kimwili siku za mwanzoni, (kwa wana wake,kisaikolojia ni watu wanao jali sana privacy sanaa katika sex kuliko wanaume), mwanamke ili afanye sex kwa uhuru na ajiachie na aifurahie,hupenda kujihakikishia USIRI, ukimya,( sasa kulingana na maisha,kuna watu wanaoa wapo kwenye nyumba za kupanga,au nyumba zao ila hazina uhuru, kisaikolojia ni makosa makubwa kufanya rendo la ndoa kwa kujiiba,kujibana,kujishtukia uwepo wa watu,au kusikiwa. Ndiyo naana Hotelini au guest inakupa uhuru wa kujiachia kihisia._
2⃣ *Sababu ya Mapumziko ya Kisaikolojia* Harakati za harusi na mapambano ya harusi huchosha mwili na akili, ndiyo maana watu hupenda kutafuta sehemu tulivu,mazingira mapya ambayo hayata kudai kuyaweka sawa tena ila tu ,uke,unywe na upumzike, bila mwingiliano na mtu yeyote na maeneo hayo niya hotel au guest, nyumbani hakuna utulivu, mnafunga ndoa tu, wapo watu wanakaa hapo kwako ndugu,jamaa wengine wanakuja kusalimia kesho yake haluna utulivu unaohitajika kwa watu wapya. Guest au Hotel mnakuwa na muda wa kutulia kutathimini na kupongezana mwa safari yote ya mwaka 1,2,3 5... Bila usumbufu wa mtu yeyote.
*NIWEKE BAYANA DHANA CHACHE POTOFU ZINAZOIBULIWA*
👉 *_Dhana ya Kuacha baraka za ndoa Guest/ hotekini badara ya Nyumbani_*  _Hii ni dhana dhaifu kwa watu dhaifu kiroho. Baraka siyo mchanga au jasho,au kimiminika kwamba vikimwagika tunaviacha kule, baraka zinabebwa katika mionyo kwa imani na si katika nguo. Kama unahisi maombi unayoombewa ya harusi yanakaa kwenye suti na shera na ngozini, wewe huna tofauti na mbeba irizi,ila bado mchanga kiroho. Kumbuka hauendi hotelini kuzini,kwamba unarnda kuanguka, unaenda kwa mapumziko na tendo halali na takatifu._
👉 *Dhana ya Kuzoa mapepo* Hii ni dhana ya watu wasiokomaa kiimani, kuna maeneo mengi kila kona,kuanzia njiani,shule,vhuoni,sokoni na hewani,mapepo yanakaa ila wana wa Mungu tunaishi na tunatembea huko na kule bila kuvaliwa na mapepo, kama unahisi hotelini ndo kuna mapepo, bado ufahamu wako wa kujua ulimwengu wa roho wa giza na wa nuru unafanyeje kazi zake uko chini sana. Mapepo yanavaa Nafsi wazi isiyo na Mungu,au dhaifu kwa imani au yenye dhambi,popote pale,shambani,njiani nk.
👉 *Dhana ya Guest/ Hoteli kuna uchafu mwingi unafanyika* hii ni dhana ya mtu mwenye ufahamu mfupi,karibu kila kitu kina uchafu, unajua Daladala(mabasi) kuna unachafu mwingi,kuanzia wa ukahaba mpaka wa kimatambiko? Unajua nguo hiyo ya mtumba unayoivaa alivaa kahaba nani au mtu mwenye mapepo gani? Ofisini unako fanya kazi unajua seat hizo zimekaliwa kwa shuguli gani? Labda niseme huu ni uchanga wa kiroho. *swali la msingi: Ukisafiri uwa unaenda na kitanda chako? Guest au hoteli unaenda kulalia nini? Au wahubiri wanapo kodishiwa hoteli,guest huwa wanaenda na vitanda vyao! Hujui sisi tubapokanyaga tunanguvu ya kumiliki na kupatawala,panatakaswa kwa matumizi yetu? Isingekuwa hivo kuna vitu vingi tungeviacha, ilibidi tumiliki vya kwetu popote duniani.*
_Ndo maana katika maombi ya Yesu akaombea wanafunzi wake,kwamba Baba siombi uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu_
👉 *Dhana ya Kuharibu pesa* Hii ni Dhana ya Akili ya kiumaskini na mtu maskini, Pesa haitakuja kutosha au kuingezeka kama haitumiwi,kujibana siyo kutajirika ila mpangilio wa maisha na malengo.
✅ Aina ya harusi yako ndo inatoa picha uende wapi,hivi unajua pesa ya honeymoon inatoka kwenye Kamati ya harusi ambayo ni michango ya watu ya harusi ambayo si pesa yako ya kuanzia maisha
👉Lakini dhana hii ya umaskini imezifanya ndoa za walokole watu wajiitao wa rohoni *Kuchuja* tangu mnaoana hakuna zawadi za surprised wala kutoka out, january mpaka December ni ndani kisa, eti kutumia laki 1 kwa out, au laki 3,si bora ufanye maendeleo🤔🤔, maendeleo gani yanayozidi kuendeleza furaha na shangwe ya ndoa?.
*MY TAKE* _Kama mtazamo wako haupo katika kutumua pesa ili ije nyingine, tulia,ila wenye mawazo ya kuongezeka na kufanikiwa,wabatumia Pesa kujenga saikolojia zao ili wafanye maendeleo kwa utulivu wa kifikira. Tangu umebana pesa umewahi kufanya kitu gani cha kutishia watu wanaotumia pesa kujenga saikolojia zao? Mbona maisha yakawaida, usiishi kwa kujibana ukingojea kutajirika kutoka hewani, mafanikio ni pamoja na kuwa na saikolojia iliyo huru na kufunguka._
*_Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)_*
WhatsApp 0755444078

KISS KWA WACHUMBA

*Habari ndugu zangu*

*_Nina swali nalo ni...Je ni makosa kwa wapenzi kubusiana (kumbusu mwenzake)?_*

Anajibu: Ev Elisha Kazimoto (Baba Evan)
*WhatsApp* 0755444078

*_Katika swali hili, lugha iliyo tumika ni lugha tata (Ambiguity ), MPENZI( Mpenzi kwa maana ya watu walio katika mahusiano ya kimapenzi-wanaoshiriki sex? Au Mpenzi kwa maana ya mtu uliyenaye katika mahusiano anaoupendeza moyo wako(mpenzi-mchumba).?_*
Kwa namna yoyote ile nitoe taswira halisi, *Kama ni suala la Mpenzi, mnaoshiriki sex, busu yoyote haina shida, simple au deep kiss haina shida,maana sex ni more than kiss* (Angalizo kwa watu waliookoka,wana wa Mungu HATUNA MSAMIATI WA MPENZI wa sex, HATUNA MCHUMBA wa sex)
Kwa habari ya mchumba kuna vitu tunaviita *_Maadili ya Uchumba kwa watu waliookoka_* hapa ndipo tunapo tofautiana kati ya wachumba wapagani, wachumba wana dini,nawachumba watakatifu(waliookoka) *MAADILI NI PAMOJA NA:
1⃣ Kulinda Ushuhuda katika kipindi cha uchumba chote, msilete tafsiri itakayo fanya watu wawaone hamjaokoka(epuka kulitukanisha jina la Yesu kwa mwenendo,tabia yenu nk.
2⃣ Kuto fanya mambo yanayoweza chochea kwa kasi hisia za miiki yenu na kuwafanya muanguke kwenye dhambi ya zinaa( mfn, sex touching,sex plays,Kisses, hasa deep kiss, hug hasa Zero distance hug (hug ya dk 1,2,5,10...mnatafuta nini)🤔🤔
3⃣Kuto kutana kwenye mazingira ya uficho yanayoweza kuwaingiza katika vishawishi vya zinaa.
*KISS & HUG*
_Kiss na hug havina ubaya wowote,wala dhambi yoyote, suala nia yenu ya kiss na hug ni nini? Je mko huru kukiss na ku hug publically? Au mpaka muwe wa 2 tu?_
Kuna dhana na mwavuli wa kiss takatifu.... Huu ni uongo ni utumiaji wa maandiko vibaya kutimiza mahitaji ya kiihisia. Kiss takatifu haitofautiani kwa jinsia zote(ndo mtume Paul aliisema) sasa kama kaja yako,dada yako,mama,bibi, mchungaji wako mana mchungaji wako na mshirika wowote waweza mpa kiss hiyo hiyo unayotaka kumpa mchumba  wako basi hiyo ndo busu takatifu kwa watakatifu wote
Kinachoongelewa na vijana wasasa kuhusu kiss siyo kiss wanaongelea ROMANCE ila wanapunguza makali kwa kuiita kiss, hivyo si jambo jema kwa wachumba wakiroho kuromance(deep kiss) mnachokitafuta si ku express love, ila mna express sex feelings zitakazo wagharimu katika safari yenu.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*

Wednesday, 11 October 2017

SEX NA KUFUNGA NA HUDUMA

*TENDO LA NDOA NA MFUNGO*
Swali: Je, Ni Sahii kushiriki tendo la ndoa mkiwa kwenye mfungo wa maombi, au unakiandaa kwenda ibadani kuhudumu.?

*Anajibu Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
_Kwanza niweke sawa dhana na tafsiri ya tendo la ndoa kwa wana ndoa. *Tendo la ndoa kwa wana ndoa ni Safi, na Takatifu, na huru kwa wana ndoa muda wowote ili mradi wamekubaliana na kwa utaratibu*_  na hiyo ni kwa mujibu wa neno la Mungu.👇👇👇👇👇
*1Wakorintho 7:1-5*


1 Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. 

2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. 

3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 

4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. 

5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 
✍ Inabidi tujue jambo moja, hakuna unajisi wowote,ubaya wowote katika tendo la ndoa, hizo ni imani potofu na misimamo binafsi si ya Neno la Mungu. *Uharamu wa tendo la ndoa,na Muda wake ni kwa watu wasiyo wana ndoa, ila kwa wanandoa ni Safi,Ruksa muda wowote* Dhana za Huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa siku ya ibada, au kama unaenda kufanya huduma, kusimama madhabahuni, huu ni ushetani, ni upotofu, ni huujumu wa ndoa, ni kuwafunga watu kongwa lisilo la haki. *_Alicho kibariki Mungu,utakihitaje kimelaaniwa? Mwanzo 1:28_* Mungu alilibariki tendo la ndoa na hakuliwekea majira wala nyakati za kuli attend,iwe asubuhi, mchana,usiku, usiku wa manane, free enjoy wana ndoa, unaenda kuimbisha saa 9 mchana, unahitaji kuburudika na kutuliza saikolojia yako hata saa 7 zimua, it's your property, zingatia tu utaratibu,muda wako na Mungu na muda wako na mpendwa wako. Ni muhubiri unaenda kuhubiri mkutano wa nje,una wife wako umemuhitaji mchana, Enjoy your blessings, wee ndo unajua muda uloutenga na Mungu na wako na mke wako. *Tendo la ndoa halina Limitation ya Kibiblia kwa wana ndoa* lavda ushauri na mawazo tu ya mtazamo na mapendekezo kulingana na hali ya mazingira,kitu ambacho siyo kanuni wala sheria.
*Tendo la Ndoa na Kufunga* _Nahisi wana ndoa wanajua nitakacho eleza hapa, kwa vijana wanaweza wasijue, Tendo la ndoa si kama kunywa chai,kuchovya mkate kwenye chai, *Ile ni Kazi Ngumu japo ni Enjoyment* ila inahitaji nguvu za ugali, muscular. *Ogopa kazi inayo toa jasho mtu* hiyo siyo mchezo mchezo.
✍Tendo la ndoa kulifanya linahitaji nguvu,uwe umeshiba,uwe na joto lawili ndo itaisimamisha misuli ya *Fimbo ya ufalme*,au mama ndo utahimili mapigo.
✍Tendo la ndoa linahitaji akili safi iliyo tulia,yenye oxygen ya kutosha ili kuibua hisia za sex, *_Sasa mtu aliye funga, ana njaa,akili inachoka,oxygen imepungua,lakini joto la mwili limeshuka, nguvi hana za kusimamisha fimbo muda mrefu kwa sababu ya chakula mwilini hakuna_* kwa sababu hiyo tendo la ndoa litakiwa gumu. Tena afadhali kidogo kwa Mwanamke anapokea,ila mwanaume anaye toa, one goal uchovu wake ni kama mwendo wa alotembea more than 5 km kwa miguu.
✍ *_Kama umefunga una nguvu za kusukuma mzigo na isikupe shida kuchoka, hakuna unajisi ingia kazini. Hivi ni vitu vilivyo barikiwa,sasa ukiokoka kupita maelezo kila kitu unakiita dhambi, kumbusu mkeo siku 6a j2 dhambi, ku sex siku ya ibada dhambi, acheni kutengeneza dhambi, Tendo la ndoa kwa mwana ndoa halina unajisi kwa siku wala muda._* Alivyo vitakasa Bwana wewe usiviite najisi, vitu vyote ni safi kwa walio safi,ila ni najisi kwa walio najisi.👇👇👇👇
*Tito 1 : 15 - Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.*
✍Mwisho ushauri wangu na taadhari yangu, tusitumie utashi wetu usio na fact za kibiblia kuonyesha kosa au dhambi, tutumie ujuzi,experience na neno la Mungu kiwaonyesha watu ukweli wa mambo.
NB: Tendo la ndoa lonahitaji utulivu, maandalizi, nguvu na muda mzuri na kuridhishana, lisifanyike kwa kukimbia kimbia au kumridhisha mtu mmoja,mnapo lifanya,muwe mmefunga,mnaenda ibadani,au mmetoka ibadani hakikisheni ni kwa furaha yenu wote na kufurahi wote pamoja.
*_Ulikuwa na mchambuzi wa masuala ya kisaikolojia na kiroho katika mahusiano na ndoa, Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)_*
WhatsApp 0755444078

Tuesday, 10 October 2017

AGANO LA UBIKIRA

*SWALI*: Bwana Yesu asifiwe.
*Ninaomba kujua kuna nguvu gani ya kiagano ktk bikira ya mwanamke.*

Au kuna agano gani alilonalo mwanamke ktk mwili wake km agano la mwanamke au mtoto wa kiume kutahiriwa baada ya siku nane kuzaliwa.

*Anajibu Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 07554440708.
_Kwanza naona muuliza swali ameuliza maswali mawili lakini yote yana dhana moja ya Agano la damu,kote kwa pnde mbili, kwa jinsia ya kike na kiume_
✍ *Agano ni nini kwanza* _Ni maridhiano,makubaliano baina ya pande mbili kwa sababu maalumu za kiupendo,kisheria,kimalengo._
✍ Agano laweza kuwa la maneno, viapo vya maneno,la uhai wa mtu,mnyama,ndege nk na la damu.
✍ Mara nyingi, *_Agano la Damu lina nguvu kubwa kuliko agano lolote,maana ni agano la uhai, (katika damu ndimo kulimo uhai)_* na Mungu tangu mwanzo alitumia agano ili la damu kwa watu wake, na shetani anapenda kulitumia kwa kuwa kuna nguvu ya uhai ambayo ndo maisha ya mwanadamu.
*Kutoka 24 : 8 - Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.*
✍ *Nianze na suala la Bikira kwa mwanamke* _ Bikira kwa mwanamke ni Alama ya Uaminifu wake kwa mume wake, ni Agano la mwili kati yake na mume wake(mwanaume).
✍Na Bikira ilikusudiwa iwe agano la mwanamke na mume wake,siyo na mume mwingine.👇👇👇👇👇
*Kumbukumbu la Torati 22 : 17 - angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji.*
_Ubikira ulifatiliwa kwa ukaribu mno,na kuweka mavazi(mashuka)kuthibitisha kama mwanadada huyu alikuwa bikira au la,na mavazi yele yalipelekwa kwa wazee wa mji kuwaonyesha huyu alikuwa bikira.
✍Katika ubikira ndimo kulimo damu,damu ndiyo agano la kuungwa na mume huyo( Labda ni semee kwanza kuhusu tendo la ndoa, Lile tendo lina kazi ya kumuunganisha mtu na mwenzie kihisia, & kimwili, na alama ya *_Agano la kuunganishwa ni Bikira na Nguvu ya Agano hilo la kuunganishwa Katika ndoa ni Damu ya Ubikira_*  (Sex inakuunga na mtu huyo mnaye sex)
👇👇👇👇👇👇👇
*1 Wakorintho 6 : 16 - Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.* Ndiyo maana likaitwa Tendo la Ndoa, watu maalumu,ili likuunge na alokuchagua Bwana,siyo ujiunganishe na kila mtu,ilikusudiwa uungwe na mmeo au mkeo.
Na Agano hilo lilikuwa ni kwa faida ya wana ndoa kwani Ubikira kwa mume na mke, _Ni Ishara ya Uaminifu, Uvumilivu, Upendo, Heshima katika ndoa_.👇👇👇👇
*Mambo ya Walawi 21 : 13 - Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.*
✍Ulitakiwa umwoe mwanamke katika ubikira wake, kulikuwa na maana kubwa na umuhimu mkubwa wa kuunganishwa na mtu mwenye Alama na Nguvu ya Agano la mwili. Japo wengi wa watu wa leo wamelichukulia kiurahisi suala la Ubikira, ndiyo maana na ndoa nyingi zinachangamoto kubwa sana ,fujo na vurugu, kuna vitu vinakosekana vya kiagano, vinavyo imarisha agano.
✍  Kufunga ndoa kuna agano la maneno lina tumika, ila Alama na Agano hilo huwa ni pete, na Nguvu ya Agano lake la mwili kwa mwanaume ni Ubikira. *_Sasa ondoa mtazamo finyo, na wa kujitetea kwa udhaifu wako, kuwa mbona ziko ndoa nyingi za waliooana bikira ila zina changoto nyingi kuliko za waliooana bikira hakuna, huo ni mtazamo finyu, wala hilo Halibadirishi formula ya Kimungu ya kuufanya ubikira uwe agano la ndoa_*
✍ _Kwa sababu hii niwatake wadada wote ambao hawajaolewa na bado wana sifa hii ya ubikira tafadhari tunza na bado nguvu ile ipo kwenye ulimwengu wa roho na kinatenda kazi. *Tunza Bikira* uliye poteza kwa kutojua, enzi za ujinga, au kwa kujua yaani ukiwa katika wokovu, hakikisha unakuwa mwaminifu katika maisha yako yote ya ujana Mungu atakutokea kwa njia nyingine._ Tafuta somo langu linalosema *Uzaliwa wa kwanza, part 1,3 & 3*
✍ *Suala la Kutahiriwa* hili nalo lilikuwa ishara ya agano kati ya watu na Mungu, agani nalo hili liba nguvu ya damu,au alama ya damu.( Hili ni Agano la mwili)👇👇👇👇
*Mwanzo 17 : 13 - Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.*
Lakini hili liliashira Usafi, Agano hili lililenga kuobyesha usafi wa watu wa Mungu kwa hiyo katika agano la kale Israeli walilifatilia sana. Tendo hilo hilo lilifanywa na YESU kwa kumwaga damu na kututahiri mioyo yetu(Tohara ilihusisha kuondoa magovi ya miili ya mwanaume(katika uume) kama ishara ya usafi,damu ilimwagika. Baada ya Kifo cha Msalama cha Yesu kila amwaminiye tayari anatahiriwa roho yake, govi la dhambi la roho linavuliwa na damu ile ile ya msalaba inakuwa imetumika kama utakaso.👇👇👇👇
*Wakolosai 2 : 11 - Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.*
✍ Sasa baada ya kuokoka, au kwa waliookoka *Tohara/Kutahiriwa* kimwili(govi la uume) halipo kiroho tema kimaagano, limebaki kiwa ni tendo la *Kiafya/ Sayansi* ila halina mahusiano tena ya kiroho.👇👇👇👇
*1 Wakorintho 7 : 19 - Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu.*
_Kwa sababu hii niwashauri watu wote wamama kwa wababa, kutafuta kutahiriwa mioyo yao maana kuna magovi ya dhambi zao,na humo ndo kuna agano takatifu la damu ya YESU lililo imara na la milele. Kwa kuhitimisha, Tuulinde ubikira wetu ambao ni Uzaliwa wa kwanza(Malimbuko ya miili yetu na roho zetu) ili tuyapate yale mema yaliyowekwa katika ubikira(limbuko)_
*_Ulikuwa na Mchambuzi wa masuala ya Kimahusiano na Ndoa Kisaikolojia na Kiroho_*
         EV ELISHA KAZIMOTO
WhatsApp 0755444078

Monday, 2 October 2017

AINA ZA MAWASILIANO YA WACHUMBA

*MAWASILIANO KATIKA UCHUMBA*
_Mahusiano ni nguvu ya kisaikolojia inayo vuta hisia na moyo wa mtu juu ya partner wake. Mahusiano hai,imara huwa kuna nguvu inayo chochea hisia,ambapo mtu huwa radhi kusema chochote na kufanya chochote kwa partner wake ili mradi amridhishe,na kumfurahisha partner wake. Hiyo ndo Saikolojia ya Mahusiano_
✍Nature ya mahusiano ni kwa kila mtu,awe ameokoka,mchungaji,nabii,mtume nk wote nguvu ni moja ya mahusiano, ila tofauti ni kwamba, *Mtu aliye okoka,aliye na Roho mtakatifu,hofu ya Mungu, Neno la Mungu,anajua katika mambo yote ya kimaisha, kunahitajika KIASI na hekima ya kulinda Ushuhuda na Utakatifu wenu* kwa maana hiyo nguvu ya saikolojia uwekwa sawa.
✍Kuna vitu vya kutofautisha, *_Mawasiliano ya sms, call au live ya kimahaba, na ya Kiupendo_* mawasiliano kwa mchumba wako yanayo lenga kufunua uchi,kutimiza hisia za ngono, kumfanya mtu atamani kutimiziwa kiu ya ngono, hayo ndo mabaya na makosa kwa wachumba WALIOOKOKA,ila kwa wapagani ni kawaidaa hawana mipaka,ila watapata shida ya kisaikolijia ya kuonjwa na kuachwa.
✍Ukweli ni kwamba unapokuwa na mchumba( Expected Wife,or Husband )mawasiliano yenu,ni tofauti naunavyowasiliana na mtu mwingine *_Na ndivyo inavyo hitajika, onyesha kupenda, onyesha kumjali,onyesha kuwa wa pekee,_* lugha za upendo, kama kumsifia alivyo mzuri, unavyo mpenda, nk,lugha za upendo, sasa usichanganye lugha za mahaba ya ngono na upendo, mambo ya *Umelala na nguo au uchi?, umevaa under wear gani? Maziwa yako yakoje, umbo la sehemu za siri likoje, njoo tulale wote, nikumbatie hapa nina baridi nk,hizo si lugha za upendo ni za mahaba,nazo uibua hisia za mwili,jambo ambalo upelekea kuingia katika zinaa kabla ya ndoa,au kujichua baada ya mazungumzo,na hiyo ndo athari zake* kujikinga tumia Lugha za upendo siyo za mahaba kwa mchumba wako, mkioana, tumia zote, moto ukipanda mna uhuru wa kuuzima na hakuna dhambi wala kuhukumiwa.
*By Ev Elisha Kazimoto*(0755444078)