🍇 *MWANA DADA ALIYESOKONI NA NI BIDHAA ADIMU*🍇🍇
_Huu ni Ujumbe wangu Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa_
🍇Mdada aliyesokoni ni yule anaye *Jitambua kuwa ni Mdada wa Kutafutwa* hii Siri weeengi inawashinda Kabisa kabisa, wadada wanaingia kwenye nafasi ya *Kutafuta badala ya Kutafutwa* hapa unaweza maliza miongo hata 4, 4.5 huja fanikiwa kupata mme.
👉Mdada anayejua yeye ni Bidhaa Adimu inayotafutwa, *Anajipanga kutafutwa* anaishi maisha ya kutafutwa, na huyo akipatikana na watafutaji *Aachiwi,achezewi wana wahi kushugulikia hatua zote awe Queen of the house* aachwi muda wa uchumba, wala kuchezewa.
*_Sifa za Mdada Adimu aliyejipanga Kutafutwa_*
🎁Maisha yake Ameyawekeza Kwa Mungu. ( _Huyu ni mdada amchaye Bwana,anajikita na mambo ya Mungu, amejiapiza kuishi maisha matakatifu na kujitenga na dhambi, Ratiba zake nyingi ni za Kiroho, kusoma Biblia,Maombi,Ibada,Huduma na utumishi mwingine wa nyumba ya Mungu_) Binti huyo anatafutwa sana maana watafutaji wanajua moyo wa huyo unamilikiwa na Mungu,majanga hayatakuwepo kwenye ndoa.
🎁Hajirahisishi kwa wanaume,ila anawapima wanaume, ( _Hana pressure ya kuolewa kiasi kwamba kila kijana anayekuja anahisi ni mwokozi wake amekuja kumwondolea aibu...Ila yeye anapima huyu aliyekuja amekuja kwa Mkono wa Bwana au wa Tamaa zake au shetani ili kuniangusha?_)kama ni kwa mkono wa Bwana anaitafuta amani ya (Kristo na Kusudi la Mungu juu ya aliye kuja huku akiyasoma maisha ya kijana ni mtakatifu au ni
mwigizaji)
🎁Anaye jishugulisha kuyamudu maisha yake ili moyo wake usinaswe na watoa zawadi ili waharibu maisha ya wadada.( _Mdada wa aina hii hakai nyumbani na kusubiri wa kumbariki au kumpa vizawadi ndo atokelezee, hapa utakuwa na mahusiano hata 10 na utaanza utapeli. Mdada Adimu anasoma mazingira yake anaanza kujishugulisha na vitu vya kuingiza kipato hata kama ni kidogo lakini anauwezo wa kumudu mahitaji madogo madogo ya kila siku huyu dada anatafutwa sana maana atakuwa msaada wa familia akiolewa si Mzigo_)
🎁Kauli zake ni Kauli za Staha( _Mdada mwenye uwezo wa kukubali kwa adabu na kumkataa mtu kwa adabu ndo bidhaa adimu, wengi wanaponzwa na mdomo wanajifanya kuwa rohoni sana, kwa wale wasiowapenda wakiwa approach wanawajibu majibu ya mkato,ya dharau,ya matusi kiasi kwamba kijana anamshukuru Mungu kwa wewe kukataa maana kama una majibu mabovu hayo hujaolewa,ukiolewa mkakwazana ndo utatukana mpaka basi_) Kinywa chako kifanye kiwe na Nidhamu ya kupendeka.
🎁Mdada asiye tumia Mahusiano kama *Chanzo cha Mapato yake*( _Kuna wadada wanageuza mahusiano kama kitega uchumi au Saccos yao ya maendeleo, huwa wavulana wao hawawaambii ila wanaumia na wanawasema kwa wenzao kuwa mchumba wake *Ni Chuma Ulete* kila kitu,kila siku ni pesa,pesa....Jiulize kama usingekuwa kwenye mahusiano ungekuwa unatunzwa na nani? Lakini kuhudumiwa ni upendo wa kutoa kama zawadi siyo Madai, mdada ambaye anaweza kukaa kwenye mahusiano hadai kutunzwa,kuhudumiwa,mpaka mkaka mwenyewe ndo anaamua kukuhudumia,huwa wana sifa kubwa na si rahisi kuachwa,ila hata yeye mdada anaweza mtafutia zawadi mkaka wake hawa ni Adimu_) Wadada wengi ni Mchwa,wanakulaa wee ili wakiachwa waseme bora nilikula vitu vyake.
🎁Mdada anayechukia NGONO kabla ya ndoa( _Wadada wenye msimamo kwenye mahusiano ya kutovuliwa nguo,kunyonywa ndimi(Romance),kuchezewa mwili wao(sexual plays,kushikwa maziwa,sehemu za siri nk)mpaka unakuwa wet unatamani umalizie kabisa sex ila basi tu, mdada ambaye hata akitishiwa kuachwa kama hatakubali sex yuko tayari kuachwa, huyo mdada Ni bidhaa Adimu_) Wengi wa wadada wamejirahisisha sana mahusiano hayaishi,hawaingii kwa ndoa wakiwa na siri kwa wachumba zao,wanakuwa wamezoeleka miili yao si mara 1,4,10.
*_Hiyo ni Hekima zangu kwako dada, ukizingatia utatafutwa na ukipatikana uachwi njiani mpaka ndoa_*
By Ev Elisha(whatsapp 0755444078)
Monday, 12 November 2018
WADADA WALIO ADIMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment