Friday, 23 November 2018

KUACHANA NA UMPENDAYE

🎁🎁 *Swali Muhimu la Kimahusiano:* _Hivi ufanye nini au utafanyaje kama mmependana na mtu(dada/kaka)mkiwa mnajiandaa kuanza michakato ya uchumba na ndoa, MUNGU akwambia HUYU SIYE MTU SAHII KWAKO muachane. *Unafanyaje*_🎁🎁
.......
.......
_Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)_

*Nihitimishe Mada hii kwa kusema mambo kama 3 hapa la kiroho na kisaikolojia na kimwili*
👉Kuanzisha mahusiano inaweza kuwa rahisi sana  maana unakuwa juu ya Hisia na nguvu ya furaha, ila kuvunja mahusiano ni kazi kubwa na gharama kubwa kwa maana *_Unakuwa chini ya Hisia na maumivu ya moyo_*
👉Kuanzisha mahusiano ni kujiongezea *Stability of mind* ila kuvunja mahusiano ni kujiongezea *Stress and Depression of heart*
👉Kwa msingi huo ni muhimu sana kutulia unapoenda kuanzisha mahusiano na mtu. Maana kuna kuhitimisha mahusiano kwa furaha( *Kuungana*) au kumaliza kwa Stress( *Kuacha au kuachwa*)
👉Katika mahusiano ni *Heri kuachwa kuliko Kuacha* anayeachwa anaulinzi wa kihisia, anayeacha anaongeza wingi wa wasiwasi kihisia.( _Anayeacha lazima aunde sababu za kutosheleza maamuzi yake ambazo baadaye kama si sahihi zaweza mgharimu katika mahusiano mengine au ndoa,ila anaye achwa anabaki na sababu moja tu nimesalitiwa nina haki_)
👉 *Nijibu swali sasa* Kumuacha mtu unaye mpenda ni kazi Kisaikolojia,ila kiroho ni kazi ndogo.
🥦Kama wote mliopendana mnamjua Mungu vizuri,haina sababu ya kuogopa ni kuitana mkakaa mkaambiana sisi tunapendana,ili tungie katika ndoa takatifu,na ndoa ni kusudi la Mungu,sasa kama *Hakuna amani kwa mmoja wetu,basi tujipe muda wa kuomba kuuliza amani hii inayopotea inamaanisha nini* wote mshugulikie hilo mpaka mpate jibu,ndo muagane kwa upendo na kuombeana kila mmoja Mungu ampe mtu wake.
🥦Suala la mtu mmoja kufanya maamuzi ya kuvunja mahusiano eti Kisa *SIJISIKII AMANI MOYONI JUU YA MAHUSIANO HAYA NI UTAPELI NA UHUNI MKUBWA* kwa nini? *_Wakati unaanza mahusiano hukulazimishwa, na pengine ulienda mbali na kusema Hakika nasikia Amani sana juu yako,nakupenda,nahisi hakuna mwingine kama wewe,namshukuru Mungu kunipa mtu kama wewe_* hayo yote uliyatoa kwenye Amani gani, ya nafsi yako,ya macho yako, au ya Kristo? Sasa kwakuwa ukimwaminisha mwenzako kuwa wa mpenda kwakuwa unaamani kuu Basi mkae tena muombe mdhibitishe hiyo hali ya amani kupotea
👉Maana kuna watu amani inapotea kwasababu zifuatazo:
🥦Walikurupuka kusema huyu ndiye kabla ya kujua Mungu karidhia au la( *Kwa tamaa zake*)
🥦Baada ya kuona Maslahi anayo tegemea huwenda hayatatimia akiwa na huyo( *Hofu ya maisha hasa kiuchumi*)
🥦Ushawishi wa marafiki,au wazazi kuhusu huyo mtu kuwa hakufai.
🥦Matarajio makubwa,lakini unaona madogo katika mahusiano
✍Kuanzisha mahusiano mapya kwa siri huku ukiwa na mtu mwingine( Huleta utata wa kujua nani ni chaguo sahihi...na lazima mmoja atavuta sana kuliko mwingine moyoni mwako)mmoja ataanza kupoteza sifa na amani juu yake itapotea.
*_Hayo mambo ndo watu uanza kusema sina Amani na mahusiano yetu,nakuanza kutafuta gia za kupiga chenga_* hapo si busara,busara kabla hamjaenda mbali,humtaki mtu mwambie mapema mkubaliane muachane kwa amani na si kiuadui.
👉Kuna wengine ambao Nature yao ni *_Ni ku hold wakaka au wadada tu,kula hela zao,muda wao,vitu vyao au kuwatumia kimwili,wakiwa hawana malengo nao, wakiona wenzao wamekazana,wanania ya Kuingia kwenye ndoa, ndipo huanza lugha za SINA AMANI MOYONI, wakiogopa hatua inayofuata ni Aidha kulipa mahari,kupelekwa kwa mchungaji au wazazi kutambulishwa,sasa anajiwahi kuvunja mahusiano kwa kisingizio cha sina Amani_* huu utapeli si mzuri.
🥦Rai yangu ya mwisho Kuvunja mahusiano si Ugomvi wala uadui,kama mlivyo toka out kuanzisha mahusiano,basi tokeni out mzungumze kuvunja mahusiano. Isipokuwa kwa mahusino ambayo huonyesha hati hati ya Revenge za ngono,huwa hayo tunashauri yavunjwe kimya kimya.
Mchambuzi na mshauri wa masuala ya mahusiano na ndoa
        *Mwanasaikolojia*
*Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)*

No comments:

Post a Comment