Friday, 23 November 2018

WACHUMBA KUITANA MAJINA YA MAHABA

💝💝 *Swali: Jaman hivi ni sahihi kwa marafiki tu wa kawaida au wadada kuitana Honey,love,sweetheart, n.k mf unakuta mdada anamuita mkaka sweetheart sio mpenx wake wala nn, au anapewa au kafanyiwa kitu na mkaka anasema asante my love. Namm huwa napenda kweli kuita watu hvo*💝💝
............
............
_Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078)_
*MADA HII IPO KISAIKOLOJIA NA KIROHO*

_Kwanza tujue kitu kimoja jina lolote ni ANWANI ya mtu aitwaye,na niufafanuzi wa Hisia alizo nazo mtu juu ya mtu,mazingira au mapito_
👉Mtoto akizaliwa anapewa jina,watoa jina HAWAITI ILI MRADI JINA, wanakuwa *Wanamsukumo* aidha wa Shukrani kwa Mungu,Mapito magumu, muujiza,mahusiano mabaya ndo utasikia majina kama SIKUJUA,TABU, SHIDA, EBENEZA,SHANGWE nk..... Kwa maana hiyo USIDHARAU NGUVU YA JINA.
👉Biblia inasema heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi, kwa nini.... Kwa sababu *_Jina linabeba nguvu ya matendo utakayo tenda_*
👉Kwa nini mtu aitwe jina zuri afurahi, naaitwe jina baya achukie? Ni kwa sababu jina lina *Tibua Hisia*
👉👆Kwamaana hiyo kama jina linatibu hisia zinazotakiwa zitoe *Matendo sawasawa na jina likiloitwa* je,vijana kuitana majina ya *Kimahaba*(Mpenzi,mke wangu,Laazizi,)nk lina athari zozote.
👆👉Kumbuka Nguvu ya neno kwa maisha yako ni *Kuishi sawasawa na Maneno yako* Biblia imesema mwanadamu ATASHIBA mema ya matunda ya midomo yake.... Jina lolote unalimwita mwenzako naye kukuita linaunda BOND kwenye akili,inayoanza taratibu kufuta mipaka muhimu kati yenu, hisia za ukaribu zinatibuliwa,na mzizi wa urafiki ukomaa,namzizi huo unaweza pelekea kuwa huru nje ya mpaka wamahusiano yenu na mwisho LOLOTE LAWEZA TOKEA(Aidha kuanzisha mahusiano ambayo hayakutarajiwa,au sex ambayo haikutarajiwa.
*NB:* UTUMIAJI WA MAJINA katika mahusiano ufuata Levels of Intimacy ndomaana tuna jina kama jina la mtu,tuna jina la rafiki,tuna jina la mchumba mtarajiwa natuna jina la mke au mme.
Swali kwako, je ukimuita rafiki mpenzi,honey,sweetheart nk mmeo,mkeo utamwitaje.....?unaweza usione shida ila KISAIKOLOJIA umejipunguzia nguvu ya Hisia za kutofautisha mwenzi wako na rafiki yako wa karibu.

*UHURU WAKO wakutumiajina hilo ndo kipimo chako cha usalama wa kihisia*
NOTE: Kwa kawaida mtu anamwita jina mtu zuri,la mahaba kulinganana degrees za huyo mtu katika moyo wake na jina likikolea uendelea kupandisha degree kwenye moyo na hisia, sasa kama rafiki atachukua jina la *Mpenzi wa Moyo* na Mchumba wako au mmeo,mkeo atachukua degrees ngapi maana hatunaga *WAPENZI WA MOYO* tuna mpenzi wa moyo....Kisaijolojia...Ndo maana inashauliwa mwite mtu jina lenye mpaka wa kuhifadhi nafasi maalumuya mtu maalumu kwako.
*_Ni sawa na mtu hata akikuiendezaje,na akakuhudumia sana huwezi muita/kumpa jina la MUNGU WANGU, nafasi hii unaiacha kwa kuwa unajua huyu nikimpasifa na jina la Mungu na Mungu ntapa lipi_*
Weka mpaka ulinde nafasi ya hisia za mtu maalumu kwako.
   *Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078)*

No comments:

Post a Comment