Thursday, 1 June 2017

HATUA MUHIMU ZA MAHUSIANO

*SWALI LA KISASA NA ATHARI ZAKE*
*Shalom nna swali wapendwa....*

*Hivi kwann sasa kumeshika kasi sana watu wakishakuwa na mahusiano tu wanapost wapenzi wao ktk mitandao ya kijamii.?????*
  _Katika Kujibu Swali hili, Mwanasaikolojia *Ev Elisha Kazimoto* anachambua hivi;_

🏹Mahusiano ni photocopy ya uchumba, ambapo original ya mahusiano anayo mwenzako  moyoni mwake, ambayo akijiridhisha ndo atakupa hiyo origina na utaichana photocopy,sasa akiigomea asikupe ndo utaumbuka,..... Kuna vitu ambavyo vijana wanapaswa kujifunza katika mahusiano (Kuna Kipindi cha Mlipuko, Kuna kipindi Cha Wasi wasi, Kuna kipindi Cha Utulivu, Kuna kipindi cha Uhakika, kuna Kipindi cha Agano) hivi vipindi vyote vina maana yake na kazi zake,usipo jua vipindi hivi utakuwa mtu wa kuumizwa na kujishangaa na kubadirisha profile picture kila muda.Kabla ya kujiachia na Sura ya mtu jua vipindi hivi vya kisaikolojia ili usijiharibu kisakolojia baada ya Malengo yako kutokamilika.
🏹Kipindi cha Mlipuko ni kipindi cha Mahusiano ya mwanzo ambapo kila mtu anakuwa na mvuto wa nje tu kwa mwenzake, hapa ndipo watu huwa na upendo wa upofu,hasikii aambaliki,hajali mvuto na hisia za mwonekano, sauti, pesa na umbo utawala hapa. (kipindi hiki hakuna aliye na details za mwenzake) ukijifanya kipindi hiki huyo wako kaa sawa unawezaachwa mkiingia kipindi cha  details
🏹Kipindi cha Pili katika mahusiano nikipindi cha wasiwasi,hapa mtu uanza kujifikiria,je ni kweli huyu ndo awe wa milele?kweli atatosha kwenye maisha yangu, hivi nikiamua kabisa nioane naye kama atabadirika itakuwaje? Hapa watu uanza kuona utofauti wa siku za kwanza wameanza mahusiano, na muda waliopo kuna tofauti ya mawasiliano,zawadi,usiriazi(seriousness )unapungua au unaongezeka. Hapa ndo kipindi watu utengenezewa mazingira ya kumwacha mtu(kumpiga kibuti)au kuamua kuwa niridhike naye tu..(hapa kuwa makini pia)usijiaminishe sanaaaa, unapoona mtu anavitabia vya Siri,vinavyokuoa mashaka PIGA CHINI KABLA YA KUMUWRKA MOYONI KAMA MTARAJIWA,ukivifumbia macho vitabia hivyo....Usidhani utambadirisha ndani,asiyebadirika kipindi cha urafiki na Uchumba huyo ni JIWE LA MTONI,linapigwa maji haliyeyuki ila LINA TEREZA TU mile na milele. PIGA CHINI HUYO.
🏹Kipindi cha Utulivu ni kipindi ambacho watu sasa uamua kuingia katika uchumba(muda huu mtu uanza kuona vitu muhiu sana kwa mwenzake anaye muhitaji,uona huyu anaweza kukamilisha ndoto zangu)kipindi hiki taarifa zinazoaminisha uzuri na ubora wa mtu uongezeka(ila hubaki maswali machache ya hivi huyu hatanisaliti kuuniumiza? Hivi tania hii mbona kama itanisumbua, nighairi au niache tu atakaa sawa)ila utulivu uongezeka.
🏹Kipindi cha Uhakika,nikipindi ambacho hata Maali imeisha lipwa,na pete imewekwa kidoleni, hapa ni muda ambao mtu amekubaliana na mapungufu yaliyopo,ameridhika na viwango alivyo navyo mwenzake, kiroho,kimwili na kiuchumi. Wengi wenye akili ya mahusiano ndo wakitaka huweka profile picture za wenzi wao, katika level hii kuvunji mahusiano ni NADRA SANA aidha pepo,au madhaifu makubwa yamejitokeza kukiwepo kupoteza uaminifu(zinaa).
🏹Kipindi cha Agano, ni hatua ya mwisho ambayo ni maamuzi yasiyo na mashaka,ya wazi ya kuridhia kuungana na mwenzake kwa kufunga ndoa. Huu ni muda Amazing, wa furaha ya kuvua ujana na kuanza ndoa.
*_Hatua hii ndo maana wakaweka Honeymoon muda kutuliza mwili,saikolojia,shukrani kwa Mungu na kwa mwenzako, kuenjoy Mahaba ulo yasotea kwa muda mrefu, My Take ukiwa na uwezo Piga Siku 7-10 Hotelini aisee_*
_Uchambuzi huu umeandaliwa na Mwanasaikolojia ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*_
          0755444078

No comments:

Post a Comment