Sunday, 18 June 2017

UNAJIITA MADAM KUMBE UMEACHIKA!

🏹🏹  *ACHA UTAPELI WA KUJIFICHA KANISANI KUMBE ULISHA ANGUKA KIROHO*🏹🏹

( *_Kujiita Madam/Kaka kumbe Ulishaachika kwenye Ndoa_*)

      Ev Elisha Kazimoto

        *0755444078*

⛱ _Shalom watu wa Mungu mnaoitazamia Mbingu takatifu zilizo wekwa tayari kwa *walio jikana na watakatifu*_ leo napenda nizungumze na wana ndoa na wana ndoa watarajiwa kuhusu kamchezo kakitapeli kanako anza kuchomoza kutoka juu kwa *_Watu Maarufu_* kanisani mpaka watu wakawaida sana ndani ya kanisa( *_Kamchezo  hako kakitapeli kanisani ni Watu kuwaacha Wenzi wao(Mke wake/mme wake)na kujipachika Jina Feki la MADAM/KAKA....._* Kutengeneza Dili la kukwapua kiurahisi kijana wa watu,au binti wawatu kiurahisi. (Acha UTAPELI wewe ni Nyoka hatari ambaye watu wote imewapasa wakukimbie na sumu yako kali yakufisha).

*_Mathayo 19 : 9 - Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini._* 

⛱ Wewe mwanamke au mwanaume unayeachana na mwenzako unatumia Biblia gani?Ukristo wa wapi huo wa kiongozi gani huyo(mmeligeuza kanisa Taasisi ya siasa ya kuoa na kuacha, kama vyama vya siasa,leo chama hiki kesho kile)acheni utapeli wewe ni *Mzinifu Mkubwa* mwana wa Jehanamu wewe.

⛱Umeachana na mmeo na kujiita *Madam* madam wa wapi, mbona hutulii bado unawavulia nguo vijana,wanaume? Unahisi umaarufu wako au unyonge wako unakupa tiketi ya *Kutuchafulia Sura na Vazi la Wokovu wetu?* Jehanamu ya moto inakungoja(mbinguni hakuna umaarufu wa pesa,uimbaji na ma CD yako au uinjilisti wako au Utume na Unabii wako)

⛱Unaacha mkeo eti Mungu amekuongoza umuoe mwingine, hivi wewe unajua Ndoa mbele za Mungu, wewe ni *Mzinifu tu kama wengine* unatumia biblia gani? Acha KUJIFICHA Nyuma ya mwavuli ⛱⛱⛱⛱wa huduma eti mimi nabii mtume,mwimbaji *wee jambazi hatari katika mwili wa Kristo* na leo nakupiga kwa mawe mpaka uache utapeli huo kwa jina la Yesu.

*_1 Wakorintho 7 : 10 - Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;_*

⛱Wokovu wetu una kanuni siyo kirabuni. Kwa nini unaachana na mwenzako? Mnaachana kwa misingi ya kimaandiko au mnaachana kwa misingi ya uhuni wako,kiburi chako ,tabia zako na uzembe wako mbele za Mungu mpaka shetani amewalipua?

⛱Haya umeaua kuachana na mwenzako unaouwezo wa *Kuilinda imani na uaminifu wako kwa Mungu usioe tena au kuolewa tena au kuwaka tamaa?* mbona baada ya kuachana na mwenzako _Unaanza kuruka fensi? Unalala na vijana vidogo vidogo kama watoto wako au wadogo zako?mbona unaangaika kuchumbia na kujirahisisha kwa wanaume? Umri wako wewe ndo wa kujirahisisha kwa vijana vidogo?wee ulishaanguka zamani, nisawa na gari bovu limesimama kumbe haliwezi kuwaka_

*_1 Wakorintho 7 : 11 - lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe._*

⛱Na ninyi *Wachungaji vipofu,mitume wenye njaa,manabii wahuni* unamfungishaje ndoa huyo Jambazi wa kike/kiume madhabahuni patakatifu Kwa Biblia ipi,andiko lipi huku ukijua huyu amevurunda kwa mme wake /mke wake?au njaa?umefungisha ndoa maskini wangapi wa aina hiyo?au unahisi Biblia inapendelea? *_Na wewe ni mtumishi Hewa tu, njaa tu, rudi msalabani_* lakini hii inatuonyesha jinsi gani Madhabau yako ni Feki, Chafu, na Ovu. Simamia kweli ya Kristo ulilinde kundi.

⛱ *_Hivi nawewe unayeoa aliyeachwa na mwenzake kwa vijitabia vyake na wewe ni mbovu, utaachwa vilevile_* jiulize kilicho mtoa kule siyo umalaika wake ila ni ushetani wake(kama ameachana na mwenzake na kuoa au kuolewa bila kuzingatia kanuni za Biblia)jua *_umeoa au olewa na jambazi lililo jeruhiwa_* ni pole sasa ila majeraha yakipona hata kama ni miaka 5, 10 baadaye litakunyonga na wewe.

*_Mithali 17 : 11 - Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu; Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake._*

⛱Makanisani kumekuwa kimya, leo Mimi kama Mjumbe mkali nimetumwa kwako, wala sina haja ya unipende au unichukie,ila ujumbe umefika, *Wewe Ni mzinifu,Tapeli na Jambazi kubwa la Kiroho kanisani* unajifichia kwenye unaarufu wako wa Kuimba, Utume,Unabii,uchungaji mbinguni na jehanamu hakuna umaarufu huo, wala hutukomoi sisi, humkomoi mmeo au mkeo,unajikomoa, kufa utakufa na jehanamu utaingia na ma CD yako ya nyimbo mpya unatunga kila siku na kuhubiri redioni utaviacha uende uchomeke peke yako.( *Wala sikuhukumu ila wewe na matendo yako ndo yanakuhukumu*) hauna la kujitetea.....

⛱ Ooho mimi huyu kwanza hatukufunga ndoa Kanisani tulioana hivi hivi(kwanza viapo ni vya wanadamu), Acha uhuni umemzalisha/mzalia watoto wa ngapi. Ulipo kuwa unafunua utupu wake ulikuwa hujui kuwa unamfunua lakini hamjafunga ndoa? *Acha uhuni wako* 

⛱Eti huyu mwenzangu simuelewi,yaani mkorofiii mi namuacha, kwani kuna aliye kutongozea huyo,si ulioana naye kwa mbwembwe? Kaa naye huyo rudi kwa Mungu umwombee akae sawa, *Acha kuharibia wenzako* walio safi wanamtaka huyo,wenye haki za kumuoa au kuolewa naye kwa kanuni za kibiblia.

⛱Oooho tangu tuoane ni vurugu tupu, naona siyo mapenzi ya Mungu, *Wee tapeli tu na muhuni* mapenzi ya Mungu unayaona leo baada ya mapenzi kugeuka shubili kaa kwenye jehanamu hiyo uloingia kwa kupenda na tamaa zako.

⛱⛱ *_Ninyi wana ndoa Majambazi mnao oana na kuachana msituharibie vijana wetu, mnabadirisha taratibu na kuondoa mipaka ya Wokovu taratibu, angalia neno hili( Mithali 22 : 28 - Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako._*) sasa vijana wanaoana na yeyote kwa kisingizio akileta za kuleta na piga chini, miaka 2 najiita *_MADAM..../KAKA..... Halafu nazoa mwingine_* mshindwe, acheni wokovu mrudi duniani kwenye ukahaba na uhuni ijulikane moja kuliko kutuchafulia upepo na sura ya wokovu tuloupokea kwa gharama kubwa msalabani. Huu ndo msimamo wa Biblia 

*_Kutoka 19 : 12 - Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa._*

_Ukiyajua hayo ni Heri ukiyatenda, Ulikuwa na mimi Mjumbe Mkali kwa Wahuni( *Mithali 17:11*) 

            *_Ev Elisha Kazimoto (Baba Eve)_*

      *0755444078*

                 ©2⃣0⃣1⃣9⃣

No comments:

Post a Comment