*HILI VAZI BASI, NALIVUA*
_Ev Elisha Kazimoto_
*0755444078*
_Shalom mwana maombi,mkeshaji,mwana maombi,mtakatifu wa Mungu uitwaye mtu wa vita,nakukaribisha sasa katika ujumbe huu wa *Operation Tupa Vazi Chakavu, Vaa Vazi Jipya* katika mkesha wa maombi_
🏹Kila vazi katika ulimwengu wa mwili lina tafsiri zake na maali pake pale linapo valiwa na mtu, kuna vazi ukivaa utasikia, _Bibi harusi, mwanasheria, mchungaji, kafiwa, huyu mjane,kahaba na mtanashati nk, vazi lina nguvu ya kukutambulisha kwa watu,eneo lolote hata kabla hujaongea *Vazi lina Nguvu ya Kukushusha au Kukupandisha* kuwa makini sasa tunapo uangalia ulimwengu wa roho_
*_Yona 3 : 6 - Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu._*
🏹Katika ulimwengu wa roho tunatambulikana pia kwa vazi,maisha yako unayoishi katika mwili yaweza kuwa ni aina ya Vazi ulilovikwa katika ulimwengu wa roho aidha *umevikwa na Mungu au Shetani na Mawakala wake* vazi hilo ndilo linakufanya uwe na nguvu katika mwili au uwe dhaifu.
*_Isaya 61 : 10 - Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu._*
🏹 Kuna watu wana maisha ya kukataliwa, mikosi, Kila mahusiano ya uchumba yanavunjika,hata yule uliyesema huyu basi tutafunga ndoa naye anapotea,kila biashara inaharibika,ndoa migogoro aiishi, *_Shida ipo kwenye vazi Ulilo vikwa, vazi la migogoro,vazi la kukataliwa,vazi la nuksi_* unahitaji kupigana katika maombi kuchana na kuvua vazi hilo.
*_Marko 10 : 50 - Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu._*
Vazi leo lazima litupwe, vazi walilokuvisha wachawi,katika ukoo lazima litupwe kuleee.
🏹Kuna mavazi ya laana walikuvika, Katika maombi ya leo tumia mstari huu, kwamba Yesu alijika vazi la Laana ili mimi nivikwe vazi la Baraka
*_Zaburi 109 : 18 - Alijivika laana kana kwamba ni vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake._*
🏹Omba vazi ambalo hata wanadamu wataligombania, kazini wataligombania,kanisani wataligombania, vijana wakiume ma wakike wataligombania.
*_Zaburi 22 : 18 - Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura._*
_Saa ya kuvua vazi baya na kuvaa vazi jipya_
*_Ev Elisha Kazimoto_*
0755444078
Friday, 2 June 2017
HILI VAZI BASI NATUPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment