Saturday, 10 June 2017

BUDGET KATIKA FAMILIA

🏹🏹 *BUDGET KATIKA FAMILIA NA UTATA WAKE*🏹🏹
    _Swali linasema hivi,:wew ni mwanamke mna familia wew na mumeo wote ni wafanyakaz,unajitoa sana na pesa za mshahara kufanya maendeleo makubwa ila unapotumia pesa ya mumeo kwa ajili ya matumiz ya nyumban anagomba sana hata kama ni elfu mbili na unakuta umemueleza kabisa?!!!je mke afanyej kuinusuru ndoa yake?_
🏹Hapa kuna vitu vya msingi vya kuvitazama sana katika ndoa ya watu wa aina hii. *_Kwanza kuna shida ambayo hawakuiweka sawa kipindi cha Uchumba_* maana kipindi cha uchumba ndipo tunaweka sawa mambo ya kifamilia( *Mfumo wa kupata watoto interval, mfumo wa kiuchumi mtakao tumia kuimarisha uchumi wa familia yenu, kama wote niwafanyakazi, mnatumiaje pesa zetu maana hiyo ndo Income yenu* kwa hiyo mkikosea kuzungumza kipindi cha Uchumba mifumo ya maisha yenu mtakavyo iendesha jua huwezi kukwepa migogoro na changamoto nyingi latika ndoa kaa sababu mnaingia kwenye mkataba wa ndoa mkiwa na mawazo tofauti sasa kuyafanya yawe mawazo sawa maana yake(Mnahitaji kipindi cha Uchumba kingine lakini ndani ya ndoa)jambo ambalo ni gumu pia kulifanya kwa ubora ila lazima mlifanye kwa mstakabari wa ndoa yenu(muda wa mazungumzo)
Ndo maana kipindi cha ucumba kikawekwa na kikashauriwa kisiwe chini ya miezi 6 na kisizidi miaka 3, kwa malengo kwamba wachumba wapate muda wa kuwekana sawa katika tofauti, na kama hakuna makubaliano ndo maamuzi ya Break up uchukuliwa(Maana ndoa ni mkataba wa kudumu)kama utaingia bila maridhiano jua ndo mwanzo wa migogoro isiyo isha.
🏹 Pili,  *Aina ya ndoa*  katika suala la Budget ndani ya familia ubora na mtafuruko katika familia unaweza tokana na Aina ya Ndoa, Ndoa nyingi zilizo pitia *Process 4 zza ndoa*ara nyingi shida hii huwa ni ndogo,au hakuna( Process ya 1.Kupenda, 2.Kuchumbia 3.Kulipa maali na 4.Kufunga ndoa,) 90% wamaume wapo radhi, cooperative na wake zao na huipa ndoa *Thamani* kuliko pesa au kitu chochote, kwa hiyo hufanya matumizi kwa madhauriano na Malengo.
🏹 Ila kwa ndoa zilizo ruka hatua 4, zenye mazinhira haya 👉(1.Imeanza ngono ndo ikazaa ndoa, 2.binti kupata mimba ndo ikalazimisha ndoa, 3.Kutumia pesa kushawishi binti akupende, au kijana akupende ikapelekea kuoana, 4.Binti kujichumbia, na kujioza) haya mazingira huondoa Thamani na nguvu ya Ndoa na kwa saikolojia ya wanaume huwa mioyo yao inakuwa na mambo 2. *Moja, Kuonyesha ubabe kwa mke wake maana siyo ndoa ya gharama, Pili .. Jeuri ya huwezi kutoka na ukitoka hana hasara.*
🏹Lakini Shida na Chimbuko la mzozo huu wa budget ya familia mwanaume kuwaka pale mke akigusa pesa ya mme wake, shida ipo hapa( *_Uelewa mdogo kuhusu ndoa na maana ya ndoa_*) katika ndoa vitu vyote ni vya pamoja, kinacho hitajika ni mipango, mazungumzo na mpangilio wa matumizi kulingana na kipato chenu.
🏹 *SULUHISHO* nini mama afanye, lazima kwanza atafakari ameingiaje katika ndoa hiyo? pili hakikisha unatumia lugha nzuri kuwasiliana na mmeo katika kila kitu, tatu Jitahidi kuongea na mwenzako kwa kila maamuzi ya kifedha unataka kuyafanya, nne jaribu kumshawishi mmeo mpange budget ya mwezi na mmeo na mpeane pesa ya ziada kila mtu kwa matumizi binafsi. tano kama mmeakoka wote ingia kwa maombi kuombea ndoa yenu. sita Onana na mwanasaikolojia kiofisi upate Counseling & Guidance.
   *Ev Elisha Kazimoto*
         0755444078

No comments:

Post a Comment