Monday, 21 January 2019

UFUNGUO WA 8

🔑🔑 *Ufunguo wa 8: Nahitaji Kujiona Sura yangu ndani ya moyo wa Mke au mme wangu*🔑🔑
_Huu ni mwendelezo wa Funguo 12 za ndoa yenye Furaha na Amani,ukiwa na mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa  na Mwanasaikolojia *Ev Elisha Kazimoto(Anointed)* WhatsApp 0755444078_
🔑Kuna vitu vinasahaurika kwa watu kwakuwa wanaviona si vya muhimu,na kuna mambo yanajengeka mioyoni ambayo hayakutarajiwa, lakini yote ni kwa sababu kuna kitu kimoja cha Kisaikolojia kimepigwa teke na wahusika aidha kwa kutojua,au malezi au mazingira yamewafanya wajivue ufahamu wa kufanya yaliyo ya msingi na washikilie yasiyo ya msingi.
🔑Furaha ya ndoa Siyo Muujiza,ni *Mchakato wa Hiyari* wa kutumia akili na maombi(kwa wale wanaoamini katika Mungu).
🔑Umewahi kujiuliza kupindi *Mnachumbiana na huyo mwenzako* moyoni mwako na akilini mwako kulikuwaje? Kulikuwa *Kumejaa Sura yake* ndiyo maana mawasiliano ya barua,ya simu,ya kutafuta kuonana yalikuwa makubwa na ya mara kwa mara sana, angaiko la moyo Usipo muona au Kusikia sauti yake kwa muda lilikuwa linakutokea. Kilicho kuwa kina fanya hayo yote ni SURA YAKE ILIJAA MOYONI MWAKO, NA YAKO ILIJAA MOYONI MWAKE.
🔑Kilicho sababisha sura yake ijae kwako na yako ijae kwake ni nini? *Jibu rahisi sana, ni Kila mmoja alikuwa anatafuta kufanya kile anacho hisi mwenzake atapendezwa nacho, na kujizuia kufanya kileambacho anahisi kitamuumiza au muudhi mwenzake.* Ila kwa sasa Sura ya mwenzako Imefutika moyoni mwako au sura yako imefutika moyoni mwake, na kama ipo basi *Haionekani vizuri ina kivuli vuli* kwa nini? _Kwasababu, haujali tena Hisia za kufurahi au kuchukia kwa mwenzako_ bali unafanya unalo hisi una utashi wa kulifanya, unasema bila kujali kama lugha hiyo ni tamu kwa mwenzako au ni chungu,inajeruhi au inaganga moyo wake.
🔑Ila ujue sura yako ikifutika ndani ya mwenzako jua *Hamtokuja kutulia kwenye Ndoa, migogoro itapoa mwezi, ujao inaanza,mwaka, ujao inaanza....* Nini mwenzako HAJIONI SURA YAKE NDANI YAKO
🔑Kulinda Furaha na Amani ya ndoa yako hakikisha unatumia ufunguo huu, *Nataka nijione Sura yangu ndani yake* ukimwangalia unaona *_Huyu ndo chaguo sahii langu, huyu ananifaa, Nisinge mpata huyu nisinge fanikiwa,amenisahaurisha machungu yangu_* Usipo ona hayo utaona Neno kubwa jeusi kwenye Paji la Uso wake linalosomeka hivi... *"Laiti ningejua Nisinge Mchagua huyu"* Sura hiyo ikisha someka moyoni mwako mtaishi ndani kwa Maigizo bila Matumaini.
_Ndoa ni yako tu haina jirani wa kukubebea, ifanye uonavyo vyema waweza ifurahia_
*By Msaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto (Anointed)*
WhatsApp 0755444078
             ©2019

No comments:

Post a Comment