Monday, 31 December 2018

UJUMBE WA MWAKA 2019

2⃣0⃣1⃣9⃣ *MWAKA WA BWANA KUTUFANYIA NAFASI NA KUTUZIDISHA* 2⃣0⃣1⃣9⃣
.......
.......
*_By Ev Elisha Kazimoto(Anointed)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
..............................
_Shalom mwana wa ufalme,mteule wa Mungu,uliye pata Nehema na Rehema za Mungu kuvuka mwaka 2⃣0⃣1⃣8⃣ na kuingia mwaka mpya huu 2⃣0⃣1⃣9⃣. Ni neema pekee na Upendeleo wa Mungu kwako na kwangu. Sasa nikukaribishe katika  *Meza ya Kinabii* juu ya mwaka mpya,upate Neno la Bwana utakalo safiri nalo ukimkumbusha Bwana kwa kila pito,changamoto na baraka zote katika mwaka 2019. Karibu_
🕰 *ANDIKO KUU: MWANZO 26:18-22, MSTARI MKUU 22* 🕰
🏁Kwanza kuna mambo ya kujifunza juu ya Jina la Mwaka, na kumshukuru Mungu. Katika jina la Mwaka kuna vitu muhimu kama 2.
1⃣ *_Mwaka wa Bwana kutufanyia nafasi_* Hapa kuna siri kubwa na Neema ya pekee, ikituonyesha kuna mazingira ya watu wameishi mwaka 2018 kwa *Kukosa mpenyo wa vitu kadha wa kadha* ,kuna vitu vimeshindikana,kuna kukata tamaa kwingi kulitokea baada ya kukosa NAFASI ya kufanikisha matarajio yao, sasa *_Bwana wa huruma mwaka huu 2019 anakuja na Kauli ya Kututengenezea Nafasi ya kupokea,kutumia,kuanzisha,kumiliki vitu mbalimbali ambavyo tulivitamani sana ila NAFASI haikupatikana_* Nafasi yaweza kuwa......
⌚Kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu.
⌚Mtaji wa kibiashara
⌚Mpenyo wa Kihuduma
⌚Wazo jipya la maendeleo
⌚Majibu ya maombi ya muda mrefu yasiyo na majibu.
_Na vitu vingine vingi ambavyo Vilikosa mpenyo wa kufanikiwa kwa mwaka 2018 kutokana na sababu za kimazingira,za vita ya kiroho, Hila za wanadamu, Muda kutotosha nk_
2⃣ *_Mwaka wa Kutuzidisha sana_* Hapa kuna siri kubwa ya kiroho ya Kulipiza mara dufu baada ya adui kutuchelewesha kufikia ndoto zetu,maono yetu,mipango yetu ambayo tulitamani kuwa tumeifikia tayari mpaka sasa,ila adui akaingilia kati na kubadiri majira,nyakati na kusudi.... *_Hayo Mungu katika mwaka huu anahitaji kuyatimiza haraka sana na kuyazidisha ili kufidia muda alotupotezea Adui_* Kumbuka Mungu wetu ni Mungu wa fidia kumbuka kwa Ayubu( *Ayubu 42:10-17*) ndiyo kazi ya Mungu akiamua KUZIDISHA, anaitwa Mungu mwenye wingi wa nguvu na akili zake hazina mipaka ( *Zaburi 147:5*) Jipange kwa 2019.
🏁 *_Sasa Tuliangalie Neno alotupa Bwana kwa mwaka huu 2019 tulichambue juu ya maisha yetu_* 🏁
Katika andiko hili kuna vitu vya kujifunza na kutiwa nguvu juu ya ufunuo huu wa KUCHIMBA VISIMA,NA KUGOMBANIWA KWA VISIMA VYAKO( *Mwanzo 26:18-22*)
1⃣ Visima, katika tafsiri ya Kiufunuo ni Vyanzo vya Baraka zako,mafanikio yako,ni chaneli za kutoka kimaisha; Hapa ndipo palipo na shuguli zako zote zinazo kuwezesha kuendesha maisha yako ya kiroho na kimwili( *_Hapa kuna huduma,kuna uchumi,kuna Elimu,kuna uchumba kuna ndoa,kuna ofisi nk_*) Mwanzo 31:1-9.
🏁Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo 2018 tulivianzisha ili *Vitufae kwenye maisha* Kama vile ISAKA alivyo chimba visima ili apate maji ya mifugo yake na matumizi mengine ili maisha yaende lakini kukatokea UPINZANI MKUBWA kwa kila KISIMA alicho chimba, kiligombaniwa na Kuporwa.
🏁 Wewe je, 2018 umejitahidi kuanzisha au kufanya nini lakini hukufanikiwa?adui Aliziba,Alipora,Aliumiza na mpaka hicho kitu UKAKIKATIA TAMAA? Lisikie Neno la Bwana 2019 _Bwana atakufanyia Nafasi na Hakuna atakaye pora kisima chako kipya utakacho chimba kwa jina la Yesu_.
2⃣ Kugombaniwa kwa Visima vyako; ( *_Siri ya kiufunuo iliyopo hapa ni Vita ya kiroho uliyokutana nayo katika harakati za kutoka kiroho au kimwili_*) Ni huduma yako imekuwa ya vita toka pande zote,kwenye ulimwengu wa roho hata kwa Wanadamu yumkini kutoka kwa watu walio wa Mungu.
🏁Isaka kila kisima alicho chimba Wachungaji wa Gerari walikigombania,Isaka akawaachia,akaenda mahara pengine na kuchimba kingine nacho wakagombania.... Akawaachia......ikawa ni mchezo huo huo.
🏁 *Huu ndo mchezo mchafu walofanyiwa watu wengi 2018* Kila jambo lililo jema unalolifanya linapigwa, unatulia,unafanya lingine, linapigwa,linaharibiwa, unajitia nguvu kutokata tamaa, Unasongwa na kukatishwa tamaa, unabadiri mwelekeo, na adui,wanadamu wenye hila wakahisi ni kama WANAKUWEZA VILEE, Nisikilize mtu wa Mungu huo mchezo mchafu ulochezewa umeishia 2018, mwaka huu _Bwana anatufanyia nafasi za kutosha,usikate tamaa, CHIMBA KISIMA KINGINE na Ole wake mtu au adui Akigombanie, ajifanye anafanya Harakati za KUKIZIBA/KUKUZIBA USIONEKANE, *Atapigwa yeye,atazibiwa mambo yake yeye, atashuka yeye*. Huu mwaka nataka ni kwambie kuna nguvu kubwa ya Mungu ya kupambana na kila Wazo ovu la Adui au la wanadamu wenye hila juu yako_ yaani huu mwaka miongoni mwa kauli zetu ni *_Usijaribu Kunizibia Kisima Changu kwa Njia yoyote Utaabishwa na Bwana anaye nifanyia nafasi_* hii kauli ni moto, itangaze kwenye maombi yako, iseme kinywani mwako,unapo hisi changamoto yoyote kiroho au kimwili.
*Ngoja nikuongezee Neno hili uone kauli hii ilivyo moto kwa Mtu YEYOTE atakaye taka kushugulika na Kisima chako mwaka 2019,bila kujali Umri,Nafasi,Jinsia,jina,Umaarufu au uwezo wa mtu, Kauli hii itawakata wote(KIKUBWA ILINDE HAKI YAKO MBELE ZA MUNGU USIWE NA HATIA).
29 Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.
Mwanzo 31:29

36 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N'nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
Mwanzo 31:36

41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.
Mwanzo 31:41

42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Mwanzo 31:42

👆👉MUNGU hajawahi Kubinya haki ya mwenye haki, ataonewa,atayumbishwa ila ni kwa kitambo tu(YAKOBO ILIPITA MIAKA 10) anabadirishiwa mshahara kwa Hila na mkwe wake... ila Kuna muda wa KUMKEMEA ADUI YAKO,bila kujali nafasi yake kwako(Labani alikuwa Baba mkwe wa Yakobo)Ila Bwana alimkemea Labani kwa Hila zake alizokuwa akimfanyia mkwe wake. Soma sura yote utapata utamu wa kupiganiwa na Mungu kwa wanadamu wenye hila kwako. *Mwanzo 31 yote*

3⃣ Majina ya Visima vilivyo gombaniwa na wachungaji wa Gerari; ( *_Hapa kuna siri ya kiufunuo, Isaka kisima cha kwanza alicho chimba wakagombania akakiita Eseki,kingine akachimba wakakigombania akakiita Sitna.... Haya majina ya tafsiri ya majina na lugha ulizo zisema,uliyo yatoa baada ya vitu ulivyo kusudia kufanikisha Kugoma,kuharibika,kuharibiwa_*)  haya siyo majina mazuri ni majina ya uchungu,... Nimepata hasara, Uchumba umevunjika,Huduma yangu Imepigwa vita na kudhohofishwa, kanisa langu limegawanyika, ndoa yangu tumetengana,hatuekewani,uchumi umeyumba,mtaji umefirisika ,nimefeli mtihani nk.... *Usikate tamaa, Chimba kisima kingine Kitakaa na utakipa jina jipya la Ushindi na furaha* Usikubali kuishia kwenye Eseki na Sitna ikawa ndo historia yako imeishia hapo, Songa mbele kuna *Rehobothi* haleluyaaa na Rehoboth ipo mwaka huu 2⃣0⃣1⃣9⃣.
4⃣Kuchimba Kisima kingine cha 3,ambacho *Hakitagombaniwa*; ( _Hapa kuna siri kubwa sana,inayoonyesha moyo wa Kutokata tamaa,kutosikiliza maneno ya Kejeli,kuvunja moyo,vikwazo nk na kuamua kusonga mbele kufanya kile ulicho kikusudia maishani mwako_)
🏁Nataka ni kwambie, ni kweli mwaka 2018,umesongwa,umekatishwa tamaa,na ulikuwa Umeapa *Huendelei tena* Lisikie Neno la Bwana, 2019 Songa mbele Bado Liko Tumaini kwa Bwana.( *Yeremia 31:17*) zamu hii utatembea kwa mkono wa Bwana akitufanyia nafasi na kutuzidisha sana
🏁Yakobo akachimba kisima cha 3 hawakukigombania, akakiita *Rehoboth akisema Bwana ametufanyia Nafasi na kutuzidisha katika nchi* kuna siri kubwa katika kuto kata tamaa na kuangalia vikwazo,mazingira na kusikiliza kelele za watu.
🏁 2⃣0⃣1⃣9⃣ Huu ndiyo muda ambao Bwana atatwambia, mlivyo kandamizwa,tukanwa,tendewa hila,poteza mweleko YATOSHA, tunageuka kuitazama nafasi mpya Bwana anayotufanyia kama familia,kama kanisa kama mtu binafsi. ( *Kumbukumbu la Torati 1:6-7, 2:3*)
🏁 2⃣0⃣1⃣9⃣ Huu ni kuda wa Maadui kuzuiliwa wasiendelee kukufatilia na kukuharibia mwelekeo wako.( *Kutoka 14:13-14, Malaki 3:11*)
🏁2⃣0⃣1⃣9⃣ Ni Muda wa Kushinda,kujenga maboma ya ulinzi kwenye ulimwengu wa roho,kufanikiwa kwa kuongezeka kwa mazidisho yatokayo kwa Bwana.( *2Mambo ya Nyakati 14:7,Kumbukumbu la Torati 5:33*)
5⃣Jina jipya la *Rehoboth* ni lugha mpya utakayo itamka katika mwaka 2019, _Bwana amenikumbuka amenipa mtoto,amenipa mke au mme,amenipa ofisi,amenipandisha cheo,nimefauru mtihani,nimejenga,nimepata usafiri, huduma yangu imepata kibali kila kona nk.( *Isaya 62:1-2*)
🏁2⃣0⃣1⃣9⃣ Huu ni mwaka wa kuachiliwa kwa kila kilichokuwa kimeshikiliwa( *Isaya 35:3-6*)
*ANGALIZO*
_Maneno haya,Unabii huu ni kwa wenye Haki wa Mungu na watakao kaa katika mstari wa Utakatifu,bidii kumtumikia Mungu na kuutafuta uso wake na Kulisikiliza Neno La Bwana na Si Maneno ya watu_
*Kama Bwana alivyo nipa nami nimekuwa mwaminifu kukufikishia, Ujumbe huu, Unanihusu kwanza mimi wa pili ni wewe ndugu katika Kristo*
By Ev Elisha Kazimoto(Anointed)
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
              ©2⃣0⃣1⃣9⃣

No comments:

Post a Comment