2⃣0⃣1⃣9⃣ *MWAKA WA BWANA KUTUFANYIA NAFASI NA KUTUZIDISHA* 2⃣0⃣1⃣9⃣
.......
.......
*_By Ev Elisha Kazimoto(Anointed)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
..............................
_Shalom mwana wa ufalme,mteule wa Mungu,uliye pata Nehema na Rehema za Mungu kuvuka mwaka 2⃣0⃣1⃣8⃣ na kuingia mwaka mpya huu 2⃣0⃣1⃣9⃣. Ni neema pekee na Upendeleo wa Mungu kwako na kwangu. Sasa nikukaribishe katika *Meza ya Kinabii* juu ya mwaka mpya,upate Neno la Bwana utakalo safiri nalo ukimkumbusha Bwana kwa kila pito,changamoto na baraka zote katika mwaka 2019. Karibu_
🕰 *ANDIKO KUU: MWANZO 26:18-22, MSTARI MKUU 22* 🕰
🏁Kwanza kuna mambo ya kujifunza juu ya Jina la Mwaka, na kumshukuru Mungu. Katika jina la Mwaka kuna vitu muhimu kama 2.
1⃣ *_Mwaka wa Bwana kutufanyia nafasi_* Hapa kuna siri kubwa na Neema ya pekee, ikituonyesha kuna mazingira ya watu wameishi mwaka 2018 kwa *Kukosa mpenyo wa vitu kadha wa kadha* ,kuna vitu vimeshindikana,kuna kukata tamaa kwingi kulitokea baada ya kukosa NAFASI ya kufanikisha matarajio yao, sasa *_Bwana wa huruma mwaka huu 2019 anakuja na Kauli ya Kututengenezea Nafasi ya kupokea,kutumia,kuanzisha,kumiliki vitu mbalimbali ambavyo tulivitamani sana ila NAFASI haikupatikana_* Nafasi yaweza kuwa......
⌚Kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu.
⌚Mtaji wa kibiashara
⌚Mpenyo wa Kihuduma
⌚Wazo jipya la maendeleo
⌚Majibu ya maombi ya muda mrefu yasiyo na majibu.
_Na vitu vingine vingi ambavyo Vilikosa mpenyo wa kufanikiwa kwa mwaka 2018 kutokana na sababu za kimazingira,za vita ya kiroho, Hila za wanadamu, Muda kutotosha nk_
2⃣ *_Mwaka wa Bwana Kutuzidisha sana_* Hapa kuna siri kubwa ya kiroho ya Kulipiza mara dufu baada ya adui kutuchelewesha kufikia ndoto zetu,maono yetu,mipango yetu ambayo tulitamani kuwa tumeifikia tayari mpaka sasa,ila adui akaingilia kati na kubadiri majira,nyakati na kusudi.... *_Hayo Mungu katika mwaka huu anahitaji kuyatimiza haraka sana na kuyazidisha ili kufidia muda alotupotezea Adui_* Kumbuka Mungu wetu ni Mungu wa fidia kumbuka kwa Ayubu( *Ayubu 42:10-17*) ndiyo kazi ya Mungu akiamua KUZIDISHA, anaitwa Mungu mwenye wingi wa nguvu na akili zake hazina mipaka ( *Zaburi 147:5*) Jipange kwa 2019.
🏁 *_Sasa Tuliangalie Neno alotupa Bwana kwa mwaka huu 2019 tulichambue juu ya maisha yetu_* 🏁
Katika andiko hili kuna vitu vya kujifunza na kutiwa nguvu juu ya ufunuo huu wa KUCHIMBA VISIMA,NA KUGOMBANIWA KWA VISIMA VYAKO( *Mwanzo 26:18-22*)
1⃣ Visima, katika tafsiri ya Kiufunuo ni Vyanzo vya Baraka zako,mafanikio yako,ni chaneli za kutoka kimaisha; Hapa ndipo palipo na shuguli zako zote zinazo kuwezesha kuendesha maisha yako ya kiroho na kimwili( *_Hapa kuna huduma,kuna uchumi,kuna Elimu,kuna uchumba kuna ndoa,kuna ofisi nk_*) Mwanzo 31:1-9.
🏁Kuna vitu kadha wa kadha ambavyo 2018 tulivianzisha ili *Vitufae kwenye maisha* Kama vile ISAKA alivyo chimba visima ili apate maji ya mifugo yake na matumizi mengine ili maisha yaende lakini kukatokea UPINZANI MKUBWA kwa kila KISIMA alicho chimba, kiligombaniwa na Kuporwa.
🏁 Wewe je, 2018 umejitahidi kuanzisha au kufanya nini lakini hukufanikiwa?adui Aliziba,Alipora,Aliumiza na mpaka hicho kitu UKAKIKATIA TAMAA? Lisikie Neno la Bwana 2019 _Bwana atakufanyia Nafasi na Hakuna atakaye pora kisima chako kipya utakacho chimba kwa jina la Yesu_.
2⃣ Kugombaniwa kwa Visima vyako; ( *_Siri ya kiufunuo iliyopo hapa ni Vita ya kiroho uliyokutana nayo katika harakati za kutoka kiroho au kimwili_*) Ni huduma yako imekuwa ya vita toka pande zote,kwenye ulimwengu wa roho hata kwa Wanadamu yumkini kutoka kwa watu walio wa Mungu.
🏁Isaka kila kisima alicho chimba Wachungaji wa Gerari walikigombania,Isaka akawaachia,akaenda mahara pengine na kuchimba kingine nacho wakagombania.... Akawaachia......ikawa ni mchezo huo huo.
🏁 *Huu ndo mchezo mchafu walofanyiwa watu wengi 2018* Kila jambo lililo jema unalolifanya linapigwa, unatulia,unafanya lingine, linapigwa,linaharibiwa, unajitia nguvu kutokata tamaa, Unasongwa na kukatishwa tamaa, unabadiri mwelekeo, na adui,wanadamu wenye hila wakahisi ni kama WANAKUWEZA VILEE, Nisikilize mtu wa Mungu huo mchezo mchafu ulochezewa umeishia 2018, mwaka huu _Bwana anatufanyia nafasi za kutosha,usikate tamaa, CHIMBA KISIMA KINGINE na Ole wake mtu au adui Akigombanie, ajifanye anafanya Harakati za KUKIZIBA/KUKUZIBA USIONEKANE, *Atapigwa yeye,atazibiwa mambo yake yeye, atashuka yeye* huu mwaka nataka ni kwambie kuna nguvu kubwa ya Mungu ya kupambana na kila Wazo ovu la Adui au la wanadamu wenye hila juu yako_ yaani huu mwaka miongoni mwa kauli zetu ni *_Usijaribu Kunizibia Kisima Changu kwa Njia yoyote Utaabishwa na Bwana anaye nifanyia nafasi_* hii kauli ni moto, itangaze kwenye maombi yako, iseme kinywani mwako,unapo hisi changamoto yoyote kiroho au kimwili.
*Ngoja nikuongezee Neno hili uone kauli hii ilivyo moto kwa Mtu YEYOTE atakaye taka kushugulika na Kisima chako mwaka 2019,bila kujali Umri,Nafasi,Jinsia,jina,Umaarufu au uwezo wa mtu, Kauli hii itawakata wote(KIKUBWA ILINDE HAKI YAKO MBELE ZA MUNGU USIWE NA HATIA).
29 Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.
Mwanzo 31:29
36 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N'nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
Mwanzo 31:36
41 Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi.
Mwanzo 31:41
42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Mwanzo 31:42
👆👉MUNGU hajawahi Kubinya haki ya mwenye haki, ataonewa,atayumbishwa ila ni kwa kitambo tu(YAKOBO ILIPITA MIAKA 10) ila Kuna muda wa KUMKEMEA ADUI YAKO,bila kujali nafasi yake kwako(Labani alikuwa Baba mkwe wa Yakobo)Ila Bwana alimkemea Labani kwa Hila zake alizokuwa akimfanyia mkwe wake. Soma sura yote utapata utamu wa kupiganiwa na Mungu kwa wanadamu wenye hila kwako. *Mwanzo 31 yote*
*_Hii ni sehemu ya kwanza ya ujumbe wa mwaka 2019,nimezifanya kuwa sehemu 2 kuruhusu wepesi wa kusoma post hii ila ni somo moja, sasa nikukaribishe katika mwendelezo wa sehemu ya pili_*
Uko nami Mnenaji wa Siri hii ya Ushindi wa mwaka 2019 *Elisha Kazimoto(Anointed)* WhatsApp 0755444078
No comments:
Post a Comment