🇹🇿 *_Sehemu ya Pili ya Ujumbe wa Mwaka 2019, MWAKA WA BWANA KUTUFANYIA NAFASI NA KUTUZIDISHA_*🇹🇿
_Uko na mimi Mnenaji wa Siri hii ya Ujumbe wa Mwaka 2019 *Ev Elisha Kazimoto (Anointed)* WhatsApp 0755444078_
..........................
Andiko letu kuu ni *Mwanzo 26:18-22*
3⃣ Majina Visima vilivyo gombaniwa na wachungaji wa Gerari; ( *_Hapa kuna siri ya kiufunuo, Isaka kisima cha kwanza alicho chimba wakagombania akakiita Eseki,kingine akachimba wakakigombania akakiita Sitna.... Haya majina ya tafsiri ya majina na lugha ulizo zisema,uliyo yatoa baada ya vitu ulivyo kusudia kufanikisha Kugoma,kuharibika,kuharibiwa_*) haya siyo majina mazuri ni majina ya uchungu,... Nimepata hasara, Uchumba umevunjika,Huduma yangu Imepigwa vita na kudhohofishwa, kanisa langu limegawanyika, ndoa yangu tumetengana,hatuekewani,uchumi umeyumba,mtaji umefikisika ,nimefeli mtihani nk.... *Usikate tamaa, Chimba kisima kingine Kitakaa na utakipa jina jipya la Ushindi na furaha* Usikubali kuishia kwenye Eseki na Sitna ikawa ndo historia yako imeishia hapo, Songa mbele kuna *Rehobothi* haleluyaaa na Rehoboth ipo mwaka huu 2⃣0⃣1⃣9⃣.
4⃣Kuchimba Kisima kingine cha 3,ambacho *Hakitagombaniwa*; ( _Hapa kuna siri kubwa sana,inayoonyesha moyo wa Kutokata tamaa,kutosikiliza maneno ya Kejeli,kuvunja moyo,vikwazo nk na kuamua kusonga mbele kufanya kile ulicho kikusudia maishani mwako_)
🏁Nataka ni kwambie, ni kweli mwaka 2018,umesongwa,umekatishwa tamaa,na ulikuwa Umeapa *Huendelei tena* Lisikie Neno la Bwana, 2019 Songa mbele Bado Liko Tumaini kwa Bwana.( *Yeremia 31:17*) zamu hii utatembea kwa mkono wa Bwana akitufanyia nafasi nankutuzidisha.
🏁Yakobo akachimba kisima cha 3 hawakukigombania, akakiita *Rehoboth akisema Bwana ametufanyia Nafasi na kutuzidisha katika nchi* kuna siri kubwa katika kuto kata tamaa na kuangalia vikwazo,mazingira na kelele za watu.
🏁 2⃣0⃣1⃣9⃣ Huu ndiyo muda ambayo Bwana atatwambia, mlivyo kandamizwa,tukanwa,tendewa hila,poteza mweleko YATOSHA, tunageuka kuitazama nafasi mpya Bwana anayotufanyia kama familia,kama kanisa kama mtu binafsi. ( *Kumbukumbu la Torati 1:6-7, 2:3*)
🏁 2⃣0⃣1⃣9⃣ Huu ni Muda wa Maadui kuzuiliwa wasiendelee kukufatia na kukuharibia mwelekeo wako.( *Kutoka 14:13-14, Malaki 3:11*)
🏁2⃣0⃣1⃣9⃣ Ni Muda wa Kushinda,kujenga maboma ya ulinzi kwenye ulimwengu wa roho,kufanikiwa kwa kuongezeka kwa mazidisho yatokayo kwa Bwana.( *2Mambo ya Nyakati 14:7,Kumbukumbu la Torati 5:33*)
5⃣Jina jipya la *Rehoboth* ni lugha mpya utakayo itamka katika mwaka 2019, _Bwana amenikumbuka amenipa mtoto,amenipa mke au mme,amenipa ofisi,amenipandisha cheo,nimefauru mtihani,nimejenga,nimepata usafiri, huduma yangu imepata kibali kila kona nk.( *Isaya 62:1-2*)
🏁2⃣0⃣1⃣9⃣ Huu ni mwaka wa kuachiliwa kwa kila kilichokuwa kimeshikiliwa( *Isaya 35:3-6*)
*ANGALIZO*
_Maneno haya,Unabii huu ni kwa wenye Haki wa Mungu na watakao kaa katika mstari wa Utakatifu,bidii kumtumikia Mungu na kuutafuta uso wake na Kulisikiliza Neno La Bwana na Si Maneno ya watu_
*Kama Bwana alivyo nipa nami nimekuwa mwaminifu kukufikishia, Ujumbe huu Unanihusu kwanza mimi wa pili ni wewe ndugu katika Kristo*
By Ev Elisha Kazimoto(Anointed)
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
©2⃣0⃣1⃣9⃣
Monday, 31 December 2018
02:UJUMBE WA MWAKA 2019SEHEMU YA 2
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment