Wednesday, 6 June 2018

SEX NA HUDUMA NA MFUNGO

*TENDO LA NDOA NA MFUNGO*
Swali: Je, Ni Sahii kushiriki tendo la ndoa mkiwa kwenye mfungo wa maombi, au unajiandaa kwenda ibadani kuhudumu.?

*Anajibu Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
_Kwanza niweke sawa dhana na tafsiri ya tendo la ndoa kwa wana ndoa. *Tendo la ndoa kwa wana ndoa ni Safi, na Takatifu, na huru kwa wana ndoa muda wowote ili mradi wamekubaliana na kwa utaratibu*_  na hiyo ni kwa mujibu wa neno la Mungu.👇👇👇👇👇
*1Wakorintho 7:1-5*


1 Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. 

2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. 

3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 

4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. 

5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 
✍ Inabidi tujue jambo moja, hakuna unajisi wowote,ubaya wowote katika tendo la ndoa, hizo ni imani potofu na misimamo binafsi si ya Neno la Mungu. *Uharamu wa tendo la ndoa,na Muda wake ni kwa watu wasiyo wana ndoa, ila kwa wana ndoa ni Safi,Ruksa muda wowote* Dhana za Huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa siku ya ibada, au kama unaenda kufanya huduma, kusimama madhabahuni, huu ni ushetani, ni upotofu, ni huujumu wa ndoa, ni kuwafunga watu kongwa lisilo la haki. *_Alicho kibariki Mungu,utakihitaje kimelaaniwa? Mwanzo 1:28_* Mungu alilibariki tendo la ndoa na hakuliwekea majira wala nyakati za kuli attend,iwe asubuhi, mchana,usiku, usiku wa manane, free enjoy wana ndoa, unaenda kuimbisha saa 9 mchana, unahitaji kuburudika na kutuliza saikolojia yako hata saa 7 zimua, it's your property, zingatia tu utaratibu,muda wako na Mungu na muda wako na mpendwa wako. Ni muhubiri unaenda kuhubiri mkutano wa nje,una wife wako umemuhitaji mchana, Enjoy your blessings, wee ndo unajua muda uloutenga na Mungu na wako na mke wako. *Tendo la ndoa halina Limitation ya Kibiblia kwa wana ndoa* labda ushauri na mawazo tu ya mtazamo na mapendekezo kulingana na hali ya mazingira,kitu ambacho siyo kanuni wala sheria.
*Tendo la Ndoa na Kufunga* _Nahisi wana ndoa wanajua nitakacho eleza hapa, kwa vijana wanaweza wasijue, Tendo la ndoa si kama kunywa chai,kuchovya mkate kwenye chai, *Ile ni Kazi Ngumu japo ni Enjoyment* ila inahitaji nguvu za ugali, muscular. *Ogopa kazi inayo toa jasho mtu* hiyo siyo mchezo mchezo.
✍Tendo la ndoa kulifanya linahitaji nguvu,uwe umeshiba,uwe na joto la mwili ndo utaisimamisha misuli ya *Fimbo ya ufalme*,au mama ndo utahimili mapigo.
✍Tendo la ndoa linahitaji akili safi iliyo tulia,yenye oxygen ya kutosha ili kuibua hisia za sex, *_Sasa mtu aliye funga, ana njaa,akili inachoka,oxygen imepungua,lakini joto la mwili limeshuka, nguvu hana za kusimamisha fimbo muda mrefu kwa sababu ya chakula mwilini hakuna_* kwa sababu hiyo tendo la ndoa litakuwa gumu. Tena afadhali kidogo kwa Mwanamke anapokea,ila mwanaume anaye toa, one goal uchovu wake ni kama mwendo wa alotembea more than 5 km kwa miguu.
✍ *_Kama umefunga una nguvu za kusukuma mzigo na isikupe shida kuchoka, hakuna unajisi ingia kazini. Hivi ni vitu vilivyo barikiwa,sasa ukiokoka kupita maelezo kila kitu unakiita dhambi, kumbusu mkeo siku ya j2 dhambi, ku sex siku ya ibada dhambi, acheni kutengeneza dhambi, Tendo la ndoa kwa mwana ndoa halina unajisi kwa siku wala muda._* Alivyo vitakasa Bwana wewe usiviite najisi, vitu vyote ni safi kwa walio safi,ila ni najisi kwa walio najisi.👇👇👇👇
*Tito 1 : 15 - Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.*
✍Mwisho ushauri wangu na taadhari yangu, tusitumie utashi wetu usio na fact za kibiblia kuonyesha kosa au dhambi, tutumie ujuzi,experience na neno la Mungu kuwaonyesha watu ukweli wa mambo.
NB: Tendo la ndoa linahitaji utulivu, maandalizi, nguvu na muda mzuri na kuridhishana, lisifanyike kwa kukimbia kimbia au kumridhisha mtu mmoja,mnapo lifanya,muwe mmefunga,mnaenda ibadani,au mmetoka ibadani hakikisheni ni kwa furaha yenu wote na kufurahi wote pamoja.
*_Ulikuwa na mchambuzi wa masuala ya kisaikolojia na kiroho katika mahusiano na ndoa, Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)_*
WhatsApp 0755444078

2 comments:

  1. Katika mstari uliouweka hapo juu, yaani 1Wakorintho 7:5 tunakutana na maneno haya; "MSINYIMANE ISIPOKUWA MMEPATANA KWA MUDA, ILI MPATE FARAGHA KWA KUSALI; MKAJIANE TENA; Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu."

    Katika mstari huu naona agizo kwamba wanandoa wasinyimane tendo la ndoa. Ila wanandoa hao hao wanaweza kunyimana kwa muda kwa kupatana ili wapate faragha ya kusali. Pia wanaonywa urefu wa muda wa kunyimana uwe na kiasi ili wasije wakafungua mlango kwa shetani kuwajaribu.
    Ikiwa watu wanaagizwa kunyimana kwa kipindi fulani salama kwao ili wapate faragha ya kusali, Je huoni kama kuna zuio ikiwa mnatafuta faragha ya kusali? Naomba ufafanuzi.

    Ikiwa mstari huo unatumia maneno MKAJIANE TENA ina maana kulikuwa na kutenganishwa, na hapa tunaona ni kule kutenganishwa katika tendo la ndoa,kwa mini FARAGHA YA KUSALI ihusishe watu kutoshirikiana tendo la ndoa kwa kipindi walichopatana kuwa ni kipindi cha faragha ya kusali?

    ReplyDelete
  2. Mume wangu amerudi!!! Baada ya miaka 1 ya ndoa iliyovunjika, mume wangu aliniacha na watoto wawili na maisha yangu yalivunjika. Nilitaka kuyamaliza, nusura nijiue maana alituacha bila chochote. Nimekuwa nimevunjika kihisia wakati huu wote na maisha yanaonekana kutokuwa na maana. Siku moja mwaminifu, nilipokuwa nikivinjari mtandao, nilikutana na baadhi ya shuhuda kuhusu Dk DAWN. Baadhi ya watu walishuhudia kwamba alimrudisha mpenzi wao wa zamani, wengine walishuhudia kwamba anarejesha tumbo na kuponya magonjwa kwa mimea. Nilipendezwa zaidi na upatanisho na mume wangu, ambao Dk. DAWN aliwezesha kumrudisha mume wangu ndani ya siku 3. Sasa mume wangu amerudi na tumekuwa tukiishi kwa furaha tangu wakati huo. Shukrani zote kwa Dk DAWN. Hapa, ninaacha mawasiliano yake kwa kila mtu. Maana kuna changamoto za aina yoyote,
    Barua pepe ( dawnacuna314@gmail.com )
    Whatsapp: +2349046229159

    ReplyDelete