Sunday, 10 June 2018

ASILI YA USHINDI WA MTU WA MUNGU

*ASILI YA USHINDI WA MTU WA MUNGU*
    _By Ev Elisha Kazinoto_(0755444078)
.......
.......
_Shalom mtu wa Mungu,katika ujumbe huu naomba watu wa aina 3 wanitegee sikio vizuri._
1⃣Mtu wa Mungu(Uliyeitwa kwa jina ka Bwana)nitegee sikio usikie ushindi wako ambavyo siyo wa kubabaisha una chimbuko imara.
2⃣Wachawi(mawakala wa Shetani)mnaotesa watu na kuwawinda kama mwindaji awindavyo ndege( mjue si rahisi kumnasa mtegoni mtu wa Mungu)
3⃣Shetani na baraza lake la mapepo(wanaoratibu matatizo katika maisha ya watu)wajue uwezo wao ulivyo wekewa mpaka na Bwana juu ya watu wa Mungu.
............................................

*(Warumi 8:31-37 )*
------------
31Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
32Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
33Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
👉 *_Mambo muhimu yakujua hapa kwa kundi la kwanza 1⃣ Mtu wa Mungu_*
✍Tendo la Mungu kuwa upande wa maisha yako(kuitwa mwana wa Mungu/mtumishi wa Mungu)tayari vitu vyote *Haviruhusiwi tena kuwa juu yako* (yaani kuwa na nguvu ya kukushinda na kukukandamiza)
*(Waefeso 1:18-23 )*
------------
18macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
19na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;
20aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
*22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo*
23ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
✍Yesu hakutolewa kwa wanadamu kwa hasara,yaani ujio wa Yesu duniani siyo tu kuokoa wanadamu,ila ni pamoja na *Kukomesha utawala wa adui ibirisi na mawakala wake juu ya kanisa* ili tusiishi kwa hofu ya mauti na mateso
*(Mathayo 16:15-18 )*
------------
15Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
*18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.*
✍Mahusiano tuliyo nayo na Bwana Yesu,kati yetu yameunganishwa na upendo mkuu usiotenganishwa kwa kitu chochote(Upendo wa mauti ni mkuu una wivu)
*(Waefeso 5:28-32)*
------------
28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
*29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.*
30Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
*32Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.*
(Palipo na upendo pana kisasi cha mauti kama utaigilia kuharibu upendo)

_"Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; *Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,* Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu."_
*(Wimbo Ulio Bora 8:6 )*
✍Dhoruba muda wote katika maisha ya mwili huu zipo kila siku,ila katika hizo zote *Lazima Kushinda* kwakuwa kinachotushindia ni Upendo wa Mauti wa Yesu Kristo tulio unganishwa naye ndiyo unao meza mishale ya maadui zetu.
*(1 Petro 1:5-6)*
------------
*5Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.*
6Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
👉 *_Mambo ya kujua katika kundi hili la 2⃣la wachawi(mawakala wa shetani)_*
✍Ramli,madawa,uganga wa aina yoyote na umaarufu wa kufanya uchawi ambao mchawi aweza kuwa nao, *_Hauruhusu kumwondolea Neema,Ulinzi,Kibali_* alicho nacho mtu,alichopewa na Mungu.
*(Hesabu 23:16-25)*
------------
16Bwana akaonana na Balaamu akatia neno kinywani mwake, akasema, Umrudie Balaki, ukaseme hivi.
17Akafika kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, Bwana amenena nini?
18Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa Sipori;
19Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
20Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.
21Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
22Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati.
*_23Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli._*  Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
...
*25Balaki akamwambia Balaamu, Basi usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa.*
👆👉 Mungu hamtoi mtu Misri(upaganini)kwenye mikatale ya dhambi,halafu aruhusu achezewe na shetani na vibaraka vyake.
👆👉Nguvu iliyo tumika kutuvuta kutoka Dhambini ni kubwa kuliko nguvu inayotuwinda kututesa muda huu wakati tupo katika neema ya Wokovu.
👉 *_Mambo muhimu kuyajua katika kundi la 3⃣ Shetani na balaza lake_*
✍Adui akipewa(kuruhusiwa)nafasi ya kukugusa kwa namna yoyote anawekewa mipaka *asifanye anavyotaka* juu ya mtu wa Mungu
(Yobu 1:8-12)
------------
8Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
9Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?
10Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.
11Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
*12Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.*
✍Mpaka anaowekewa shetani katika kukugusa  popote pale *unaendana na kiwango cha imani yako* kwa hiyo usitegemee mtu wa Mungu kushindwa na jaribu lolote.
_"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."_
*(1 Wakorintho 10:13 )*
👉Kwa makundi hayo matatu,yote yanapaswa kujua kuwa vita yoyote inayo muhusisha *Mtu wa Mungu,Wachawi(mawakaka wa ibirisi,au ibirisi na baraza lake la mapepo* vita hiyo haimuhusu mtu ni Bwana ndiye anapigana nayo kwakutangaza ushindi kwa mtu wake.
*(1 Samueli 17:47-50 )*
------------
46Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
*47Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.*
...
49Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
50Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.
*_Mungu akubariki kwa ujumbe huu alonipa Bwana,kwaajili yatu wote wanaompenda Bwana lakini wanapitia vita kali ya kiroho katika maish yao_*
     By Ev Elisha Kazimoto
     Whatsapp 0755444078

No comments:

Post a Comment