Tuesday, 26 June 2018

MIPAKA YA HOUSE GIRL

Shalom. ‼
Swali kwa wote❓
🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆
Jamani mke Na mume ni wafanyakazi,  Na wapo busy Na kazi kila moja,

Je ni vizuri house girl kupika chakula cha Mume endapo mke atakuwa busy kazini???

⭕Kama Jibu Ndio au Hapana, Je ni Kwa nini??

⭕Usiijibu tu haraka ❗❗fikiria kihekima.

👆👆👆👆👆
*Mwana Saikolojia wa Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto (0755444078 whatsapp )Anajibu kama ifuatavyo*
....................................*Tuhitimishe Mada hii Kisaikolojia na Kijamii*
_Kwanza Muuliza swali ameweka viangalizo(conditions)nikama swali amelirahisisha tayari,kwamba *Je,ni vizuri au Vibaya,house girl akipika chakula cha mme wake KAMA mama yuko busy kazini?* hapo ndo mzizi wa hoja upo_
👉Kwanza wana ndoa lazima mjipambanue ninyi ni ndoa ipi(ya wafanyakazi wote,mfanyakazi mmoja,au wote si wafanyakazi, na kazi zenu zinakula muda kiasi gani na muda wa nafuu ya kazi zenu ukoje,niwaajili au mmejiajili) kisha pambanua ndoa yenu ni ya aina ipi nirahisi mama kama MSIMAMIZI MKUU wabmambo ya familia ikiwemo budget za matumizi ya ndani,breakfast na lunch,na dinner (chai asubuhi, chakuja cha mchana na usiku)atajua namna ya kupangilia ambo ya familia kwa ustawi wa familia yake.
👉Pili lazima wana ndoa mjue familia yenu ni ya aina ipi(familia ndogo,familia kubwa)una watoto wadogoau wakubwa wawezao kufanya majukumu ya kifamilia au wote nitegemezi wanasubiria kika kitu wafanyiwe.
👉Mama,ujue mmeo ni mme wa aina ipi( *Chifu,Rafiki, Dis minder) ukisha jua aina ya mme ujipange kukabiliana na aina ya familia ulo nayo kutoa huduma kama mama ili uendane na saikolojia ya mmeo.
_Baada ya mambo haya sasa twende kujibu hoja ya muuliza swali_

1⃣Mama mwenye familia ni muhimu kujua, kuoata house girl hakuondoi,au kupunguza wajibu wako kama mama wa familia na kwa mme wako.
2⃣Mama ni muhimu kujua,wewe ndo mlinzi wa mme wako katika mazingira yanayoweza onekana kumvutia sana mmeo,akahamisha attention yake kwako na kuhamishia kwa house girl au mdogo wako.
3⃣Hakikisha unasoma mazigira ya mmeo kujua vitu anavyo pendelea,na mazingira anayopendelea hakikisha hivyo unavifanya wewe kwa bidii na ubora zaidi kila siku.
4⃣Hakikisha unashuka na kuwa mnyenyekevu kwa mmeo,kumthamini na unapo muhudumia muhudumie haswaa kama mama.
_Baada ya Maangalizo hayo turudi kujua house girl katika familia_
👉Kupata house girl ni maamuzi ya watu 2 baada ya kuona wapi *Pana mapungufu* na nani aje kusaidia kazi(KUSAIDIA) je, ni house girl au house boy? Ni maamuzi ya watu 2 na wanajua kwa nini wamemleta, hivyo WAMERIDHIA tuna changamoto hapa huyu aje asaidie kulingana na ( *Aina za familia,na kazi mlizo nazo*) sasa anapo kuja kusaidia ndipo mama anaitazama ( *aina ya mume aliye naye*) ili kuruhusu kazi zinazofanywa na house girl au house boy ziwe na mipaka ipi.
👉 *SI KOSA KAMA HOUSE GIRL ATAPIKA CHAKULA CHA FAMILIA AU BABA(naanza kujibu swali sasa)* Kutegemea Mama yupo wapi,anafanya nini,muda wake wa kuwahi kupika na familia kula itakuwa muda gani.( *kama mnatoka kazini wote saa 10,11,12 hamja pata lunch lakini mama unauwezo wa kuagiza house girl akaandaa ili msishinde Njaa,fanya hivyo)( KULINGANA NAAINA 3 ZA MMEO)
👉Lakini NIMAKOSA MAKUBWA *Kutengeneza mazoea ya kila siku chakuka cha familia,kuandaliwa na house girl*) mwanamke mjanja.... _Muda alo busy anahimiza chakula cha familia kiandaliwe na anakihakikisha kabka hakija letwa mezani kama kitamfaa na mme wake, *Lakini anapo pata nafasi yoyote ya kuandaa chakula anahakikisha anatulia kumuandalia mmewe kitu kizuri zaidi ya anavyoandaa house girl* na ni makosa makubwa house girl kuwa mkali wa mapishi kukuzidi mama,tafuta hata walimu wa mapishi hata ingia online search namna ya kupika chakuka flani_
👉Pamoja na ubize wote wa kazi za huwezi kukosa siku 2,au 3 ukamwambia house girl kaa pembeni nimwandalie mme wangu na familia chakula bora zaidi
👉Na mme Rafiki,anaona,anajua how far mke wagu yupo na majukumu mengi.
👉Kama aina ya mme wako ni CHIFU,juavni mtu asiye tazama unafsnya nini,unamajukumu gani,uko busy kiasi gani...Yeye anachojali TIMIZA WAJIBU KWAKE WEWE KAMA WEWE KWAKE( not good this type) ndoa haiwezi kuwaya furaha na mambo yote hayata fanyika kwa upendo,furaha na ubunifu,bali kama WAJIBU. Hapo mama jitese zaidi hata kukubali vitu vingine viharibike visiende vema lakini utimize wajibu wako.
👉Kama mmeo ni RAFIKI, hakikisha unamshirikisha mambo yako kama rafiki,unapo pata nafasi na ujitahidi kuiata nafasi nyingi nyingi kumfurahisha mmeo kama rafiki,mwandalie vitu vizuri anavyopoenda,muhudumie kwa nguvu zote mpaka appreciate(akukubali kuwa naam) ili hata muda uke upo busy na kazi za serikali,au biashara ajue mke wangu akioata nafasi uwa ananifanyia kweli mambo mazuri.(USIMPOTEZE RAFIKI) hata house girl ajue ukiwepo mambo ni moto,unamjali mmeo haswaa.
👉Kama mmeo ni DIS MINDER (yaani yeye hajali) umefanfa wewe,au mtu mwingine,ilimmradi mambo yameenda...Chunga sana usijisahau ukamwachia house girl au boy,kazi hakikisha unaonyesha utofauti wa wewe na wasaidizi wako hao kwa mmeo.

NB: *Katika majukumu yote hakikisha unaweka mipaka ya mambo kadhaa,hata housegirl ajue kuwa hapa kwa namna yoyote,mama awe busy,au awe huru siruhisiwi kugusa ni mama tu* kika mtu ana mambo yake mi nakupa mfano ya general,ila kika mtu ana uzito wake....... Ya jumla *Usiruhusu house girl afanye haya,Kuingia chumbani kwako,kufua nguo za mmeo hasa za ndani,kutandika kitanda cha mmeo,kudeki chumbani kwako,kumpelekea mmeo maji bafuni* hayo baadhi......... Na mengine wewe binafsi utaona haya ni yangu tu....Fanya hivo
*Kwa ujumla wake, Ndoa aihitaji mazoea,inahitaji ujanja na maarifa ya juu,ili kulinda hisia za mwenzako,lakini kumfanya mwenzako akufurahie. Kwa hiyo ni mama tafuta njia nzuri za kumfurahisha mmeo na kumpendeza afurahie uwepo wako kwenye familia*
👉Wanaume tujifunze kuwa waume RAFIKI ili kuruhusu akili yako na moyo wako na macho yako kuona hali ya mkeo aliyo nayo na KUMUHURUMIA,kujua hajafanya hili si kwamba ni uzembe au hajali,ila ni kwasababu katingwa,kachoka,huwa akipata nafasi anafanya kwa asilimia za kutosha. Basi muhurumie,mpe pole,msifie,mfariji,mpongeze,MSAIDIE inapo bidi.
👉 Mme *Chifu Aheshimiwi,Anaogopwa* woga siyo kupendwa ni Kukwepa Shari, sasa usijivune kwakuwa unaogopwa,ila jua mkeo kakuzidi Akili Anakwepa Shari ili maisha yaende.
@Kubadirika ni Muhimu ili ulete radha ya ndoa iliyokusudiwa na Mungu na kisaikolojia.
👉Mwana mama kuhurumiwa na kusaidiwa,si kigezo cha kukwepa wajibu wako,ila umetengenezewa mazingira na mmeo mwenye maarifa ya juu ya *kupalilia upendo* katika ndoa yenu.

*_Uchambuzi wa mada hii umeandaliwa na Mwana Saikolojia wa Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)_*

No comments:

Post a Comment