Sunday, 26 November 2017

SWALI: STYLE ZA SEX NANI AANZISHE

Swali: *Hivi ni vibaya mwanamke kuanzisha style mpya ya sex kwa mume wake? Au anatakiwa atumie mbinu gan kuianzisha?*

Anajibu: Ev Elisha Kazimoto(Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa)
WhatsApp 0755444078
_Kwanza Ndoa ni uwanja wa watu wawiliwa amani,furaha na upendo na uhuru, mwana ndoa anahitaji kuwa huru kwa mwenzake,na kila linalofanyika ni la kwenu wawili, sasa maudhui ya umoja wa wana ndoa yakibadirika ndoa inakuwa chungu,na ndoa ikiingiwa tu na mdudu uwezekano wa kwenda mbinguni,unaanza kuwa mdogo_
👉 Kweli ni kwamba ndoa ni mlango, ni chombo kizuri cha usafiri kwenda mbi guni au jehanamu, ambao hamjaoa au kuolewa, kwenye ndoa hupaswi kuishi katika ndoa kwa kujikaza au kiugumu, jua mbingu una asilimia 10 kati ua 100 kuiona. Ndiyo maana tunawashauri vijana usiingie kwa ndoa kutafuta sex, tafuta kusudi la Mungu, usitamfute mtu wa mitoko na kukidhi mahitaji ya kiuchumi, tafuta na omba mtu atakaye kusogeza karibu na Mungu na kukufanya utimize kusudi la Mungu.
👉Unapo kwenda kuoa au kuolewa jua ndoa yaweza kuwa ngumu au nzuri(nyepesi)kutokana na aina ya ndoa utakayo chagua kuishi.
Kuna aina 3 za ndoa, *Moja , Ndoa ya Kirafiki, pili Ndoa ya Kitoto, tatu Ndoa ya kibosi* wengi hasa wasiopenda kujifunza na hasa walokole(siwasemi vibaya maana miongoni mwa walokole mimi ni namba moja najivunia neema hii) ila wengi wao maarifa ya kidunia wameyatupilia mbali kwa kisingizio cha wanajua tu maarifa ya biblia nayo hawako vizuri,kwa hiyo kote hawako vizuri ndo maana ndoa zinakuwa ngumu sana wengi wao wana ndoa za KIBOSI hapo ni amri,uchifu, nk lakini ndoa ya kitoto ni kucheza na kufurahi na kusameana,ndoa ya kirafiki ni kusaidiana ka hivyo ku mshave mwenzako,kumuogesha,kusaidiana vikazi vya haoa na pale kwa upe do si kwa kuagizana.
Kuna kawimbi ka wahuni wa imani, kutafuta namna gani ya kutengeneza vitisho kwa watu,au tofauti ya imani nawe uwe ni mwana imani iliyo tofauti na wengine,bila kuzingatia neno la Mungu na Nature of Creation.(  _Wanasema wana ndo kufanya tendo la ndoa kwa style mbalimbali ni dhambi, ni style moja tu ya chali mama baba juu ndo takatifu_) Huu niuhuni mkubwa wa kiroho.
Mungu alipotuumba alitupa intelligence(Akili) . Sasa imani ya style hii takatifu na hii dhambi ni mavumbuzi ya wanadamu,Ukisema neno dhambi ni Katazo la Kimungu. Sasa sijawahi soma aina ya style kwenye biblia, ila intelligence ya uumbaji inatusaidia  kutafuta pozi zuri la kufurahia sex. Kwani nani alikupa agizo la ukilala ulalie mkono wa kulia au kushoto,au chali...kwa nini huwa unajigeuza ukilala? Ni katika kutafuta pozi la kuenjoy usingizi alotuumbia Mungu hivyo hivyo na styyle za sex.
Zipo zaidi ya style 100 za sex ila nyepesi 15,inategemea na flexibility ya miili yenu wotw wawili.
NB: *_Kilicho marufuku na dhambi kwa raha zenu zoote,kwa mifumo yenu yote, style zenu zote msifanye machukizo ya kuingiliana kinyume na maumbile(msibadiri matumizi ya asili ya mwanamke au mwanamme)neno limesema hivyo._*
👉Kwa suala la nani wa kuanzisha zoezi la kunlbadiri style kati ya mwanamke au mwanamme ni yeyote ila Kisaikolojia, kabla ya tendo la ndoa mwanamke anakuwa na aibu, na akili inashuka, wakati huo mwanaume hana aibu,aikili inachaji asilimia mia, sex ikianza in and out...mwanaume anapoteza akili(akili inashuka) mwanamke ujasiri unaongezeka na akili inaongezeka, na controller wa game ni mwanamke ... Shida maarifa kwa wana ndoa zero,hakuna watu wa kujitoa muhanga ku calculate mambo ya mahusiano kwa kina, tunaishia kufundishana kanisani MSINYIMANE,MTII MMEO NA MPENDE MKEO semina zote. Hii ndo Shida .Uliza wana ndoa wenye umri miaka 15 mpaka 50 kwenye ndoa, usikie haya tunayo fundisha na kufundishwa kizazi hiki kama wao waliyapata. Kwanza  kujadiri mambo haya ya sex enzi hizo ni dhambi kubwa,ukiyasikia unaingia maombi ya kufunga siku 3 kujitakasa. Mmmh shida kweli. Ndoa zilitembelea kwenye neema ya Mungu tu 100% bila maarifa mengine, sasa dunia ya sasa siku za mwisho maarifa yameongezeka,usipo kuwa nayo ndoa utaichukia.
👉Tendo la ndoa lina nogeshwa na vitu vingi tangu kuandaliwa na wakati linafanyika. Vitu kama kiss,romance,sex play nk.
Nijambo la kushangaza kukwepa romance ya mke wako au mmeo, moja ni dalili ya kutokomaa kisaikolojia katika ndoa, lakini kuna mambo ya msingi kwa wana ndoa kuyaweka vizuri, USAFI WA KINYWA, ili usiwe kero kwa mwenzako harufu mbaya. Pili busu haiwi ya fujo, iwe ya kitaratiibu,yakimahaba, iwe na maandalizi ya gentle touching,sex touch & sex play ndo romance inakuja automatically, siyo unavamia kichwa cha ntu na kuromance.
👉 Ndoa nyingi watu wanaishi kwa fujo kukuru kakara, hawana vionjo vipya,hawajui jipya,hilo hilo waliloanza nalo mpaka kuzeeka ndo hilo,mpaka ndoa inachosha, kazi za walimu,wasomi na watumishi wahubiri kunusurisha ndoa za wana wa Mungu kwa kufundisha kwa kina.
👉 *_Sasa tuhitimishe hii topic hivi, Tendo la ndoa kwa wana ndoa kwanza ni Huru, ni la raha,si la kulazimishana, siyo la kuibiana ni suala la makubaliano baina ya watu wawili, linahitaji kugusa feelings,kuongea kuhusu hisia zako kwa mwenzako, unataka akufanyie nini,ashike wapi, akaeje, tendo la ndoa halifanywi kibubu, gizani,ghafla linahitaji maandalizi ya kisaikolojia na kimwili,hakuna mwenye hati miliki ya tendo kuliko mwenzake wote mnapaswa kufurahia na kufikishana kwenye kilele cha raha_*

Kwa wakati wa tendo ongeeni raha unayo ihisi,unatamani uhisi nini zaidi,sema na mwenzako tukae hivi sasa,muulize mkao huo anahisi raha au kuchoka na kuumia,hapa ni mtu yeyote kuongea.
Shida watu tangu siku ya kwanza ya ndoa sex ni kifo cha mende,mpaka first born,2,5,.   Huu ni ushamba na kuchokesha ndoa na miili yenu.
Wana ndoa wengi wanafanya tendo la ndoa kama WAJIBU ,au kutimiza hisia zao ila si kama ENJOYMENT.

Badirika usiwe Regidy,Static, conservative utamchoka mwenzako.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078

No comments:

Post a Comment