💔💔 *MWANZO WA MPASUKO KATIKA NDOA*💔💔
*_Lecture from Material Adimu University(Group)_*
*Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor)*
WhatsApp 0755444078
_Shalom mwana darasa na mwana ndoa uliye nje ya darasa la chuo hiki cha mtandaoni kinacho kokotoa masuala ya Mahusiano kwa vijana na NDOA, hii ni miongoni mwa Lecture katika chuo hiki chini ya mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa Ev Elisha Kazimoto, karibu uongeze maarifa kuhusu *Viashiria vya mwanzo wa mpasuko katika ndoa* uwe makini katika ndoa yako_
❣Kwanza kabisa kabla ya kujua mwanzo wa mpasuko wa ndoa inabidi ujue dhana ya ndoa ndo utajua kwa nini mpasuko utokea. *_"Wakati unafunga ndoa mlifungishwa ndoa watu wawili wewe na mmeo /mkeo,waliowekewa pete 💍💍 ni ninyi wawili,mlokuwa mnashangiliwa ni ninyi wawili,mliopewa zawadi ni ninyi wawili,mlopelekwa Honeymoon/nyumbani baada ya harusi ni ninyi wawili, mlofunguliana nguo na kujuana miili yenu na kushiriki tendo la ndoa ni ninyi wawili, watu wengine wooote, wachungaji,mitume,manabii,wainjilisti,marafiki,wazazi,ndugu na majirani waliishia kuwatazama,nakuwatakieni maisha mema na wengi waliishia ukumbini au sebuleni na kama kuna yeyote alifanikiwa kufika chumbani kwenu ni siku hiyo tu hapamuhusu tena..."_* hiyo ndo dhana ya ndoa uliyoingia inakuonyesha wahusika wa raha na taabu ni ninyi wawili tu na Mungu wenu.
❣Ndoa inakuwa tamu na raha endapo wawili wanaweza kukabiliana na changamoto za maisha kama watu wawili na Mungu wao.
❣Ndoa yako inakuwa na heshima,na mwenzako umamuona wa maana pale kukiwa na USIRI wa maisha yenu ya ndoa,raha na changamoto zenu mzijue ninyi na mzishugulikie ninyi, hapo ( *_hakuna mzazi,ndugu,mchungaji wala shemasi wala mtume na nabii_*)ni ninyi wawili tu,hapo ndoa yenu itaenda miongo mingi kwa utulivu na upendo na furaha.
❣Ndoa ina utamu kama hutatengeneza mazingira ya kuichoka na ukajua namna ya kushughulikia vyanzo vya mpasuko.
*_Sasa baada ya kuiangalia dhana ya ndoa katika kuwepo kwake,nikupeleke katika mazingira yanayoweza kuipasua ndoa yako Kisaikolojia, kiroho mpaka kimwili_* ukiyajua hayo utailinda ndoa yako.
👉Kwanza inabidi ujue mpasuko wa ndoa kisaikolojia tunasema unaanzia Katika Saikolojia(Akili/Hisia) ndo utaona unatokea mpasuko wa kiroho(kuacha wokovu au kuanguka dhambini)na kumalizikia kimwili kutengana kabisa(Divorce)💔kuachana. Lakini mpasuko huu usababishwa na matendo ya kisaikolojia (kihisia kuingia dosari) fuatana nami ujue kona hizi;
💔 *Kona ya kwanza ya Mpasuko Kumuona wa kawaida sana mmeo/mkeo* Wanasaikolojia tukisemaga mambo haya madogo watu huyaona yakawaida sana maana walitegemea yasemwe makuubwa,kumbe ndoa haibomolewi kwa kuwa mwanaume hujajenga nyumba,kununua gari,huna pesa za matumuzi ya familia,hivyo ni vitu vya nje vya hitimisho la vidogo vya kihisia. SIKILIZA....
👆👉Miongoni mwa ngome ya hisia inayo linda mahusiano ya ndoa ni kulinda *Upekee wa huyo uliye mchagua* yaani maamuzi ya kuoana na huyo ukawaacha wadada wote,vijana wote ukaambata na huyo kisaikolojia iliashiria huyo ni *Unique*(sio wa kawaida) sasa kuna mambo ukiyafanya kwake,uliongea kwake mpaka akaona unafaa,yakianza kubadirika,maana yake unafuta upekee na kuweka ukawaida utakao pasua hisia zako kwake,na hisia zikiisha pasuka💔ndoa hiyo inaanza safari ya kuelekea kaburini.
👉 *Utajuaje mwenzako anaanza kufuta upekee wako na kukuweka katika ukawaida utakao pelekea ndoa kupasuka?*
1⃣Kuna lugha hakuwai kukuambia sasaivi anakuambia.( kuna lugha ngumu ambazo kabisa msemaji anajua hii itamchana moyo,itamtoa machozi,itamfikirisha lakini itamfanya ajione duni UKITAMKIWA) Mfano: _Wanaume huwa mko wa ovyo, wanawake hamnaga akili, kwenu ninyi ni watu wa ajabu, huna pa kwenda wewe nikikuacha,sioni faida yako au umuhimu wako humu kwangu,nilikosea kuoa,kuolewa, laiti ningejua nk,nk_ lugha hizo ukianza kuzisikia jua ni mwanzo wa kuondolewa kwenye umaalumu(upekee na kuwa wa kawaida)na zikizoeleka masikioni mwako saikolojia ya mpasuko wa ndoa itachukua nafasi kupelekea mpasuko wa kimwili na kiroho kwa waliookoka(kuachana na kuanguka dhambini) kwa watu wa kawaida Usaliti na visasi vitachukua nafasi mpaka hapo ndoa hakuna tena.
2⃣Ulikuwa unashirikishwa mambo ya mipango mbalimbali ya familia,kwa sasa unashtukia hili limefanyika,unaambulia kupewa taarifa ya yaliyo tekelezwa au unayaona yamefanyika ila huna maelezo yake. ( _Mpaka hapo jua nimeisha kuwa wa kawaida,sina umaalumu tena niliokuwa nao naulizwa kwanza,iki kikoje,nifanyeje hapa,unaonaje hakuna tena)jiandae kisaikolojia muda unavyozidi kwenda mtaachana msipo chukua hatua za dhati.
3⃣Ulikuwa ukimkosea mwenzako au akikukosea,haraka sana unasema samahani,au unaombwa samahani, ila sasa kimya kimya,ukilalamika unapewa majibu makali na magumu. ( _Msamaha ukishaanza kuwa mgumu kuombwa au kutolewa jua umekuwa wa kawaida,wewe na makosa au maumivu ni haki yako kukaa nayo_) ndoa hiyo inajiandaa kupasuka.
💔 *Kona ya Pili ni Kupeleka kesi ya ninyi wawili kwa mtu wa tatu yeyote awasuruhishe* Kisaikolojia hatuamini na ndivyo ilivyo mtu wa tatu kuwaletea amani na maelewano yenu wawili, haitatokea na haipo,kinacho fanyika pale mmejichezea saikolojia zenu kuzivisha hofu ya watu ila mgogoro wa nafsi uko pale pale na unakua taratibu. *_Na ndiyo maana uliza,fanya uchunguzi wana ndoa walioshitakiana kwa kosa moja,ndo ulikuwa mwanzo wa kesi ya pili,ya tatu,nakuendelea hata mkikaa miaka 10 bila kushitakiana,lazima ufa mliouwela utaibua shitaka lingine hata kama mna miaka 50 katika ndoa mtashitakiana tena_*) hakunaga msuluhishi wa hisia,kuna msuluhishi wa maslai(pesa,chalula,mavazi,maendeleo nk)ila hisia msuhishi huwa ni nafsi yako tu,uigeuze iamini kile unachotaka kukiamini. ( *_Narudia tena,ukiktaka kukomaa kisaikolojia katija mahusiano ya ndoa, Mzazi,Mchungaji wako,ndugu na rafiki Hatokupa majibu ya kuponya HISIA ndoa ni hisia siyo vitu,ninyi wawili kwa changamoto yoyote,tatizo la mwenzako kero IMALIZE WEWE NA YEYE bora ikuchukue hata miezi,siku na masaa ila muimalize ninyi_*)Uliyezoea kushitaki shitaki kila mkihitirafiana na mwenzako ndoa ya utulivu na amani hutoipata,ila utakuwa na vipindi vya mapumziko ya migogoro ila siyo suluhisho la migogoro. Ambaye hujawai mshitaki mwenzio omba na hakikisha hauanzishi safari isiyo isha ya migogoro na mashitaka.
👆👉 _Hata ofisi zetu za wanasaikoloji(Counselors hatutatui migogoro yako,ila uzuri na ubora wa wataalamu Nikukupa maarifa,mbinu wewe binafsi uende ufanye marekebisho ya makosa na hitirafu tunazo kuonyesha,hapo unaufuta mgogoro wote._)
💔 Kugomea tendo la ndoa au kushiriki kwa masharti Hapa kuna hitirafu nyingi,kwakuwa ni tatizo ndani ya tatizo, yaani tendo la ndoa ni la Hisia halafu lipo katika kuharibu hisia,mpaka mfanye tendo la ndoa kunahitaji kutengeneza mazingira ya utulivu wa akili,inayoshawishi kuibua hisia za kuhitajiana kimwili, sasa ikitokea mambo yaumizayo yanaanza kujengwa katika moyo wa mtu uua hisia,kuhitaji tendo la ndoa kunaanza kuwa kugumu,ikifikia hatua mnaona ugumu wa kushiriki tendo la ndoa,mwaweza pitisha wiki,1,3,5,miezi mpasuko wa kisaikolojia tayari upo unafuata wa kimwili. ( _Hakikisha unaepuka maneno,lugha,matendo na mazingira ya kuua hisia zako na za mwenzako,ili muendelee kushiri tendo la ndoa kwa amani na Uhuru kwakuwa tendo la ndoa linawaunganisha kihisia na kuwaunga pamoja kimwili na kisaikolojia na kuchochea upendo kati yenu_)
❣❣ *_Hii ni lecture ya kwanza usikose mfululizo wa lecture hizi katika chuo chetu cha Material Adimu cha mtandaoni,tumalenga kuimalisha Mahusiano ya vijana na mahusiano ya ndoa Kiroho na Kisaikolojia, tumepanua wigo wa kusaidia watu bapo tuna pia Darasa la Tiba ya Kisaikolojia kwa mahusiano na ndoa( Psychological Healing Class, Nitalinda Ndoa yangu, Paradise University)hayo ni baadhi ya magroup yaliyo branch ya chuo hiki. Kutana na Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto(Group Admin and founder)katika madarasa yote hayo upate kupona._*
WhatsApp 0755444078
Fb Elisha Kazimoto
Instagram Elisha Kazimoto
Twitter kazimoto_elisha(Elisha kazimoto)
Blog Materialadimuuniversity2017
Google Andika MATERIAL ADIMU utakutana na masomo mengi kwenye blog.
*_Mahusiano na ndoa havina mzoefu na mkongwe vinahitaji kila siku uongeze Maarifa mapya_*
@Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)
Sunday, 10 December 2017
MPASUKO WA NDOA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment