Friday, 31 March 2017

WAKIMBIZE MAADUI ZAKO

🗡🗡🗡 *KIMBIZA MAJESHI YA ADUI WALOPANDA JUU YAKO* 🗡🗡🗡
    _0755444078_
  *Ev Elisha Kazimoto*
_Shalom mwana maombi,mtu wa vita,uliyenolewa na Bwana upigane na ushinde katika kila vita, leo ni Mkesha wa *Operation Kimbiza Adui zako hadi watokomee*_
*YEREMIA 50:41-44*
_41 Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia._

42 Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli. 
44  *_Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?_*
👉Kila mara yanatumwa majeshi yaliyo elekezwa kuvuruga maisha yako, kuvuruga ndoa,uchumi,elimu na mfumo mzima wa maisha.
👉Majeshi hayo(mapepo na wachawi) yanatumia mazingira yako kukutia katika mazingira magumu.
👉Majeshi ya vita ya maadui mengine yanatoka kwenye familia,ntaani kwako,ofisini kwako na hata kanisani kwako yote kasi ni moja yazingire maisha yako na kuua yote uliyo nayo.
👉Tazama jeshi hilo linapanda na silaha za(magonjwa,chuki,mauti,dhoruba,umaskini,mikosi na nuksi) silaha zinalengo la kukuzimisha na kukupunguzia nguvu ya kushinda
✍ *_Lakini tunaye Bwana atushindiaye,simama kama mwombaji utoe upanga wako uwakimbize maadui na usiwaache kuzingira maisha yako,piga,ponda ruhusu silaha za Mungu ziwatawanye,kimbiza...Amuru wapigwe kwa mapigo,vunja miguu yao,wakimbize wasionekane tena katika mipaka yako_*
Maombi yetu huwa ni moto na kauli zetu zenye muunganiko wa Neno la Mungu huwa ni Upanga mkali hakuna adui wa kusimama mbele yako ukianza kuwasha moto.
*_Yoshua 1 : 5 - Hapatakuwa mtu ye yote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha._*
👉Anza kusema mchawi,huruhusiwi kusimama mbele yangu,magonjwa hurusiwi kusimama mbele yangu, nguvu ya kufeli darasani hurusiwi kusimama mbele yangu, umaskini,migogoro ya ndoa,utasa na kukataliwa hamrusiwi kusimama mbele yangu *Kimbia mtoweke mbele yangu* safisha mazingira yako,mipaka yako isisikike harufu ya maadui.
   *By Ev Elisha Kazimoto*
         _0755444078_

No comments:

Post a Comment