*ADHABU INAYO MFAA ADUI YAKO NI APIGWE UPOFU*
_Na Ev Elisha Kazimoto_
*0755444078*
_Shalom mwana wa Mungu,mpiganaji wa vita ya kiroho,katika mkesha wa leo wa maombi ya operation *PIGA UPOFU ADUI APOTEE NJIA* ninakuletea ujumbe wa neno la Mungu utakao kuongoza katika vita hivi na utwae Ushindi wako kwa jina la Yesu_
Kabla ya kuanza mapambano lazima ujue *Sumu,Hila,Uuaji na Ubaya wa Adui* katika maisha yako.
*Mithali 19 : 21 - Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama*
*_Maadui wote hawa uwaonao kwenye ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili(Mapepo na Wachawi,wanadamu) ndani yao wamejaa Hila na sumubyakuua mafanikio yako,maisha yako ya kiroho,hyduna yako,ndoa yako,uchumi wako,kazi yako na ofisi yako hata uzao wako na Afya yako,waweza kuonekana kwa macho wanacheka,lakini ndani yao na mikakati yao na vijao vyao vya siri ni Kuua_* sasa hii ni Saa ya Kuwapiga Upofu Wapotee Njia.
*MWANZO 19:9-11*
9 _Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango._
10 Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.
11 _Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango._
✍Kuna ufunuo mkubwa katika mistari hii na tukio la ujio wa Malaika kwa Lutu na Ghasia za watu waovu kuwatafuta malaika wawatende mabaya.
✍Katika maisha kuna Vitu vya baraka vinaletwa au vimeletwa na Mungu katika maisha yako vikufanikishe,vikuinue vikusaidie, lakini kuna maadui wamevivizia na wanavisonga wakidai vitoke kwenye maisha yako,wanahitaji kuviharibu.
✍Wachawi wameizonga familia yako,ndoa yako uchumi wako mpaka hauna amani(kama watu wa sodoma walivyo izonga nyumba ya Lutu wakiwataka malaika wawatende uovu,hata Lutu akakosa amani)Suluhisho lilikuwa nikuwapiga Upofu watu hawa,wakapotea njia biashara ikawa imeisha.
✍Usiwatolee maadui vitu vyako vya thamani kwasababu ya hofu kwao(kama Lutu alitamani awape Mabinti zake mabikira ili wasiwasumbue wageni wake) *Usiwape, Mwambie Bwana Wapige Upofu wapotee njia nisonge mbele*.
✍Je,kuna watu wanakutelemkia katika maisha yako?wamekuzingira kona zote huoni pa kutokea,unahisi maisha magumu? Usiogope,yupo *Bwana Mpiga Upofu kwa Maadui* mwite sasa awapige Upofu hao nao watajikuta mikononi mwa adui zao.👇👇👇👇
2 _Wafalme 6 : 18 - Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha._
✍Adui yako hawezi acha kukufatilia katika maisha yalo,ndoa yako,ofisi yako au elimu yako kama *Bado Anaona* macho ni taa,yanasaidia kufatilia,yanaonyesha njia yakupitia,ili *Adui Aache Kukufatilia* Mpige Upofu,Ziba macho yake,atapotea NJIA.👇👇👇👇
_Luka 11 : 34 - Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza._
✍Sasa twende kutoa adhabu kwa kila adui aonekanaye kuwa msumbufu katika maisha yetu,juu ya kanisa la Bwana,kazini,ofisini,katika ndoa,darasani,kwenye Afya,kwenye uchumi nk👇👇👇👇👇
_Kumbukumbu la Torati 28 : 28 - Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;_
*Mpige Adui kwa Wazimu,na Upofu apotelee mbali kwa jina la Yesu,kinywa chako ni Upanga,anza kushulikia wachawi hao*.
*By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)*
0755444078
No comments:
Post a Comment