Tuesday, 14 March 2017

SAIKOLOJIA YA WAKAKA KATIKA MAHUSIANO

*SAIKOLOJIA YA VIJANA WA KIUME KATIKA MAHUSIANO*
       _Ev Elisha Kazimoto_
      *0755444078*
_Shalom mabinti,leo nahitaji kuongea na mabinti,ambao bado hawajaolewa,wanatafutwa,na wao wanatafutwa,wako tayari kupokea maombi ya kijana kulingana na vigezo ulivyo jiwekea_ Katika uchambuzi huu kuna vitu mtoto wa kike unahitaji kuvijua na kuviwekea umakini,maana wengi *Wamejikuta wanakaa bila kuolewa(wanachelewa kuolewa)si kwamba ndo malengo yao au mpango wa Mungu ila nikwasababu walishindwa kujua saikolojia ya vijana walio mpitia kumchumbia,wengine wakaishia kutopata mtu tena,wengine,wakaishia kuchumbiwa tu bila kuolewa,wengine wakaishia tumiwa tu kimwili,kuzalishwa na kuwa chombo cha starehe na kijana kujie dea* Nini kosa, *_Tambua Saikolojia ya vijana uweze kuingia kwenye ndoa kwa wakati na mtu sahihi_* tuwe pamoja katika uchambuzi huu,Ndoa sahii ipo si bahati ni mipango na maamuzi ( _Ev Elisha Mwanasaikolojia atakujuza maarifa hao_)
✍ *_Kosa kubwa wadada wanafanya ni kushindwa kutofautisha upendo halisi wa Ndoa na Upendo(Tamaa ya Ngono)_*wadada wengi wakiona kijana amemu approach basi wengi wao hujiachia,na pale wakiambiwa wewe ni mzuri,nimeona unafaa kuishi nawe,na hakika tutaoana,basi hapo ndipo saikolojia ya kike uingiliwa,na Wao uhamisha maisha yao yote,(nafsi,roho na mwili)na kuyaweka Rehani mikononi mwa kijana na *Hapo ndo saikolojia ya kiume uanza kukua na kutawala*
👉 Binti unapaswa kujua hakuna kijana yeyote duniani wa kuapproach binti kwa maneno mepesi yasiyo na ushawishi wa kitu kinaitwa NDOA( labda kama anajua wewe ni malaya wakuuza mwili anahitaji kununua) _Vijana wote wanasaikolojia moja wanaamini hivi, *Binti yeyote duniani anahitaji Ndoa,kuolewa na ndo Neno linawasumbua,hakuna binti anahitaji kuchezewa ila kuolewa,kwa hiyo lugha ya kwanza kumpata binti yeyote,uwe unamwitaji kingono kwa muda,au kumuoa ni mwambie Ntakuoa,atakupa moyo wake wote_
(kwa hiyo binti unahitaji kuwa makini baada ya kuambiwa ndoa,siyo mwisho wa usalama wa kujihakikishia ndoa,kuna safari nyingine ya pili ya kudhibitisha lugha ya ndoa,au ngono au ni partnership.
✍ *_Kosa kubwa la Pili wadada wanafanya ni Kujichumbia kabla ya Kuchumbiwa_* kuna kitu ni (Intrinsic force of love)msukumo wa ndani wa kupenda mtu hata kabla yeye hajakupenda, hapa wengi huchemka,unahitaji kuwa makini sana,ikitokea Unapata *_Intrinsic force of love kwa kijana_*kabla ya yeye kukutamkia kuwa anakupenda,usiju Ukajichumbia kabla ya kuchumbiwa unaweza ishia kuumizwa,au kupotezewa muda.
👉Kuna vitu wasichana wanashindwa kuelewa kwenye saikolojia ya vijana, *Kuna kupendwa, Kutamaniwa,na Kufurahiwa* Kijana Akikupenda Anatamka nia yake kwa uwazi,na anakuwa na anaanza kutamani kupata jibu,na akipata jibu kuna vitu ataanza navyo ntavibainisha mwisho wa uchambuzi.(Kwa kijana anaye kupenda usije ukajichumbia kumtengenezea mazingira ya wazi kuwa akuchumbie,kaa Nutral,mweshimu endelea na business zako,atakuja na utapendwa sanaa,ukijilengesha hata akija umepunguza asilimia za upendo na unaweza ukaachwa asije,au mkaishia katikati ya mahusiano.
👉Ukitamaniwa,utasumbuliwa sana kwa pressure bila uvumilivu na hakutakuwa na neno jipya la lengo kuu la maisha ya ndoa,kwa kijana huyu,ukijichumbia kabla ya kukujia maadam unaona anakufatilia,au unaona nikama ana mwelekeo wa kutosema utaishia kuumizwa au njiani.
👉Kuna kijana anakufurahia,yaani unampendeza,ulivyo tu ,mambo yako anakufurahia,anatamani kuwa karibu na wewe tu, (Ila hana mpango wa kukuoa)hawa ni aina ya vijana ambao hupenda Companion ship ya jinsia ya kike( *_anaweza kuwa rafiki yako wakaribu sana kama mchumba,mpenzi wako hata miaka 5,na ukala pesa zake za kutosha ila hautakuja kuolewa naye,mtaongea mambo ya ndoa,ya watoto ila hafanyi maamuzi ya kuku engage 💍.
👉(Kwa vijana wa aina hii 2,kutamaniwa na kufurahiwa binti ukijichumbia kabla ya kuchumbiwa utaumizwa),
👉(Kwa kijana anaye kupenda,atafunguka,usione anavyokuonyeshea kukuhitaji wewe ukamu overtake kujichumbiauta poteza nafasi yako na upendo mwingi aliokuwa nao kwako utashuka)
✍ *_Kosa kubwa lingine wadada wanafanya pasipo kujua au kwa kujua,ila nje ya saikolojia ya vijana ni Kutoa majibu mepesi katika maswali magumu,na kutoa majibu magumu katika maswali mepesi_* hii ni kama imekukoroga ila ndo ilivyo,unampoteza mtu kwa kutojua nyakati na saikolojia yake. Mabinti wengi akiwa hayupo katika nafasi ya Uhitaji mkubwa,aidha kuna kijana anamtarajia kichwani,au wakati alio nao yuoo kwenye chati ya mvuto mkubwaaa wa foleni za vijana,ndo muda mabinti hutoa majibu Magumu kwa 6a kukatisha tamaa,kudharau kwa vijana wenye maswali mepesi ya nimekupenda tuoane.
👉 Hapo majibu magumu yanatolewa yanayofanya vijana saikolojia zao ziinuke za kukudharau na kupeana taarifa kuhusu tabia zako,katika wale watakao pata taarifa zako za majibu yako magumu kuna watakao jitoa kuja kujusumbua wakuze upuuzi wako,kuna watakao kukwepa nakuonyana kutokuendea.(mpaka hapo upo hatarini kupata mtu asiye sahii au kuumizwa tu ,maana hawaji kukuoa ila kukukomoa)
👉Kuna muda wakati(miaka ya mdada inaanza kusogea,mvuto wa kubabaisha watu unaanza kupungua na walio kufahamu,kusumbua enzi hizo kuisha na kuwa tayari na watu wao au ndoa zao,saikolojia ya kike uanza kuyumba ndipo *Majibu mepesi hutolewa na wadada* muda huo kwa maswali magumu ya kufanya ngono ili muoane hupewa majibu ya Yes,maswali ya kuchumbiwa na mpagani,mtu wa imani dhaifu hupewa majibu ya Yes. (Hapa ndipo mabinti huzoa mimba,hupoteza ubikra,uchezewa na kuachwa,huacha wokovu ili uolewe,ndipo huanza kuwatafuta aliowapa majibu magunu kipindi kile,ili awape majibu mepesi kwa sasa)sasa ukikutana na kijana katili ulompa majibu magumu,saizi unampa mepesi hakuoi mpaka amekuchezea kimwili mpaka akuchoke,then akuache,au akuoe kwa kukuhurumia.
*Saikolojia ya Kijana Muoaji iko hivi*
👉Akikupenda anakufungukia kwa namna ya utilivu,adabu na kwa utaratibu.(hakai kimya baada ya kukusoma)
👉Ataeleza nia yake ya kukuoa itakayo ambatana na vitendo vya kauli yake.nia ya kuoa siyo ngono
👉Ataanza kukuleta katika mikakati ya ndoa,siyo simu na outing za I miss u,mwaaah,nakupenda tu,ila ni mikakati ya maisha ya baadaye.
👉Atakuheshimu kama mtarajiwa wale na atauheshimu mwili wako,atataka iwe heshima ya ndoa,hata hisia zikimzidia,aweza eleza hisia zake(matter of love)lakini atasimamia heshima yako na yake na ya Mungu.
👉Ataanza kukuingiza katika program za Kimungu ili kuandaa harusi na ndoa ya utukufu wa Mungu.
👉Ngono na uchafu wote,hutausikia kinywani mwake,bali kusisitiza usafi na uaminifu kati yenu.
_Mbali na hayo saikolojia ya kijana kama haina hiya,basi ndo saikolojia za wanao tamani,furahia uwepo wako_
Ulikuwa na mimi Mchambuzi mtaalamu wa mahusiano na ndoa, *Ev Elisha Kazimoto* (Baba Eve)
        *0755444078*

No comments:

Post a Comment