💍💍 *UKICHAGUA VIBAYA,UTAISHI VIBAYA,UKICHAGUA VIZURI UTA ENJOY MAISHA*💍💍
_Ev Elisha Kazimoto_
*0755444078*
_Shalom vijana mnaojiandaa kuoa na kuolewa,na wale mlo katika mahusiano ya uchumba,leo nasema nanyi kwa ufupi sana kuhusu Hatima yako itokanayo na uchaguzi katika ndoa_
*_Mithali 22 : 1 - Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu._*
✍Kuna changamoto kubwa kwa vijana katika kuchagua wenzi wao wa maisha,utata huu unakuja pale kijana anapotaka kupata mtu kulingana na Plans/Interests zake(hapa ndipo palipo na kichefuchefu)
✍Kila chaguo nyuma yake kunamsukumo wa *Matamanio,Lengo na matarajio na muono wa macho ya muhusika* hiki ndo kichefuchefu kilicho wafanya wengi walipoingia kwenye ndoa Waanze Kutapika na Kuishiwa nguvu za kuishi katika ndoa.
✍Sasa watu wanakosea kuchagua kwa sababu ya kuwa na *Msingi Mbovu wa Kiroho, Msingi mbovu wa Malezi,Mazoea Mabaya ya maisha,Makundi ya watu wasio na malengo, Mtazamo/muono usio na nguzo shawishi* Vijana kuwa na umakini katika maandiko hayo juu katika (Bold style)kilio na vicheko katika ndoa vimetokana na maneno hayo,hata wewe uliye katika ndoa, _Umepotelea humo au umepata faida kutoka humo_
✍Unahisi kwa nini Biblia inasema *_Heri kuchagua jina jema kuliko Mali nyingi_* Jina ni Mtaji na Mali nyingi ni Faida,sasa upofu mwingi kwa vijana ni kukimbilia kuchagua faida na kuacha mtaji, sasa siku zote hakuna faida bila mtaji,na sibkila faida ni halali au njema(mfano kuna wenye mali nyingi lakini wamezipata kwa kafara,dhoruma,wizi na urithi na Akili ya Kimaendeleo)hawa wote wanaonekana wamefanikiwa ila ndani ya maisha yao kuna maumivu na wengine kicheko.
✍Msingi mbovu wa Kiroho(yaani kutokuwa na wokovu halisi,au wokovu wa njia panda,michanganyo) kumewafanya vijana kuchagua wenzi kwa hisia zao na mitazamo yao na si katika mapenzi ya Mungu. _Mtu asiye na msingi mzuri wa kiroho hana mahusiano mazuri na roho mtakatifu hivyo hata wakati wa uchaguzi wa wenzi Roho wa Bwana huwa kimyaa,na kusababisha mtu kutumia akili yake na kuingia katika ndoa mbovu_
( *_Nikuulize kijana, hivi umeokoka kweli? Maisha yako ya kiroho yanaushawishi mbele za Mungu hata ukastahili kupewa mme/mke na Mungu?, hivi kona unazopiga na mabinti na vijana halafu unasema mimi namtumikia Mungu ni sahihii kupewa mtu mwema? Wangapi umewaonja na wamekuonja kwa ridhaa yako,halafu unategemea kuwa na ndoa sahii ya baraka?_* huo ndo msingi mbovu wa wokovu nauongelea urakao kufanya uchague bomu la ndoa.
✍Msingi mbovu wa malezi umezigharimu ndoa nyingi na umekuwa kitanzi cha uchaguzi wa mwenzi. Kuna watoto wamelelewa malezi yaskujiachia,wanafanya wanavyo taka,wanaonywa kwa kubembelezwa( Imewafanya vijana wawe na kiburi,kujiona na dharau)wakati wa kuchagua mwenzi lazima uumie. ( *_Kuna walio lelewa kwa kupewa maneno ya wewe utaoa/kuolewa kwenye familia tajiri, mtu mwenye pesa,dactor,lawyer,nk na kuwafanya wawe na jeuri,wawe na nyodo,kujikadiria,kupotezea vijana wanaokuja kuchumbia_*) Na hii ndo imewafanya wengi kuingia kwenye ndoa feki za tamaa zao na siyo mpango wa Mungu.
✍Kuna watu wamezoea vibaya kiasi kwamba wanahitaji mazoea hayo wapate wenzi walio na mazoea hayo( _Kuna waliozoea maisha ya kuhurumiwa,kudekezwa,kuheshimiwa hata ka ni kadogo,anakuwa anahitaji achukuliwe hivyo hivyo_)ifike hatua ujue mazoea ya kwalo siyo ya mwenzi utakaye mpata,jua kubadirika na muda na mazingira.
_Kwa ujumla, ndoa siyo taasisi ya ili mradi nimepata mtu wa kunioa,au wa kumuoa,ndoa ni zaidi ya kutimiza tamaa za mwili,kuzaa watoto na ku make life,ndoa ni chombo maalumu kinacho kuunfanisha wewe na Mungu au kukutenganisha na Mungu, chombo cha kutuliza maisha yako au kukupa Stress(msongo wa mawazo),kukupatanisha na watu au kukutenganisha na watu, Si kila ndoa mnapo oona kina pesa,mmeoana mnacheka nje ya utaratibu wa Kimungu ukahisi ita Last katika vicheko,bado safari ya ndoa ina mwitaji Mungu mwanzoni mwake,safarini mwakebhadi mwishoni mwake, kosa kubwa kwa vijana ni kuanza na Mungu ila wakati wa kuchagua na kuoana wana mtupa Mungu,ili waje wamuokote ndani ya ndoa hiyo ni bonge la Mistake_Mimi nakuhasa Anza na Mungu kila hatua na Mungu utasafiri vizuri na mpenzi wako hadi kifo.
*_By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve )_*
*0755444078*
Thursday, 13 April 2017
CHAGUO BAYA LA KUOA/KUOLEWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment