👑 *VITOTO (VISICHANA) VYA 2000* 👑
........................................
PART III
Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa
*Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)*
Phone :0755444078
2. *Mme uliye naye ni chaguo lako la kwanza na la mwisho ndo maana mkaoana* unadhani mlivyoanza miaka ya kwanza mlikuwa mnakinzana hivo? Mliishi vizuri, mlielewana, mlikosana na mkasahishana na mkaendelea na amani yenu na upendo wenu, na akuna aliyekuwa na uwezo wa kumvuta mbali nawe, kwakuwa Hekima zako na maamuzi yako, na uchaguzi wako ulikusukuma kumlinda kwa Wivu mkubwa akae kwako.
👉Ila ulipoanza kumuona kama amwendani, kama ulitafutiwa, kama msumbufu kwako, mkorofi kwako, Ukasogeza moyo mbali wa kumkubali kama Chaguo lako la furaha ambalo unatakiwa kulilinda, ndipo *Wajanja vitoto vya 2000 vilikuja na mbinu za Kuonyesha Kujali na kuthamini Uanaume wake* Wamefanikiwa, watafanikiwa kumpora kwako.
👉Kama ulimpata mmeo huyo kiuhalali,Ulioana naye kwa kukubaliana, Basi Unawajibu wa Kukubaliana Tena naye namna ya kuishi kulingana na Anavyopenda yeye na wewe unavyopenda mbali na hapo.. Utaporwa.
3. *Miaka mlokaa pamoja Humjui Mmeo!* Utaibiwa mapema sana.
👉Wanasaikolojia wanasema, ukikaa na mme au mke kuanzia siku 1 mpaka miaka 9, mkigombana na kuitirafiana ni haki yenu maana bado hamjuani vizuri.
👉Ila kuanzia umri wa miaka 9 nakuendelea mkigombana, na kuitirafiana kiasi kwamba msielewane mpaka ndoa yenu ijulikane kwamba *Mgogoro wa ugomvi wenu ni huu* Basi ninyi ni Wapumbavu msiosaidika, na Mmoja kati yenu alitakiwa ASIOE MPAKA UZEE AU ASIOLEWE MPAKA ubibi kizee. Kwa nini?
👉Miaka 9, 10, 15, 20.... *Ujui Mme wangu Anatekwa hisia na mambo gani?*
👉Ujui mme wangu ni mdhaifu kwenye mambo gani kihisia? Na hapa panaweza tumiwa na wajanja kumchukua kwangu?
👉Ujui mme wangu anachukia nini ukifanya?
👉Ujui kumdanganya mmeo mpaka akaona ni kweli japo unajua si kweli ila lengo uweke amani ya ndoa yenu.
👉Ujui namna ya kumfurahisha mmeo,hata kama amechukia au ana stress ni mambo gani ukiyafanya anarudi kwenye mood?
👑Sasa wanawake wengi wa 1980s, 1990s wamefeli hapo, Anakosea, Anajihesabia haki, Hajui namna ya Kumrudisha mme haraka kwenye mood kutumia vitu anavyopendelea, naye Anakaza Uso wa kununa mwanzo mwisho.
👑Kinachotokea ni nini, Vitoto vya *2000 viko makini na Neno Am Sorry Love, Am sorry baby, It will Never Happen Again, Sitakuumiza tena eeh?, Nambie unachotaka nifanye ntafanya ili uwe na Amani na furaha yetu irudi* Kwa maneno hayo machache MMEO ANAPORWA mbele yako asubuhi unaona.
4. Kuna Kosa la Kiufundi na la Kisaikolojia, wana ndoa wanafanya( mama) Kumuona mmeo wakawaidaaa, hana maajabu yoyote kama useless man(kwa kutumia Kosa au Makosa mlokosana). Ndo maana una Mtreat, unamchukulia kawaida, na haumpi heshima yake, uzito wake, na nafasi yake kwasababu ya mazoea na KUTOFUNDWA NA WAZAZI.
👉Changamoto kubwa ya Kizazi cha 1980s, na 1990s, na 2000s *Akija Fundwa na Mama Zao* wanafundana wao kwa wo mitandaoni na kwenye Saloon. Hapo hamuwezi kukaa na Waume, tutakuwa na Single Mother wengi na Wajane, na Walioachika wengi.
👉Hata wewe msomaji, moyoni mwako unajua, Mama Yako Alikufunda? Akakupa Miiko ya Ndoa na namnaya Kukaa na mme kwenye nyakati zote? Au Una Weza Kujivunia Ndoa ya Mama yako, aumaisha ya mama yako kwa baba yako ili na wewe Uwe na Adabu na heshima na utilivu kwa mmeo?
👉Haya mambo sisi tuliookoka Tueongezewa Jicho la tatu, Kuna Roho za kifamilia,kiukoo za Kupiga vita kwenye maombi na kwa kujilazimisha kwa vitendo kuzikimbia ili Ndoa yako idumu... Usipo kuwa makini unakuta Roho ya Bibi yako. mama yako, dada yako inakufuata wakati una Neema ya Wokovu ya kukuepusha na Nguvu hizo.
👉Huyo mmeo unayemuona wakawaida sana na hana jipya kwako,Ila pembeni yako, wamama,wadada, na hata wanaume wenzake wanamuona ni Mtu Special, mtu ambaye Atakuwa au anakuwa Karibu naye, kuitwa kwa jina lake *Anafaidi, Amependelewa* na wana WISH INGEWEZEKANA WAKAPATA HATA NAFASI YA SAA 1 waonyeshe unyenyekevu wao na heshima yao kwake wange fanya kwa bidii.
👉Hivi ndivyo Vitoto vya 2000 Uvizia hiyo nafasi, utakuta, *Vina nyenyekea, Vinaheshimu, vinatambua na kujali, maneno, hisia, sauti ya mmeo* sanaaaa ila wewe ujali hapo ndo Kuibiwa Uanzia hapo. Usipo badirika Mmeo anaibiwa kwa Heshima na Kusikilizwa.
👉Mama inabidi ujue kwamba mwanaume niliye naye Si wakawaida, afanani na wa wengine, huyu anaubora wake,sifa zake, na nguvu zake, lazima Nitambue hilo na nimpe heshima yake ili Aridhike na heshima yangu asirubuniwe na heshimaza za nje.
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)_
Phone: 0755444078
No comments:
Post a Comment