Saturday, 28 June 2025

VITOTO VYA 2000(PART II)

👑 *VITOTO VYA (VISICHANA ) VYA 2000* 👑
........................................
              PART II
_Na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa_
Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)
Phone: 0755444078
*26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;Waefeso 4:26*

*27 wala msimpe Ibilisi nafasi. Waefeso 4:27*
👑Ukiichunguza mistari hii nikama imeruhusu Kufanya Makosa, ila umepewa Taadhari Makosa kama binadamu, ila Uwe makini Makosa yakiendelea sana yatazaa Hatari ya Muharibu Kupata nafasi ya Kuharibu. ( *Nitarudi kuchambua*)
👑Wamama wenye Umri mzuri kwenye Ndoa Msiokuwa Vitoto vya 2000, miaka 30-45 mna kwama wapi kwenye Ndoa Mpaka Mnaibiwa Waume zenu na vitoto vya 2000?
👑Nina Maswali kadhaa naomba ujiulize vema halafu ntakwambia Ulipo kwama, Kama wa Kupona Upone kama unaendelea kulia na kulalamikia vitoto vya 2000 uendelee hivo hivo mpaka unazeeka ila Utabaki Sanamu la kwenye ndoa, una mme mwili, ila Roho na Hisia ziko kwingine, au Utaachika.
👑1️⃣ Hivi uliingia kwenye ndoa kwa hiari au kwa kulazimishwa?
👑2️⃣Hivi Mme uliye naye Ulitafutiwa au mlipendana na mkaona ndo mnaweza ishi pamoja?
👑3️⃣Hivi kwa miaka uliyokaa na mmeo Humjui mpaka anakuja mtu mgeni kumjua kuliko wewe na kufanikiwa kukupora?
👑4️⃣Hivi unajua Mmeo niwakawaida kwa watu wengine kama wewe unavyohisi niwakawaida kwako?
👑5️⃣Hivi Unajua kwamba Wezi, Mwizi Aibagi sehemu yenye ULINZI mkali,  wanaibaga sehemu iliyoachwa wazi au bila ulinzi?
👑Hayo maswali 5 ukielewa moja moja Utarudishiwa akili yako na Utakaa na mmeo kwa Utulivu sana na kufurahia na Autaibiwa kizembe tena.
👑Vitoto vya 2000 vimefanikiwa kuiba waume za watu kwa Kutumia Mapungufu ya wanawake wasiojali na hasa *Wanawake wa Kilokole* ambao wametumia MWAVULI WA WOKOVU kufanya Ubabe na kuishi kama wajane wasio na wanaume Wakidhani *Neema ya Wokovu waliyo nayo wao na waume zao Ni Mnyororo mkali usio mruhusu kujitikisa kwenye ndoa, atatulia hata angenyanyaswa kwenye ndoa* hili ndilo LANGO LA 1 LA UHARIBIFU WA NDOA ZA WANA WA MUNGU.
👑Nikinukuu maneno ya Askofu mkuu wa Kanisa la Kiroho la TAG, katika kongamano moja aliwahi kusema *Wanawake wa kilokole ni WAPUMBAVU walio wengi wameshindwa kuishi kama wanawake kwa waume zao*......... Mwisho wa kunukuu( nenda kaitafute YouTube).
👑Sasa vitoto vya 2000 vimeiba na vinaendelea kuiba na vitaendelea kuiba Wanaume wa wanawake wa miaka ya 1980s,1990s kwa sababu zifuatazo za maswali yale juu 5.
1. *Mwanamke uliingia kwenye ndoa kwa hiari Kutimiza Matakwa ya Ndoa* Kama ukufundwa na Wazazi wako(mama yako), basi ulipata hasara ya kwanza... Ilibidi ujue Matakwa ya Ndoa unayoiendea Uende Ukayatimize kwa bidii (HUWEZI KUIBIWA MME Ukiwa unatimiza Matakwa ya Ndoa)
👉 Kiroho(Kiimani/Kikanisa)Ulitakiwa ufundwe na mfungisha Ndoa akueleze matakwa ya ndoa uliyoichagua kwa hiari uende ukayatimize kwa moyo wote, (kama ukumsikiliza vizuri ulikuwa unawaza usiku wa Honeymoon) hiyo ndo Hasara ya 2 Usingeibiwa mmeo na vitoto vya 2000.
👉Nimezungumza *Kufundwa, na Kufundishwa* Ujue Matakwa ya Ndoa na uyatimize kwa bidii huwezi ibiwa mme.
👉Vitoto vya 2000 *Vinafundwa na Mitandao ya Kijamii Matakwa ya ndoa na Havijaingia kwenye ndoa Vinatumia Maarifa hayo Kuwapata Wanaume Waliokosa Furaha ya Ndoa kwasababu mwenye ndoa(mwenye mme wake) kashindwa kutimiza matakwa ya ndoa*
👉Baadhi ya Matakwa ya ndoa ni yapi?
A) utii kwa mme wako, hapa si suala la kumpigia magoti mme, ila mme yeyote anahitaji kuona,kukaa karibu na mke wake ambaye Kile anachomwambia kufanya, kutofanya, kufuata, Anakitii na hata kama hakubaliani nacho *Analugha,Matendo ya Staha na ushawishi* kwa mme wake kughairisha kile kitu.
👉Vitoto vya 2000 viko makini Kutii na kusikiliza, na kutekeleza MATAKWA ya mmeo kwa GHARAMA zozote, ila wewe Unarumbana na kuzozana, au Majibu ya mkato kwa  mmeo yasiyoonyesha unyenyekevu kwake hapo( Hutoboi) Wanamchukua mmeo mapema sana.
👑Ongeza Umakini na Adabu kwa Mmeo.
*Sehemu ya Pili imekamilika karibu sehemu ya tatu*
_Ulikuwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)_
Phone : 0755444078

No comments:

Post a Comment