Saturday, 28 June 2025

VITOTO VYA 2000(PART I)

๐Ÿ‘‘๐Ÿ‘‘ *VITOTO(VISICHANA) VYA 2000* ๐Ÿ‘‘๐Ÿ‘‘
_Imeandaliwa na Mwalimu na Mtaalamu wa Saikolojia ya Mahusiano na Ndoa_
*Ev Elisha Kazimoto(C.E.O-GFI)*
Phone: 0755444078
........................................
             *PART I*
_Shalom shalom wale mnaojiita watoto wa 1980s,1990s na wale mnaoitwa watoto wa 2000 wote kwa pamoja Amani ya Bwana iwe nanyi_
๐Ÿ‘‘Kuna lugha hii iliyo shika kasi hasa katika mitandao ya kijamii na kwenye vinywa vya Wanawake wengi walio kwenye Ndoa wakijaribu *Kubainisha Hatari, Ubovu na Ubaya wa Vitoto vya 2000(visichana)* kama Virusi hatari kwa Ndoa zao.
๐Ÿ‘‘Baada ya Kusikia na kuendelea kufanya Utafiti wa Kisaikolojia kujua Chanzo cha Jina hili na sifa hizi kushika kasi kwa nyakati kama hizi, Kama *Mwanasaikolojia na Mshauri wa Ndoa nikapata Cha Kuzungumza* na Kusaidia Kizazi cha 2000 na cha miaka ya 1980s,1990s.
๐Ÿ‘‘Nianze na Neno la Mungu chimbuko la Hekima zote za Saikolojia, kabla sijaenda kwenye Kweli za Wanasailolojia.
*Yeremia 31:22 Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.*
๐Ÿ‘‘Enyi wana ndoa, Enyi Wamama, Kabla ya Kutoa Majina yoyote na sifa zozote njema au mbaya kwa kizazi kinachoibukia, Lazima kwanza Turudi kwenye Neno la Mungu linasemaje Kuhusu Ndoa yako.
๐Ÿ‘‘ *Ndoa Ni Taasisi Nyeti sana* Inayo hitaji Mtu mwenye akili Timamu ( _Nimewahi kuandika makala miaka ya 2017 inayosema *Ndoa inahitaji mtu Mwenye Akili Timamu* nenda kwenye blog yangu au Google andika hivyo ( Ndoa inahitaji mtu mwenye akili Timamu Material Adimu_) hii makala ina dawa nzuri ya uponyaji kwa wana ndoa.
๐Ÿ‘‘Sasa Kumeibuka wimbi kubwa la Wadada wadogo kiumri (vitoto vya 2000 na Mashangazi ya miaka 1970s Kumiliki *Wanaume wa wamama wa miaka ya 1980s, 1990s* kiasi ambacho kimezaa Lugha mtandaoni, Vitoto vya 2000.
๐Ÿ‘‘Hii Lugha ina maana gani kwa wana ndoa? Hizi lawama kwa kizazi cha watoto wadogo mabinti wa 2000 kuzoa Umaarufu usio na sababu wa *Kuiba, Kubeba, Kumiliki wanaume wa watu umetoka wapi?*
๐Ÿ‘‘Kisaikolojia, Kuna *Makosa Makubwa* yanafanywa na Wanawake, wanaojiita *Wanawake wa 1990s, 1980s wenye ndoa zao* makosa ya Kiulinzi yaliyo toa Nafasi nzuri sana ya Bure kwa *Wajanja, Wasichana werevu wenye haja ya Mapenzi* Kuchukua waume zao.( Nitaelezea.....)
๐Ÿ‘‘Kiroho, Wanawake hawa wenye ndoa wamefanya Makosa makubwa ya Kibiblia ambayo, *Wamempa Ibirisi Nafasi* ya Kushambulia Ndoa zao Vizuri bila kutumia nguvu kubwa.
๐Ÿ‘‰Hapo unahitaji kutulia kujifunza vizuri usikosee.
*Hii ni Sehemu ya Kwanza, karibu kuendelea sehemu ya pili*

No comments:

Post a Comment