👑 *VITOTO(VISICHANA)VYA 2000* 👑
........................................
PART IV
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto( CEO-GFI)_
Phone :0755444078
5. *Wanaiba Pasipo na Ulinzi.* Ni makosa ya kiufundi kulalamikia mwizi wakati unajua KUFURI YAKO AU MLANGO WAKO NI MBOVU.
👉Suala la ulinzi ni changamoto kubwa kwa baadhi ya wanawake, Ogopa kitu Biblia imetamka wazi MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME.....
👉Anaye linda anajua *Mali zilizomo ndani, Thamani ya kilichomo ndani, na anajua Aina ya wezi watakao kuja kuiba wanapeleka wapi*
👉Hivi unadhani kuna siku mwislamu atakuja Kukuibia Nguruwe? Au Mlokole kukuibia kreti za bia na sigara? Wezi wa vitu husika wanajulikana wataiba nini na kuvipeleka wapi.
👉Sasa Mwanamke Ukiambiwa Kumlinda Mwanaume, *ULINZI WA KWANZA NI KULINDA HISIA ZAKE* Siku ukidharau Hisia za mmeo ndo siku Umeanza kumpoteza kwa wezi.
👉Ukiambiwa Kumlinda mwanaume, *ULINZI WA PILI NI WA HESHIMA YAKE* Mwanaume akigundua kuna namna Haumpi heshima yake Ataitafuta kwa watu wengine wanaofanana na wewe(mwanamke/wanawake).
👉Ukiambiwa kumlinda mwanaume, *ULINZNI WA TATU HAKIKISHA UMEMPA UHURU WA KUSEMA CHOCHOTE KWAKO NA UMSIKILIZE* Ukiona mwanaume Ameacha Kukusema iwe kwa uzuri au ubaya kukurekebisha, akaona anaposema unamuona kero...Aisee Huna mme kashaenda kuwasema wengine waliotayari kusemwa na wakafuata.
👉Ukiambiwa Kumlinda mwanaume, *ULINZI WA NNE, MRUHUSU NAFURAHIA USUMBUFU WAKE KWENYE TENDO LA NDOA kama ni mzima wa eneo hilo siyo mgonjwa.
👉Miongoni mwa ALAMA ZA KUKWAMBIA BADO UJAIBIWA MME NI KUONA USUMBUFU WAKE KWENYE TENDO LA NDOA mara kwa mara kama dozi ya dawa.
👉Ukiona mme wako AMEACHA USUMBUFU kwako, kero juu ya tendo la ndoa kuna mambo 3 yametokea.
1.Amepata mbadala wako
2.Ni mgonjwa kwenye mifumo yake.
3.Ujiongezi kumfurahisha kitandani...Mpaka hapo Utaporwa.
👑Nini ufanye katika usumbufu wa mmeo katika tendo la ndoa, SOMA Majira, Tumia Kauli Tamu na Buni Mbinu za Ktuliza hisia kirafiki.
👉Tafauti na hapo wanasaikolojia wanasema unaweza Kaa na mtu aliyekuacha zamani kihisia ila uko naye kimwili, ila kuna mtu anamiliki Hisia zake, na Akimuona Anajisikia Raha na Amani kuliko wewe.
👑Kwa hiyo, Lugha ya *Vitoto vya 2000* ni vikali, Pisi kali, vinavunja ndoa za watu, Si za kweli, kama ni Sura uzuri walio nao ni wakawaida kama wako ndo maana na wewe Uliolewa ni kwasababu ya uzuri ulio mdatisha mmeo, kama ni Maumbile wana kama yako ndo maana mmeo alikuoa wewe, mnachotoafutia wewe mama wa 1980s, 1990s ni kwamba *Wewe Hauko Serious na Mali yako kuilinda, Wao wako serious na Kutafuta mtu aliyeumizwa kwake wampe furaha* Kazi yako kubwa OGOPA KUMUUMIZA mwenzako madaktari uchwara wengi mtaani watamvamia kumtibu hutampata, na akiponea mikononi mwao hao madaktari wa mtaani (vitoto vya 2000) unakazi ya kumrudisha kwako kihisia na kimwili.
NB: _Vitoto vya 2000 niwashauri na ninyi, si kwamba mtaa kwenye chati mpaka mfikishe miaka 30, 40 mtafutika, tulia mtafute ndoa zenu, jifunzeni kutokana na makosa ya dada zenu mjipange kutoyafanya pale mkipata ndoa zenu, mbali na hapo nanyi mtafanya makosa yale yale nanyi watakuja *Vitoto vya 2020* vitawatoa machozi kama mnavyota machozi ya wenzenu wa 19980s na 1990s_
Ulikuwa nami mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa
*Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)*
Phone no. 0755444078