Saturday, 28 June 2025

VITOTO VYA 2000(PART IV)

👑 *VITOTO(VISICHANA)VYA 2000*  👑
........................................
               PART IV
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto( CEO-GFI)_
Phone :0755444078

5. *Wanaiba Pasipo na Ulinzi.* Ni makosa ya kiufundi kulalamikia mwizi wakati unajua KUFURI YAKO AU MLANGO WAKO NI MBOVU.
👉Suala la ulinzi ni changamoto kubwa kwa baadhi ya wanawake, Ogopa kitu Biblia imetamka wazi MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME.....
👉Anaye linda anajua *Mali zilizomo ndani, Thamani ya kilichomo ndani, na anajua Aina ya wezi watakao kuja kuiba wanapeleka wapi*
👉Hivi unadhani kuna siku mwislamu atakuja Kukuibia Nguruwe? Au Mlokole kukuibia kreti za bia na sigara? Wezi wa vitu husika wanajulikana wataiba nini na kuvipeleka wapi.
👉Sasa Mwanamke Ukiambiwa Kumlinda Mwanaume, *ULINZI WA KWANZA NI KULINDA HISIA ZAKE*  Siku ukidharau Hisia za mmeo ndo siku Umeanza kumpoteza kwa wezi.
👉Ukiambiwa Kumlinda mwanaume, *ULINZI WA PILI NI WA HESHIMA YAKE* Mwanaume akigundua kuna namna Haumpi heshima yake Ataitafuta kwa watu wengine wanaofanana na wewe(mwanamke/wanawake).
👉Ukiambiwa kumlinda mwanaume, *ULINZNI WA TATU HAKIKISHA UMEMPA UHURU WA KUSEMA CHOCHOTE KWAKO NA UMSIKILIZE* Ukiona mwanaume Ameacha Kukusema iwe kwa uzuri au ubaya kukurekebisha, akaona anaposema unamuona kero...Aisee Huna mme kashaenda kuwasema wengine waliotayari kusemwa na wakafuata.
👉Ukiambiwa Kumlinda mwanaume, *ULINZI WA NNE, MRUHUSU NAFURAHIA USUMBUFU WAKE KWENYE TENDO LA NDOA kama ni mzima wa eneo hilo siyo mgonjwa.
👉Miongoni mwa ALAMA ZA KUKWAMBIA BADO UJAIBIWA MME NI KUONA USUMBUFU WAKE KWENYE TENDO LA NDOA mara kwa mara kama dozi ya dawa.
👉Ukiona mme wako AMEACHA USUMBUFU kwako, kero juu ya tendo la ndoa kuna mambo 3 yametokea.
1.Amepata mbadala wako
2.Ni mgonjwa kwenye mifumo yake.
3.Ujiongezi kumfurahisha kitandani...Mpaka hapo Utaporwa.
👑Nini ufanye katika usumbufu wa mmeo katika tendo la ndoa, SOMA Majira, Tumia Kauli Tamu na Buni Mbinu za Ktuliza hisia kirafiki.
👉Tafauti na hapo wanasaikolojia wanasema unaweza Kaa na mtu aliyekuacha zamani kihisia ila uko naye kimwili, ila kuna mtu anamiliki Hisia zake, na Akimuona Anajisikia Raha na Amani kuliko wewe.
👑Kwa hiyo, Lugha ya *Vitoto vya 2000* ni vikali, Pisi kali, vinavunja ndoa za watu, Si za kweli, kama ni Sura uzuri walio nao ni wakawaida kama wako ndo maana na wewe Uliolewa ni kwasababu ya uzuri ulio mdatisha mmeo, kama ni Maumbile wana kama yako ndo maana mmeo alikuoa wewe, mnachotoafutia wewe mama wa 1980s, 1990s ni kwamba *Wewe Hauko Serious na Mali yako kuilinda, Wao wako serious na Kutafuta mtu aliyeumizwa kwake wampe furaha* Kazi yako kubwa OGOPA KUMUUMIZA mwenzako madaktari uchwara wengi mtaani watamvamia kumtibu hutampata, na akiponea mikononi mwao hao madaktari wa mtaani (vitoto vya 2000) unakazi ya kumrudisha kwako kihisia na kimwili.
NB: _Vitoto vya 2000 niwashauri na ninyi, si kwamba mtaa kwenye chati mpaka mfikishe miaka 30, 40 mtafutika, tulia mtafute ndoa zenu, jifunzeni kutokana na makosa ya dada zenu mjipange kutoyafanya pale mkipata ndoa zenu, mbali na hapo nanyi mtafanya makosa yale yale nanyi watakuja *Vitoto vya 2020* vitawatoa machozi kama mnavyota machozi ya wenzenu wa 19980s na 1990s_
Ulikuwa nami mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa
*Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)*
Phone no. 0755444078

VITOTO VYA 2000(PART III)

👑 *VITOTO (VISICHANA) VYA 2000* 👑
........................................
          PART III
Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa
*Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)*
Phone :0755444078

2. *Mme uliye naye ni chaguo lako la kwanza na la mwisho ndo maana mkaoana* unadhani mlivyoanza miaka ya kwanza mlikuwa mnakinzana hivo? Mliishi vizuri, mlielewana, mlikosana na mkasahishana na mkaendelea na amani yenu na upendo wenu, na akuna aliyekuwa na uwezo wa kumvuta mbali nawe, kwakuwa Hekima zako na maamuzi yako, na uchaguzi wako ulikusukuma kumlinda kwa Wivu mkubwa akae kwako.
👉Ila ulipoanza kumuona kama amwendani, kama ulitafutiwa, kama msumbufu kwako, mkorofi kwako, Ukasogeza moyo mbali wa kumkubali kama Chaguo lako la furaha ambalo unatakiwa kulilinda, ndipo *Wajanja vitoto vya 2000 vilikuja na mbinu za Kuonyesha Kujali na kuthamini Uanaume wake* Wamefanikiwa, watafanikiwa kumpora kwako.
👉Kama ulimpata mmeo huyo kiuhalali,Ulioana naye kwa kukubaliana, Basi Unawajibu wa Kukubaliana Tena naye namna ya kuishi kulingana na Anavyopenda yeye na wewe unavyopenda mbali na hapo.. Utaporwa.
3. *Miaka mlokaa pamoja Humjui Mmeo!* Utaibiwa mapema sana.
👉Wanasaikolojia wanasema, ukikaa na mme au mke kuanzia siku 1 mpaka miaka 9, mkigombana na kuitirafiana ni haki yenu maana bado hamjuani vizuri.
👉Ila kuanzia umri wa miaka 9 nakuendelea mkigombana, na kuitirafiana kiasi kwamba msielewane mpaka ndoa yenu ijulikane kwamba *Mgogoro wa ugomvi wenu ni huu* Basi ninyi ni Wapumbavu msiosaidika, na Mmoja kati yenu alitakiwa ASIOE MPAKA UZEE AU ASIOLEWE MPAKA ubibi kizee. Kwa nini?
👉Miaka 9, 10, 15, 20.... *Ujui Mme wangu Anatekwa hisia na mambo gani?*
👉Ujui mme wangu ni mdhaifu kwenye mambo gani kihisia? Na hapa panaweza tumiwa na wajanja kumchukua kwangu?
👉Ujui mme wangu anachukia nini ukifanya?
👉Ujui kumdanganya mmeo mpaka akaona ni kweli japo unajua si kweli ila lengo uweke amani ya ndoa yenu.
👉Ujui namna ya kumfurahisha mmeo,hata kama amechukia au ana stress ni mambo gani ukiyafanya anarudi kwenye mood?
👑Sasa wanawake wengi wa 1980s, 1990s wamefeli hapo, Anakosea, Anajihesabia haki, Hajui namna ya Kumrudisha mme haraka kwenye mood kutumia vitu anavyopendelea,  naye Anakaza Uso wa kununa mwanzo mwisho.
👑Kinachotokea ni nini, Vitoto vya *2000 viko makini na Neno Am Sorry Love, Am sorry baby, It will Never Happen Again, Sitakuumiza tena eeh?, Nambie unachotaka nifanye ntafanya ili uwe na Amani na furaha yetu irudi* Kwa maneno hayo machache MMEO ANAPORWA mbele yako asubuhi unaona.
4. Kuna Kosa la Kiufundi na la Kisaikolojia, wana ndoa wanafanya( mama) Kumuona mmeo wakawaidaaa, hana maajabu yoyote kama useless man(kwa kutumia Kosa au Makosa mlokosana). Ndo maana una Mtreat, unamchukulia kawaida, na haumpi heshima yake, uzito wake, na nafasi yake kwasababu ya mazoea na KUTOFUNDWA NA WAZAZI.
👉Changamoto kubwa ya Kizazi cha 1980s, na 1990s, na 2000s *Akija Fundwa na Mama Zao* wanafundana wao kwa wo mitandaoni na kwenye Saloon. Hapo hamuwezi kukaa na Waume, tutakuwa na Single Mother wengi na Wajane, na Walioachika wengi.
👉Hata wewe msomaji, moyoni mwako unajua, Mama Yako Alikufunda? Akakupa Miiko ya Ndoa na namnaya Kukaa na mme kwenye nyakati zote? Au Una Weza Kujivunia Ndoa ya Mama yako, aumaisha ya mama yako kwa baba yako ili na wewe Uwe na Adabu na heshima na utilivu kwa mmeo?
👉Haya mambo sisi tuliookoka Tueongezewa Jicho la tatu, Kuna Roho za kifamilia,kiukoo za Kupiga vita kwenye maombi na kwa kujilazimisha kwa vitendo kuzikimbia ili Ndoa yako idumu... Usipo kuwa makini unakuta Roho ya Bibi yako. mama yako, dada yako inakufuata wakati una Neema ya Wokovu ya kukuepusha na Nguvu hizo.
👉Huyo mmeo unayemuona wakawaida sana na hana jipya kwako,Ila pembeni yako, wamama,wadada, na hata wanaume wenzake wanamuona ni Mtu Special, mtu ambaye Atakuwa au anakuwa Karibu naye, kuitwa kwa jina lake *Anafaidi, Amependelewa* na wana WISH INGEWEZEKANA WAKAPATA HATA NAFASI YA SAA 1 waonyeshe unyenyekevu wao na heshima yao kwake wange fanya kwa bidii.
👉Hivi ndivyo Vitoto vya 2000 Uvizia hiyo nafasi, utakuta, *Vina nyenyekea, Vinaheshimu, vinatambua na kujali, maneno, hisia, sauti ya mmeo* sanaaaa ila wewe ujali hapo ndo Kuibiwa Uanzia hapo. Usipo badirika Mmeo anaibiwa kwa Heshima na Kusikilizwa.
👉Mama inabidi ujue kwamba mwanaume niliye naye Si wakawaida, afanani na wa wengine, huyu anaubora wake,sifa zake, na nguvu zake, lazima Nitambue hilo na nimpe heshima yake ili Aridhike na heshima yangu asirubuniwe na heshimaza  za nje.
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)_
Phone: 0755444078

VITOTO VYA 2000(PART II)

👑 *VITOTO VYA (VISICHANA ) VYA 2000* 👑
........................................
              PART II
_Na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa_
Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)
Phone: 0755444078
*26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;Waefeso 4:26*

*27 wala msimpe Ibilisi nafasi. Waefeso 4:27*
👑Ukiichunguza mistari hii nikama imeruhusu Kufanya Makosa, ila umepewa Taadhari Makosa kama binadamu, ila Uwe makini Makosa yakiendelea sana yatazaa Hatari ya Muharibu Kupata nafasi ya Kuharibu. ( *Nitarudi kuchambua*)
👑Wamama wenye Umri mzuri kwenye Ndoa Msiokuwa Vitoto vya 2000, miaka 30-45 mna kwama wapi kwenye Ndoa Mpaka Mnaibiwa Waume zenu na vitoto vya 2000?
👑Nina Maswali kadhaa naomba ujiulize vema halafu ntakwambia Ulipo kwama, Kama wa Kupona Upone kama unaendelea kulia na kulalamikia vitoto vya 2000 uendelee hivo hivo mpaka unazeeka ila Utabaki Sanamu la kwenye ndoa, una mme mwili, ila Roho na Hisia ziko kwingine, au Utaachika.
👑1️⃣ Hivi uliingia kwenye ndoa kwa hiari au kwa kulazimishwa?
👑2️⃣Hivi Mme uliye naye Ulitafutiwa au mlipendana na mkaona ndo mnaweza ishi pamoja?
👑3️⃣Hivi kwa miaka uliyokaa na mmeo Humjui mpaka anakuja mtu mgeni kumjua kuliko wewe na kufanikiwa kukupora?
👑4️⃣Hivi unajua Mmeo niwakawaida kwa watu wengine kama wewe unavyohisi niwakawaida kwako?
👑5️⃣Hivi Unajua kwamba Wezi, Mwizi Aibagi sehemu yenye ULINZI mkali,  wanaibaga sehemu iliyoachwa wazi au bila ulinzi?
👑Hayo maswali 5 ukielewa moja moja Utarudishiwa akili yako na Utakaa na mmeo kwa Utulivu sana na kufurahia na Autaibiwa kizembe tena.
👑Vitoto vya 2000 vimefanikiwa kuiba waume za watu kwa Kutumia Mapungufu ya wanawake wasiojali na hasa *Wanawake wa Kilokole* ambao wametumia MWAVULI WA WOKOVU kufanya Ubabe na kuishi kama wajane wasio na wanaume Wakidhani *Neema ya Wokovu waliyo nayo wao na waume zao Ni Mnyororo mkali usio mruhusu kujitikisa kwenye ndoa, atatulia hata angenyanyaswa kwenye ndoa* hili ndilo LANGO LA 1 LA UHARIBIFU WA NDOA ZA WANA WA MUNGU.
👑Nikinukuu maneno ya Askofu mkuu wa Kanisa la Kiroho la TAG, katika kongamano moja aliwahi kusema *Wanawake wa kilokole ni WAPUMBAVU walio wengi wameshindwa kuishi kama wanawake kwa waume zao*......... Mwisho wa kunukuu( nenda kaitafute YouTube).
👑Sasa vitoto vya 2000 vimeiba na vinaendelea kuiba na vitaendelea kuiba Wanaume wa wanawake wa miaka ya 1980s,1990s kwa sababu zifuatazo za maswali yale juu 5.
1. *Mwanamke uliingia kwenye ndoa kwa hiari Kutimiza Matakwa ya Ndoa* Kama ukufundwa na Wazazi wako(mama yako), basi ulipata hasara ya kwanza... Ilibidi ujue Matakwa ya Ndoa unayoiendea Uende Ukayatimize kwa bidii (HUWEZI KUIBIWA MME Ukiwa unatimiza Matakwa ya Ndoa)
👉 Kiroho(Kiimani/Kikanisa)Ulitakiwa ufundwe na mfungisha Ndoa akueleze matakwa ya ndoa uliyoichagua kwa hiari uende ukayatimize kwa moyo wote, (kama ukumsikiliza vizuri ulikuwa unawaza usiku wa Honeymoon) hiyo ndo Hasara ya 2 Usingeibiwa mmeo na vitoto vya 2000.
👉Nimezungumza *Kufundwa, na Kufundishwa* Ujue Matakwa ya Ndoa na uyatimize kwa bidii huwezi ibiwa mme.
👉Vitoto vya 2000 *Vinafundwa na Mitandao ya Kijamii Matakwa ya ndoa na Havijaingia kwenye ndoa Vinatumia Maarifa hayo Kuwapata Wanaume Waliokosa Furaha ya Ndoa kwasababu mwenye ndoa(mwenye mme wake) kashindwa kutimiza matakwa ya ndoa*
👉Baadhi ya Matakwa ya ndoa ni yapi?
A) utii kwa mme wako, hapa si suala la kumpigia magoti mme, ila mme yeyote anahitaji kuona,kukaa karibu na mke wake ambaye Kile anachomwambia kufanya, kutofanya, kufuata, Anakitii na hata kama hakubaliani nacho *Analugha,Matendo ya Staha na ushawishi* kwa mme wake kughairisha kile kitu.
👉Vitoto vya 2000 viko makini Kutii na kusikiliza, na kutekeleza MATAKWA ya mmeo kwa GHARAMA zozote, ila wewe Unarumbana na kuzozana, au Majibu ya mkato kwa  mmeo yasiyoonyesha unyenyekevu kwake hapo( Hutoboi) Wanamchukua mmeo mapema sana.
👑Ongeza Umakini na Adabu kwa Mmeo.
*Sehemu ya Pili imekamilika karibu sehemu ya tatu*
_Ulikuwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)_
Phone : 0755444078

VITOTO VYA 2000(PART I)

👑👑 *VITOTO(VISICHANA) VYA 2000* 👑👑
_Imeandaliwa na Mwalimu na Mtaalamu wa Saikolojia ya Mahusiano na Ndoa_
*Ev Elisha Kazimoto(C.E.O-GFI)*
Phone: 0755444078
........................................
             *PART I*
_Shalom shalom wale mnaojiita watoto wa 1980s,1990s na wale mnaoitwa watoto wa 2000 wote kwa pamoja Amani ya Bwana iwe nanyi_
👑Kuna lugha hii iliyo shika kasi hasa katika mitandao ya kijamii na kwenye vinywa vya Wanawake wengi walio kwenye Ndoa wakijaribu *Kubainisha Hatari, Ubovu na Ubaya wa Vitoto vya 2000(visichana)* kama Virusi hatari kwa Ndoa zao.
👑Baada ya Kusikia na kuendelea kufanya Utafiti wa Kisaikolojia kujua Chanzo cha Jina hili na sifa hizi kushika kasi kwa nyakati kama hizi, Kama *Mwanasaikolojia na Mshauri wa Ndoa nikapata Cha Kuzungumza* na Kusaidia Kizazi cha 2000 na cha miaka ya 1980s,1990s.
👑Nianze na Neno la Mungu chimbuko la Hekima zote za Saikolojia, kabla sijaenda kwenye Kweli za Wanasailolojia.
*Yeremia 31:22 Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.*
👑Enyi wana ndoa, Enyi Wamama, Kabla ya Kutoa Majina yoyote na sifa zozote njema au mbaya kwa kizazi kinachoibukia, Lazima kwanza Turudi kwenye Neno la Mungu linasemaje Kuhusu Ndoa yako.
👑 *Ndoa Ni Taasisi Nyeti sana* Inayo hitaji Mtu mwenye akili Timamu ( _Nimewahi kuandika makala miaka ya 2017 inayosema *Ndoa inahitaji mtu Mwenye Akili Timamu* nenda kwenye blog yangu au Google andika hivyo ( Ndoa inahitaji mtu mwenye akili Timamu Material Adimu_) hii makala ina dawa nzuri ya uponyaji kwa wana ndoa.
👑Sasa Kumeibuka wimbi kubwa la Wadada wadogo kiumri (vitoto vya 2000 na Mashangazi ya miaka 1970s Kumiliki *Wanaume wa wamama wa miaka ya 1980s, 1990s* kiasi ambacho kimezaa Lugha mtandaoni, Vitoto vya 2000.
👑Hii Lugha ina maana gani kwa wana ndoa? Hizi lawama kwa kizazi cha watoto wadogo mabinti wa 2000 kuzoa Umaarufu usio na sababu wa *Kuiba, Kubeba, Kumiliki wanaume wa watu umetoka wapi?*
👑Kisaikolojia, Kuna *Makosa Makubwa* yanafanywa na Wanawake, wanaojiita *Wanawake wa 1990s, 1980s wenye ndoa zao* makosa ya Kiulinzi yaliyo toa Nafasi nzuri sana ya Bure kwa *Wajanja, Wasichana werevu wenye haja ya Mapenzi* Kuchukua waume zao.( Nitaelezea.....)
👑Kiroho, Wanawake hawa wenye ndoa wamefanya Makosa makubwa ya Kibiblia ambayo, *Wamempa Ibirisi Nafasi* ya Kushambulia Ndoa zao Vizuri bila kutumia nguvu kubwa.
👉Hapo unahitaji kutulia kujifunza vizuri usikosee.
*Hii ni Sehemu ya Kwanza, karibu kuendelea sehemu ya pili*