🎣🎣 *HATARI USIYO IONA KATIKA MAHUSIANO KATI YA KIJANA WA KIKE NA WAKIUME* 🎣🎣
Imeandaliwa na Mchambuzi wa Musuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*( Psychologist)
WhatsApp 0755444078
Facebook Ev Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
_Shalom vijana wote wenye ndoto za kimaisha za kiroho na za kimwili, na wote walio na mipango muhimu katika Ufalme wa Mungu kama kumtumikia Mungu katika huduma yoyote *mfano..Kuhubiri,Uimbaji,kupiga vyombo vya mziki na huduma nyinginezo* Somo hili litakufaa na kukukomboa na *Siri Usiyoijua na hatari usiyoiona iliyo nyuma ya Mahusiano uliyo nayo kati yako na rafiki yako huyo wa kike au wa kiume* Litakusaidia sana kutimiza ndoto zako na usipo jua basi utaishia njiani,utabaki na Historia *Nilikuwa* ila haitakuwa tena_
🎣🎣 *HATARI USIYO IONA KATIKA MAHUSIANO KATI YA KIJANA WA KIKE NA WAKIUME* 🎣🎣
Imeandaliwa na Mchambuzi wa Musuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*( Psychologist)
WhatsApp 0755444078
Facebook Ev Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
_Shalom vijana wote wenye ndoto za kimaisha za kiroho na za kimwili, na wote walio na mipango muhimu katika Ufalme wa Mungu kama kumtumikia Mungu katika huduma yoyote *mfano..Kuhubiri,Uimbaji,kupiga vyombo vya mziki na huduma nyinginezo* Somo hili litakufaa na kukukomboa na *Siri Usiyoijua na hatari usiyoiona iliyo nyuma ya Mahusiano uliyo nayo kati yako na rafiki yako huyo wa kike au wa kiume* Litakusaidia sana kutimiza ndoto zako na usipo jua basi utaishia njiani,utabaki na Historia *Nilikuwa* ila haitakuwa tena_
ANDIKO KUU LA SOMO
LUKA 19:41-44
*41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,*
*42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.*
*43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;*
*44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.Luka 19:44*
🎣Kwenye mistari hii kuna vitu kama 6.
1️⃣Kuna mji umeonekana(mtu)
2️⃣Kuna mtu anajua siri au ameona hatari juu ya mji(mtu) ambayo mji(mtu) haoni.
3️⃣Kuna mtu anaona uchungu kwa yajayo juu ya mji(mtu)
4️⃣Kuna kitu kibaya (Mji) haujui...(Laiti ungejua....)ila siri imefichwa
5️⃣Kuna nyakati za Uharibifu zinakuja juu ya mji(mtu)..Ambapo adui watazingira pande zote wafanye uharibifu
6️⃣Matokeo ya siri ikitimia ni Kufutika kabisa kwa mji(mtu)
🎣 *_Katika Tasnia ya Mahusiano kuna nguvu kubwa ya upendo na ushawishi uwa inajengeka ndani ya mioyo na akili za watu walio katika mahusiano_*
🎣Nguvu kubwa hiyo ya upendo na ushawishi Uongeza nguvu ya ( *Kuaminiana kwa kiwango cha Kutoshutukiana*)
🎣Kuaminiana kukiongezeka na kuimarishwa, utengeneza mazingira ya *Kuondoa mipaka flani flani* ya kujizuia kutofanya mambo flani flani ya kihisia, kuchochea hisia kwa mwenzako.
🎣Mipaka ya kuogopana na kuoneana Aibu ikianza kufutika....Kunazaliwa *Kujisahau*
🎣 KUJISAHAU....Ni *_hali ya mtu kuto tambua Nafasi yake, Heshima yake, mipaka yake, kushindwa kutambua hatari yoyote na kuona mambo yote ni sawa_*
🎣Hali ya kujisahau ikianza kukomaa inaweza zaa *Kutojizuia*..... Hali hii ni ile ambayo mtu *_Anaona jambo hili ni baya au halifai lakini kuna nguvu inayomsukuma kufanya hata kama anaona ni hatari_* maana nguvu ya Kujizuia imeisha ondoka ndani yake.
🎣Kwa mazingira hayo mtu anaweza anza kufanya ubaya wakati *Aupendi ubaya* anafanya ubaya kwakuwa Hana nguvu ya kujizuia, hawezi kujizuia kwakuwa alishaondoa mipaka.
🎣Mazingira haya yakifikiwa ndipo vijana/watu walio kwenye mahusiano wanaweza kufanya mambo yafuatayo
1.Kufanya *Romance*
2.Kuridhishana kihisia *kwa michezo ya kimahaba*(Kushikana shikana maeneo nyeti ya kihisia)
3.Kutumiana picha na video za uchi
4.Kushiriki Ngono...Tukio la mwisho hilo katika mchakato wa mahusiano.
*Na hii ndo Hatari iliyofichwa kwa vijana wengi* pamoja na kwamba wengi wana Imani ya Kujiamini kwamba wao wako Imara hawawezi Kufanya Ngono labda wawe wameamua.... Hiyo ji kweli kwa baadhi...Ila *Mchakato wa Kuanguka uwa hauendi Gafla* unaenda taratibu sana jambo ambalo uwezi kulishutukia kwa haraka.
ANGALIZO KWENYE MAHUSIANO, UKIONA MAMBO YAFUATAYO YAMETOKEA KATI YENU ITAKUGARIMU KUPONA.
_Ni vigumu kuelewa Elimu hii ya Kisaikolojia ninayo kupa ila ukikaa na kutajitazama utagundua kuna hatari tiyari umeisha ingia_
1.Ukianza Romance( Utakuja kuiacha) unaweza jizuia mara moja,mara mbili ila *Utarudia tu*(Msingi wa zinaa unaanza kujengwa taratibu)
2.Ukianza Kushika au kushikwa Maeneo yanayo ibua hisia(Utaacha,utarudia) maana mwili unazoea hisia za furaha. *Unaweza jikaza kujizuia kwa wengine ila kwa mtu wako wa karibu itakushinda*(huo ndo mwanzo wa kuisogelea zinaa)
3.Ukianza kutamani na kutumia mazingira ya kukaa peke yenu wawili msikoonekana na mtu mwingine, na nafsi zenu hazitamani kukaa mahali pa wazi, *Mtajikuta mmefanya matendo ambayo hamkutegemea kuyafanya* ila hamtaweza kujizuia.
3.Ukishazoelea mazingira ya kumtembelea mwenzako kwake, guest huwezi acha hata kama unahisi hatari,nguvu ya mahusiano itakusukuma kwenda tu.
*Ushauri wa Kiroho na Kisaikolojia kwako kijana kama ujaathirika na hali hii*
👉Usiruhusu upendo uzibe macho yako ya kuona hatari iliyombele zako ya kiroho na kisaikolojia.
👉Usiruhusu Maeneo yako ya mipaka yako yashikwe au usiruhusu hisia zako zikupelekee kushika maeneo yaibuayo hisia zako
👉Peaneni elimu na taadhari kama marafiki mliopo kwenye mahusiano ili mkae katika mipaka yenu
👉Kila mmoja jiwekee msimamo wa kutofanya makosa hayo uliyo yajua.
*Kama tayari Umeathirika,una kazi ya kifanya na inaumiza,na itakuchukua muda kuzoea* Fanya mazoezi ya kubadiri mazoea mliyozoeshana na rafiki yako ili ujinasue katika hatari ijayo.
*_Imeandaliwa na mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Ev Elisha Kazimoto
No comments:
Post a Comment