πͺπͺ *ILI KUSHINDA UNAHITAJI MAMBO 2..UHODARI NA USHUJAA*πͺπͺ
Mnenaji: *Ev Elisha Kazimoto*
ANDIKO KUU: *2Mambo ya Nyakati 13:1-18* πππππ _Ukisoma mistari hiyo kwa utulivu halafu njoo hapa kwenye Ufafanuzi wa Roho Mtakatifu_
πKila mtu aitwaye mshindi, maana yake *Amepita kizuizi kilicho lenga kumzuia asiende alikokusudia* kwenda.
πKushinda pia ni kupata,kuona ulichokuwa unakitarajia......Ikiwa ni baada ya kuzuiliwa na kitu,mtu,mazingira au hali,iliyowekwa maalumu kwaajili yako kukuzuia.
πͺ *UHODARI* ni Tabia au hali ya *Kujiamini* kutokana na mafunzo,mazoezi,kinga au mtu aliye nyuma yako kukusaidia.
πKila mtu aliye Hodari ana namna ya wapi anapata nguvu ya kujiamini.
πKwa ujumla UHODARI ni KUJIAMINI.
πͺUSHUJAA....Ni hali na moyo wa Mapigano yazaayo Ushindi.
πMtu shujaa maana yake ana Rekodi ya kupigana na kushinda mpinzani wake.
πUshujaa ni moyo uliotayari kupigana na kushinda.
NB1,: *_Msingi wa Imani yetu ya watu tuliookoka ni Sisi ni Hodari(kwakuwa aliyenyuma Yetu ana nguvu kuliko yeyote na chochote kikwazo,au adui tutakaye kutana naye kutuzuia,au kutudhuru_*
KUMBUKUMBU LA TORATI 31:1-6
NB2: _Maisha yetu sisi watu tuliookoka, niya USHUJAA kwakuwa sisi ni watu wa vita,mapigano kwenye ulimwengu wa roho na Tunashinda kabla ya pambano kwakuwa *Vita si yetu ni ya Bwana* hivyo Ushindi ni Lazma_
*Waefeso 6:10-12, Warumi 8:31,37, 1Samweli 17:46-47*
Imendaliwa na *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
No comments:
Post a Comment