*PESA INA NGUVU KUBWA KATIKA MAHUSIANO*
_Swali na penda kujua mahusiano kati pesa na upendo wa dhati katika mahusiano ya uchumba au ndoa_
*Anajibu. Msaikolojia na Mshauri wa masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto* 0755444078
*Mahusiano na Pesa ni kama Shilingi yenye pande mbili* Mahusiano ni mwitikio wa Hisia za mtu juu ya mwingine baada ya kuona huyo mtu anaweza kidhi mahitaji ya ya kisaikolojia na kiroho na kimwili. Upendo unaambatana na utimilifu wa Hisia za mtu juu ya mtu. *Hisia zinahusika na mwonekano wa nje wa mtu, upendo unahusika na kukubali mtu alivyo kwa kuhitaji faida yake iwe kwako pia*
Pesa ni miongoni mwa vitu vinavyo tengeneza mwonekano wa mtu,.... Na pesa ni nyenzo inayo rahisisha mahusiano yaende kwa ulaini na wepesi. *Kuna vitu vinavyo chochea upendo na kulinda amani ya ndoa kisaikolojia ila hivyo vitu vinahitaji pesa ili vifanyike*
(kuvaa vzr,kula vizuri,outing,surprise,gift havifanyiki kwa maombi vinafanyika kwa Pesa,na Upendo siyo maneno ni Matendo, na matendo ni pesa.
*NB kwa Vijana* _mwenye pesa anakauli(that's biblical),mwenye pesa ni Romamtic(that's Psychological),mwenye pesa ndo anaye vutia(attractive)( that's Physical )mwenye pesa ndo anaweza kuenjoy maisha ya Kiroho(that's spiritual) sasa kijana wa kiume TAFUTA PESA, usidharau kazi, acha kufunga tai ndefu mpaka magotini( *Usinipite mwokozi* )unachumbia wadada wanakukataa unaanza kuwalaani kuwa hawataolewa.... Wee ndo hautaoa unaye mtaka,utaoa yulee alopoteza matumaini ambaye hakuwa chaguo lako_
Biblia imesema pesa ndo jawabu la mambo yote, sasa wewe unahitaji kila kitu kiwe cha kiroho. TAFUTA PESA, maisha ni mepesi ukiwa na pesa,hauna pesa ugomvi mwingi wa vitu vidogo ndani ya nyumba.
NARUDIA VIJANA TAFUTA PESA, upendo ni matendo siyo maneno.
*_Usichanganye mambo hapa, si kwamba Pesa ndo inaleta upendo wa dhati, Ila pesa Inachochea Upendo,kama hakuna pesa kuna siku huo upendo unaousikia utashuka,utakuwa dhaifu,uta collapse,utaishi kwa kuumia na kunungunika ndipo tafsiri ya upendo wa dhati itakuwa imefutika._*
Kumbuka hakuna binadamu aliyeumbiwa *Kuvumilia matatizo* tunavumilia kwasababu No *Alternative* hakuna njia mbadala.
*Ev Elisha Kazimoto*
0755444078
No comments:
Post a Comment