Thursday, 15 March 2018

UZAZI WA MPANGO

*UZAZI WA MPANGO UKOJE KIROHO NA KISAIKOLOJIA KWA WANA NDOA*
   _By Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
_Tunapo hitimisha mada kwanza niweke sawa dhana hii ya *UZAZI WA MPANGO NA NJIA ZAKE*, Kwa tafsiri nyepesi uzazi wa mpango ni Makubaliano ya wanandoa namna ya kupata watoto wao kwa interval ya muda na kwa idadi husika_(hii ndo tafsiri ya Uzazi wa mpango). Swali je, *Kuweka huu mpango kati ya wanandoa ni Dhambi au Siyo dhambi* Majibu unayo wewe mwenyewe kwakuwa Roho wa Mungu umshuhudia kila mmoja kwa nafsi yake juu ya HAKI na DHAMBI. Lakini Biblia imetupa kujua uwezo tuliopewa wa AKILI na tukaambiwa tuzitumie Ipasavyo.
Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.

1 Wakorintho 15:34
*_Kwanini kuambiwa tutumie Akili ipasavyo?_* ni kwasababu kuu 2. Moja, si kika jambo limeandikwa kwenye Biblia kuwa ili kifanyike hivi au vile ila Uwezo wa Akili tuliopewa na Mungu unatusaidia kuyafanya maisha yetu yaende vema bila kutafuta wapi pameandikwa fanya hivi au usifanye hivi.
Pili, Tuna sehemu ya Uungu(uwezo mkubwa wa Kimungu)wa kurativu mambo kwa usahihi *Kulingana na tunavyo yaona mazingira na maisha* ( ulifika wakati Mungu akaona mnara wa babel unajengwa,akaona hapa kutatokea shida akaamua kuangusha, hivo hivo alipoona dhambi zimezidi duniani aliamua kumtuma Yesu)ninamaanisha nini *Mungu alifanya kazi kwa kuangalia nyakati na majira*

*_Uzazi wa mpango ni Hiyari ya mtu,ukiweza kuzaa kila mwaka sawa,watoto 20 sawa siyo dhambi,watoto 2, 1 sawa ila katika hayo yote usiharibu Kusudi la Mungu kwa Mtu aliyeletwa duniani au aliye uhai tumboni, nitafafanua_*
✍Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.

Mithali 19:14
_Wewe uzaaye 10,20...... Hakikisha unatimiza andiko hili kwa watoto wako hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwa kila azaaye_ kuna watu wanatumia andiko la *Mwanzo 1:28...Zaeni mkaijaze nchi,kwa andiko hilo usema kupangilia idadi ya watoto ni dhambi* _ swali la msingi kwako ni INCHI INAJAZWA KWA WATU WANGAPI na wewe unapambana ufikishe ngapi ndo uwe umetimiza andiko? Swali la pili, nchi gani unataka kuijaza uloambiwa na wewe upo nchi gani? Swali tatu... Niwatu wangapi waliambiwa waijaze nchi, na wewe ni mtu wa ngapi? Swali la nne, Nchi itajaa kwa muda gani(mwaka gani)na wewe unapambana uijaze mwaka gani.( *Haya ni maswali muhimu sana kutafakari,siyo unachukua andiko unatembea nalo wala hujui maana yake*)
Hakikisha watoto wako wana maisha yanayowafanya wafurahie kuja duniani, *Usipambane kuleta duniani bila kupambana watoto wafurahie maisha ya kuja duniani* labda ni kujengee dhana hii ya Biblia Mungu hakukusudia watu wapambane na maisha,yeye aliandaa mazingira tangu siku ya kwanza mpaka ya 6 ndo akamuumba Mtu na akamweka maali vitu vyote tayari vipo ( *Mungu kama baba aliandaa urithi wa watoto wake waukute,na mke akamuozea Adamu*) _Adamu alikuwa ana spend Ready made things_ na ndo mpango wa Mungu watoto wa spend issues ready made na baba zao.
Kwa kutotumia akili ipasavyo za Kimungu sasa watoto hawakuti urithi,wanakatiwa kipisi (piece)cha aridhi ila kila kitu mtoto anajipambania na *nakulaani kwa nini alizaliwa na baba yule na asiwe mwingine* Hii ndo mimi naiita tatizo kubwa la wazazi wanaotumia andiko la vibaya la kuijaza nchi. *Note* *_Hakuna idadi maalumu ya hawa ndo utawatunza vyema_* idadi ni akili yako,maisha yako,mipango yako ndo itakupa wapi waje duniani..... Na wala usiseme Mungu ndo kawaruhusu wote hawa 12mimi ningefanyeje? Mungu alipoumba aliweka mfumo wa multiplication (kuongezeka) kila ukipanda unazalisha ( *Ni mfumo uliwekwa*) wewe ndo wa kuu *Monitor* ila usipo uongoza hata 20utafika wala halaumiwi Mungu wewe ndo msimamizi wa mfumo.
*_Suala la njia ipi itumike kupangilia mfumo wa uletaji watoto duniani lipo katika Uwezo wa Akili yako uloumbiwa,wala si katika maandiko, jambo kubwa na muhimu pamoja na akili ulopewa,wewe uliyeokoka umeongezewa na Uwezo wa Roho kwa nini usifanye mambo kwa ubora zaidi_* zaidi ya hayo yote wapo madaktari wa kimwili wanaotoa *Elimu juu njia moja moja ya uzazi wa mpango,faida na athari na inafanyaje kazi*

NOTE: *_Kwa upande wa ushauri wangu wa kiroho, Tafuta kujua njia sahihi isiyo husika na Kusitisha uhai wa Kiukbe ambacho kineisha tungwa na kuwa Nafsi hai yule ni mtu, anayo roho,nafsi na mwili,kusitisha maisha yake ni Killing like Abortion, tafuta njia zinazo pambana kuzuia yai na mbegu visirutubishwe kuwa kiumbe_*

By Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & Counselor)
0755444078

No comments:

Post a Comment