Saturday, 24 March 2018

MTU WA TABIA HII PIGA CHINI

*UKIONA MWENZAKO ANAMAMBO HAYA NA HABADILIKI PIGA CHINI,USIJIKAZE KUINGIA NAYE KATIKA NDOA*
    Ev Elisha Kazimoto
Whatsapp 0755444078
*_Kuna jambo moja na la muhimu watu wengi katika mahusiano linawapiga chenga, ni Kuchunguza Mwenzake anayetaka kuingia naye katika ndoa, kubaini Vitabia sumu ana viashiria vya migogoro ya ndoa,kuvibaini na kuvifayia maamuzi magumu mapema ili kuepusha changamoto kwenye ndoa_*
👉Ni heri kuvunja mahusiano kuliko kuvunja ndoa au kuishi kwa kujikaza kwenye ndoa.
👉Ukishindwa kumbadirisha mwenzako katika mahusino yenu usije ukajidanganya kuwa utambadirisha ndani ya ndoa.
Kauli ni hii *Ukiona Vijitabia hivi mwenzako haiviachi ana ving'ang'ania PIGA CHINI huyo*
✍Ana mambo ya siri,si muwazi,anakuficha ficha vitu sana...Huyo mtu piga chini,utaumiza moyo wako bure kwa kukosa ushirikiano katika ndoa
✍Anazira zira mara kwa mara pale unapomkosea tu kidogo.... Anaye zira zira piga chini.
✍Ukiona ana kiburi sana,jeuri hata akikosea anakuwa mzito kukuomba msamaha,hataki kabisa piga chini huyo ni mwiba.
✍Anakulinganisha na wavulana au wasichana wengine pale anapokukosoa,piga chini...Wewe ni wewe wala huwezi kuwa kama flani.
✍Hapendi kushauriwa,anataka afanye anachotaka yeye,anachojua yeye ndo kizuri wewe mawazo yako hamna, huyo piga chini....
✍Ana Masharti mengi mengiii yasiyo na msingi, huyo piga chini....
✍Anayeendesha mahusiano kwa kusikiliza nyumbani wamesema hivi au vilee,huyo piga chini....
✍Hataki kujishugulisha na kazi atafute pesa,...Anapenda kuulamba tu....Huyo piga chini.
✍Mkali sana,hataki umzoee muwe kama rafiki piga Chini,ndoa siyo kituo cha polisi.
✍Anahitaji umsikilize yeye tu na ufuate mambo yake,ila yeye hakusikilizi,Piga Chini, ndoa siyo jeshi haiendeshwi kwa Amri ya Amili jeshi,ni mazungumzo na makubaliano.
✍Mvivu kwa mambo ya Mungu hata ukimuhimiza, huyo atakuwa mzigo kwako kwenye ndoa usiobebeka. huyo piga chini Haraka sana Uvivu wa kiroho na hatari kuliko uvivu wa kimwili,kimwili wewe waweza pambana ukamtunza ila kiroho kila mtu anambingu yake lakini majibu mnapokea kama mwili 1.....PIGA CHINI.
✍Mara kwa mara anakuambia mambo ya X friend wake, huyo piga chini.....
*_Hayo ni baadhi ya mambo very critical ya kisaikolojia,usiyapuuze yatakugharimu_*
_Ukipenda na Usiwe na macho ya kuona madhaifu na kuyakwepa,jiandae kuishi jela la maisha na furaha ya maisha hutaiona_

Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto
0755444078

Wednesday, 21 March 2018

PESA KATIKA MAHUSIANO

*PESA INA NGUVU KUBWA KATIKA MAHUSIANO*
_Swali na penda kujua mahusiano kati pesa na upendo wa dhati katika mahusiano ya uchumba au ndoa_
*Anajibu. Msaikolojia na Mshauri wa masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto* 0755444078
*Mahusiano na Pesa ni kama Shilingi yenye pande mbili* Mahusiano ni mwitikio wa Hisia za mtu juu ya mwingine baada ya kuona huyo mtu anaweza kidhi mahitaji ya ya kisaikolojia na kiroho na kimwili. Upendo unaambatana na utimilifu wa Hisia za mtu juu ya mtu. *Hisia zinahusika na mwonekano wa nje wa mtu, upendo unahusika na kukubali mtu alivyo kwa kuhitaji faida yake iwe kwako pia* 
Pesa ni miongoni mwa vitu vinavyo tengeneza mwonekano wa mtu,.... Na pesa ni nyenzo inayo rahisisha mahusiano yaende kwa ulaini na wepesi. *Kuna vitu vinavyo chochea upendo na kulinda amani ya ndoa kisaikolojia ila hivyo vitu vinahitaji pesa ili vifanyike*
(kuvaa vzr,kula vizuri,outing,surprise,gift havifanyiki kwa maombi vinafanyika kwa Pesa,na Upendo siyo maneno ni Matendo, na matendo ni pesa.
*NB kwa Vijana* _mwenye pesa anakauli(that's biblical),mwenye pesa ni Romamtic(that's Psychological),mwenye pesa ndo anaye vutia(attractive)( that's Physical )mwenye pesa ndo anaweza kuenjoy maisha ya Kiroho(that's spiritual) sasa kijana wa kiume TAFUTA PESA, usidharau kazi, acha kufunga tai ndefu mpaka magotini( *Usinipite mwokozi* )unachumbia wadada wanakukataa unaanza kuwalaani kuwa hawataolewa.... Wee ndo hautaoa unaye mtaka,utaoa yulee alopoteza matumaini ambaye hakuwa chaguo lako_

Biblia imesema pesa ndo jawabu la mambo yote, sasa wewe unahitaji kila kitu kiwe cha kiroho. TAFUTA PESA, maisha ni mepesi ukiwa na pesa,hauna pesa ugomvi mwingi wa vitu vidogo ndani ya nyumba.
NARUDIA VIJANA TAFUTA PESA, upendo ni matendo siyo maneno.
*_Usichanganye mambo hapa, si kwamba Pesa ndo inaleta upendo wa dhati, Ila pesa Inachochea Upendo,kama hakuna pesa kuna siku huo upendo unaousikia utashuka,utakuwa dhaifu,uta collapse,utaishi kwa kuumia na kunungunika ndipo tafsiri ya upendo wa dhati itakuwa imefutika._*

Kumbuka hakuna binadamu aliyeumbiwa *Kuvumilia matatizo* tunavumilia kwasababu No *Alternative* hakuna njia mbadala.
*Ev Elisha Kazimoto*
0755444078

Thursday, 15 March 2018

UZAZI WA MPANGO

*UZAZI WA MPANGO UKOJE KIROHO NA KISAIKOLOJIA KWA WANA NDOA*
   _By Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
_Tunapo hitimisha mada kwanza niweke sawa dhana hii ya *UZAZI WA MPANGO NA NJIA ZAKE*, Kwa tafsiri nyepesi uzazi wa mpango ni Makubaliano ya wanandoa namna ya kupata watoto wao kwa interval ya muda na kwa idadi husika_(hii ndo tafsiri ya Uzazi wa mpango). Swali je, *Kuweka huu mpango kati ya wanandoa ni Dhambi au Siyo dhambi* Majibu unayo wewe mwenyewe kwakuwa Roho wa Mungu umshuhudia kila mmoja kwa nafsi yake juu ya HAKI na DHAMBI. Lakini Biblia imetupa kujua uwezo tuliopewa wa AKILI na tukaambiwa tuzitumie Ipasavyo.
Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.

1 Wakorintho 15:34
*_Kwanini kuambiwa tutumie Akili ipasavyo?_* ni kwasababu kuu 2. Moja, si kika jambo limeandikwa kwenye Biblia kuwa ili kifanyike hivi au vile ila Uwezo wa Akili tuliopewa na Mungu unatusaidia kuyafanya maisha yetu yaende vema bila kutafuta wapi pameandikwa fanya hivi au usifanye hivi.
Pili, Tuna sehemu ya Uungu(uwezo mkubwa wa Kimungu)wa kurativu mambo kwa usahihi *Kulingana na tunavyo yaona mazingira na maisha* ( ulifika wakati Mungu akaona mnara wa babel unajengwa,akaona hapa kutatokea shida akaamua kuangusha, hivo hivo alipoona dhambi zimezidi duniani aliamua kumtuma Yesu)ninamaanisha nini *Mungu alifanya kazi kwa kuangalia nyakati na majira*

*_Uzazi wa mpango ni Hiyari ya mtu,ukiweza kuzaa kila mwaka sawa,watoto 20 sawa siyo dhambi,watoto 2, 1 sawa ila katika hayo yote usiharibu Kusudi la Mungu kwa Mtu aliyeletwa duniani au aliye uhai tumboni, nitafafanua_*
✍Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.

Mithali 19:14
_Wewe uzaaye 10,20...... Hakikisha unatimiza andiko hili kwa watoto wako hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwa kila azaaye_ kuna watu wanatumia andiko la *Mwanzo 1:28...Zaeni mkaijaze nchi,kwa andiko hilo usema kupangilia idadi ya watoto ni dhambi* _ swali la msingi kwako ni INCHI INAJAZWA KWA WATU WANGAPI na wewe unapambana ufikishe ngapi ndo uwe umetimiza andiko? Swali la pili, nchi gani unataka kuijaza uloambiwa na wewe upo nchi gani? Swali tatu... Niwatu wangapi waliambiwa waijaze nchi, na wewe ni mtu wa ngapi? Swali la nne, Nchi itajaa kwa muda gani(mwaka gani)na wewe unapambana uijaze mwaka gani.( *Haya ni maswali muhimu sana kutafakari,siyo unachukua andiko unatembea nalo wala hujui maana yake*)
Hakikisha watoto wako wana maisha yanayowafanya wafurahie kuja duniani, *Usipambane kuleta duniani bila kupambana watoto wafurahie maisha ya kuja duniani* labda ni kujengee dhana hii ya Biblia Mungu hakukusudia watu wapambane na maisha,yeye aliandaa mazingira tangu siku ya kwanza mpaka ya 6 ndo akamuumba Mtu na akamweka maali vitu vyote tayari vipo ( *Mungu kama baba aliandaa urithi wa watoto wake waukute,na mke akamuozea Adamu*) _Adamu alikuwa ana spend Ready made things_ na ndo mpango wa Mungu watoto wa spend issues ready made na baba zao.
Kwa kutotumia akili ipasavyo za Kimungu sasa watoto hawakuti urithi,wanakatiwa kipisi (piece)cha aridhi ila kila kitu mtoto anajipambania na *nakulaani kwa nini alizaliwa na baba yule na asiwe mwingine* Hii ndo mimi naiita tatizo kubwa la wazazi wanaotumia andiko la vibaya la kuijaza nchi. *Note* *_Hakuna idadi maalumu ya hawa ndo utawatunza vyema_* idadi ni akili yako,maisha yako,mipango yako ndo itakupa wapi waje duniani..... Na wala usiseme Mungu ndo kawaruhusu wote hawa 12mimi ningefanyeje? Mungu alipoumba aliweka mfumo wa multiplication (kuongezeka) kila ukipanda unazalisha ( *Ni mfumo uliwekwa*) wewe ndo wa kuu *Monitor* ila usipo uongoza hata 20utafika wala halaumiwi Mungu wewe ndo msimamizi wa mfumo.
*_Suala la njia ipi itumike kupangilia mfumo wa uletaji watoto duniani lipo katika Uwezo wa Akili yako uloumbiwa,wala si katika maandiko, jambo kubwa na muhimu pamoja na akili ulopewa,wewe uliyeokoka umeongezewa na Uwezo wa Roho kwa nini usifanye mambo kwa ubora zaidi_* zaidi ya hayo yote wapo madaktari wa kimwili wanaotoa *Elimu juu njia moja moja ya uzazi wa mpango,faida na athari na inafanyaje kazi*

NOTE: *_Kwa upande wa ushauri wangu wa kiroho, Tafuta kujua njia sahihi isiyo husika na Kusitisha uhai wa Kiukbe ambacho kineisha tungwa na kuwa Nafsi hai yule ni mtu, anayo roho,nafsi na mwili,kusitisha maisha yake ni Killing like Abortion, tafuta njia zinazo pambana kuzuia yai na mbegu visirutubishwe kuwa kiumbe_*

By Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & Counselor)
0755444078

Wednesday, 7 March 2018

PINDUA

*MKESHA WA MAOMBI YA KUPINDUA WAVAMIZI WA MAENEO*

     *_Mnenaji Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp *0755444078*
_Huu ni usiku wa washindi,ni usiku wa watu wenye malenho ya kimaisha kupata mpenyo wao,ni usiku wa ukombozi kwa vitu vilivyo vamiwa na maadui na kuviteka,leo tunavikomboa kwa upako mkuu wa Yesu Kristo, ni usiku wa kurejesha sura halisi ya vitu vilivyo poteza suea yake ya asili,ni usiku wa kurudisha matumizi ya awali ya mofumo ya maisha yetu,ambayo adui amevamia na kuanzisha matumizi yake ya uharibifu._
13 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.
Yohana 2 :13

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
Yohana 2 :14

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
Yohana 2 :15

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
Yohana 2 :16
*_Kabla ya kuoambana katika maombi,ni vizuri ukajua matumizi ya asili ya mifumo yako ya kimaisga,ukajua sura halisi na asili ya ndoa yako,biashara yako,elimu yako,uchumba wako,kazi yako,na ulivyo kusudiwa viwe ujiulize je,ndivyo vilivyo,au matumizi na sura imebadirishwa na wahuni,maadui_*
✍ Yesu akaiona nyumba ya sala(hekalu)imebadirishiwa matumizi,imekuwa ya biashara,imekuwa ya wabadili fedha, *Ndipo Yesu kwa hasira ya kiroho akatengeneza kikoto cha kamba na kuanza pindua pindua,ili kurydisha sura na uhasilia*
✍Iko mifumo ya ya maisha yako imebadirishiwa matumizi ma sura yake,unahitaji kutengeneza kikoto cha maombi nakuanza kupindua pindua *_kurudisha heshina na upendo wa ndoa yako,kurudisha ofisi yako,mtaji wako,uchumi wako,mme wako na mke wako,mchumba wako na akili yako darasani_*  simama sasa Muulize adui(mchawi,pepo,shetani) kuwa ,Je, _Mungu akunipa maisha haya,(ndoa,uchumi,huduma,elimu,kazi nk)nivifurahie? Mbona sasa umeyafanya maisha yangu kuwa machungu?_ *Hapo anza kupindua moja kwa moja kwa mamlaka ya jina la Yesu,piga,pindua,haribu ita sura na matunizi asili ya maisha yako* naamini sasa waweza ingia katika maombi kwa Ujasiri.

   *Mwana wa Vita Ev Elisha Kazimoto*
      0755444078