👹👹 Somo La Leo *UCHAWI HAUJAWAHI KUISHINDA NGUVU YA MUNGU*👹👹
*_Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Call 0657557570
_Sauti kutoka Bonde la Mateso_
_Haleluya, atukuzee Mungu asiyetutoa kuwa mawindo kwa maadui zetu. Hii ni sauti ya mtu apazaye kutoka katika Bonde la mateso ikisema *Bado Liko Tumaini kwa Bwana Yesu* na huu ndo ukweli niliouona katika Bonde la Mateso ya kuwa *Uchawi Haujawahi kuwa Juu ya Nguvu za Mungu* Karibu katika Ujumbe huu wenye Nguvu ya kubadili mtazamo na maisha yako ya kiroho na Imani yako katika Bwana Yesu_
*KUTOKA 7:8-12*
8 Bwana akanena na Musa na Haruni, akawaambia,
9 Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka.
10 _Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka._
11 *_Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao_*.
12 *_Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao_*.
👉👹 *Uchawi* ni Nguvu za giza, zinazotumiwa na watu walioamua kumtumikia shetani katika sekta hiyo ya uchawi ili *_Kuua, Kudhohofisha,Kuharibu,na kupoteza mwelekeo wa_* wa maisha ya watu wasio na hatia na walio na hatia katika ufalme wa giza.
*_Mtu mwenye Akili ndiye Mwenyekushinda Uchawi_*
*Zaburi 14:2,Mithali 15:24,Mika 6:9,Mathayo 7:24*
_Nizungumzie mtu mwenye akili ndipo utajua kuwa kushinda na kushindwa kwako na wachawi ni matokeo ya uwezo wa Akili ya Kimungu aliyo nayo mtu. Na baada ya somo hili umuombe Mungu akuongezee Akili ya Kimungu upate kushinda_
👉(Mithali 15:24.... Inaongelea mtu mwenye akili njia ya uhai uenda juu,sikiliza, mchawi hawezi pambana na wewe ukiwa juu,yeye ni mtu wa ufalme wa chini,ili akushinde lazima apige akili yako urudi chini,ndo akabiliane na wewe) ukiwa na uwezo wa kukaa kiroho juu utawashinda maadui wote.
👉Mtu mwenye Akili ni mwenye uwezo mbele ya adui yake, hata adui anajua hakuwezi kirahisi.
👉Mtu mwenye Akili anauwezo wa kupambanua mitego na njia za adui(wachawi) na njia sahihi ya Mungu.
👉Mtu mwenye Akili maamuzi yake,matendo yake ni kwa faida ya ufalme wa Mungu na nafsi yake.
*_Tukiwa na Akili yaani Uwezo ya Kimungu uchawi utamezwa mbele yetu_*( KUTOKA 7:12)
_Hivi umewahi kutafakari pale Haruni alipotupa fimbo chini ikawa nyoka ,na wachawi wa Farao wakatupa fimbo zao chini zikawa nyoka,ila fimbo ya Haruni ikazimeza,ulisha waza Haruni alipo ichukua fimbo yake ilo kuwa nyoka,ikageuka kuwa fimbo Wachawi Walibaki na nini?_ Jibu jepesi; *Fimbo zao zilishamezwa,walibaki mikono mitupu,ila Haruni tu na fimbo yake*
👉Hapo ndo ujue uchawi mbele ya mwenye Akili(uwezo wa Kimungu )unamezwa halafu adui anabaki bila bila,mpaka anakuogopa.
*_Uwezo wa Kutambua,kupambanua unakufanya kuwa mtu hatari kwa Wachawi na adui yako anaye tumia mitego ya siri_*
( *1Samweli 18:20-28, Luka 12:54-57, 19:41-44*)
👉Ukiwa na uwezo wa kutambua mambo wewe si rahisi kutekwa na wachawi na kukuharibia mwelekeo wa maisha yako.
👉Njia anayoitumia adui kukunasa kwa hila,ukiqa mtu mwenye akili na mwepesi wa kutambua,hiyo hiyo njia ndo itatumika kukuletea ushindi na adui yako (mchawi kuaibika).
👉 _Lakini fahamu hili, Maamuzi yako na matendo yako,huwafanya watu,(Maadui na wenye haki)Kutambua kuwa ni Nguvu ipi,ya ufalme upi inatumiliki(1Smweli 18:28, Marko 8:31-33)_
*ANINA ZA WACHAWI NA UCHAWI WAO*
1⃣ Wachawi walogao kwa kutumia madawa *Mambo ya Walawi 19:26*
2⃣ Wachawi walogao kwa maneno(watu watumiao maneno kwa lengo la kuua,kudhohofisha,kuharibu na kupoteza mwelekeo wa maisha ya mtu) *Isaya 32:7-8*
3⃣ Wachawi(watu wenye roho ya kichawi,matendo ya kichawi)wakiwa na dawa au bila dawa. *1Samweli 18:10-11, Yoshua 9:4-17, Zaburi 10:7, 31:13, 36:3, Mithali 12:20*
4⃣ Wachawi walio tafuta uchawi kwa sababu zao za kulipa kisasi,au maangaiko kwa waganga wa kienyeji kutafuta majibu ya matatizo yao. *Kutoka 7:22, 2Mambo ya Nyakati 16:12,Isaya 19:3*
5⃣ Wachawi walio rithishwa na wazazi wao. Kila mzazi humrithisha mwanae vitu vyema au vibaya ili kuendeleza sifa ya mzazi, kwa faida ya mzazi au mtoto mwenyewe. *Kumbukumbu la Torati 21:15-17, Ayubu 13:26*
6⃣ Wachawi wanao tumikishwa na nguvu ya kichawi bila kujua(matokeo ya kutokaa katika nafasi ya kiroho sawa sawa, au kwakuwa rafiki na wachawi) *Isaya 14:3,1Wafalme 12:4,Wagalatia 4:3,Isaya 19:3*
_Hizo zote ni aina za wachawi wanao tumika kuharibu,kuua na kupoteza mweleo wa watu,kanisa,ndoa,kazi na elimu nk,ila ukiwa mtu mwenye akili na awezaye kutambua hao wote watamezwa mbele yako_
👉👹Unapo mzungumzia mchawi,unazungumzia Mtu aliyebeba roho ya Mauti(ya kuua)bila kujali Undugu,cheo,pesa au Damu yake.
🏹Kuna mtu mmoja tu, *Aliye na Uwezo wa Kumfanya Mchawi Arudi nyuma na Kupigwa vikali Akimsogelea, naye ni Mtu ALIYEOKOKA na Hana Hofu juu ya Nguvu za kichawi juu yake* maana yake hapa si kuokoka tu, bali uwe na Maarifa ya kupambana na wachawi na USIWAOGOPE SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO,KUWAKEMEA.
🏹Wachawi hupenda kushindana na mtu yeyote anayesema,au onyesha *Yesu Yu Juu ya Uchawi wao* neno hilo,usemi huo,harakati hizo zitawafanya waanze kukupima,kukupinga kwa *Sumu zote na dawa zote za kichawi*(Unaweza ona Musa na Haruni pale *Kutoka 7:10-11* kuonyesha uweza wa Kimungu,nao wakataka kudhohofisha watumishi wa Mungu kwa kutengeneza nyoka bandia)
🏹Ila siku zote, Wachawi hushindana lakini Hubanwa dakika za mwisho( *mstr 12*) Nyoka zao zikamezwa na uchawi wao ukadharauliwa kwa kuwa kwa Mungu huyu Yehova UCHAWI UNAMEZWA.
👹👹 *_Wachawi Juweni Mipaka Yenu,na mjue Uwezo wa Wana wa Mungu aliye Hai_*👹👹
👉Si kila shambulio utalifanya kwa wana wa Mungu litafanikiwa,Kuna mipaka mikubwa ya Mungu kulinda watumishi wake
*HESABU 23:11-23*
11 Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.
12 Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile Bwana atialo kinywani mwangu?
👉Mkishambulia watu wa Mungu,mkawajeruhi Siyo ushindi wenu ila Mmetegewa Tanzi,Mungu akigeuza shambulio hilo Nimauti kwenu
*ISAYA 47:9-12*
9 lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.
10 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.
11 Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua.
12 Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.
👉Jua neno Moja mchawi, *_Katika harakati zako za kupambana na watu wa Mungu,ili uue,uharibu au udhohofishe, utaishia kupigwa na Mungu kwa laana kuu na kuishia kuzikwa_*
👉Jambo la pili la kufahamu wachawi, ni *_Haitatokea,na haijawi tokea,Mungu awaachie wachawi Muue au kuharibu Kazi ya Mungu au Watumishi wa kweli wa Mungu_* haitatokea hata siku moja.
*_Nguvu ya Mwili ni Ukamilifu/Uimara wa Viungo_*
*Warumi 12:4-5*
4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;
5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
👉Katika mambo hupaswi kudharau ni Uzima wa Kiungo(viungo) katika mwili.
👉Ukiona mwili ni dhaifu,unashindwa kufanya kazi flani jua kuna Kiungo kimoja wapo kimevamiwa na maradhi.
👉Kila kazi bora hutokana katika viungo imara vya mwili.
*Hii ndiyo athari ya adui,mchawi akimfanikusha mtu mmoja ndani ya kanisa kumteka,wengi(kanisa)hupata shida,mtikisiko.*
*1Wakorintho10:15-17*
4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;
5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
👉Tukidharau uathirika wa kiungo kimoja kutekwa na wachawi,tujiandae kuuguza mwili mzima.
👉Tukiwa na maamuzi magumu ya kushugulikia ukombozi/uzima wa kiungo kimoja kanisani,tunaanda mtembeo wa Nguvu za Mungu kanisani.
*_Ukiona Mchawi, Juwa Umeona Magonjwa Sugu na Hatari Yafuatayo_*
_kwanza inabidi ujue ugonjwa ni nini na nguvu yake ndo utaelewa nini na maanisha kuwa mchawi yeyote ni sawa sawa kabisa na Magonjwa Hatari na sugu kama *Ukimwi,TB,Kansa na Malaria* kwa kuyataja baadhi_
🏹Taadhari zichukuliwazo kujikinga na Magonjwa haya,ndizo hizo hizo taadhari za kiroho zichukuliwazo kujikinga na Mchawi.
🏹Madhara yatokanayo na Magonjwa hayo tajwa hapo juu kwa maisha ya mtu,ndo madhara hayo ya kiroho yatokanayo na mashambulizi ya mchawi.
🏹 *_Roho wa Bwana akupe kujua mahusiano haya na madhara haya ya Mchawi yalivyo sawa na Magonjwa hayo sugu_* ila kama Dawa, na kinga zipo za magonjwa hayo basi na mchawi tutamshugulikia kwa Ufunuo huo huo.
🏹 *_Kazi za mchawi na za Magonjwa sugu ni Moja, Kuua, Kudhohofisha na kuharibu pindi viingiapo katika maisha ya mtu_* Namfundisha mtu mmoja Askari wa kiroho juu ya vita vya kiroho dhidi ya mawakala wa Ibirisi( *Wachawi*)
🏹 Hatuogopi magonjwa,ila tunatumia nguvu zote kuyapinga,kujikinga nayo, hivyo hivyo na wachawi, *_Hatuogopi kuwasema,kazi zao,uharibifu wao na namna ya kuwashinda_* Kama tukiwaogopa ndipo watapata nafasi ya kufuta historia ya ushindi wetu juu yao( *Warumi 8:37*)
🏹 Siku zote ukiwa na bidii kufunua siri za adui,ndivyo anavyozidi kukuogopa, ila akigundua hutaki shari naye ndipo atakushambulia kwa ghafla na kukufuta.
🏹 _Wewe uliyeokoka,uliye naakili timamu jua haya kuhusu Wachawi kama Ugonjwa_
1⃣ Mchawi na Ukimwi hawanatofauti, Ukishirikiana naye,kwa kujua kuwa ni mchawi au hujui kuwa ni mchawi *_Lazima Utapoteza Kinga za Roho za kushinda matatizo yoyote katika maisha_* mchawi akiishaingia maishani mwako anatafuna uwezo wa kumshtukia,macho ya kiroho,uwezo wa kufanikiwa nk.(UKIMWI)
👉Tunajikinga naye kwa kutojamiana naye(Urafiki)kutotumia vifaa vya ncha kali naye(Zawadi)
*_Mithali 15 : 27 - Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi._*
2⃣Mchawi na Malaria ni kitu kimoja, wanatumia vitu vidogo sana kama lugha za urafiki,zawadi,dawa,(mbu) kuwateka watu ila wakisha kuteka ndoa yako,uchumi wako,elimu yako,madhara yake ni makubwa(ugonjwa wa malaria)
👉Tunajikinga na hawa viumbe Wachawi(mbu wa malaria)kwa kukaa kwenye Chandarua ya maombi,utakatifu,maarifa dhidi yao) *Waefeso 6:10-17*
3⃣Mchawi na Kansa ni kitu kimoja (Asili yao ni wakiingia katika mfumo wa maisha,ni kuutafuna mdani kwa ndani)ikilipuka nje uwezo wa kutibu ni mdogo ila mauti uchukua nafasi kubwa.
*_Kwa nini tusifundishe kanisa kuwa na maombi ya vita,akili na ujasiri wa kusema kazi za wachawi,mbinu zao,na kuwapiga katika maombi kila siku ili wadhohofike kila siku,ili kanisa la Bwana liwe salama?_* Tuliopewa Agizo na Bwana,tutasema,tutafundisha,tutawakemea wachawi na kufichua siri zao, WALA KUTULOGA,KUTUUA WALA KUTUDHOHOFISHA HAWAWEZI. Maana hatuneni kwa shauri letu bali kwa shauri la Bwana. ( *YEREMIA 47:7*)
_Hii ndiyo jumla ya maneno yaujumbe huu kwa kanisa na watumishi wote wa kweli wa Yesu Kristo,katika kizazi hiki kinacho tishwa na uchawi mwingi,mtaani na hata makanisani, ( *Hatufi mara mbili katika Kristo, Tulishakufa na tu hai katika Bwana na Uhai wetu UMEFICHWA katika Kristo*,)kilicho fichwa hakionekani,wachawi hawatauona uhai wetu milele,piga,kemea,fichua siri zao kaa katika Utakatifu uhai wako Umefichwa._
*_Wakolosai 3 : 3 - Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu_*
Kwa Dozi za kiroho,Mikutano ya Injili iliyo hai, Semina na Makongamano ya Neno la Mungu ya watunishi,vijana,wamama,wana ndoa na wanafunzi wa sekondari na vyuo Wasiliana nami: Ev Elisha Kazimoto
*WhatsApp 0755444078*
Call 0657557570
Fb Elisha Kazimoto
Blog. Materiladimuuniversity2017blogsport
No comments:
Post a Comment