*USIMUHURUMIE SISERA NAYE HANA HURUMA KWAKO*
_Mkesha wa Operation Toboa vichwa vya Masisera katika Maisha yetu_
*Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
_Shalom,leo katika mkesha wa maombi,wana wa vita tunahitaji kushugulikia kwenye ulimwengu wa roho,akina Sisera waliokuwa mwiba katika Ndoa,uchumi,elimu,kazi na huduma zetu_
*_Waamuzi 4 : 3 - Wana wa Israeli wakamlilia Bwana; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini._*
👉Ni kwa muda gani umeonewa na umaskini? Migogoro ya ndoa?uchumba una vunjika ovyo ovyo bila sababu kubwa?huduma yako ibashuka? Jua nyuma ya matatizo hayo kuna akina Sisera watesi(wachawi,mapepo na falme za giza na maroho ya kifamilia)
👉Ili ushinde vita hivyo, lazima usiwe na huruma pale unapoingia katika maombi ya leo kupigana Sisera.
*_Waamuzi 5 : 26 - Akanyosha mkono wake akashika kigingi, Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi; Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake. Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake._*
👉Ni mwendo wa KUTOBOA tu leo, shika Nyundo(jina la Yesu),shika kigingi(Imani)twanga Sisera huyo kichwaji(mchawi huyo ,mganga wa kienyeji,kahaba huyo aloiba mmeo,alofunga tumbo lako usizae, alofunga mchumba wako,uchumi wako,elimu yako na ajira yako)
*_Ezekieli 12 : 5 - Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale._*
👉Ni mwendo wa KUTOBOA kuta na kuchomoa vitu walivyo vifungia maadui. Toboa kuta, *_kuta za Tambiko,zindiko,kafara_*zilizo jengwa na maadui kuziba baraka zako.
*_Ezekieli 12 : 7 - Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao._*
👉Ni mwendo wa KUTOBOA na kuhamisha vyombo vyetu(ndoa,afya,huduma,vipawa,karama, elimu,kazi na uchumi)vitoe gizani viliko fichwa.
*_Marko 2 : 4 - Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza._*
👉Wakiziba sehemu zote( *TUNATOBOA*) hata mahali ambapo hawakutegemea mpaka tupate haki zetu.
_Kila mmoja kwa hasira ya Roho wa Bwana sema, *Natoboaaa kuta hizo, na dari zao kwa jina la Yesu* mpaka nifike kwa muujiza wangu leo._
*Pokea Message hii Fupi ikusaidie kuomba katika mapambano yako tutashinda*
_Kwa Msaada wa kiroho,operation za kiroho,Mikutano ya Injili ya Yesu Kristo,makongamano ya kiroho,ya vijana,wamama,wana ndoa na Watumishi katika utumishi wasiliana nami, *Ev Elisha Kazimoto*_
👉 Fb Elisha Kazimoto
👉WhatsApp 0755444078
👉Call 0657557570
Sunday, 2 July 2017
TOBOA SISERA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment