*MBELE YAKO KUNAHITAJI KUSAFISHWA. NDO UFANIKIWE*
_Katika Ibada 02/07/2017 na *Ev Elisha Kazimoto*_
WhatsApp 0755444078
_Shalom, leo Mungu akufungue macho uone mbele unakoenda vikosi vya Adui wachafu walivyo kaa wakikungoja kuzuia,kubadirisha mwelekeo wa safari yako_
👉Kanuni ya maisha ya kiroho na kimwili ni kujongea kwa kwenda mbele na si nyuma.
👉Na adui yeyote hachezi na unako toka,ana cheza na unako kwenda.
👉Na heshima na sifa ya mtu,haipo anakotoka ipo anakokwenda.
👉Maadui wakifauru kukaa na kuchafua njia iliyo mbele yako,basi wameweza kuharibu future yako yote.
👉 _Ndiyo maana Bwana anasema kuwaondoa makabila(mataifa)adui wa Israel mbele yao ili waifikie ahadi ya Mungu_
*KUTOKA 23:20-23*
20 Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.
21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.
22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.
23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.
👉Mataifa hayo(mabaya na makali kwa Israel ) yanasimama badala *_Adui zako wachawi,mapepo,waganga wa kienyeji,magonjwa sugu,na matatizo yote yanayo kukabili_* Sasa Mungu inabidi ayaondoe mbele zako ndo ufanikiwe.
*_Kutoka 23 : 27 - Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao._*
👉Hakuna kitu kibaya kwa mtu uliyeokoka mwana wa vita, uwe mtu wa *Kawaida mbele ya Adui zako* utaonewa kila kona,na utakuwa dumple la adui.
👉Katija maombi yako ya kila siku mwambie Bwana *_Safisha mbele yangu,na upeleke utisho mbele yangu_* Adui zangu wafadhaishwe kwa sura yangu,sauti yangu,mtoko wangu. (Mwambie Bwana *_Nipelekee malaika mbele yangu malaika wa utisho,hata maadui walio kalia baraka zangu na haki zangu waziachie kwa kutetemeka_)*
*_Kutoka 23 : 31 - Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako._*
👉Bwana anaposafisha mbele yako,omba pia Bwana akuwekee mipaka katika ulimwengu wa roho,mipaka ya utawala wako,mipaka ya ulinzi wa maeneo na vitu vyako.
*_Sasa waweza anza kuomba ukisafisha mbele yako kwaajili yako na vizazi vyako_*
_Kwa Mafundisho,ushauri wa kiroho na opreation za kiroho, huduma za mikutano ya Injili,Makongamano ya kiroho ya Watumishi,wana ndoa,vihana,wamama na seminaza neno la Mungu, wasiliana nami_
👉Fb Elisha Kazimoto
👉WhatsApp 0755444078
👉Call 0657557570
No comments:
Post a Comment