Wednesday, 12 July 2017

UCHAWI UNA UKOMO WAKE

👹👹  Somo La Leo *UCHAWI HAUJAWAHI KUISHINDA NGUVU YA MUNGU*👹👹
    *_Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Call 0657557570
_Sauti kutoka Bonde la Mateso_
_Haleluya, atukuzee Mungu asiyetutoa kuwa mawindo kwa maadui zetu. Hii ni sauti ya mtu apazaye kutoka katika Bonde la mateso ikisema *Bado Liko Tumaini kwa Bwana Yesu* na huu ndo ukweli niliouona katika Bonde la Mateso ya kuwa *Uchawi Haujawahi kuwa Juu ya Nguvu za Mungu* Karibu katika Ujumbe huu wenye Nguvu ya kubadili mtazamo na maisha yako ya kiroho na Imani yako katika Bwana Yesu_
*KUTOKA 7:8-12*
8 Bwana akanena na Musa na Haruni, akawaambia, 

9 Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka. 

10  _Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka._

11  *_Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao_*. 

12  *_Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao_*.
👉👹 *Uchawi* ni Nguvu za giza, zinazotumiwa na watu walioamua kumtumikia shetani katika sekta hiyo ya uchawi ili *_Kuua, Kudhohofisha,Kuharibu,na kupoteza mwelekeo wa_* wa maisha ya watu wasio na hatia na walio na hatia katika ufalme wa giza.
*_Mtu mwenye Akili ndiye Mwenyekushinda Uchawi_*
*Zaburi 14:2,Mithali 15:24,Mika 6:9,Mathayo 7:24*
_Nizungumzie mtu mwenye akili ndipo utajua kuwa kushinda na kushindwa kwako na wachawi ni matokeo ya uwezo wa Akili ya Kimungu aliyo nayo mtu. Na baada ya somo hili umuombe Mungu akuongezee Akili ya Kimungu upate kushinda_
👉(Mithali 15:24.... Inaongelea mtu mwenye akili njia ya uhai uenda juu,sikiliza, mchawi hawezi pambana na wewe ukiwa juu,yeye ni mtu wa ufalme wa chini,ili akushinde lazima apige akili yako urudi chini,ndo akabiliane na wewe) ukiwa na uwezo wa kukaa kiroho juu utawashinda maadui wote.
👉Mtu mwenye Akili ni mwenye uwezo mbele ya adui yake, hata adui anajua hakuwezi kirahisi.
👉Mtu mwenye Akili anauwezo wa kupambanua mitego na njia za adui(wachawi) na njia sahihi ya Mungu.
👉Mtu mwenye Akili maamuzi yake,matendo yake ni kwa faida ya ufalme wa Mungu na nafsi yake.
*_Tukiwa na Akili yaani Uwezo ya Kimungu uchawi utamezwa mbele yetu_*( KUTOKA 7:12)
_Hivi umewahi kutafakari pale Haruni alipotupa fimbo chini ikawa nyoka ,na wachawi wa Farao wakatupa fimbo zao chini zikawa nyoka,ila fimbo ya Haruni ikazimeza,ulisha waza Haruni alipo ichukua fimbo yake ilo kuwa nyoka,ikageuka kuwa fimbo Wachawi Walibaki na nini?_ Jibu jepesi; *Fimbo zao zilishamezwa,walibaki mikono mitupu,ila Haruni tu na fimbo yake*
👉Hapo ndo ujue uchawi mbele ya mwenye Akili(uwezo wa Kimungu )unamezwa halafu adui anabaki bila bila,mpaka anakuogopa.
*_Uwezo wa Kutambua,kupambanua unakufanya kuwa mtu hatari kwa Wachawi na adui yako anaye tumia mitego ya siri_*
( *1Samweli 18:20-28, Luka 12:54-57, 19:41-44*)
👉Ukiwa na uwezo wa kutambua mambo wewe si rahisi kutekwa na wachawi na kukuharibia mwelekeo wa maisha yako.
👉Njia anayoitumia adui kukunasa kwa hila,ukiqa mtu mwenye akili na mwepesi wa kutambua,hiyo hiyo njia ndo itatumika kukuletea ushindi na adui yako (mchawi kuaibika).
👉 _Lakini fahamu hili, Maamuzi yako na matendo yako,huwafanya watu,(Maadui na wenye haki)Kutambua kuwa ni Nguvu ipi,ya ufalme upi inatumiliki(1Smweli 18:28, Marko 8:31-33)_
*ANINA ZA WACHAWI NA UCHAWI WAO*
1⃣ Wachawi walogao kwa kutumia madawa *Mambo ya Walawi 19:26*
2⃣ Wachawi walogao kwa maneno(watu watumiao maneno kwa lengo la kuua,kudhohofisha,kuharibu na kupoteza mwelekeo wa maisha ya mtu) *Isaya 32:7-8*
3⃣ Wachawi(watu wenye roho ya kichawi,matendo ya kichawi)wakiwa na dawa au bila dawa. *1Samweli 18:10-11, Yoshua 9:4-17, Zaburi 10:7, 31:13, 36:3, Mithali 12:20*
4⃣ Wachawi walio tafuta uchawi kwa sababu zao za kulipa kisasi,au maangaiko kwa waganga wa kienyeji kutafuta majibu ya matatizo yao. *Kutoka 7:22, 2Mambo ya Nyakati 16:12,Isaya 19:3*
5⃣ Wachawi walio rithishwa na wazazi wao. Kila mzazi humrithisha mwanae vitu vyema au vibaya ili kuendeleza sifa ya mzazi, kwa faida ya mzazi au mtoto mwenyewe.  *Kumbukumbu la Torati 21:15-17, Ayubu 13:26*
6⃣ Wachawi wanao tumikishwa na nguvu ya kichawi bila kujua(matokeo ya kutokaa katika nafasi ya kiroho sawa sawa, au kwakuwa rafiki na wachawi) *Isaya 14:3,1Wafalme 12:4,Wagalatia 4:3,Isaya 19:3*
_Hizo zote ni aina za wachawi wanao tumika kuharibu,kuua na kupoteza mweleo wa watu,kanisa,ndoa,kazi na elimu nk,ila ukiwa mtu mwenye akili na awezaye kutambua hao wote watamezwa mbele yako_
👉👹Unapo mzungumzia mchawi,unazungumzia Mtu aliyebeba roho ya Mauti(ya kuua)bila kujali Undugu,cheo,pesa au Damu yake.
🏹Kuna mtu mmoja tu, *Aliye na Uwezo wa Kumfanya Mchawi Arudi nyuma na Kupigwa vikali Akimsogelea, naye ni Mtu ALIYEOKOKA na Hana Hofu juu ya Nguvu za kichawi juu yake* maana yake hapa si kuokoka tu, bali uwe na Maarifa ya kupambana na wachawi na USIWAOGOPE SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO,KUWAKEMEA.
🏹Wachawi hupenda kushindana na mtu yeyote anayesema,au onyesha *Yesu Yu Juu ya Uchawi wao* neno hilo,usemi huo,harakati hizo zitawafanya waanze kukupima,kukupinga kwa *Sumu zote na dawa zote za kichawi*(Unaweza ona Musa na Haruni pale *Kutoka 7:10-11* kuonyesha uweza wa Kimungu,nao wakataka kudhohofisha watumishi wa Mungu kwa kutengeneza nyoka bandia)
🏹Ila siku zote, Wachawi hushindana lakini Hubanwa dakika za mwisho( *mstr 12*) Nyoka zao zikamezwa na uchawi wao ukadharauliwa kwa kuwa kwa Mungu huyu Yehova UCHAWI UNAMEZWA.
👹👹 *_Wachawi Juweni Mipaka Yenu,na mjue Uwezo wa Wana wa Mungu aliye Hai_*👹👹
👉Si kila shambulio utalifanya kwa wana wa Mungu litafanikiwa,Kuna mipaka mikubwa ya Mungu kulinda watumishi wake
*HESABU 23:11-23*
11  Balaki akamwambia Balaamu, Umenitendea nini? Nimekuleta ili Uwalaani adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa kabisa.
12 Naye akajibu, akasema, Je! Hainipasi kuangalia, niseme neno lile Bwana atialo kinywani mwangu?
👉Mkishambulia watu wa Mungu,mkawajeruhi Siyo ushindi wenu ila Mmetegewa Tanzi,Mungu akigeuza shambulio hilo Nimauti kwenu
*ISAYA 47:9-12*
9 lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno. 

10 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi. 

11 Kwa sababu hiyo ubaya utakupata; wala hutajua kutopoa kwake; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa utakupata kwa ghafula, usioujua. 

12 Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda. 
👉Jua neno Moja mchawi, *_Katika harakati zako za kupambana na watu wa Mungu,ili uue,uharibu au udhohofishe, utaishia kupigwa na Mungu kwa laana kuu na kuishia kuzikwa_*
👉Jambo la pili la kufahamu wachawi, ni *_Haitatokea,na haijawi tokea,Mungu awaachie wachawi Muue au kuharibu Kazi ya Mungu au Watumishi wa kweli wa Mungu_* haitatokea hata siku moja.
*_Nguvu ya Mwili ni Ukamilifu/Uimara wa Viungo_*
*Warumi 12:4-5*

4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 

5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
👉Katika mambo hupaswi kudharau ni Uzima wa Kiungo(viungo) katika mwili.
👉Ukiona mwili ni dhaifu,unashindwa kufanya kazi flani jua kuna Kiungo kimoja wapo kimevamiwa na maradhi.
👉Kila kazi bora hutokana katika viungo imara vya mwili.
*Hii ndiyo athari ya adui,mchawi akimfanikusha mtu mmoja ndani ya kanisa kumteka,wengi(kanisa)hupata shida,mtikisiko.*
*1Wakorintho10:15-17*

4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 

5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
👉Tukidharau uathirika wa kiungo kimoja kutekwa na wachawi,tujiandae kuuguza mwili mzima.
👉Tukiwa na maamuzi magumu ya kushugulikia ukombozi/uzima wa kiungo kimoja kanisani,tunaanda mtembeo wa Nguvu za Mungu kanisani.
*_Ukiona Mchawi, Juwa Umeona Magonjwa Sugu na Hatari Yafuatayo_*
_kwanza inabidi ujue ugonjwa ni nini na nguvu yake ndo utaelewa nini na maanisha kuwa mchawi yeyote ni sawa sawa kabisa na Magonjwa Hatari na sugu kama *Ukimwi,TB,Kansa na Malaria* kwa kuyataja baadhi_
🏹Taadhari zichukuliwazo kujikinga na Magonjwa haya,ndizo hizo hizo taadhari za kiroho zichukuliwazo kujikinga na Mchawi.
🏹Madhara yatokanayo na Magonjwa hayo tajwa hapo juu kwa maisha ya mtu,ndo madhara hayo ya kiroho yatokanayo na mashambulizi ya mchawi.
🏹 *_Roho wa Bwana akupe kujua mahusiano haya na madhara haya ya Mchawi yalivyo sawa na  Magonjwa hayo sugu_* ila kama Dawa, na kinga zipo za magonjwa hayo basi na mchawi tutamshugulikia kwa Ufunuo huo huo.
🏹 *_Kazi za mchawi na za Magonjwa sugu ni Moja, Kuua, Kudhohofisha na kuharibu pindi viingiapo katika maisha ya mtu_* Namfundisha mtu mmoja Askari wa kiroho juu ya vita vya kiroho dhidi ya mawakala wa Ibirisi( *Wachawi*)
🏹 Hatuogopi magonjwa,ila tunatumia nguvu zote kuyapinga,kujikinga nayo, hivyo hivyo na wachawi, *_Hatuogopi kuwasema,kazi zao,uharibifu wao na namna ya kuwashinda_* Kama tukiwaogopa ndipo watapata nafasi ya kufuta historia ya ushindi wetu juu yao( *Warumi 8:37*)
🏹 Siku zote ukiwa na bidii kufunua siri za adui,ndivyo anavyozidi kukuogopa, ila akigundua hutaki shari naye ndipo atakushambulia kwa ghafla na kukufuta.
🏹 _Wewe uliyeokoka,uliye naakili timamu jua haya kuhusu Wachawi kama Ugonjwa_
1⃣ Mchawi na Ukimwi hawanatofauti, Ukishirikiana naye,kwa kujua kuwa ni mchawi au hujui kuwa ni mchawi *_Lazima Utapoteza Kinga za Roho za kushinda matatizo yoyote katika maisha_* mchawi akiishaingia maishani mwako anatafuna uwezo wa kumshtukia,macho ya kiroho,uwezo wa kufanikiwa nk.(UKIMWI)
👉Tunajikinga naye kwa kutojamiana naye(Urafiki)kutotumia vifaa vya ncha kali naye(Zawadi)
*_Mithali 15 : 27 - Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi._*
2⃣Mchawi na Malaria ni kitu kimoja, wanatumia vitu vidogo sana kama lugha za urafiki,zawadi,dawa,(mbu) kuwateka watu ila wakisha kuteka ndoa yako,uchumi wako,elimu yako,madhara yake ni makubwa(ugonjwa wa malaria)
👉Tunajikinga na hawa viumbe Wachawi(mbu wa malaria)kwa kukaa kwenye Chandarua ya maombi,utakatifu,maarifa dhidi yao) *Waefeso 6:10-17*
3⃣Mchawi na Kansa ni kitu kimoja (Asili yao ni wakiingia katika mfumo wa maisha,ni kuutafuna mdani kwa ndani)ikilipuka nje uwezo wa kutibu ni mdogo ila mauti uchukua nafasi kubwa.
*_Kwa nini tusifundishe kanisa kuwa na maombi ya vita,akili na ujasiri wa kusema kazi za wachawi,mbinu zao,na kuwapiga katika maombi kila siku ili wadhohofike kila siku,ili kanisa la Bwana liwe salama?_* Tuliopewa Agizo na Bwana,tutasema,tutafundisha,tutawakemea wachawi na kufichua siri zao, WALA KUTULOGA,KUTUUA WALA KUTUDHOHOFISHA HAWAWEZI. Maana hatuneni kwa shauri letu bali kwa shauri la Bwana. ( *YEREMIA 47:7*)
_Hii ndiyo jumla ya maneno yaujumbe huu kwa kanisa na watumishi wote wa kweli wa Yesu Kristo,katika kizazi hiki kinacho tishwa na uchawi mwingi,mtaani na hata makanisani, ( *Hatufi mara mbili katika Kristo, Tulishakufa na tu hai katika Bwana na Uhai wetu UMEFICHWA katika Kristo*,)kilicho fichwa hakionekani,wachawi hawatauona uhai wetu milele,piga,kemea,fichua siri zao kaa katika Utakatifu uhai wako Umefichwa._
*_Wakolosai 3 : 3 - Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu_*
Kwa Dozi za kiroho,Mikutano ya Injili iliyo hai, Semina na Makongamano ya Neno la Mungu ya watunishi,vijana,wamama,wana ndoa na wanafunzi wa sekondari na vyuo Wasiliana nami: Ev Elisha Kazimoto
*WhatsApp 0755444078*
Call 0657557570
Fb Elisha Kazimoto
Blog. Materiladimuuniversity2017blogsport

Thursday, 6 July 2017

NGUVU KUU 7 ZA MWANAMKE

Nguvu kuu 7 alizonazo mwanamke

MUUNGWANA BLOG / 9 hours ago

Nguvu kuu 7 alizonazo mwanamke

1. Uwezo wa kuona na kugundua ya mbeleni (anawezakuona kisichosemwa au kitakachokuja).               Anatumia mlango wa sita wa fahamu unaoitwa EPS
2. Ananguvu ktk kinywa chake kuliko nguvu za mwili kwa mwanaume. Athari za kutotumia kinywa       chake vema ni kubwa zaidi.
3. Nguvu na uwezo wa kuendeleza uumbaji
4. Nguvu ya ushawishi
5. Nguvu na uwezo wa kustahimili. Kuvumilia. Kubeba mazito.
6. Nguvu na uwezo wa kujadili bei (bargaining power)
7. Uwezo wa kuwaathiri watoto (positively or negatively)

ILI NGUVU HII ITENDE KAZI
1. Tumia vema kinywa chako
2. Tumia vema ushawishi wako
3. Jitambue

Sunday, 2 July 2017

TOBOA SISERA

*USIMUHURUMIE SISERA NAYE HANA HURUMA KWAKO*
   _Mkesha wa Operation Toboa vichwa vya Masisera katika Maisha yetu_
    *Ev Elisha Kazimoto*
   WhatsApp 0755444078
_Shalom,leo katika mkesha wa maombi,wana wa vita tunahitaji kushugulikia kwenye ulimwengu wa roho,akina Sisera waliokuwa mwiba katika Ndoa,uchumi,elimu,kazi na huduma zetu_
*_Waamuzi 4 : 3 - Wana wa Israeli wakamlilia Bwana; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia kenda; naye akawaonea wana wa Israeli kwa nguvu muda wa miaka ishirini._*
👉Ni kwa muda gani umeonewa na umaskini? Migogoro ya ndoa?uchumba una vunjika ovyo ovyo bila sababu kubwa?huduma yako ibashuka? Jua nyuma ya matatizo hayo kuna akina Sisera watesi(wachawi,mapepo na falme za giza na maroho ya kifamilia)
👉Ili ushinde vita hivyo, lazima usiwe na huruma pale unapoingia katika maombi ya leo kupigana Sisera.
*_Waamuzi 5 : 26 - Akanyosha mkono wake akashika kigingi, Nao mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi; Akampiga Sisera kwa hiyo nyundo, akamtoboa kichwa chake. Naam, alimpiga akamtoboa kipaji chake._*
👉Ni mwendo wa KUTOBOA tu leo, shika Nyundo(jina la Yesu),shika kigingi(Imani)twanga Sisera huyo kichwaji(mchawi huyo ,mganga wa kienyeji,kahaba huyo aloiba mmeo,alofunga tumbo lako usizae, alofunga mchumba wako,uchumi wako,elimu yako na ajira yako)
*_Ezekieli 12 : 5 - Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale._*
👉Ni mwendo wa KUTOBOA kuta na kuchomoa vitu walivyo vifungia maadui. Toboa kuta, *_kuta za Tambiko,zindiko,kafara_*zilizo jengwa na maadui kuziba baraka zako.
*_Ezekieli 12 : 7 - Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao._*
👉Ni mwendo wa KUTOBOA na kuhamisha vyombo vyetu(ndoa,afya,huduma,vipawa,karama, elimu,kazi na uchumi)vitoe gizani viliko fichwa.
*_Marko 2 : 4 - Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza._*
👉Wakiziba sehemu zote( *TUNATOBOA*) hata mahali ambapo hawakutegemea mpaka tupate haki zetu.
_Kila mmoja kwa hasira ya Roho wa Bwana sema, *Natoboaaa kuta hizo, na dari zao kwa jina la Yesu* mpaka nifike kwa muujiza wangu leo._
     *Pokea Message hii Fupi ikusaidie kuomba katika mapambano yako tutashinda*
_Kwa Msaada wa kiroho,operation za kiroho,Mikutano ya Injili ya Yesu Kristo,makongamano ya kiroho,ya vijana,wamama,wana ndoa na Watumishi katika utumishi wasiliana nami, *Ev Elisha Kazimoto*_
  👉 Fb Elisha Kazimoto
👉WhatsApp 0755444078
👉Call 0657557570

MBELE YAKO PASAFISHWE

*MBELE YAKO KUNAHITAJI KUSAFISHWA. NDO UFANIKIWE*
   _Katika Ibada 02/07/2017 na *Ev Elisha Kazimoto*_
WhatsApp 0755444078
_Shalom, leo Mungu akufungue macho uone mbele unakoenda vikosi vya Adui wachafu walivyo kaa wakikungoja kuzuia,kubadirisha mwelekeo wa safari yako_
👉Kanuni ya maisha ya kiroho na kimwili ni kujongea kwa kwenda mbele na si nyuma.
👉Na adui yeyote hachezi na unako toka,ana cheza na unako kwenda.
👉Na heshima na sifa ya mtu,haipo anakotoka ipo anakokwenda.
👉Maadui wakifauru kukaa na kuchafua njia iliyo mbele yako,basi wameweza kuharibu future yako yote.
👉 _Ndiyo maana Bwana anasema kuwaondoa makabila(mataifa)adui wa Israel mbele yao ili waifikie ahadi ya Mungu_
*KUTOKA 23:20-23*
20 Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. 

21 Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake. 

22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 

23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali. 
👉Mataifa hayo(mabaya na makali kwa Israel ) yanasimama badala *_Adui zako wachawi,mapepo,waganga wa kienyeji,magonjwa sugu,na matatizo yote yanayo kukabili_* Sasa Mungu inabidi ayaondoe mbele zako ndo ufanikiwe.
*_Kutoka 23 : 27 - Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao._*
👉Hakuna kitu kibaya kwa mtu uliyeokoka mwana wa vita, uwe mtu wa *Kawaida mbele ya Adui zako* utaonewa kila kona,na utakuwa dumple la adui.
👉Katija maombi yako ya kila siku mwambie Bwana *_Safisha mbele yangu,na upeleke utisho mbele yangu_* Adui zangu wafadhaishwe kwa sura yangu,sauti yangu,mtoko wangu. (Mwambie Bwana *_Nipelekee malaika mbele yangu malaika wa utisho,hata maadui walio kalia baraka zangu na haki zangu waziachie kwa kutetemeka_)*
*_Kutoka 23 : 31 - Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako._*
👉Bwana anaposafisha mbele yako,omba pia Bwana akuwekee mipaka katika ulimwengu wa roho,mipaka ya utawala wako,mipaka ya ulinzi wa maeneo na vitu vyako.
*_Sasa waweza anza kuomba ukisafisha mbele yako kwaajili yako na vizazi vyako_*
_Kwa Mafundisho,ushauri wa kiroho na opreation za kiroho, huduma za mikutano ya Injili,Makongamano ya kiroho ya Watumishi,wana ndoa,vihana,wamama na seminaza neno la Mungu, wasiliana nami_
👉Fb Elisha Kazimoto
👉WhatsApp 0755444078
👉Call 0657557570