Monday, 13 February 2017

VALENTINE DAY

❤❤ *HAPPY LOVE IN MY MARRIAGE/RELATIONSHIP*❤❤
    *_By Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
      *0755444078*
( *14 February 2017*)
_Shalomwana ndoa,uliye katika mahusiano ya uchumba,uliye katika mahusiano ya urafiki na wewe unaye fumba macho na kufumbua ukiwaza nani atakuwa sehemu ya furaha ya maisha yangu kama mke/mme wangu,nikukaribishe katika uchambuzi huu muhimu wa siku hii ya WAPENDANAO_ Si hiitaji kukufundisha maana,wala chimbuko la Valentine day,sihitaji kukufundisha kama ni siku ya shetani,mizimu,wafu,wazinifu,wala siku takatifu,wala ibada kwa Mungu wala kwa shetani,hiyo si kazi yangu leo maana hainiongezei kitu wala kunipunguzia kitu kimwili wala kiroho, *_maana niliye rohoni nitazamavyo na nitafsirivyo sivyo kama watu wadunia watazamavyo,watafsirivyo na watendavyo,siku zote,tarehe zote ni za Bwana adui kadandia njiani_* Laikini *Mithali 23:7a* _Maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo_.
❤Siku hii ya Leo inayo baba ujumbe wa siku ya wapendanao,nataka niwatafakarishe walio kwente ndoa,mahusiano na uchumba,wakati wengine wanaitazama ni siku ya michepuko,zinaa,siku ya miungu....ndo tafsiri huwenda ni kweli,au siyo kweli (kama zikivyo siku za juma, huziita na kuzitafsiri hivi, *Saturday =Satan day, Sunday=Sun day nk*)Tafsiri hizi mbovu hazitufanyi kuacha kuzitumia siku hizi kumwabudu Mungu wetu na kumfurahia Yesu Kristo, just ufahamu wako ukoje wa kiroho, *_Hivyo hivyo siju ya leo 14/2/2014  nakutafakarisha saikolojia ya mahusiano ya wapendanao Intimate love_* uwe na uwezo wa kufurahia mahusiano yako daima. *( Ev Elisha Baba Eve nakukaribisha kwenye uchambuzi*)
❤ *ULIYE KATIKA NDOA*(MME) Unakumbuka kwa nini ulienda kumchumbia huyo mkeo?unakumbuka mara ya kwanza ulipo mwona moyo wako na akili yako ilimtafsiri vipi?Unakumbuka maneno ya kwanza ya kumtamkia nia yako ulivyo yapangilia?Unakumbuka baada ya kumwambia hisia zako juu yake,alikujibuje? Unakumbuka ule muda wa kusubiria jibu lako la ombi la kumuoa moyo wako ulikuwa katika hali gani?je,unakumbuka siku ya Kupewa jibu lako la NDIYO(YES)ulikuwa una furaha gani,?Je unakumbuka neno la kwanza ulilo mwambia baada ya jibu la Yesu? ( *_Majibu ya maswali hayo ndiyo Nguzo ya siku hii ya Wapendanao,kurudisha Harufu ya PENZI LA KWANZA lililo na harufu nzuuri kwenu wana ndoa_*)
(MKE) Una kumbuka vijana wangapi walikuahidi kukuoa na kukuacha?,unakumbuka vijana wangapi walisema sitakuumiza moyo wako lakini wakakuumiza hata wengine(wakakujua kimwili,kukubebesha mimba na kukuacha?),Unakumbuka Siku alipo kuja huyo mmeo uliwaza huwenda ni kama wale walivyo tangulia kukuumiza?Unakumbula alipo kupa ombi lake ulijibuje,siku unapanga kumrudishia jibu ulivyokuwa unasikia moyoni, unakumbuka safari ya uchumba wenu tabia uliyokuwa unaionyesha kwake?unakumbuka siku ya harusi ulikuwa na furaha gani kuona wadada wote wanakumezea mate ukiwa kwenye shera wao wako kwa sare za purple,kitenge na saee za baby yellow?unakumbuka honeymoon?unakumbuka maisha ya kwanza na huduma za mwezi wa kwanza wa ndoa ulizo kuwa unazitoa? ( *Majibu ya maswali hayo ndo Muhimili wa siku hii ya wapendanao na harufu nzuri ya ndoa yako*)
❤Katika siku za maisha yako,furaha,upendo na amani vinatengenezwa na wewe siyo vina shushwa kama mvua🌧🌧🌧🌧. Huna haja ya kuchepuka,kuchana,kuikimbia ndoa,kumkatia tamaa mwenzako,bado kuba nafasi ya kuifurahia ndoa. *_Love(upendo)tafsiri yake nyepesi ni Nguvu ya kugundua madhaifu ya mwenzako na kumkubali katika madhaifu yake huju ukimsaidia kwa moyo wa furaha kuondoka katika madhaifu ili mfurahie uwepo wa kuwa pamoja, udhaifu wake usikufanye kumsukumia mbali,ila mlete karibu kwa sura ya upole na matumaini_* Walio na Mungu tunaongeza na maombi ya kumfungua,kumtengeneza kunfanya akufae. (mwisho usikubali kupoteza kuamini mwenzako hakufai tena kwasababu ya changamoto za mpito katika maisha ya mahusiano. Amini uzuri wake wa kwanza Utarejea) *YEREMIA 31:17*
*_Yeremia 31 : 17 - Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe._*
❤ *ULIYE KWENYE UCHUMBA* Katika siku hii ya wapendanao,tafakari haya, Je,msukumo wa kumtafutavau kumkubali huyo awe mtarajiwa wako wa maisha,ulitokana na nini?na umbo lake,pesa,elimu,kabila,classmate,schoolmate,ukoo,au shinikizo la familia,au kwasababu mlijuana kimwili mkiwa marafiki,ana mimba yako,una mtoto wake?au kwasababu *_Uliona vitu adimu ulivyo vipenda vya Kimungu,kimawazo yake,na mtazamo wake ni wa kwenda mbali kimaisha,na nitafauti na wengine ulio dhani waweza kuwa wazuri? Umejipangaje kumfanya mwenzako aendelee kujuona wewe wa thamani maishani mwake na usimkere wala kukukera?...katika mambo yote usidharau vichocheo vya upendo sasa na baada ya ndoa,heshima,utii,kunyenyekea,zawadi,lugha nzuri,care na kumwambia mwenzako we mzuri Nakupenda_*
❤ *ULIYE SINGLE* Unanafasi kubwa kufanya maamuzi sahihi kama ukitulia na kutafuta maarifa ya mahusiano,usitumie mifano ya walioshindwa kuandaa safari ya ndoa yako,ndoa yako itakuwa mbaya kuliko za walio shidwa tayari. Amini Mungu ni mtoa vyema,omba mtumikie usijichanganye ukapoteza sifa ya kupata kitu kizuri.
_Mwana Saikolojia na Mchambuzi wa mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)naishia hapo nikutakie Mwanzo mpya wa Mahusiano yako na mwenzako katika tarehe hii 14/2/2017 siku ya wapendanao_
Makala hii ni kwa Watu wote Walioko kwenye Ndoa,Uchumba na Wanao tafuta na kutafutwa.
*_Special thanks ni kwa Mpe dwa wangu, Queen Evelyne Elisha,Much Appreciations to your love God bless you_*
Kwa mawasliano zaidi;
Facebook Elisha Kazimoto
Instagram Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078
Group WhatsApp Material Adimu University.
Blog. Materialadimuuniversity2017email babaeve75@gmail.com
   *_Utakuwa na nguvu na ubora kwa kitu ulicho na Maarifa ya kutosha kwacho,usicho kijua utakuwa Dhaifu_*

No comments:

Post a Comment