Tuesday, 31 October 2023

NJIA PANDA YA NDOA

💢💢 *NJIA PANDA YA NDOA ZA KIROHO* 💢💢
*_Imeandaliwa na Mtaalamu wa Saikolojia ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Mkurugenzi wa Shirika la Gospel Foundation Tanzania(GFI)_*
Mawasiliano: 0755444078
Email: babaeve755@gmail.com
........................................
_Shalom kwa wana ndoa wote(Maana yake Amani kwa wote waliofunga agano la kuishi pamoja kama mke na mme_
💢Leo nakuletea uchambuzi wa *Kisaikolojia na Kiroho juu ya Ndoa zote zinazo Pumulia Mashine(ziko njia panda) huu ni uchambuzi wa Uponyaji* kama utakuwa UJAFA NAFSI YAKO, kuna watu wamekufa nafsi tayari hao kila kitu uwa wanakiona UONGO ua Hakiwezekani tena.
💢Ila wale wanaoumwa wakikubali kupata dawa wanapona nawale wanao hisi harufu au homa ya shida katika ndoa wakipata dozi hii wanapona.
💢Ndoa nikitu pekee sana duniani(Siyo mbinguni) mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa, nasema duniani, Ndoa ndo *Chombo pekee cha Kutuliza Msongo walo wa mawazo, Ndo chombo pekee Kinaweza kukuua Kabla ya wakati wako wa kufa, ndo chombo pekee kinaweza kukupa maendeleo ya Kimaisha na ndo chombo pekee kinaweza kukufanya Maskini wa kutupwa, ndo chombo pekee kinaweza kukupa Heshima katika jamii na ndo chombo pekee kinaweza kukuvua nguo na kukupa aibu kuu katika jamii ndo Chombo pekee kinaweza Kukulinda ukawa Salama na ukaishi maisha ya Amani na ndo chombo pekee kinaweza kukufanya uishi kama mkimbizi katika nchi ya ugeni,mwisho ndo Chombo pekee kinaweza Kukuandalia njia Ya kwenda mbinguni kwa amani na ndo chombo pekee kinaweza kukuandalia Barabara ya Kwenda Jehanamu aidha unataka au hutaki kwenda jehanamu(mmmmh Hiyo ndo Ndoa) Weka pembeni masuala ya Upako,Imani,nk hayo yanamchango wake mimi nazungumzia Hapa Duniani katika maisha ya kila siku kama Taasisi,nisikilize katika uchambuzi huu wa Kisaikolojia na Kiroho*
💢Kuna kitu walebwa ndoa zinaitwa za Kimungu aunza kiroho KINAKOSEWA sana baada ya Kuoana si *Wanaume wala Wanawake*(wawe wako kiroho sana au hawako kiroho sana wengi siyo wote Wanakikosea) na ndicho kimeziweka ndoa nyingi Njia panda.
💢Kuna maumivu makubwa sana ambayo mama uwezi jua au ambiwa na mmeo Unayo mpatia(akikwambia utajilaumu kamwe) vilevile kuna maumivu baba unampa mkeo akikwambia utajiona ufai kwake kabisa ila *Ameamua kunyamaza tu* Moyo unatiririka Damu akijua yeye mwenyewe( *Hizo ndo uwa sumu za mwili na sumu za wokovu kiroho*) _utaona magonjwa mara presha,vidonda vya tumbo,kuumwa kichwa, kupoteza hamu ya mambo ya Mungu kidogo kidogo_ kumbe ni Maumivu aliyo nayo ambayo Anashindwa kukwambia, au anakosa njiambadala ya kuyatatua maana,kila njia amejaribu UMESHINDWA kubadirika, sasa njia zoote zinazo baki ni Hatarishi kwake kuzichukua LIVE, inabidi AVILIE NDANI KWA NDANI hii ndo hatari sana.
💢Kuna kitu Biblia ilisema sijui kama umewahi kukijua nguvu yake.... *_Aliyeoa au kuolewabAnajishugulisha namna ambavyo atakavyo mpendeza mmewe au mkewe_*
💢Hii sentensi ya Kibiblia niya kisaikolojia Typically siku mwana ndoa yeyote akielewa Mtume Paul alilenga na alimaanisha nini NDOA ZOTE zitapona na amani na furaha na Uaminifu utarejea ndani ya ndoa.
*33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.1 Wakorintho 7:33*

*34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.1 Wakorintho 7:34*
💢Unapaswa kujua kwamba Ndoa niya duniani, unapaswa kujua namna ya kufanya umfanye mwenzako ATULIE NA AKUONE WEWE TU ili kama yupo rohoni atulie mbele ya Mungu kutengeneza mahusiano mazuri na Mungu.
💢Kujishugulisha na mambo ya dunia hii ili kumpendeza mwenza wake *Kisaikolojia ni kusoma Saokolojia ya mwenzako,kujua nini Kinamchukulia nafasi katika maisha yake kwakona kukifanya ili Saikolojia yake itulie*
💢Tuna wanandoa wengi wapo kwenye ndoa, waimbaji,wahubiri, wana huduma mbalimbali ila SAIKOLOJIA ZAO HAZIJATULIA kwa maana hiyo hata HUDUMA au Kiroho chao KIPO KWA NEEMA TU ya Mungu ila tuna sema *They are Vulnerable to Fall Down* yaani wako kwenye hatari ya Maanguko ila wanashikiliwa na Neema ya Mungu na LEGACY ya Kazi  aidha waliyo ifanya katika ujana wao ndo maana wana survive.
💢Alieyo oa au kuolewa kujishugulisha na mambo ya dunia hii ili wampendeze mwenzake, ni *Kufanya mambo ya Kudhibiti Hisia za mwenzako ziwe juu yako na aifurahie ndoa yaani afurahie Kuishi nawe*
💢Hapa kuna maswali inabidi ujiulize,..
1️⃣Nini mwenzangu kinamchukulia time baada ya kuoa au kuolewa UJITAHIDI kumfanyalia..... Mwingine anahitaji ;
1)Heshima sana, yaani ukimpa heshima na kumfanyia mambo ya kumuheshimu aaah anasikia raha.
2)Mwingine ni Lugha nzuri, yaani anahitaji maneno laini na matamu ya mahaba aah anaenjoy.
3)Mwingine ni sex( yaani ndo kama chakula au maji yake) yaani akihitaji sex muda wowote pasiwepo vikwazo na visababu vya ajabu ajabu au masharti aaah anasikia ni kama ameoa au ameolewa na bonge la mtu pekee duniani.
4)Mwingine anahitaji kujaliwa, kuhudumiwa, akipata vitu hivyo yaani yeye anasikia dunia yote yake.
_Yako na mambo mengine na mengine hapo nimekupa mifano tu michache sasa wewe *FIKIRIA WAZA NI KIPI UWA KINA KUCHUKULIA AKILI YAKO KWENYE NDOA KWA MWENZAKO* hicho ndo ambacho anasema Hujishugulisha na dunia hii Ili ampendeze mwenzake_
💢Ndoa nyingi zinaingia NJIA PANDA kwakuwa Watu *Awajishuguli na Dunia Hii namna ya Kumpendeza mwenzake* Maadamu alishaoa au kuolewa anaona imeisha kwani utaenda wapi,kwani kunaaja gani ya kujiangaisha.
💢Wanasahau kwamba kuna Gharama ya Kumpata mtu(kuna maangaiko ya dunia hii kumpata mke au mme,ila pia kuna Gharama ya kumlinda mwenzako)baada ya kumuoa au kuolewa naye.
💢Ndoa nyingi wanaishi pamoja ndani kwenye nyumba moja ila Kila mmoja yupo Nje ya nyumba kisaikolojia.
💢Ndo maana kunawanandoa wengi ambao *Wanaweza Kufurahishwa haraka sana, Kufarijiwa sana, kupendwa sana na watu wa nje kuliko wa ndani* Una dhani nini shida, Saikolojia ya mwenzake Kujishugulisha na dunia hii ampendeze mwenzake HANA, ila kuna watu wa nje wanaweza Kujua namna ya kumpendeza mtu mwimgine ambaye ndo MMEO AU MKEO.
💢Kuna janga moja la SILENCE RELETIONSHIP ambalo kwa sasa linazikumba ndoa nyingi(WAO HAWAJUI) anayejua wewe umebahatika na ukibahatika USIPANIC angalia UNAKOSEA WAPI  *Rekebisha Utaona mwenzako Anaua Mahusiano ya Kimya kimya,Kimya kimya unabaki wewe* usije angaika Kupambana kuzuia mahusiano ya kimya kimya kwa kelele zako bila Kuangalia wapo umekosea.
💢Kisaikolojia tunasema, *Ukiona mtu aliye kwenye mahusiano flani ya uchumba au ndoa* anaanzisha mahusiano mengine ya kimya wakati hatangazi kuyaacha ya kwanza waziwazi jua...
1.Kuna GAP(ufa) moyoni, au akilini ambalo limetafutiwa wakuliziba kimya kimya ili asogee mbele.
2.Kuna Tabia ya kutoridhika ambayo niya asili hii inatokana kurithi au makundi.
3.Kuna kuchoka na kuzoea mahusiano yasiyo na ubunifu wa jambo jipya(yanatafutwa mapya maana kila mahusiano mapya yana ubunifu wa jambo jipya kila siku)ndo maana Biblia ikasema *Unatakiwa Ujishugulishe na Dunia hii ili ujue namna ya kumpendeza mwenzako kila siku* kujishugulisha ni kubuni kila siku unatafuta jambo jipya.
2️⃣Nini nikifanya namuondoa mwenzangu kwenye Mood kabisa na anaweza chukia siku nzima hata wiki.
💢Unajua kuna watu ambao uwa *Awajali Hisia za Mwenzake* hata kidogo, anaweza fanya lolote,akaamua lolote liwalo na liwe hii inaua Hisia za mwenzako sana kiasi kwamba unampelekea *Akuone ni Mtu baki tu kwenye maisha yake, basi tu anaishi nawe ndo shida* ila hana hamu nawe kwa lolote.
💢Ndo maana wana sailolojia wanasema *Fanya kitu kinachoitwa Mistake Analysis kwa mwenzako kwa makusudi na baadaye usizirudie* yaani unamkosea mwenzako mambo mbalimbali unamnyima haki zake flabi flani kwa vipindi kadhawakadha kutafuta kujua *Nini Kina mwondoa kwenye furaha na changamko lake kwako* ukisha jua weka nyota USITHUBUTU kufanya kosa hilo,labds itokee kama ajali na ikitokea wahi kumwomba msamaha kabla moyo wake aujararuliwa na kukufuta. *Huko ndo kunaitwa Kujishugulisha na mambo ya dunia hii Ili Kumpendeza mwenzako*
💢Kwani wewe unahisi kujishugulisha na dunia hii ni nini? ( _Kupika? Kufua? Kuosha vyombo? Kununua nguo? Kuacha pesa za matumizi nyumbani?_) hayo yako ndani ila nikuchanganua kila siku kujua *Dunia hii tuliyomo,inamwitaji mmeo kiasi gani, inamwitaji mkeo kiasi gani, inamuwinda mmeo au mkeo kiasi gani halafu sasa wewe ujipange Kuidhibiti isimpore mikononi mwako*
💢Ukumbuki Yesu alisema kwamba baba wote ulionipa _Hakuna atakaye mpokonya mkononi mwangu hata mmoja, au hakuna niliye mpoteza isipokuwa mwana wa uptevu (Yuda)_
💢Inabidi mwanandoa wewe upambane kwenye nafasi yako kujishugulisha na dunia Kutimiza Wajibu wako kwa mwenzako hata kama kuna Upotevu wowote unazaliwa au unatokea kwa mwenzako YEYE AJIHUKUMU MWENYEWE kwa Nafsi yake,lakini asiseme sentensi ya Adamu ya Mke Uliye nipa ndo Amenisababisha( Wewe Usiwe Sababu).
💢Namalizia kwa kusema kwamba, *_Kwa nyakati za sasa dunia inaenda kasi sana kuziharibu ndoa nyingi, ndo maana watu kujiua ni kwingi, watu wanakufa katika umri mdogo tofauti za zamani watu ambao walikufa katika uzee na wakizikana mke na mme wakiwa wote, kwa sasa Divorce nyingi, Single Parent family ndo nyingi, wengine wanaishi kiugumugumu kwa aibu ya kuachana wataonekanaje kwa watu au kanisani._* Nini kifanyike sasa ili kwamba Tutoke Njia panda?
1️⃣Kwasasa Wanahitajika Wana Saikolojia wengi sana watusaidie kutibu majeraha ya kisaikolojia ya Wana ndoa na mahusiano(Wafundishe na kufundisha)
2️⃣Wafanyaji wa Utafiti waongeze Uwanja wa kufanya utafiti juu ya Vyanzo ya Migogoro ya ndoa na waje na Masuruhisho yake yafundishwe siku kwa siku.
3️⃣Watumishi wa Mungu wajikite katika Kufundisha watu neno la Mungu na kuwasihi watu Warudi kwenye Msingi wa Mwongozo wa Neno la Mungu kuhusu Nafasi, Wajibu na Haki za Mwana ndoa(Ke kwa Me)
4️⃣Mwanandoa Usimkatie Tamaa mwenzako, anaweza kuwa hivyo kwasababu ya Ujinga wa Kutojifunza na Malezi hafifu aliyo yapata kwenye familia, endelea kumwelekeza kwa upendo na wewe kujifunza zaidi ili umbadirishe.
*_Hii Imeandaliwa na Mwanasailojia Ev Elisha Kazimoto(Mkurugenzi wa Shirika la Vijana la Injili Duniani(GFI)_*
Phon: 0755444078
Email :babaeve755@gmail.com
Facebook :Ev Elisha Kazimoto.
YouTube channel.. Ev Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment