Friday, 14 July 2023

USHINDI UNAHITAJI AKILI

🥅🥅 *USHINDI WOWOTE UNAHITAJI AKILI* 🥅🥅

ANDIKO KUU NI ZABURI 53:2
*_2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.Zaburi 53:2_*

_Imeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(CEO-GFI)_
Whatsapp *0755444078*
_Haleluya mwana wa Mungu uliye okoka na unayempenda Bwana na kukumtumikia kwa moyo wako wote, leo nina ujumbe wako maalumu kutoka kwa Bwana karibu ubarikiwe na uinuliwe_
✍️Ushindi wowote katika maisha ya kiroho au ya kimwili unahitaji *Akili* tena Ikiwa ni maisha ya Kiroho tunasema unahitaji *Akili ya Kimungu kubwa*
✍️Lakini mtu mwenye akili Biblia imesema ni yule mtu *Amtafutaye Bwana* huyo ndo Kabisa Amefuzu katika Elimu ya Mungu anastahili kukabidhiwa Gamba la Kiroho kwamba huyu ana *Akili*
Hivi kwanza tujue AKILI NI NINI?
1️⃣Akili ni Nuru, ni nguvu ya kutoa mwangaza wakati wa giza.
✍️Ndiyo maana wakasema Elimu ni mwanga wa maisha.
✍️Sasa kiroho tunasema mtu amtafutaye Bwana ana akili na kama ana akili maana yake *Ana Nuru katika Giza* linalo shindana naye.
2️⃣Akili ni Mlango wa Ushindi.
✍️Wakati watu wanajiuliza nafanyaje kutoka hapa mbona kama niko gerezani, Amtu amtafutaye Bwana mwenye *Akili ana mlango wa kutokea*
✍️Ujasoma andiko linalosema *Njia za Kutoka Mautini zina yeye Bwana?* Akili ni Mlango wa kutokea katika mapigano yako.
3️⃣Akili ni Stamina ya kuhimili Mapito.
✍️Vita,Mapito tunayokutana nayo yanalenga *Kututoa Relini, uhame njia* lakini mtu amtafutaye Bwana, mwenye *Akili ana Stamina* hatoki mchezoni kisa vita au majaribu.
4️⃣Akili ni nguvu ya kudharau kelele za Maadui nyuma yako.
✍️Siku zote adui upiga kelele ili akutishe, akytengenezee hofu uache kumtegemea na kumwangalia Bwana umwangalie yeye ili akumalize.
✍️Sasa, mtu mwenye *Akili amtafutaye Bwana akipigiwa kelele yeye anainua macho yake kwa Bwana* hana haja na kuangalia adui au kusikiliza adui anasema nini, sikia Mungu anasema nini nawe wakati huo wa Vita.
5️⃣Akili ni Nguvu ya Maamuzi inayo jua wakati wa kusema na wakati wa kunyamaza.
✍️Si kila wakati unalazimishwa Kusema Useme, na si kila wakati unalazimishwa kunyamaza untamaze.
✍️Kuweza hayo unahitaji *Akili inayo mtafuta Bwana* itakupa wakati sahihi wa kuyafanya hayo yote mawili Kusema na Kunyamaza na hapo *Umewaweza Adui Zako*
✍️Una jua nini, Wakati Adui anategemea useme na hausemi, *Inamuuma* na wakati anategemea *Unyamaze ila we ndo Unasema inamuuma pia*

_Kwanini Mungu anatafuta mtu mwenye Akili Duniani kwa mujibu wa Zaburi 53:2?_
✍️Kwanza inabidi ujue Mungu anafanya kazi na wanadamu( Warumi 8:28).
✍️Kwa maana hiyo ili kutimiza kusudi lake anawataka awapate watu wenye Akili ndo wanauwezo wa Kutimiza kusudi la Mungu duniani.
1️⃣Mtu mwenye Akili anauwezo wa kutimiza kusudi la Mungu bila kuzuiwa na mazingira magumu.
2️⃣Mtu mwemye Akili anaisikiliza Nia ya Mungu(Kristo)ndani yake na si Nia ya watu juu yake.
✍️Katika pointi hizo 2 juu soma *1Samweli 17:26-30* utaona Nia za watu juu yako nikukuzuia usiende au kutimiza kusudi la Mungu.
3️⃣Mtu mwenye Akili aumizwi na vita juu yake, bali anaumizwa na maamuzi ya kupoteza alichokibeba ndani yake kwasababu ya vita juu yake.
✍️Unajua nini, Vita yoyote inayokuja juu yako hailengi maisha yako au wewe kama wewe, vita yoyote inalenga *Kuua au Kupoteza Ulichokibeba* (Kusudi la Mungu ndani yako) MATHAYO 2:13
✍️Herodi alikuwa ataki kuua Yesu, alikuwa anataka kuua Mfalme wa Wayahudi(Yesu alitambulishwa ni mfalme wa Wayahudi) maana yake Herode hana ufalme tena(hii mdo ilikuwa hofu ya Herode) kumbe Yesu ufalme wake si wa ulimwengu huu.
4️⃣Mtu mwenye Akili Aishi kwa kauli za *Watu wananisemaje tu* bali Mungu na Nafsi yake inasemaje kwa habari yake? *Mathayo 16:13-17*
✍️Watu wana muono wao juu yako, kuna wanaokuoa *_vibaya, kuna wanaokuona mtu mwema, kuna wanaokuona mtu jeuri, una kiburi, unajiinua, unajisifu, maskini, mjinga, local sana, mshamba sana, unamuda mchache utapotea_* Kila mtu anamuono wake juu yako.
✍️Kwa maana hiyo usilazimishe wote wakuone unavyo jiona.
✍️Wanafunzi wa Yesu walimpa majibu Yesu ya watu wanavyo muona Yesu, kila mtu alikuwa na jibu lake hata wale ulio *Hisi wangekuona Unavyojiona wewe utashangaa nawao wanaungana na watu wengine wanaokuona tofauti na ulivyo*  ndicho kilitokea kwa Yesu.
✍️Yesu akawauliza na ninyi mnasemaje? WOTE WALIBAKI KIMYA IKIWA NAMAANA NA WAO WALIMUONA YESU KWA NJIA ILE ILE YA WATU WALIVYOKUWA WAKIMSEMA YESU TOFAUTI.
✍️Ila Mungu ni mwema sana katika weengi wanaokuzema tofauti KUNA PETRO WAKO mmoja tu *Atautambulisha Uhalisia wako* huyo ndo atawajulisha wengine wewe ni nani.
✍️Kuna watu uwa wanaumizwa na *Kusemwa Vibaya* mmmmh hicho nikiwango kidogo cha Akili ya Kimungu, ujasikia Biblia inasema *Amebarikiwa(Heri) Astahimiliye Majaribu?* Maana yake nini?
👉Unabaraka kama ukiwa na uwezo wa kuendelea na wokovu ikiwa wewe unapigwa vita usiokoke.
👉Umebarikiwa wewe unayeweza kuendelea Kumtumikia Mungu kwa moyo wote wakati Unazushiwa Mabaya.
👉Umebarikiwa wewe unayeweza kuendela na huduma bila kukata tamaa wakati huduma yako inapigwa Vita kila kona. *YAKOBO 1:12*
*_Hizi ndo baraka Biblia inazitoa kwa watu wenye Akili yaani uwezo wa Kukaa kwenye Reli ya Kiroho wakati wanakutana na Tufani ya kuwavunja Moyo_*
✍️Mungu akupe Akili, Akupe Neema ya Kumtafuta Yeye, Akupe Neema ya Kuendelea mbele katika nyakati zote.
*Hili ndo Neno la Bwana kwako,kutoka katika kinywa cha mtumishi wa Mungu*

Ev Elisha Kazimoto(C.E.O-G.F.I)
Whatsapp: 0755444078
Email: babaeve755@gmail.com
Facebook: Ev Elisha Kazimoto
YouTube channel :Ev Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment