Sehemu ya 2 ya somo la uzaliwa wa kwanza 👇👇👇
⚽3⃣ *UZALIWA WA KWANZA WA MWILI WAKO (UBIKRA)*⚽3⃣
❤ _Kuna balaa moja chini ya jua linaloendelea hapa chini ya jua katika kizazi hiki, cha vijana wa kike na wa kiume waliookoka Kupoteza, kuuza Uzaliwa wa Kwanza wa mili yao_
❤ Imefikia hatua ya kuzoeleka kuwa hakuna binti Bikra, au kijana bikra, hii ni hatari kubwa kwa future (maisha ya baadaye) ya vijana, hatari kubwa kwa Ndoa za vijana wa sasa.
❤ Kijana nisikilize nikupe Hekima ya Kimungu, _Unapo poteza Uzaliwa wa Kwanza wa mwili wako, moja kwa moja umepoteza na Uzaliwa wa Kwanza wa Wokovu, hata ukirudisha uzaliwa wa kwanza wa Wokovu hutapata original blessings ambazo ulitakiwa uzipate, unakumbuka Esau alibarikiwa na yeye alipo lia sana na kuomba abarikiwe(toba) ila baraka zile zilikuwa hafifu wala hazikuwa na nguvu kama za Yakobo za uzaliwa wa kwanza_
❤ Vijana wengi kwa sasa wamedharau uzaliwa wa kwanza wa miili yao, wameuza Ubikra wao kwa mlo mmoja, wamesahau uzaliwa huu, una *_nguvu kubwa katika maisha yao ya ndoa, maana unaleta mke/mme sahihi wa kuoana naye, Unaleta Uaminifu katika ndoa, Unaleta Amani na upendo katika ndoa, Unatuliza changamoto yoyote inayoibuka katika ndoa, unaleta kuishi bila stress(msongo wa mawazo) , Unaleta kujiamini, unaleta kuthamimiana, unaleta maendeleo ya familia._* Lakini kinacho endelea sasa ni hatari, katika vijana 10 wanao oa/kuolewa 7 wamepoteza uzaliwa kwanza wa Ubikra, wengine katika uchumba, wengine wamepotezea chuoni, shuleni, ofisini na mitaani tu. Hii ni hatari sana._Nikama limekuwa la kawaida kufanya uasherati ila hujui gharama yake katika maisha ntakufumbua macho katika somo hili
❤ _Kijana Zinaa unayoiendekeza wa sasa wakati hujaoa/kuolewa, Lazima ikugharimu tu, lazima ulipwe uhuni na Utapeli wa kuuza uzaliwa wa kwanza wa mwili wako kwa kisa cha mchumba wangu asiniache, bosi Mwenye pesa amenishawishi, nimezidiwa na hisia, nimekaa bila kuoa au kuolewa, sijui Dakitari amesema nisipo zaa mapema sitaweza kuzaa baadaye,kwa sababu yoyote Utalipa gharama, kilio kikuu_kina kusubiri tangu siku hiyo umeuza uzaliwa wa kwanza (ulipo fanya zinaa) haya yote yanakusubiri wewe....
1⃣ *Kuto oa/kuolewa na mtu Sahii kitakacho kufanya usifurahie maisha ya ndoa*
2⃣ *Kubeba mimba usiyo ifurahia, na mtoto anazaliwa ana roho ya kukataliwa*
3⃣ *Kutoa mimba na kupata Laana ya kuua na ugonjwa wa Kisaikolojia*
4⃣ *Kupoteza heshima katika jamii na mbele za Mungu*
5⃣ *Kupoteza uhuru wa kuingia katika mahusiano kwa furaha na ujasiri*
❤ _Hayo ni baadhi ya mambo yakutokea kabla ya kuingia katika ndoa, na baada ya kuingia kwenye ndoa hiyo ndo safari itakayo kufanya ujutie tendo la siku moja la Zinaa_ *Tujifunze mbinu zinazo wanasa watu katika zinaa, Shida, na Uchungu wa Zinaa na ikisha fanyika nini kinatokea, Tuwaaangalie watu hawa 4,utagundua upo kundi la mtu gani kati ya hawa 4. AMNONI, TAMARI, YUSUFU NA MKE WA POTIFA_*
❤( 2 Samweli 13 : 1 - Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda.)
_Dada, kuna watu wanakupenda/wanakutamani si kwa kukuuoa ila kukuharibia Uzuri wako na nguvu ya uzaliwa wa kwanza wa mwili wako (Ubikra)_
❤ ( 2 Samweli 13 : 2 - Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote)
_Dada kuna watu wanaugua kisa tu uzuri wako nao wanashindwa kukuingia kwa sababu ya Nguvu ya uzaliwa wa kwanza wa Wokovu, laikini wanajiandaa kwa mbinu mpya mpaka wa kupore Ubikra wako na Wokovu wako ambazo ndo nguzo na dira za maisha yako ya furaha na ushindi._
(2 Samweli 13 : 5 - Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake.)
_Kuna mbinu mpya ya kubembeleza, kutishia kujiua, kutumia pesa, kukuita hotelini, kukutoa out, kukupa zawadi za gharama, Kujifanya Anaokoka na mtumishi wa Mungu, kutishia kuvunja uchumba_ Akikunasa katika moja wapo kwisha habari yako.
2 Samweli 13 : 10 - Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani.
_Huu ndo upofu wa wadada wengi, hivi inakuwaje unamwamini kijana yoyote hata kama ameokoka kiasi cha kwenda chumbani kwake, au kukutana guest, au nyumbani kwake Geto, lugha za naumwa njoo nyumbani unaenda peke yako, niletee smartphone 📱 yangu hotel flani na unaenda peke yako, lazima uache kule uzaliwa wa kwanza wa mwili wako (BIKRA)_
2 Samweli 13 : 11 - Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu.
_Haya ndo Majanga yanawakumba wa dada wengi, ata wewe unaye soma ujumbe huu, na matukio haya hayafanywi na Stranger people (watu hatari/adui no ni mchumba, rafiki wa karibu, mshirika mwenzako, mtu uliye mwamini. Ndicho kilimkumba Tamari_
2 Samweli 13 : 13 - Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.
_Tamari alijua aisee ukisha haribu ni Aibu ya milele maishani mwako, akasema ntaiweka wapi aibu yote hii ya kupoteza uzaliwa wa kwanza wa mwili wangu_
2 Samweli 13 : 14 - Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.
_Wanaume waharibifu ukisha ingia ndani ya 18 zao hawasikii kitu mbaka wamekuondolea uzaliwa wa kwanza wa mwili wako_
2 Samweli 13 : 15 - *Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako*.
_Haya ndo matokeo baada ya Zinaa (kupoteza uzaliwa wa kwanza wa mwili wako, hawakuhitaji, mimba hataki, matumizi hupati, kukuoa hakuoi, unabaki kujililia, na wengine waliamua kujiripua kuolewa na huyo mpangani ili watunze mimba na mtoto_
*Kuna mtu mmoja aligundua thamani ya uzaliwa wa kwanza wa mwili wake, naye ni YUSUFU, alipo tiwa mazingira yakutokea uzaliwa wa kwanza wa mwili wake, asema nifanyeje ubaya huu ni mkose Mungu?*
Mwanzo 39 : 7 - Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
_wee wanao kushawishi mbona hawaeleweki na wana kuzuzua? Ungepata jaribu la Yusufu ungechomoka kweli?_
*Mwanzo 39 : 10*- *Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.*
_Huu ndo msimamo wa kijana anaye jitambua_
❤❤ *_Raha ya muda mfupi huleta majuto ya muda mrefu_*❤❤
No comments:
Post a Comment